Thursday, September 30, 2010

IFUATAYO NI CCM

 ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2010 – 2015
UTANGULIZI
1. Katika Uchaguzi wa kushindanisha vyama vingi vya siasa ili kutwaa Dola na
  kuunda Serikali kila Chama hutarajiwa kuandaa Ilani ya Uchaguzi. Ilani hutafsiri
 na huelezea Sera za Chama kuhusu maeneo muhimu ya siasa, uchumi na jamii
na hutoa maelezo fasaha kuhusu mikakati ya utekelezaji wa sera zinazonadiwa
pindi wagombea wake wakifanikiwa kushinda. Aidha hutoa ahadi kwa Wananchi
kuhusu mambo ambayo Chama kitaelekeza na kusimamia Serikali kutekeleza.
Kwa hiyo Ilani ya Uchaguzi ni Maelezo ya Sera katika kipindi husika, na inalenga
kuwaeleza Wananchi ni mambo gani Chama kitafanya iwapo kitashinda Uchaguzi
na kuunda Serikali. Ilani hii ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2010 hadi 2015
inalengo hilo hilo.
2. Ilani hii ya CCM imejengeka katika kukiri kwamba changamoto kwa Serikali
  katika kipindi hiki ni ya Kujenga Uchumi wa Kisasa na Taifa Linalojitegemea. Vile
 vile CCM inatambua kuwa modenaizesheni ya uchumi na Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi ndiyo mikakati sahihi ya kujenga uchumi wa kisasa. Aidha mafanikio
ya azma hii unategemea kutambua hali na mazingira ya kisiasa, kiuchumi na
kijamii ya karne ya ishirini ya dunia na ya nchi.
HALI YA DUNIA, MAJUKUMU YALIYOMBELE YETU NA MIKAKATI YA
MAENDELEO KWA TANZANIA
Dunia Ilivyo sasa
3. Dunia ya leo imegawanyika katika nchi za kaskazini na nchi za kusini. Nchi zote
  za dunia kwa ujumla wake zimeathirika na mtikisiko wa fedha na uchumi. Athari
 za mtikisiko huo zinaonekana kutofautiana kutoka nchi moja kwenda nchi
nyingine. Aidha nchi za Kaskazini zilizoendelea zimeathirika zaidi kuliko nchi za
Kusini. Hata hivyo, athari ndogo kwa Nchi ya Kusini huongeza tatizo la Umaskini
na changamoto ya ujenzi wa uchumi.
4. Ilani hii ya CCM inatolewa katika mazingira ya hayo. Nchi yetu ni nchi miongoni
  mwa nchi za Kusini na kwa hiyo mtikisiko mdogo umetuongezea makali ya tatizo
 letu la msingi la uchumi ulio nyuma.
1
5. Aidha tatizo la nchi yetu ni la uchumi ulio nyuma na tegemezi. Jitihada zinapaswa
  kuchukuliwa ili kuondokana na hali hiyo. Katika mazingira ya dunia ya sasa ya
 kiuchumi na kisiasa, bila kufanya hivyo uchumi wa soko wa dunia, utandawazi na
nguvu za kiuchumi za nchi za kaskazini utaendelea kuididimiza nchi yetu katika
lindi la umasikini, uchumi duni na tegemezi.
6. Katika kutimiza azma ya kujinasua kutoka mazingira hayo na kuelekeza nchi
  katika Kujenga Uchumi wa Kisasa na Taifa Linalojitegemea, Ilani hii inajikita
 katika kuendeleza mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025
(SMT), 2020 (SMZ).
Hali ya Nchi yetu
7.
Pamoja na mafanikio mengi tuliyopata na changamoto zilizojitokeza, tuna fursa
kubwa ya kuendelea kujenga uchumi wa kisasa ili kumudu ushindani katika
mazingira ya utandawazi na kuongeza tija kwa kasi zaidi. Nchi yetu inatambua
kuwa changamoto kubwa inayotukabili ni suala la Mapinduzi ya kilimo, ufugaji,
uvuvi na viwanda.
Tukiyamudu Mapinduzi hayo, uchumi utakuwa wa kisasa unaoweza kuzalisha
ziada kubwa ya mali na kutoa huduma za kijamii zilizo bora zaidi kwa manufaa
ya wananchi wote. Matokeo yake ni kwamba kila mwaka nchi itazalisha chakula
cha kutosha na kuuza nje ziada ili kupata fedha za kigeni.
8.
Chama kupitia Dira 2025 (SMT) na 2020 (SMZ), Mwelekeo wa Sera wa Miaka ya
Tisini na Mwelekeo wa Sera za CCM Katika Miaka ya 2000 hadi 2010 kimeelekeza
suluhisho la kuondokana na hali ya uchumi wetu kuwa nyuma na tegemezi ni
kufanya modenaizesheni ya uchumi. Mchakato wa modenaizesheni ya uchumi
na kuitoa nchi yenye uchumi tegemezi kuelekea uchumi wa kisasa unahitaji
kuzingatia vipaumbele vya msingi vifuatavyo:
(a) Kutilia mkazo katika matumizi ya maarifa ya kisasa (sayansi na teknolojia).
(b) Kuandaa raslimali watu katika maarifa na mwelekeo.
2
(c) Kufanya mapinduzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
(d) Kufanya mapinduzi ya viwanda ambavyo ndivyo kiongozi wa uchumi wa
   kisasa.
(e) Mapinduzi katika nishati na miundombinu ya kisasa.
Lengo la msingi katika kukabiliana na vipaumbele hivi ni kuchochea uwezo wa
kuongeza uzalishaji, jambo ambalo litawezekana kutokana na kuongezeka kwa
ufanisi na tija na ziada kubwa katika uchumi.
Majukumu ya Msingi
9.
Hatua za msingi kuanzisha mchakato wa Kujenga Uchumi wa Kisasa zilishaanza.
Kinachohitajika kwa sasa ni kuongeza kasi, utashi na dhamira ya ujenzi wa
uchumi wa kisasai na kwa muda mfupi uliopangwa katika Dira za Maendeleo
2025 na 2020. Chama cha Mapinduzi kinaweka bayana kuwa Ilani ya Uchaguzi
Mkuu wa Mwaka 2010 itajikita katika kuendeleza jitihada na kuanzisha hatua ya
mwanzo na ya msingi ya mapinduzi kuelekea modenaizesheni ya uchumi na
ujenzi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea. Katika kipindi cha Ilani hii
2010-2015 mchakato wa kujenga uchumi wa kisasa utekelezwa katika maeneo
yafuatayo:-
(a) Kuimarisha na kuboresha elimu.
(b) Kuandaa raslimali watu katika maarifa na mwelekeo.
(c) Kufanya mapinduzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
(d) Kufanya mapinduzi ya viwanda.
3
(e) (f) Upatikanaji wa nishati yenye uhakika na nishati mbadala.
(g)
10.
Kuinua matumizi ya maarifa, yaani sayansi na teknolojia katika uchumi wa
nchi.
Ujenzi wa miundombinu ya kisasa.
Kwa kutekeleza haya, Chama cha Mapinduzi kitakuwa kimeandaa mazingira ya
kuondoa unyonge na shida zinazowasibu wananchi wake zinazotokana na
umaskini na uchumi ulioduni. Aidha Ilani hii itakuwa kielelezo cha dhamira ya
Serikali ya Awamu ya Nne ya kuhakikisha kuwa inaitoa Tanzania kutoka uchumi
ulio nyuma na tegemezi na kupambana na umaskini kwa hamasa, dhamira na
kasi kubwa.
SURA YA KWANZA
MAFANIKIO YA KIUCHUMI NA KIJAMII MIAKA 5
YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE
11.
Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005-2010, ililenga katika kutekeleza
kipindi cha pili na cha mwisho cha Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya
2000-2010, na kutekelezwa katika kipindi cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya
4
Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Jakaya
Mrisho Kikwete.
12.
Katika kipindi hiki Serikali ilitekeleza kwa mafanikio makubwa Mwelekeo wa Sera
za CCM katika miaka ya 2000-2010 na Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2005-
2010 kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Malengo ya Milenia.
Aidha, kutokana na mafanikio hayo Serikali imeweza kuendeleza na kuimarisha
huduma za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Mafanikio ya Kiuchumi:
13.
Katika kipindi hiki Serikali imeweza kutekeleza mipango yake kwa ufanisi
mkubwa na kuleta mafanikio ya kiuchumi yafuatayo:-
(a) Ukuaji wa uchumi ulifikia wastani wa asilimia 6.7 mwaka 2010
   ukilinganishwa na wastani wa 4.5 mwaka 2005.
(b) Mapato ya ndani ya Serikali yaliongezeka kutoka wastani wa Shilingi Bilioni
   177 kwa mwezi mwaka 2005 hadi kufikia wastani wa Shilingi bilioni 390
  sawa na ongezeko la zaidi ya mara mbili kwa mwezi mwaka 2010.
(c) Mfumko wa bei ulibaki katika tarakimu moja tangu mwaka 2000 hadi 2007
   isipokuwa mwaka 2008 ambapo ulifikia kiwango cha 10.3 kutokana na
  mtikisiko wa uchumi duniani.
(d) Bajeti ya Sekta ya Kilimo imeongezeka kutoka asilimia 4.5 mwaka 2005
   hadi asilimia 7.9 mwaka 2010.
  Kutokana na umuhimu unaoongezeka
 wa kilimo cha umwagiliaji nchini kama hatua ya uhakika ya kupambana na
njaa, Serikali imechukua hatua za kuimarisha mkakati wa umwagiliaji na
miundombinu yake, kwa kuendeleza hekta 289,245 za kilimo na kuweka
miundombinu ya umwagiliaji. Hatua hii imeongeza ufanisi wa matumizi ya
maji kwa umwagiliaji kutoka asilimia 12 iliyokuwepo kabla na kufikia
asilimia 30. Aidha, ufanisi huo umeongeza mavuno ya zao la mpunga
kutoka wastani wa tani 1.8 kwa hekta na kufikia tani 5 kwa hekta.
(e) Ukuaji wa Sekta ya Viwanda umeongezeka kutoka asilimia 8.4 mwaka
   2005 hadi asilimia 9.9 mwaka 2008.
(f) Sekta ya Madini imekuwa na kuleta mafanikio yafuatayo:-
(i) Kukamilika kwa Sera ya Madini ya mwaka 2009.
(ii) Kuanzishwa kwa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania.
5
(iii) Kukamilisha ramani tatu za kijiolojia zinazoonyesha uwepo wa
     madini Tanga, Nachigwea na Liganga.
(iv) Kutengwa kwa maeneo ya wachimbaji wadogo katika maeneo ya
    Kilindi, Winzo, Mvomelo, Melela, Rwamagaza, Nyarugusu, Maganzo
   na Mererani. Maeneo hayo yana jumla ya kilometa za mraba
  5,876.5.
(v) Mchango wa Sekta ya Madini kwenye pato la Taifa umeongezeka
   kutoka asilimia 2.4 mwaka 2005 hadi asilimia 2.6 mwaka 2008.
(vi) Mapato ya Serikali kutokana na uchimbaji mkubwa yameongezeka
    kutoka Sh. 457.4 bilioni mwaka 2005 hadi Sh. 840.0 bilioni mwaka
   2008.
(vii) Thamani ya madini yanayouzwa nje imeongezeka kutoka dola za
     Marekani 727.45 milioni mwaka 2005 hadi dola 1,075.9 milioni
    mwaka 2008.
(vii) Ajira katika uchimbaji mkubwa imeongezeka kutoka wafanyakazi
     7,000 mpaka 13,000.
Mafanikio katika Sekta ya Miundombinu
14. Kipindi cha miaka kumi iliyopita cha 2000 – 2010 kimeshuhudia kuwepo kwa
     ujenzi mkubwa wa miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na madaraja
    nchini. Miradi yote ya ujenzi ambayo haikukamilishwa kati ya 2000 – 2005
     imekamilishwa kati ya 2005 – 2010 na kuanzishwa ujenzi wa miradi mipya.
      Kitakwimu, ujenzi wa miradi 15 kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa
     Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010. Aidha, ujenzi ambao
    unaendelea ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4 na wakati
   huo huo miradi 7 ya barabara yenye jumla ya Km. 1,562 inaendelea kufanyiwa
  upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi. Hiki ni kielelezo dhahiri cha mafanikio
 makubwa ambayo yameiweka nchi yetu katika chati ya kuwa na miundombinu ya
kisasa ya barabara.
(a) Barabara
Serikali imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa barabara kama ifuatavyo:-
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
Dodoma

Manyoni
-
(127)
Singida

Shelui -
(Km 110)
Nzega – Ilula na Tinde - Isaka
(Km 169)
Nangurukuru – Mbwemkuru - Mingoyo (Km 190)
6
(v)
(vi)
(vii)
(viii)
(ix)
(x)
(xi)
(xii)
(xiii)
(xiv)
(xv)
Mkurunga

Kibiti
-
Pugu

Kisarawe
-
Singida

Isuna
-
Kyamyorwa – Buzirayombo – Geita
Kigoma

Kidahwe
-
Chalinze – Morogoro - Melela
-
Tunduma

Songwe
-
Dodoma

Morogoro
-
Tarakea – Rongai – Kamwanga -
Rombo Mkuu –
Tarakea
-
Geita

Busisi
-
(Km
(Km
(Km
(Km
(Km
(Km
(Km
(Km
(Km
(Km
(Km
121)
6.6)
63)
220)
36)
129)
71)
256)
32)
32)
92)
Miradi ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ni:-
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
(vi)
(vii)
(viii)
(ix)
(b)
Manyoni

Isuna
-
(Km 54)
Kagoma

Lisahunga
-
(Km 154)
Tabora – Malagarasi – Uvinza – Kigoma (Km 364)
Ndundu

Somanga
-
(Km 60)
Arusha

Namanga
-
(Km 105)
Tanga

Horohoro
-
(Km 65)
Mwandiga

Manyovu
-
(Km 60)
Masasi

Mangaka
-
(Km 54)
Singida – Babati – Minjingu
-
(Km 224)
Bandari
(i) Bandari ya Kigoma
Bandari ya Kigoma imeimarishwa kwa kununua mtambo wa kuondoa
mchanga na hivyo kuongeza kina katika bandari hii. Kujengwa kwa
Cherezo (docking yard) kunasaidia ukarabati wa meli na hivyo
kuongeza usalama wa wasafiri.
(ii) Bandari ya Kasanga
Kukamilika ujenzi wa gati la Bandari ya Kasanga ambapo sasa meli
mbili zinaweza kutia nanga kwa wakati mmoja.
7
(iii) Uchukuzi kwa njia ya maji
Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari (TPA) imeandaa Mpango Kabambe
wa Bandari (Ports Master Plan) ambao umebainisha miradi mbalimbali
ya uendeshaji na upanuzi wa huduma za bandari.
Serikali imekamilisha uanzishaji wa Wakala za Uwezeshaji wa Biashara
na Uchukuzi katika Ukanda wa Kati (Central Corridor Transit Transport
Facilitation Agency – TTFA) na Ukanda wa TANZAM (Dar es Salaam
Corridor) ambazo zitakuwa zikiratibu huduma za usafirishaji
zinazopitishwa nchini mwetu na hivyo kuvutia wafanyabiashara
kutumia miundombinu yetu ya uchukuzi na usafirishaji).
(c)
Vivuko
Kukamilisha ujenzi wa kivuko kipya cha Rugezi katika wilaya ya
Ukerewe Mkoa wa Mwanza ambao unaendelea hivi sasa.
Mafanikio ya Kijamii
Elimu
15.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Serikali ya CCM imeendelea kufanya
upanuzi mkubwa wa elimu katika ngazi zote. Kwa kushirikiana na wananchi na
kwa kupitia programu na miradi mbalimbali kama vile MMEM, MMES na MEMKWA
yamepatikana mafanikio makubwa kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari,
ufundi na mpaka elimu ya juu. Elimu ya Watu Wazima na elimu maalumu nayo
imepewa msukumo maalumu.
(a)
Elimu ya Awali
(i) (ii)
(b)
Idadi ya madarasa ya shule za Awali imeongezeka kutoka 18,455
mwaka 2005 hadi 28,048 mwaka 2009.
Wanafunzi wa Elimu ya awali wameongezeka kutoka 638,591
mwaka 2005 hadi 873,981 mwaka 2009, wakiwemo wanafunzi
2,146 wenye mahitaji maalumu.
Shule za Msingi
(i)
Shule za msingi zimeongezeka kutoka 13,679 mwaka 2005 hadi
15,675 mwaka 2009.
8
(ii) (iii)
(c)
Idadi ya wanafunzi wa shule za msingi imeongezeka kutoka
7,083,063 mwaka 2005 hadi kufikia 8,441,553 mwaka 2009.
Uandikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu umeongezeka kutoka
18,982 mwaka 2005 hadi 27,422 mwaka 2009.
Sekondari
(i) Idadi ya shule za sekondari imeongezeka kutoka 1,745 (1,202 za
   Serikali na 543 zisizo za Serikali) mwaka 2005 hadi shule 4,102
  (3,283 za Serikali na 819 zisizo za Serikali) mwaka 2009.
(ii) Uandikishaji wa wanafunzi (kidato cha 1-4) uliongezeka kutoka
    401,598 mwaka 2005 hadi 1,401,559 mwaka 2009. Hili ni ongezeko
   la asilimia 179.
(iii) Serikali imejenga madarasa 11,266, nyumba za walimu 986 na
     shule za hosteli 52 katika kata 2,575 zilizopo.
(iv) Uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha 5 hadi 6 uongezeka
    asilimia 0.6 mwaka 2005 hadi asilimia 1.5 mwaka 2009.
(v)
(d)
Serikali imegharamia elimu ya sekondari kwa wanafunzi 41,211
wanaotoka katika familia zenye kipato duni ambapo jumla ya
Shilingi 6,677,537,600 zilitumika katika miaka ya 2006 na 2007.
Vyuo vya Ufundi
(i) (ii)
(e)
Udahili wa wanafunzi wa vyuo vya ufundi umeongezeka kutoka
40,059 mwaka 2005/2006 hadi kufikia 48,441 mwaka 2008/2009.
Ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa vyuo vya ufundi
kufikia 210 mwaka 2009 kutoka 183 mwaka 2005.
Pia vyuo vya ufundi stadi vimeongezeka kutoka 260 mwaka 2005
hadi 932 mwaka 2009.
Vyuo Vikuu
(i)
Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka 26 mwaka 2005 hadi
kufikia 32 mwaka 2009. Kati ya hivyo vipya kimoja ni cha Serikali
kinachojengwa
Dodoma
ambacho
kitakapokamilika
kitakuwa na wanafunzi 40,000 na kuwa ndicho kikubwa kuliko
vyote nchini.
9
(ii) (iii) Kati yao wanafunzi 69,250 walipata mikopo ya elimu ya juu.
(iv)
(f)
Wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo nchini
waliongezeka kutoka 55,296 mwaka 2005/2006 hadi 118,000
mwaka 2009/2010.
Jumla ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya mikopo iliongezeka kutoka
Tshs. 56.1 bilioni mwaka 2005/2006 hadi Tshs. 243 bilioni mwaka
2010.
Vyuo vya Ualimu
(i) (ii) Mpaka kufikia mwaka 2009 vyuo 79 nchini vimekuwa vikitoa
        mafunzo ya ualimu. Kati ya vyuo hivyo 34 ni vya Serikali na 45 ni
       vya watu na mashirika binafsi.
(iii) Idadi ya walimu wa awali iliongezeka kutoka 11,148 mwaka 2005
     na kuwa 16,597 mwaka 2009.
(iv) Walimu wa shule za msingi waliongezeka kutoka 135,013 mwaka
    2005 na kufikia 154,895 mwaka 2009.
(v) Idadi ya walimu wapya wa sekondari waliohitimu katika vyuo vikuu
   hapa nchini imeongezeka kutoka 500 mwaka 2005 hadi 19,124
  mwaka 2010 kati yao 7,004 ni wa Diploma na Digrii 12,120.
(vi) Serikali ilitoa Shilingi bilioni 22.5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba
    2,501 za walimu wa shule za sekondari.
(vii)
(g)
Serikali imepanua mafunzo ya walimu na kuishirikisha sekta binafsi.
Miundombinu imeongezeka ambapo hadi mwaka 2009 nyumba za
walimu 26,848, madarasa 79,102 na matundu ya vyoo 97,603
vimejengwa.
Vitabu na Vifaa vya Kufundishia
Kumekuwepo na ongezeko kubwa katika bajeti ya sekta ya elimu ambalo
limesaidia katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa vitabu na vifaa vya
kufundishia.
Afya
10
16.
Utoaji wa huduma za Afya uliendelea kuboreshwa kwa kiasi kikubwa na kuleta
mafanikio yafuatayo:-
(a) Kutoka mwaka 2005 hadi 2009, jumla ya zahanati 464, vituo vya afya 98
   na nyumba za waganga 394 zilijengwa.
(b) Zahanati 1,037, vituo vya afya 285 na hospitali 112 zimekarabatiwa.
(c) Zahanati zimeongezeka kutoka
   2009.
(d) Vituo vya afya vimeongezeka kutoka 526 hadi kufikia 663 mwaka 2009.
(e) Idadi ya Madaktari imeongezeka kutoka 3,528 mwaka 2005 hadi 4,502
   mwaka 2010. Vile vile idadi ya Madaktari Wasaidizi imeongezeka kutoka
  9,028 hadi 14,017 katika kipindi hicho hicho.
(f) Idadi ya Wauguzi na Wakunga imeongezeka kutoka 18,123 mwaka 2005
   hadi 23,886 mwaka 2010.
(g) Chanjo ya watoto dhidi ya kifua kikuu, polio, kifaduro, pepopunda, donda
   koo na homa ya ini iliongezeka kutoka watoto 1,243,388 mwaka 2005
  hadi 1,356,421 mwaka 2009. Aidha, watoto waliopatiwa chanjo ya surua
 imeongezeka kutoka 1,267,716 hadi 1,455,100 katika kipindi hicho hicho.
(h) Katika kuzuia na kudhibiti malaria Tanzania Bara vyandarua 9,000,000
   vyenye viuatilifu vimegawiwa kwa watoto wenye umri wa miaka 5 mwaka
  2009/2010 bila malipo. Aidha, vyandarua 4,200,000 vya hati punguzo
 viliuzwa kwa mama wajawazito.
(i) Vifo vya watoto chini ya miaka 5 vimepungua kutoka 158 kwa kila 1000
   mwaka 2005 hadi 75 kwa kila 1000 mwaka 2010.
(j) Aidha, katika kuleta ufanisi wa huduma za afya, mashine za kuchunguza
   damu, uwezo wa figo na ini pamoja na mashine za X-Ray zimewekwa
  katika kila hospitali ya wilaya na huduma za maabara zimeimarishwa.
(k) Kitengo cha magonjwa ya moyo kimeanzishwa na upasuaji unafanyika
   nchini.
  Aidha, mashine 7 za kusafisha figo zimefungwa na hivyo
 kuwezesha usafishaji wa figo kufanyika hapa nchini.
(l) Maambukizi ya UKIMWI yamepungua kutoka asilimia 7 na kufikia asilimia
   5.
4,679 mwaka 2006 hadi 5,422 mwaka
11
Maji
17.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Serikali imeendeleza juhudi za
kuwapatia wananchi wa Tanzania maji safi na salama. Katika kufanya hivyo
Serikali imeongozwa na lengo la kuwapatia maji watu wa mijini kwa asilimia 90
na watu wa vijijini kwa asilimia 65. Miongoni mwa mafanikio makubwa
yaliyopatikana katika kipindi hiki ni pamoja na haya yafuatayo:-
(a) Mpaka mwaka 2009 kwa vijijini upatikanaji wa maji ulifikia asilimia 58.3 na
   mijini asilimia 80.3.
(b) Miradi 138 imekamilika katika wilaya mbalimbali hapa nchini na watu
   wanapata maji safi na salama.
  Miradi mingine mingi inaendelea
 kutekelezwa mijini na vijijini kwa ajili hiyo.
(c) Kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria. Mradi huu wa
   aina yake na wa kihistoria unawahakikishia wananchi wenzetu wapato
  milioni moja wa Mikoa ya Shinyanga na Mwanza kupata maji safi na
 salama.
(d) Miradi 53 ya maji katika miji mikuu ya wilaya na miji midogo imefanyiwa
   ukarabati.
(e) Miradi 7 ya taifa na 8 ya miji mikuu ya wilaya imekarabatiwa.
Usawa wa Jinsia
18.
Kwa kuzingatia Imani ya CCM juu ya usawa wa binadamu na wito wa kimataifa
juu ya usawa wa jinsia, Serikali chini ya uongozi wa CCM imeweza kutekeleza
yafuatayo:-
(a) Kuongeza ushiriki wa wanawake katika Bunge, Baraza la Wawakilishi na
   Madiwani kutoka asilimia 30 hadi 40. Aidha, ushiriki wa wanawake
  umeongezeka pia katika nafasi mbalimbali za uongozi na utendaji
 Serikalini na katika Taasisi za Umma.
(b) Kuanzisha Benki ya Wanawake.
(c) Kupitisha Sheria ya Mtoto.
12
SURA YA PILI
KUJENGA MSINGI WA UCHUMI WA KISASA WA TAIFA LINALOJITEGEMEA
19.
Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2010 hadi 2020 umeainisha jukumu
kubwa la nchi yetu katika kipindi hiki ni kutekeleza lengo la Dira 2025 la kuleta
mapinduzi ya uchumi yatakayoitoa nchi kutoka kwenye dimbwi la uchumi ulio
nyuma na tegemezi na kuiingiza katika mkondo wa uchumi wa kisasa wa taifa
linalojitegemea. Ili kufikia lengo hili Mwelekeo wa CCM unahimiza Serikali
kutekeleza majukumu yafuatayo:-
(a) Kujenga Uchumi wa Kisasa
modenaizesheni ya uchumi
wa
Taifa
Linalojitegemea,
yaani
(b) Kutekeleza Sera ya Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi
(c)
Kutekeleza Sera ya Dola Kupanga Mipango na Kusimamia Uchumi
(d) Kuongeza uwezo wa Maarifa (sayansi na teknolojia) katika nchi kwa kutilia
mkazo ubora wa Elimu na Raslimali Watu ya Nchi.
(e) Kuweka msingi wa miundombinu ya uchumi wa kisasa kwa kuhakikisha
nishati yenye uhakika na uboreshaji wa miundombinu na huduma za
kiuchumi kwa jumla.
(f)
Kutumia fursa za kijiografia katika kukuza uchumi wa kisasa wa nchi.
13
(g) Kuhimiza Watanzania kujenga utamaduni wa kufanya kazi
(h) Kuhakikisha uwiano wa mapato ili kujenga amani katika nchi na utulivu wa
uchumi na maendeleo
(i)
20.
Kuweka methodolojia ya kusimamia utekelezaji wa majukumu haya ili
kuhakikisha yanafanikiwa
Changamoto za kuibadili nchi yetu kutoka uchumi ulio nyuma na tegemezi
kuelekea kwenye uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea ni nyingi. Uzoefu wa
utekelezaji tulioupata katika kipindi cha Mwelekeo wa Miaka 2000 hadi 2010 na
kipindi cha Ilani ya Uchaguzi ya 2005 hadi 2010 cha Awamu ya Nne unaonyesha
kuwa jukumu hili linapaswa liendelezwe katika kipindi cha Ilani hii kwa
kuzingatia:
(a) Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025
(b) Dira ya Maendeleo Zanzibar 2020
(c)
Malengo ya Milenia
(d) Mpango
wa
Kukuza
Uchumi
na
Kupunguza
Umaskini
Tanzania,
(MKUKUTA)
(e) Mkakati wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA)
(f)
Kilimo Kwanza
21. Ilani hii ya 2010-2015 inalenga kuongeza kasi ya utekelezaji wa mchakato wa
kujenga uchumi wa kisasa na taifa linalojitegemea kwa kuwashirikisha na
kuwawezesha kiuchumi wananchi.
22. Dhana ya Kujenga Uchumi wa Kisasa inalenga katika modenaizesheni ya uchumi.
Modenaizesheni kimsingi ni kuongeza maarifa na matumizi ya sayansi na teknolojia
katika sekta za uzalishaji. Modenaizesheni ya uchumi inalenga katika kuongeza
uzalishaji, ufanisi na tija katika uchumi hususan katika kilimo, ufugaji, uvuvi na
viwanda.
23. Mapinduzi ya kilimo ni msingi wa ukombozi wa uchumi wa nchi yetu. Katika kipindi
cha Ilani hii 2010-2015 utekelezaji utaelekezwa katika modenaizesheni ya kilimo
kwa kutilia mkazo Programu ya Kilimo Kwanza, upatikanaji fedha za uwekezaji
14
katika sekta ya kilimo, mbegu bora, zana za kisasa,matumizi ya mbolea, elimu kwa
wakulima kuhusu kanuni za kilimo, huduma za ugani, mikopo kwa wakulima,
upatikanaji wa masoko, utafiti na matokeo, kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.
24. Kufikiwa kwa lengo hili kutategemea sana mchango wa Serikali katika kusimamia
mikakati ya kusimamia mapinduzi ya kilimo, ya kuunda Benki ya Kilimo na kutoa
msukumo wa kimaeneo, kimkoa na kikanda katika mazao, uwekezaji na masoko.
25. Ufugaji ni moja ya sekta zinazohitaji kusimamiwa ili iweze kuchangia ipasavyo
katika uchumi wa kisasa. Katika kipindi cha Ilani 2010-2015 mkazo utaelekezwa
katika matumizi ya maarifa katika sekta ya mifugo. Jukumu kuu la msingi katika
ufugaji litakuwa ni kuleta mabadiliko yatakayoiondoa sekta hii kutoa uduni wa
ufugaji na kuwabadili wafugaji wetu kutoka wafugaji
wahamaji. Mkazo
utaelekezwa katika kutatua matatizo ya malisho na maji na kuwafikisha wafugaji
katika ukulima mchanganyiko na ufugaji wa mabandani wenye tija kubwa,
utakaotoa nyama na maziwa bora.
26. Uvuvi ni moja ya sekta za uchumi ambazo hazijapatiwa msukumo wa kutosha.
Modenaizesheni katika uvuvi italenga katika kuwapatia maarifa wavuvi
yatakayobadili na kuongeza uzalishaji wa samaki. Kuongeza ufanisi na tija na
kubadili maisha ya wavuvi ni moja ya mapinduzi yanayolengwa katika Ilani ya
2010-2015. Katika kutekeleza hili Serikali itatilia mkazo uwezeshaji wa wavuvi,
kuendeleza viwanda vya samaki, kusimamia uvunaji endelevu wa samaki katika
bahari kuu.
27. Modenaizesheni ya uchumi itazingatia umuhimu wa viwanda kuwa ni kiongozi wa
uchumi wa kisasa. Katika kuzingatia ukweli huu Ilani hii ya 2010-2015 itatekeleza
dhana hiyo kutoa msukumo katika mapinduzi ya viwanda, kuhamasisha maendeleo
ya sayansi, teknolojia na uhandisi, viwanda vya msingi, viwanda vya kati na
viwanda vidogo.
28. Ufikiaji wa lengo letu kla ujenzi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea
utategemea sana ushiriki wa wananchi wetu kupitia Sera ya Chama ya Uwezeshaji
Wananchi. Sera hii itatekelezwa na kuimarishwa katika kipindi cha Ilani hii kwa
Serikali kuendeleza yafuatayo:
(a)
Mkakati wa MKURABITA
15
(b) Ushirika
(c) Mifuko ya Uwezeshaji:-
(i) Mfuko wa Wajasiriamali Wadogo
(ii) Mfuko wa Mikopo Makampuni ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati
    (SMEs)
(iii) Mfuko wa Pembejeo za Kilimo
(iv) Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(v) Benki ya Wanawake
29. Aidha Sera ya Uwezeshaji itapewa msukumo mkubwa ili Watanzania waweze
kuwezeshwa kushindana katika uchumi wa dunia na ule wa kanda.
30. Nchi yetu inahitaji uchumi imara na unaokua kwa kasi kubwa na endelevu ili
kutatua tatizo letu la umaskini na utegemezi. Ni mapinduzi ya kilimo na viwanda
ndiyo yatakayotuhakikishia kufika katika lengo hilo na nchi yetu kuwa na uchumi
wa kati.
16
SURA YA TATU
SEKTA ZA UZALISHAJI MALI
Mapinduzi ya Kilimo
Kilimo ndio msingi wa uchumi wa kisasa na njia sahihi ya kuutokomeza
umasikini.
31.
Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwa dhati kwamba kilimo cha kisasa
kinachotumia Kanuni na zana bora za kilimo ndio ufunguo wa maendeleo ya
uchumi wa nchi yetu. Kilimo cha kisasa kina uwezo wa kutoa mazao mengi zaidi
kutoka kila ekari iliyolimwa. Kwa nchi yetu, ziada hiyo ya mazao ina faida kubwa
zifuatazo:-
(a) (b) Kulipatia Taifa mavuno mengi ya kuuza ili kupata fedha za kigeni kwa ajili
       ya maendeleo ya nchi.
(c) Ziada ya mazao huunda mazingira muafaka ya kuanzishwa viwanda vya
   usindikaji na utengenezaji wa bidhaa za viwandani.
(d)
32.
Kuipatia kila familia, kijiji na Taifa chakula cha kutosha ili kukomesha njaa.
Familia yenye ziada ya mazao huutokomeza umaskini kwa kuuza ziada
hiyo kwenye soko na kupata fedha za kujiletea maendeleo.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ya utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2005-
2010, Serikali zetu zilichukua hatua kubwa katika kukipatia kilimo mwelekeo wa
17
kisasa ili kiondokane na zana duni, mashamba madogo, kutozingatia kanuni bora
za kilimo na kuridhika na mavuno ya kujikimu.
33.
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo ya utekelezaji wa Ilani ya 2010-2015,
Chama kitazielekeza Serikali kutekeleza kwa ukamilifu malengo ya Mpango wa
Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP) pamoja na kaulimbiu ya Kilimo
Kwanza inayotoa msukumo katika kutekeleza mambo yafuatayo:-
(a) Kuanzisha Benki ya Kilimo yenye uwezo mkubwa ili ianze kuwakopesha
   wakulima wakubwa na wadogo kwa masharti nafuu.
(b) Kutumia uongozi shirikishi katika kusimamia kilimo na kuwafikishia
   wakulima vijijini maarifa yanayohusu kanuni za kilimo bora cha mazao
  wanayolima.
(c) Kuziweka tayari Benki Kuu na Hazina kukipatia kilimo chetu fedha za
   kutosha kwa kuhakikisha kwamba Bajeti ya Serikali haiwi kizuizi cha
  maendeleo ya kilimo nchini.
(d) Kuongeza upatikanaji na utumiaji wa pembejeo za kilimo, hususan
   mbolea, mbegu na miche bora na kuweka mfumo utakaohakikisha
  upatikanaji wa pembejeo hizo kwa wakulima.
(e) Kuongeza upatikanaji na matumizi ya zana za kilimo kwa kuishirikisha
   sekta binafsi, kuhamasisha na kuwezesha vikundi vya wakulima, hususan
  vijana kupata mikopo ya pembejeo na zana za kilimo kutoka kwenye
 Mfuko wa Pembejeo.
(f) Kuimarisha mashamba ya mbegu ya serikali ili kuongeza uzalishaji wa
   mbegu bora za mazao ya nafaka, mikunde na mbegu za mafuta na
  kuzisambaza kwa walengwa ili wazitumie.
(g) Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya kilimo ya aina zote, hususan mazao
   makuu ya biashara, mazao ya chakula, mboga na matunda, mbegu za
  mafuta na muhogo ili mavuno makubwa ya kila zao yapatikane ifikapo
 mwaka 2015 kwa viwango vinavyopimika.
(h) Kuweka msukumo mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji maji katika maeneo
   stahiki ili kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2015 karibu asilimia 25 ya
  mahitaji yetu ya chakula inapatikana kwa njia ya kilimo hicho.
(i) Kuimarisha huduma za ugani kwa kuongeza kasi ya kufundisha na kuajiri
   wataalam wa fani mbalimbali hasa wenye vyeti vya kilimo na kuwaeneza
  wanakohitajika hasa vijijini na kuwajengea mazingira mazuri ya kazi.
18
(j) Kuimarisha huduma za udhibiti wa visumbufu na magonjwa ya mimea
   kwa kujenga uwezo wa kudhibiti visumbufu vya mazao mara
  vinapojitokeza ili kumwezesha mkulima kupunguza upotevu wa mazao
 kabla na baada ya mavuno.
(k) Kuhamasisha ujenzi na matumizi ya maghala bora ya kuhifadhia mazao na
   kutoa mafunzo juu ya teknolojia sahihi za hifadhi bora kwa lengo la
  kupunguza upotevu wa chakula. Mpango mkakati uandaliwe wa kupanua
 hifadhi ya mazao ya chakula katika maeneo ya nchi ambako mazao ya
chakula yanalimwa kwa wingi.
(l) Kuimarisha usindikaji wa mazao mbalimbali katika ngazi ya kaya ili
   kuongeza thamani na muda wa matumizi na upatikanaji wa chakula kwa
  ujumla.
(m) Kupima maeneo ya kilimo na mashamba ya wakulima wapate hati miliki
   na kuhimiza matumizi bora ya ardhi ili kupunguza migogoro ya kijamii
  kama vile kati ya wazalishaji wa mazao na wafugaji.
(n) Kusimamia utaratibu wa mashindano ya kilimo kinachozingatia kanuni
   bora za kilimo kati ya vijiji, kata, tarafa, wilaya na mikoa.
(o) Kuimarisha uongozi wa Vyama vya Ushirika na kuvijengea uwezo
   kujiendesha kwa ufanisi.
(p) Kuimarisha shughuli za ukaguzi na usimamizi wa Vyama vya Ushirika
   nchini.
(q) Kuweka kanda zinazoeleweka za mazao ya chakula na ya biashara kwa
   kuzingita hali ya hewa na uzoefu uliopo. Mazao yanayohusika yalimwe
  kwa wingi katika kanda hizo.
(r) Kuwezesha Halmashauri 133 kununua vitendea kazi kwa wataalamu
   ifikapo mwaka 2015.
(s) Kuzalisha mbolea kwa wingi kwa ajili ya mapinduzi ya kilimo
   tunayoyafanya na kuhamasisha makampuni ya mbolea ili yaingize mbolea
  kwa wingi kukidhi mahitaji ya tani 385,000 ifikapo mwaka 2015.
Sekta ya Umwagiliaji
19
34.
Kutokana na umuhimu wa Sekta ya Umwagiliaji katika kukuza uchumi wa taifa
na wa wananchi katika kipindi hiki kwa kuongeza uhakika wa upatikanaji wa
chakula nchini, Chama kitaitaka Serikali kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendelea kutekeleza umwagiliaji kupitia Programu ya Maendeleo ya
   Sekta ya Kilimo kwa kuongeza eneo lenye miundombinu ya umwagiliaji
  kutoka hekta 326,492 za Juni 2010 hadi hekta 1,000,000 ifikapo mwaka
 2015 na hivyo kujitosheleza kwa zao la mpunga. Sekta binafsi
itashirikishwa katika uendelezaji na uwekezaji kwenye kilimo cha
umwagiliaji.
(b) Kukamilisha Mkakati na Sheria ya Umwagiliaji.
(c) Kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji kwa wakulima
   wadogo na wa kati ili kuongeza uzalishaji na ufanisi wa matumizi ya maji;
(d) Kujenga na kukarabati mabwawa ya kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua na
   mito kwa ajili ya umwagiliaji;
(e) Kujenga uwezo wa Taasisi zinazohusika na umwagiliaji katika ngazi ya
   taifa, Halmashauri na wakulima katika usimamizi na uendeshaji endelevu
  wa miradi ya umwagiliaji.
(f) Kutoa msukumo mpya katika uanzishwaji wa kituo cha mafunzo na
   shughuli za utafiti wa umwagiliaji na matumizi bora ya maji.
Mapinduzi ya Ufugaji
35. Tanzania hivi sasa inakadiriwa kuwa na ng’ombe milioni 19.1, mbuzi milioni 13.6,
     kondoo milioni 3.6, nguruwe milioni 1.6 na kuku milioni 56. Kati ya ng’ombe
      hao, 605,000 ni wa maziwa. Aidha, kati ya kuku hao, 22 milioni ni wa kisasa
     wakiwemo milioni 8 wa mayai na milioni 14 wakiwa ni wa nyama.
36. Hivyo, bado nchi yetu inafuga ng’ombe 18,496,000 na kuku milioni 34 kwa
     utaratibu wa jadi likiwemo tatizo sugu la wafugaji kuhamahama wakitafuta
    malisho na maji.
37. Kutokana na ufugaji huo kuwa wa jadi kwa sehemu kubwa, mchango wa mifugo
   kwenye uchumi wa Taifa na katika kuutokomeza umasikini bado ni mdogo sana.
  Kwa mfano, mwaka 2007 sekta ya mifugo ilichangia kwenye pato la Taifa asilimia
 4.7 ambapo mwaka 2008 mchango wake ulishuka hadi asilimia 4.6 tu.
38. Katika kipindi cha Ilani hii ya miaka 2010-2015, Chama Cha Mapinduzi
   kitazielekeza Serikali kuiendeleza sekta ya mifugo kwa ari zaidi, nguvu zaidi na
20
kasi zaidi ili kuiwezesha kutoa mchango mkubwa kwenye pato la Taifa kwa
kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Serikali iandae programu kabambe ya kuendeleza sekta ya mifugo na
   ufugaji. Programu hiyo ijumuishe pamoja na mambo mengine masuala ya
  uendelezaji wa maeneo ya malisho, kuchimba na kujenga malambo,
 mabwawa, majosho na huduma za ugani ili hatimaye wafugaji
waondokane na ufugaji wa kuhamahama.
(b) Benki ya Kilimo itakayoanzishwa iwe pia Benki ya Mifugo ili iweze pia
   kutoa mikopo kwa wasomi wenye nia ya kufuga na kuwawezesha kuingia
  kwa wingi katika ufugaji wa kisasa.
(c) Kuelimisha wafugaji uwiano kati ya idadi ya mifugo na eneo.
(d) Serikali isimamie kwa ufanisi mkubwa mradi wa kopa ng’ombe, lipa
     ng’ombe kama hatua ya kueneza ufugaji wa kisasa wenye tija kubwa.
(e) Kuendeleza elimu kwa Wafugaji ili wajue kuwa mifugo waliyonayo ni mali
   inayoweza kuvunwa katika umri na uzito muafaka unaokidhi mahitaji ya
  soko, ili kuwaondolea umaskini wao badala ya kuridhika na wingi wa
 mifugo iliyo duni na maisha ya kuhamahama.
(f) Uzalishaji wa mitamba upanuliwe kwa kiwango kikubwa kwa Serikali
   kuivutia na kuiwezesha sekta binafsi katika uzalishaji na ufugaji wa kisasa.
(g) Kufufua na kujenga majosho na malambo mapya kwa ajili ya mifugo na
   kuhimiza uogeshaji endelevu.
(h) Kuimarisha utafiti wa mifugo kwa kuboresha na kuhifadhi kosaafu za
   mifugo ya asili ili kuongeza uzalishaji na tija.
(i) Kuimarisha huduma za ugani na mafunzo ya wataalamu na wafugaji.
(j) Kuongeza na kuimarisha vituo vya uzalishaji mbegu bora za mifugo na
   kuhimiza matumizi ya mbegu hizo.
(k) Kuimarisha huduma za afya ya mifugo kwa kudhibiti magonjwa ya mifugo
   hasa ya milipuko na uanzishwaji wa Maeneo Huru kwa Magonjwa ya
  Mifugo.
21
(l) Kuhimiza wafugaji watekeleze kanuni za ufugaji bora na kuingia katika
   ufugaji endelevu wa kisasa na kibiashara unaozingatia hifadhi ya
  mazingira.
(m) Kuhamasisha uanzishaji na uimarishaji wa vikundi vya ushirika wa
   wafugaji.
(n) Kuhamasisha ushirikishwaji wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma
   mbalimbali za mifugo.
Mapinduzi ya Uvuvi
39. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi yenye maeneo mengi na makubwa ya
   maji baridi na maji ya bahari yaliyosheheni rasilimali nyingi za uvuvi ambamo
  shughuli za uvuvi hufanyika. Nchi yetu ina ukanda wa pwani wenye urefu wa
 kilometa 1,424 na upana wa maili za majini zipatazo 200.
Eneo hilo
limegawanyika katika maji ya Kitaifa yenye upana wa maili za majini 12 sawa na
kilometa za mraba 64,000 kwa upande mmoja na upande wa pili ni wa Bahari
Kuu yenye upana wa maili za majini 188 sawa na kilometa za mraba 223,000.
40. Eneo letu la maji baridi lenye maziwa makubwa 3 na madogo 29 lina jumla ya
   kilometa za mraba 54,277 ambazo zinaweza kutumika kwa uvuvi. Katika
  maeneo hayo ya maji baridi na maji ya bahari, mwaka 2008 jumla ya tani
 335,024 za samaki zilivuliwa nchini. Kati ya hizo, tani 324,960 sawa na asilimia
97 zilivuliwa na wavuvi wadogo wapato 170,038 sawa na wastani wa tani 1.9
kwa kila mvuvi kwa mwaka. Aidha, tani 10,114 zilizobaki zilivuliwa na meli
kubwa katika Bahari Kuu. Sekta ya uvuvi mwaka 2007 ilichangia asilimia 1.6 tu
kwa pato la Taifa na asilimia ndogo zaidi ya 1.3 mwaka 2008.
41. Kwa kuzingatia ukubwa wa maeneo yetu ya uvuvi na uwingi wa rasilimali za
   uvuvi tulizonazo, Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha Ilani hii ya 2010-2015
  kitazielekeza Serikali kuiendeleza sekta ya uvuvi ili iwe ya kisasa zaidi na iweze
 kuchangia kwa kiwango kikubwa kwenye pato la Taifa kwa kuchukua hatua
zifuatazo:-
(a) Wizara ianzishe na kuendesha vyuo vyake vya uvuvi ili iweze kuandaa
   wataalam wengi wa sekta ya uvuvi kukidhi mahitaji yote yanayotakiwa
  kwa ajili ya kuboresha uvuvi nchini.
(b) Kuweka ulinzi madhubuti wa bahari zetu dhidi ya wavuvi haramu ikiwa ni
   pamoja na kukamata vyombo vyao vya uvuvi na kuwatoza fidia kwa
  mujibu wa sheria.
22
(c) Kuweka na kutekeleza programu yenye malengo yanayopimika mwaka
   hadi mwaka kuhusu haja ya kuleta mapinduzi ya uvuvi yanayotumia zana
  na maarifa ya kisasa.
(d) Kuimarisha ushirikishwaji wa jamii na wadau katika ulinzi, usimamizi na
   matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi.
(e) Kuimarisha miundombinu ya uvuvi kwa kujenga mialo, masoko ya kisasa,
   vituo vya kutotolea vifaranga vya samaki na maabara.
(f) Kuboresha mazao ya uvuvi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya soko la ndani
   na nje ya nchi.
(g) Kujenga mazingira ya kuvutia uwekezaji katika sekta ya uvuvi hususan
   ujenzi wa viwanda vya kusindika samaki.
(h) Kuhamasisha wawekezaji wa ndani na wa nje kuwekeza katika uvuvi
   kwenye Bahari Kuu.
(i) Kuimarisha na kuendeleza uanzishwaji wa maeneo tengefu kwenye
   maziwa makuu hususani Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.
(j) Kuhamasisha uimarishaji na uanzishaji wa vikundi vya ushirika wa wavuvi
   na wafugaji wa samaki.
(k) Kuimarisha usimamizi wa mazingira katika maeneo ya uvuvi, ukuzaji wa
   viumbe kwenye maji na maeneo tengefu.
(l) Kuhimiza shughuli mbadala za kiuchumi kwa jamii za wavuvi ili kupunguza
   shinikizo la uvuvi kwenye maji ya asili na maeneo tengefu.
Wanyamapori na Misitu
42. Wakati tunapata uhuru mwaka 1961, nchi yetu ilikuwa na misitu mingi ambayo
   hivi sasa imepungua kutokana na ongezeko kubwa la makazi ya watu na
  kupanuka kwa kilimo. Aidha, kutokana na ukataji ovyo wa misitu na uwindaji
 haramu wa wanyamapori, rasilimali hizo zinaweza kutoweka kwenye uso wa nchi
yetu na kuleta jangwa kama Taifa halitakuwa makini kiasi cha kutosha katika
hifadhi ya misitu na wanyamapori.
43. Umuhimu wa wanyamapori na misitu ambao Taifa limeutambua tangu mwanzo
   wa uhuru wetu, sasa unazidi kuongezeka siyo tu katika kuvutia watalii nchini
  lakini pia katika kutunza mazingira yanayotuzunguka ya hewa, udongo na maji ili
23
nchi yetu iweze kutoa mchango wake stahiki katika kupunguza kasi ya
mabadiliko ya tabianchi ambayo yameikumba sayari dunia tunamoishi.
44.
Katika kipindi cha Ilani hii, Chama Cha Mapinduzi kitaitaka Serikali ielekeze nguvu
zake katika kuhifadhi, kulinda, kuendeleza, kudumisha, kuboresha na kuvuna
maliasili ya wanyamapori, misitu na nyuki kwa manufaa ya Taifa kwa kuchukua
hatua zifuatazo:-
(a) Kuongeza msukumo katika kuendeleza ufugaji wa nyuki kwa ajili ya
   kuzalisha asali na nta kibiashara.
(b) Kuweka utaratibu shirikishi wa upandaji miti, uvunaji na udhibiti wa moto.
   Ushirikishaji huo utakuwa wa sekta binafsi, NGOs na vijiji.
(c) Kuwezesha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi kunufaika na rasilimali
   za wanyamapori na misitu.
(d) Kuboresha miundombinu
   wanyamapori na misitu.
(e) Kuendelea kuboresha mazingira ya makazi ya watumishi wanaoishi katika
   mazingira magumu.
ndani
ya
mapori
ya
akiba,
hifadhi
za
Utalii
45. Katika kipindi cha miaka 2005-2010, Serikali chini ya uongozi wa CCM imeitumia
   Bodi ya Utalii kutangaza kwa bidii vivutio vya utalii tulivyonavyo ndani na nje ya
  nchi kwa kuandaa, kuchapisha na kusambaza vipeperushi ambapo jumla ya
 vipeperushi 30,000, nakala 30,000 za filamu, majarida 30,000, DVD 30,000 na
taarifa 5,000 zilichapishwa na kusambazwa ikiwa ni pamoja na kushiriki katika
maonyesho 21 nje ya nchi. Aidha, vituo vya CNN vilitumika kurusha matangazo
ya utalii wetu kwa miezi sita mfululizo tangu Septemba 2007 hadi Februari 2008.
46. Kutokana na juhudi hizo idadi ya watalii wa ndani iliongezeka kutoka wastani wa
   436,000 mwaka 2005/2006 hadi 639,000 mwaka 2008/2009. Wakati huo huo
  idadi ya watalii waliotembeleaTanzania kutoka nchi za Asia iliongezeka kutoka
 23,542 mwaka 2006 hadi watalii 26,070 mwaka 2009. Katika masoko ya zamani,
idadi ya watalii iliongezeka kutoka 612,754 mwaka 2005 hadi watalii 770,376
mwaka 2008. Sekta ya utalii katika kipindi hicho iliingizia Taifa jumla ya dola za
Marekani bilioni 2.8.
24
47.
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii, Chama kitaielekeza Serikali iendelee
kuitangaza hazina ya utalii tuliyonayo kwa mbinu za kisasa ili kukuza zaidi
mchango wa utalii kwa pato la Taifa kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kujenga Chuo Cha Utalii ili kuimarisha mafunzo ya hoteli na utalii kwa
   lengo la kuongeza wingi na ubora wa watumishi wa huduma hizo.
(b) Kukuza mwamko na kuendesha kampeni za kuwashawishi Watanzania
   kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii.
(c) Kupanua wigo wa aina za utalii kwa kuendeleza utalii wenye kuhusisha
   utamaduni, mazingira, makumbusho (historia) na michezo kama vile
  golfu.
(d) Kujihusisha kwa ukamilifu katika kutangaza fursa za kitalii zilizomo nchini
   na kuongeza bajeti ya kutangaza utalii ifanane na zile za nchi jirani.
(e) Kufanya juhudi maalumu za kutafuta masoko mapya ya utalii katika nchi
   zinazoinukia kiuchumi kama vile China na nchi nyingine za Asia.
(f) Kuandaa mikakati ya kuziba mianya ya uvujaji wa mapato ya utalii.
(g) Kuhimiza wawekezaji wa ndani na nje kujenga hoteli za kitalii za hadhi ya
   nyota 3 hadi 5.
(h) Kuzitathmini hoteli zilizopo na kuzipanga katika madaraja ya nyota
   zinayostahili. Wakati huo huo kuhakikisha kuwa hoteli zinakuwa katika
  hali ya unadhifu.
(i) Kuendeleza jitihada za kuhifadhi mazingira katika mbuga za wanyama,
   misitu fukwe, za bahari na maziwa.
(j) Kuwavutia watalii wa nje kwa kuboresha huduma na uzalishaji wa bidhaa
   zenye ubora kwa kutumia teknolojia rahisi na za kisasa ili ziwavutie
  watalii.
(k)
Kuhakikisha kuwa kuna usafiri wa uhakika wa ndege ili kuimarisha utalii.
Mapinduzi ya Viwanda
48.
Katika kipindi cha miaka 2005-2010, Sekta ya viwanda ilitarajiwa kukua kufikia
asilimia 15. Ukuaji halisi uliongezeka kutoka asilimia 8.5 mwaka 2005/2006 hadi
asilimia 9.9 mwaka 2008/2009. Matatizo ya msingi yaliyosababisha ukuaji wa
sekta ya viwanda kuwa na sura hiyo ni pamoja na haya yafuatayo:-
25
(a) (b) Uwekezaji mdogo kwenye maendeleo ya viwanda, hasa viwanda mama na
       viwanda vya usindikaji wa mazao ya kilimo.
(c) Uduni wa teknolojia zinazotumiwa na wazalishaji.
(d)
49.
Kukatikakatika mara kwa mara kwa maji na umeme viwandani.
Udhaifu wa menejimenti na stadi za biashara na masoko.
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010 – 2015, Chama Cha Mapinduzi
kitaitaka Serikali iikuze sekta ya viwanda kutoka asilimia 9.9 ya sasa hadi asilimia
15 mwaka 2015 kwa kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo endelevu
ya sekta za viwanda, biashara na masoko kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
(a) Kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji na biashara katika
   soko la ushindani.
(b) Kujenga na kuimarisha ujuzi katika biashara na kuweka msukumo zaidi
   katika kutumia fursa za masoko.
(c) Kujenga mifumo imara ya viwanda, biashara na masoko yenye kuendeleza
   na kukuza mauzo nje.
(d) Kuimarisha kifedha Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) ili kiwe chombo
   madhubuti cha kuchochea mapinduzi ya viwanda nchini kwa kutoa mikopo
  ya muda mrefu na riba nafuu kwa wawekezaji wakubwa, wa kati na
 wadogo nchini kote.
(e) Kuwekeza katika mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma, Chuma cha
   Liganga na viwanda vya kemikali na mbolea katika Kanda za Maendeleo
  kikiwemo kiwanda cha mbolea aina ya UREA mkoani Mtwara na
 kuwezesha kiwanda cha Minjingu kuzalisha mbolea bora ya NPK na MPR ili
kufikia lengo lililowekwa.
(f) Kuimarisha uzalishaji mali viwandani kwa kuvifufua na kuviendeleza kwa
   teknolojia ya kisasa viwanda vyote ambavyo viliuzwa huko nyuma na
  kisha kutelekezwa.
(g) Kuboresha vivutio kwa ajili ya uwekezaji kwenye viwanda vitakavyotumia
   malighafi mbalimbali ziliopo nchini vikiwemo viwanda vya nguo, ngozi,
  usindikaji wa matunda, mbogamboga na usanifu wa madini ya vito.
26
(h) (i) Kuendelea kutekeleza mkakati unganishi wa kufufua na kuendeleza
       viwanda vya ngozi.
(j)
50.
Kuendelea kuhamasisha uanzishaji na uimarishaji wa Maeneo Maalumu ya
Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZ) na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi
(SEZ).
Kuandaa taarifa kuhusu fursa za uwekezaji katika miradi ya maendeleo ya
viwanda nchini.
Kuhusu viwanda vidogo, Serikali itatekeleza yafuatayo:-
(a) (b) Kuongeza mchango wa viwanda vidogo na biashara ndogo (SMEs) katika
       pato la Taifa kutoka asilimia 33 ya GDP hivi sasa kufikia asilimia 40 mwaka
      2015.
(c) Kuendeleza, kuzalisha na kusambaza teknolojia za kuongeza thamani ya
   mazao kupitia vituo vya SIDO vilivyopo Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Lindi,
  Iringa na Kigoma.
(d) Kutoa elimu na kuwajengea uwezo wakulima wa kusindika mazao kabla ya
   kuyauza kama vile usindikaji wa asali, utengenezaji wa mvinyo,
  utengenezaji wa juisi pamoja na ufungashaji wa bidhaa kwa kutumia
 teknolojia ya TBS.
(e) Kuwaunganisha wajasiriamali wadogo
   yaliyotayari kununua bidhaa zao.
(f) Kujenga uwezo wa SIDO na kuwatafutia vyanzo vya fedha ili
   kuwawezesha kutoa mafunzo ya usindikaji kwa wajasiriamali wadogo.
  Aidha, Sheria iliyoanzisha SIDO itafanyiwa mapitio ili iendane na mahitaji
 ya uchumi wa sasa.
(g)
51.
Kuendeleza programu ya Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini kwa kutoa
ushauri, mafunzo, mitaji na huduma za kiufundi kwa wajasiriamali.
Kuendeleza miundombinu ya viwanda vidogo na biashara ndogo.
na
makampuni
makubwa
Kuhusu biashara, Serikali itatekeleza yafuatayo:-
27
(a) (b) Kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali kuhusu mbinu za
       kuyafikia masoko ya nje.
(c) Kuendelea na majadiliano ya ubia wa kiuchumi kati ya Jumuiya ya Afrika
   Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Ulaya (EU).
(d) Kuendelea na utekelezaji wa uanzishwaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la
   Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuendelea kutekeleza Itifaki ya Biashara ya
  Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
(e)
52.
Kuhamasisha matumizi ya fursa za masoko ya ndani, kikanda na
kimataifa, zikiwemo fursa za masoko ya AGOA, EBA, China, Japan, Canada
na India ili kukuza biashara ya nje kwa kiwango kikubwa.
Kufanya utafiti wa kina juu ya gharama za kufanya biashara nchini kwa
lengo la kupunguza gharama hizo na kuchochea ukuaji wa biashara.
Kuhusu Mapinduzi ya kilimo, Serikali itatekeleza yafuatayo:-
(a) (b) Kuratibu na kuhamasisha ushiriki wa wajasiriamali wa Tanzania katika
       maonesho ya biashara ya kimataifa ndani na nje ya nchi.
(c) Kufanya utafiti wa masoko na bei ili kupanua wigo wa mahitaji ya masoko
   ya bidhaa zetu.
(d)
53.
Kuanzisha vituo vitatu vya biashara vya kanda katika mikoa ya Mwanza,
Mbeya na Arusha.
Kuanzisha programu ya kuwa na utambulisho wa kitaifa kwa bidhaa.
Kuhusu masoko, Serikali itatekeleza yafuatayo:-
(a) Kukamilisha mkakati wa Sera ya Masoko na Bidhaa za Kilimo.
(b) Kuendeleza miundombinu ya masoko ya mikoa na kuanzisha masoko
   katika vituo vya mipakani ili kukuza biashara ya ndani na kikanda.
(c) Kutekeleza mkakati wa kukuza mauzo nje na mpango unganishi wa
   biashara.
(d) Kuendeleza biashara ya ndani ikiwa ni pamoja na kujenga dhana ya
   kutumia bidhaa zilizozalishwa Tanzania (NUNUA BIDHAA ZA TANZANIA).
28
(e) (f) Kuwalinda wajasiriamali wa ndani kwa kutoingiza bidhaa mbalimbali
       kutoka nje ambazo zinaua soko la ndani la bidhaa zao, kwa mfano
      samani.
(g) Kupanua matumizi ya simu za viganjani katika kutoa taarifa za bei ya
   mazao na masoko kwa wakati. Aidha, kuangalia uwezekano wa kuanzisha
  mbao za matangazo katika ngazi ya Wilaya na Mkoa ili kutoa taarifa
 mbalimbali ikiwemo bei na masoko kwa wakati muafaka.
(h) Kuendeleza mchakato wa kuanzisha Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara.
(i) Kuendeleza miundombinu ya masoko na kuanzisha masoko mipakani
   kama vile Karagwe, Kigoma, Holili, Horohoro, Namanga, Sumbawanga,
  Taveta na Tarakea.
(j) Kuendeleza utekelezaji wa Mfuko wa Stakabadhi za Mazao Ghalani.
(k) Kushirikiana na Sekta Binafsi katika kubuni na kutekeleza mikakati ya
   masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.
(l) Kuendeleza na kuboresha mfumo wa ukusanyaji, uhifadhi, uchambuzi na
   usambazaji wa taarifa za masoko.
(m)
54.
Kuboresha na kupanua wigo wa biashara mtandao katika ngazi ya Wilaya,
Mkoa hadi Taifa.
Kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa kutekeleza Sheria ya Usajili
wa Shughuli za Biashara (BRELA).
Utekelezaji kamili wa malengo ya sehemu hizi nne za viwanda, biashara, Kilimo
Kwanza na masoko unahitaji upatikanaji wa mitaji kwa wawekezaji na huduma
za maji na umeme zisizo katikakatika mara kwa mara. Serikali itatakiwa
kukabiliana na changamoto hizo kwa kasi na viwango stahiki.
MADINI
55.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ya 2005-2010, Chama Cha Mapinduzi
kiliielekeza Serikali kuchukua hatua zenye lengo la kuharakisha ukuaji wa
mchango wa Sekta ya Madini kwenye uchumi wa Taifa.
Baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana kutokana na hatua hizo ni haya
yafuatayo:-
29
(a) (b) Kuanzishwa kwa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania.
(c) Kukamilisha ramani mpya za kisasa za Kijiolojia zinazoonyesha uwepo wa
   madini Tanga, Nachingwea na Liganga.
(d) Kutengwa kwa maeneo ya wachimbaji wadogo katika maeneo ya Kilindi,
   Winzo, Mvomero, Melela, Rwamgaza, Nyarugusu, Maganzo na Merelani.
(e) Mapato ya Serikali kutokana na uchimbaji mkubwa yameongezeka kutoka
   Sh. 457.4 bilioni mwaka 2005 hadi Shilingi 840.0 bilioni mwaka 2008.
(f) Thamani ya madini yanayouzwa nje imeongezeka kutoka dola za Marekani
   727.45 milioni mwaka 2005 hadi dola 1,075.9 milioni mwaka 2008.
(g)
56.
Kukamilika kwa Sera ya Madini ya Mwaka 2009 na kupitishwa kwa Sheria
ya Madini ya Mwaka 2010.
Ajira katika uchimbaji mkubwa imeongezeka kutoka wafanyakazi 7,000
mpaka 13,000.
Katika kipindi cha Ilani hii ya 2010 – 2015, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza
Serikali iendelee kukuza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa kwa
kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuendelea kuliimarisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili liweze
   kushiriki katika umiliki wa migodi mikubwa na ya kati na katika utoaji
  huduma katika sekta ya madini na litumike kuwaendeleza wachimbaji
 wadogo.
(b) Kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya madini kwa kujenga uwezo wa
   Serikali katika usimamizi, uimarishaji wa miundombinu zikiwemo ofisi,
  vitendea kazi, kuongeza na kuwaendeleza wataalamu kwenye sekta ikiwa
 ni pamoja na kuimarisha wakala za Geological Survey of Tanzania (GST)
na Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA).
(c) Kusimamia na kuhamasisha uwekezaji, utafutaji, uchimbaji na uongezaji
   thamani katika madini ili kukuza mchango wa sekta hiyo katika pato la
  Taifa.
(d) Kuwaendeleza wachimbaji wadogo katika utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji
   na biashara ya madini, kuwarasimisha, kuwatafutia maeneo,
  kuwawezesha kupata mikopo na mitaji kwa kuanzisha mifuko maalumu,
 kuwapa mafunzo, teknolojia bora na maarifa. Aidha, katika kuhakikisha
30
wachimbaji wadogo wanachangia katika uchumi wa nchi yatawekwa
mazingira mazuri ya kuwawezesha kuendesha shughuli za madini kwa
usalama na kutunza mazingira.
(e) Kuendelea kuimarisha ukaguzi wa migodi katika masuala ya usalama,
   utunzaji wa mazingira na afya migodini.
(f) Kujenga uwezo wa utaalamu wa kushiriki kwa ukamilifu katika mikataba
   yote ya madini kwa lengo la kulinda maslahi ya nchi.
(g) Kuandaa soko bora la ndani la kuuzia madini lililowazi ili madini yetu
   yasiuzwe kilanguzi nje ya nchi.
(h) Serikali kuwa na hisa katika uchimbaji mkubwa wa madini.
(i) Kuandaa mkakati wa uchimbaji wa madini ya “uranium” tuliyonayo ili
       yachangie katika modenaizesheni ya uchumi.
(j) Serikali ihakikishe kwamba migodi yote mikubwa inapata huduma zake
   kutoka hapa hapa nchini kama vile vyakula, ulinzi n.k.
(k) Kuongeza uwezo wa kitaalamu kwa Watanzania wanaojishughulisha katika
   Sekta ya Madini.
SURA YA NNE
SEKTA YA MIUNDOMBINU NA HUDUMA ZA KIUCHUMI
ARDHI
57. Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake kinatambua kwamba ardhi ndiyo rasilimali
   namba moja katika modenaizesheni ya uchumi wa nchi yetu. Aidha, ardhi
  wanayomiliki wananchi katika familia zao au mtu mmoja mmoja ni mtaji wao wa
 kutegemewa siyo tu kwa kuwapatia ajira ya kudumu kupitia kilimo bali pia
kupitia ardhi wanaweza kuitumia kama dhamana kupata mikopo katika vyombo
vya fedha. Kwa kuwa ardhi huwa haiongezeki lakini matumizi na watumiaji
wanaongezeka kila siku, ili kuondoa migogoro baina ya watumiaji wa ardhi, upo
umuhimu wa ardhi yetu yote ipimwe, ipangiwe mipango ya matumizi bora, na
imilikishwe kwa wananchi.
58. Katika kipindi cha miaka ya 2005-2010, Chama Cha Mapinduzi kiliielekeza Serikali
   kupitia Ilani yake kuanza utekelezaji wa Mkakati wa Kurasimisha Rasilimali na
  Biashara Tanzania (MKURABITA), kwa lengo la kutambua rasmi rasilimali za
31
wanyonge ambazo bado ziko kwenye sekta isiyo rasmi ili zitumike kuwawezesha
kuwa washiriki kwenye uchumi rasmi wa Taifa. Vile vile kutambua na kupima
mipaka ya vijiji na kuvipatia Hati za Vijiji (Village Land Certificates), kurahisisha
upatikanaji wa hatimiliki za ardhi kwa wananchi, kupima na kutayarisha ramani
za msingi za nchi yetu kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo.
59.
Katika kipindi cha Ilani hii ya miaka ya 2010-2015, Chama kinazitaka Serikali
kulinda na kuendeleza kwa ari na nguvu zaidi mafanikio ambayo yamepatikana
kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya na Miji, kukamilisha kazi ya
   upimaji wa mipaka ya vijiji vipya na kupanga mpango wa matumizi bora
  ya ardhi. Vile vile kuwahamasisha wananchi kuchangia upimaji wa
 mashamba yao na kuwapatia hatimiliki za kimila, pamoja na kujenga
masjala za ardhi katika ngazi za Wilaya na Vijiji.
(b) Kutekeleza Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi wenye program 12
   ambazo ni programu ya kuimarisha TUME, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Misitu,
  Wanyamapori, Madini, Nishati, Miundombinu, Rasilimali maji, Utalii na
 Uwanda/Uoto Asili kwa lengo la kukamilisha kazi ya upangaji wa matumizi
bora ya ardhi nchini.
(c) Kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi wasio na ardhi kupatiwa
   ardhi katika maeneo mengine ya nchi.
(d) Kusajili Hatimiliki na Nyaraka za Kisheria 300,000 na kuifanyia
   marekebisho Sheria ya Usajili wa Hati, Sura ya 334 ili kuboresha kazi ya
  usajili wa Hati na Nyaraka mbali mbali.
(e) Kuimarisha Ofisi ya Ardhi ya Kanda ya Kusini katika Mji wa Mtwara na
   kuanzisha Kanda mpya ya Magharibi itakayokuwa Mjini Tabora na Kanda
  ya Dar es Salaam.
(f) Kuziwezesha Halmashauri za Miji na Wilaya zote nchini kuweka na
   kuutumia mfumo wa kutumia teknolojia ya kompyuta katika kutoa
  huduma za ardhi kwa kuimarisha na kuboresha utunzaji wa kumbukumbu
 za upimaji ardhi, na kuzibadilisha kutoka mfumo uliopo sasa kuwa wa
kielektroniki.
(g) Kwa kushirikiana na Halmashauri za Miji na Wilaya kutambua ardhi kwa
   ajili ya kuanzisha Hazina ya Ardhi (Land Bank) kwa ajili ya wawekezaji wa
  ndani na nje ya nchi.
32
(h) (i) Kutoa elimu kwa umma juu ya Sheria za Ardhi, Sheria ya Mipangomiji,
       Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi na sheria zingine zinazohusiana
      na utawala wa ardhi.
(j) Kuzijengea uwezo Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji kuajiri wataalamu
   wa kutosha wa sekta ya ardhi na kununua zana za kisasa za kupima ardhi
  na usanifu wa ramani.
(k)
60.
Kuzijengea uwezo Halmashauri za Miji na Wilaya ziweze kupima viwanja
vingi na kuuza kwa wanaohitaji kwa kutumia mfuko wa mzunguko (Plot
Development Revolving Fund).
Kuboresha utendaji kazi wa Mabaraza ya Wilaya ya Ardhi na Nyumba 39
yaliyopo na kuanzisha Mabaraza mapya 50 (wastani wa mabaraza 10 kwa
kila mwaka) kwenye wilaya zenye migogoro mingi ya ardhi na nyumba.
Pamoja na Serikali kutekeleza majukumu ya jumla yaliyoelezwa hapo juu kuhusu
ardhi, Chama Cha Mapinduzi kitaitaka Serikali kutekeleza mambo yafuatayo
katika maeneo maalumu:-
(a)
Nyumba
(i) Kushirikisha Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa
   vya Ujenzi (NHBRA) katika kufanya tafiti mbali mbali za vifaa vya
  ujenzi wa nyumba bora kwa teknolojia rahisi na gharama nafuu na
 kufikisha matokeo ya utafiti huo kwa wananchi.
(ii) Kuzielekeza Serikali za Mitaa kuratibu na kusimamia upatikanaji wa
    ardhi na uendelezaji wa miundombinu ili kuwezesha makampuni ya
   uendelezaji milki na watu binafsi kujenga nyumba na uendelezaji
  wa miji kwa namna bora na endelevu.
(iii) Kuhakikisha kwamba ujenzi wa nyumba na majengo yanayotumiwa
     na umma unazingatia mahitaji maalumu hususan ya watu wenye
    ulemavu.
(iv) Kuhakikisha kuwa jumla ya nyumba 15,000 (kwa wastani nyumba
    3,000 kila mwaka) zinajengwa na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC)
   kwa kushirikiana na sekta binafsi.
(v) Kuhimiza uanzishwaji wa vyama vya ushirika wa nyumba, na pia
   vikosi vya ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu katika
33
ngazi za Wilaya na Kata; ili kuwezesha wananchi wa kipato cha
chini kufaidika na mikopo ya nyumba.
(vi) (vii) Kubadili Mfuko wa Mikopo ya Nyumba kwa watumishi wa Serikali
          kuwa Mfuko wa Dhamana ya Mikopo ya nyumba kwa madhumuni
         ya kuwafikia watumishi wote wa umma.
(viii) Kulielekeza Shirika la Nyumba la Taifa kuwa mwendelezaji ardhi
      mkubwa (Master Estate Developer) na kujenga nyumba nyingi kwa
     ajili ya kuuza au kupangisha kwa wananchi wote na hasa watu wa
    kipato cha kati na cha chini.
(ix) Kutunga sheria itakayowataka wote wanaojenga nyumba bora na
    majengo mbalimbali mijini na vijijini kujenga miundombinu ya
   kuvuna na kutumia maji ya mvua.
(x) Kukamilisha utungaji wa Sera ya Taifa ya Nyumba (Housing Policy).
(xi) Kuandaa mpango wa kampeni ya kitaifa katika kila wilaya
    kuhakikisha kuwa wananchi wanajijengea nyumba bora.
(xii)
(b)
Kuboresha mazingira ya upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya ujenzi
wa nyumba kwa masharti nafuu, kuwahamasisha wananchi
kuzielewa Sheria ili wazitumie kupata mikopo ya muda mrefu kwa
ajili ya kujenga au kununua nyumba na kuhamasisha mabenki na
vyombo vingine vya fedha kutoa mikopo ya ujenzi wa nyumba ya
muda mrefu na yenye riba nafuu.
Kuweka mazingira yatakayowezesha ujenzi wa nyumba wa
gharama nafuu.
Mipango Miji
(i) Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa programu ya Taifa ya
   Kurasimisha Makaazi nchini.
  Programu hii itakuwa dira ya
 kuboresha makaazi na kukabiliana na tatizo la ujenzi holela nchini.
Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itaendeleza kasi
ya Urasimishaji wa ardhi na nyumba katika Majiji na Hamashauri za
Miji na Wilaya na kutoa leseni za makazi.
(ii) Kukasimu kazi za uidhinishaji wa ramani za mipango miji, ramani za
    upimaji ardhi na taarifa za uthamini wa ardhi katika ngazi za
   Kanda, Mikoa na Wilaya ili kazi zote hizo zifanyike katika ngazi za
  chini bila urasimu wowote.
34
(iii) (iv) Kuanzisha mji wa kisasa wa Kigamboni (Kigamboni New City).
(v)
(c)
Kuanzisha miji midogo pembezoni mwa miji mikubwa ili kupunguza
msongamano katikati ya miji yote mikubwa tukianzia na Jiji la Dar
es Salaam (Satellite Towns).
Kushirikiana na Halmashauri za miji na majiji kutekeleza mpango
wa kuboresha makazi yaliyojengwa kiholela (Slum Improvement
Programmes).
Upimaji na Ramani
(i) Kutekeleza mradi kabambe wa kuweka kituo cha kupokea picha za
   Satellite (Satellite Imagery Receiving Station) kitakachorahisisha
  upimaji wa ardhi yote nchini na pia kitarahisisha utayarishaji wa
 ramani kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
(ii) Kukamilisha Sera ya Taifa ya Upimaji na Ramani, kutayarisha
    Sheria ya Upimaji na Ramani, na kuanzisha Mfuko wa kulipa Fidia
   ya Ardhi nchini.
(iii) Kukamilisha upimaji na uwekaji wa alama 600 za mtandao wa
     upimaji nchini, ambazo zitakuwa na wastani wa umbali wa kilomita
    30 kati ya alama moja na nyingine kwa maeneo ya vijijini na
   kilomita 10 kwa maeneo ya Mijini ili kupunguza gharama za
  upimaji ardhi nchini.
(iv) Kuanza kupima na kutayarisha ramani katika maeneo ya majini
    (baharini na katika maziwa) kwa kushirikiana na mashirika ya
   kimataifa ya Haidrografia.
(v) Kwa kushirikiana na nchi tunazopakana, kuimarisha alama za
   mipaka, na pia kulitafutia ufumbuzi tatizo la mpaka baina yetu na
  nchi ya Malawi katika Ziwa Nyasa.
NISHATI
61.
Ujenzi wa msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea unaotumia kwa
wingi sayansi na teknolojia katika shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma,
35
unahitaji huduma za umeme na maji zinazotolewa kwa uhakika. Hivi sasa
asilimia 90 ya nishati tunayotumia nchini inatokana na tungamotaka (biomass)
wakati mafuta ya petroli na umeme hutupatia asilimia 10 tu ya mahitaji yetu.
Upatikanaji huu wa nishati siyo muafaka kwa Mapinduzi ya viwanda
tunayoyahitaji.
62.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali chini ya uongozi wa Chama Cha
Mapinduzi imeshughulikia maendeleo ya sekta ya nishati na kupata mafanikio
makubwa yakiwemo yafuatayo:-
(a) (b) Mikoa ya Mtwara na Lindi kupata umeme wa uhakika unaozalishwa kwa
       gesi asilia ya Mnazi Bay.
(c) Kuongezeka kwa uzalishaji umeme nchini kutoka kwenye miradi ya Kihansi
   MW 180, Songas MW 180, Ubungo MW 100 na Tegeta MW 45.
(d) Kukamilika kwa miradi ya upelekaji umeme katika Makao Makuu ya Wilaya
   za Serengeti, Ludewa, Mbinga, Simanjiro, Kilolo, Bahi na Mkinga.
(e) Kukamilika kwa Sheria ya Nishati Vijijini na kuanzishwa kwa Wakala na
   Mfuko wa Nishati Vijijini.
(f)
63.
Kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Songo Songo na kuanza kutumia gesi
asilia katika kuzalisha umeme.
Kuweka mfumo wa mikopo ya muda mrefu kwa waendelezaji wadogo wa
nishati vijijini.
Katika miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya 2010 – 2015, Chama kitaitaka
Serikali kuongeza kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa nishati ya umeme kutoka
MW 1051 hadi MW 1722 (sawa na ongezeko la MW 671) na kupunguza ile ya
tungamotaka kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuboresha sera, sheria na kanuni zinazoongoza sekta ya nishati nchini.
(b) Kuunganisha gridi ya Tanzania na gridi za nchi jirani ili kuimarisha
   upatikaji wa umeme nchini.
(c) Kukamilisha upelekaji wa umeme kwenye Mikoa na Wilaya ambako gridi
   ya Taifa haijafika. Aidha, mkakati kabambe wa kupeleka umeme vijijini
  utaandaliwa na kutekelezwa kwa kumshirikisha Wakala wa Nishati Vijijini
 (REA).
36
(d) Kuimarisha mfuko wa nishati vijijini kwa kubuni vyanzo vya ziada vya
   kuchangia mfuko huu.
(e) Kuandaa na kutekeleza mpango utakaoipunguzia TANESCO baadhi ya
   majukumu na kuishirikisha sekta binafsi katika kuongeza na kuimarisha
  uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa nishati ya umeme nchini.
 Uzalishaji wa umeme kwa kutumia rasilimaji za maji zilizopo utaendelea
kuwa moja ya majukumu ya TANESCO.
(e) Kuendeleza na kupanua uzalishaji, usambazaji na matumizi ya gesi asilia;
   na
(f) Kuendeleza utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini.
(g) Kujenga mradi wa umeme wa Kinyerezi wenye uwezo wa MW 240.
(h) Kuendeleza mradi wa umeme wa Kiwira (MW 200) na Mchuchuma (MW
   240), Ngaka (MW 200) vitakavyozalisha umeme unaotokana na makaa ya
  mawe.
(i) Kuanza utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme (358MW) kwa kutumia
   maji katika bonde la mto Ruhuji.
(j) Kuzalisha umeme (300MW) kutokana na gesi asili ya Mnazi Bay.
(k) Kupanua mitambo ya kusafisha gesi na bomba la kusafirisha gesi kutoka
   Songo Songo hadi Dar es Salaam.
(l) Kutekeleza mradi wa usambazaji wa gesi asili Dar es Salaam kukidhi
   mahitaji ya sekta mbalimbali.
(m) Kufanya tathmini na kujenga mfumo wa kusambaza gesi asilia nchini.
(n) Kuanza mchakato utakaowezesha utekelezaji wa mradi wa kufua umeme
   kwenye vyanzo vya maji katika maporomoko ya Stiegler’s Gorge, Ruhuji,
    Rumakali, Mpango, Nsovwe na Ruvuma.
(o) Kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta na bomba la kusafirisha mafuta
   kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza (1200 km).
(p) Kuongeza kasi ya uunganishwaji umeme kupitia mifumo nje ya gridi kwa
   kuhamisha matumizi ya nishati jadidifu kama umeme wa jua, upepo na
  tungamotaka kupitia mradi wa TEDAP.
37
(q) Kuandaa programu ya kupunguza matumizi ya umeme hususan viwandani
   na majumbani.
(r) Kufufua na kupanua mitambo ya TPDC ya kusafishia mafuta na
   kuhakikisha kwamba mitambo hiyo inafanya kazi wakati wote.
(s) Kuwa na mpango wa kuhimiza matumizi ya nishati mbadala ya jua, upepo
   na fungamotaka (biogas).
(t) Kuanza utekelezaji wa njia Kuu ya Umeme ya Zambia, Tanzania na Kenya
   (ZTK) inayounganisha mitandao ya Umeme ya nchi za Mashariki ya Afrika
  na nchi za Kusini.
(u) Kukamilisha utekelezaji wa mradi wa KV 132 wa Makambako-Songea
   utakaofikisha umeme wa gridi wilaya za Songea, Namtumbo, Mbinga,
  Nyasa na Ludewa.
(v) Kuongeza ushiriki wa sekta binafsi ili iwekeze katika uzalishaji wa nishati
   mbadala kutokana na jua, upepo, biogas na vyanzo vingine kwa kiwango
  kikubwa na kuongeza uwezo wa usambazaji kwa gharama nafuu zaidi kwa
 njia ya ubia wa sekta ya Umeme na Sekta binafsi (PPP).
(w) Kuongeza uwezo wa gridi ya Taifa toka MW 240 hadi MW 400.
MIUNDOMBINU
Barabara
64.
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani ya miaka ya 2010 – 2015, Chama
kitaielekeza Serikali kuyalinda na kuyaendeleza mafanikio kwa kuchukua hatua
zifuatazo:-
(a)
Kuimarisha Mfuko wa Barabara (Tanzania Road Fund)
Kuendelea kuimarisha Mfuko wa Barabara kwa kufanya yafuatayo:-
(i) Kubuni na kupanua wigo wa vyanzo vya mfuko wa barabara ili
   kuongeza kiwango cha Mfuko.
(ii) Kuandaa mkakati endelevu wa kukarabati barabara na madaraja nchini
    ili kuinua uhai wa miundombinu hiyo na kupunguza kwa kiwango
38
kikubwa gharama za kuzikarabati.
(b) Kutenga fedha za maendeleo ya barabara za miji ikiwemo Dar es Salaam,
   Arusha na Mwanza na kuangalia uwezekano wa kuunda chombo maalumu
  cha kusimamia na kuendeleza ujenzi wa barabara za mijini.
(c) Kukamilisha ukarabati wa barabara zote ambao unaendelea na
   ujenzi kwa kiwango cha lami ambao umekwisha anza katika
  Barabara Kuu na Barabara za Mikoa kama ifuatavyo:





























Manyoni – Isuna (Km 54);
Kagoma – Biharamulo – Lusahunga (Km 154);
Ndundu – Somanga (Km 60);
Sumbawanga – Matai – Kasanga (Km 112);
Marangu – Tarakea – Rongai – Kamwanga (Km 98);
Minjingu – Babati – Singida (Km 222);
Korogwe – Handeni (Km 65);
Mziha – Turiani – Magole (Km 84.6)
Dumila – Kilosa (Km 63)
Bariadi – Lamadi (Km 71.8);
Mbeya – Chunya – Makongolosi (Km 115);
Tanga – Horohoro (Km 65);
Masasi – Mangaka (Km 54);
Makofia – Msata (km 64);
Mwandiga – Manyovu (km 60);
Handeni – Mkata (km 54);
Kisarawe – Maneromango (Km 54);
Njombe – Makete (Km 109).
Barabara ya Kilwa/DSM (km 12);
Barabara ya Mandela (km 16);
Msimba – Ikokoto – Mafinga (Km 219);
Arusha – Namanga (Km 105);
Chalinze – Segera – Tanga (Km 245); na
Isaka – Lusahunga (km 242)
Kwasadala-Masama (Km 12.2);
KiboshoShine-Kwa Raphael-International School (Km 43);
RauMadukani-Mawela-UruNjari (Km 12.5);
KiruaNduoni-Marangu Mtoni (Km 31.5);
Kahama Mjini (Km 5).
(d) Kuanza Ujenzi mpya na ukarabati kwa Kiwango cha Lami Barabara
Zifuatazo:
39






























Bunda – Kisorya – Nansio (Km 93);
Tunduma – Sumbawanga (Km 230);
Rujewa – Madibira – Mafinga (Km 151);
Babati – Dodoma – Iringa (Km 523);
Sumbawanga – Kanyani – Nyakanazi (Km 562);
Nata – Fort Ikoma (Km 141);
Nzega – Tabora (Km 116);
Manyoni – Itigi – Tabora (Km 264);
Ipole – Koga – Mpanda (Km 255);
Makurunge – Saadani – Pangani - Tanga (Km 178);
Matai – Kasesya (Km 65);
Mangaka – Mtambaswala (Km 65);
Mto wa Mbu – Loliondo – Mugumu – Nata – Makutano (Km 452);
Kyaka – Bugene (km 59);
Mbinga – Mbamba bay (Km 66);
Tunduru – Namtumbo (Km 194);
Kamwanga – Sanya Juu (Km 75);
Tabora – Urambo (Km 90);
Uvinza – Kidahwe (Km 77);
Daraja la Malagarasi na barabara zake (Km 48);
Uyovu – Bwanga – Biharamuro (Km 112);
Kisesa –Usagara (Km 17);
Namtumbo – Songea (Km 70);
Peramiho – Mbinga (Km 78);
Kawawa Jct – Mwenge – Tegeta (Km 17);
Segera – Same – Himo (km 261);
Makambako – Songea (km 295);
Mtwara – Masasi (km 200);
Arusha – Moshi – Himo – Holili (km140);
Arusha – Minjingu (km 104);
Nyanguge – Musoma – Sirari (km 262); na
Sanya Juu – Bomang’omba (Km 25).
(e) Kuzifanyia Upembuzi na Usanifu Barabara Zifuatazo:-
• Tabora – Mambali – Bukene – Itobo – Kahama (Km 149);
• Lupilo – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Kitanda (km 396);
• Ifakara – Mahenge ( Km 67);
• Kibondo – Mabamba (km 35);
• Kolandoto- Lalago - Mwanhuzi - Matala - Oldeani Jct (km 328);
• Omugakorongo – Kigarama – Murongo (km 105);
• Mpemba – Isongole (Tanzania/Malawi) (km 49);
• Soni – Bumbuli –Dindira – Korogwe (km 74);
40









Makofia – Mlandizi – Vikumburu (Km 148);
Kibaoni – Majimoto – Inyonga Km 162);
Mpanda- Ugala – Kaliua – Ulyankulu – Kahama (km 428);
Makongolosi- Rungwa – Mkiwa (km 412);
Mtwara – Newala – Masasi (km 209);
Handeni – Kiberashi – Kondoa – Singida (Km 460);
Kibaha – Mapinga (Km 23);
Geita-Bukoli-Kahama (Km 107);
Mbande-Kongwa Jct – Mpwapwa (Km 50).
·
Vivuko
65.
Kuandaa utaratibu wa kununua vivuko vipya vyenye uwezo wa kubeba
tani 50 kila kimoja kwa ajili ya maeneo yafuatayo:-
(a)
(b)
(c)
(d)
Msanga Mkuu (Mtwara),
Rusumo (Kagera),
Itungi Port – Matema (Kyera) na
Kilambo (Mtwara) kitakachotoa huduma kati ya Tanzania na
Msumbiji.
66. Madaraja
(a) Kuanza ujenzi wa daraja la mto Kilombero na daraja la mto Mwatisi
   katika mkoa wa Morogoro.
(b) Kuanza ujenzi wa daraja la Malagarasi, Kigoma.
(c) Kukamilisha maandalizi na kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ili
   kuunganisha Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam.
(d) Kuanza ujenzi wa daraja la Nangoo (Mtwara), Sibiti (Singida), Ruhekei
   (Mbinga) na Mbutu (Igunga).
(e) Kuanza usanifu wa daraja la Ruhuhu (Ruvuma).
67. Usafiri na Uchukuzi
(a) Kuendelea kuiimarisha Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kwa lengo la
kuipa uwezo wa kutoa huduma bora kwa kusafirisha abiria na mizigo ya
ndani na nchi jirani. Pia, reli itaendelezwa kama mhimili wa mpango wa
maendeleo wa eneo la Ukanda wa kati.
41
(b) Kushirikiana na Serikali za Rwanda na Burundi, kuanza ujenzi wa reli
mpya kutoka Dar es Salaam kwenda Kigali (Rwanda) na Msongati
(Burundi).
(c) Kuimarisha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kwa
kuboresha miundombinu ya reli na kuendeleza juhudi za kubadilisha
mfumo wa uendeshaji wa shirika kwa lengo la kuboresha huduma za
abiria na mizigo.
(d)
Kujenga na kuimarisha miundombinu ya Reli na Bandari kwa kukamilisha
mtandao wa reli na kuunganisha bandari ya Tanga na reli ya Arusha -
Musoma:-
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
Ujenzi wa bandari mpya eneo la Mwambani (Tanga),
kuboresha reli ya Tanga – Arusha,
kujenga reli mpya kati ya Arusha na Musoma,
Kuboresha bandari ya Musoma.
(e) Kuanza ujenzi wa reli ukanda wa Mtwara kwa kuchukua hatua za
   maandalizi ya mradi wa ujenzi wa reli ya Mtwara – Mchuchuma – Liganga.
(f) Kuendeleza huduma za uchukuzi kwenye maziwa kwa kuimarisha bandari
   za Kigoma, MbambaBay, Mwanza, Bukoba na Nansio.
(g) Kuboresha huduma za uchukuzi katika Bandari za Mwambao :
(i)
(ii)
(iii)
Kupanua bandari ya Dar es Salaam na Mtwara
Kujenga bandari mpya Bagamoyo
Kujenga magati katika bandari za Mafia na Lindi.
(h) Kutekeleza Programu ya Uwekezaji Katika Sekta ya Uchukuzi kwa kuvutia
   wawekezaji binafsi katika uendeshaji wa sekta ya uchukuzi kwa kuzingatia
  Sera ya Sheria ya ushirikishaji wa sekta binafsi (PPP).
(i) Kuimarisha usafiri wa anga iIi uchangie kwenye pato la Taifa kwa
   kuchukua hatua zifuatazo:
(i) Kuimarisha na kuboresha kiwanja cha JNIA kwa kujenga jengo jipya
   la abiria na majengo mengine ya huduma za abiria.
(ii) Kukamilisha na kutekeleza Mpango Kabambe wa Usafiri wa Anga.
42
(iii)
Kukamilisha ujenzi wa kiwanja kipya cha Kimataifa cha
cha Songwe (Mbeya)
ndege
(iv) (v) Kufanyia upembuzi na usanifu kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha
        Bagamoyo.
(vi) Kukamilisha uboreshaji wa viwanja vya ndege vya Mwanza na
    Mtwara.
(vii) Kukamilisha uboreshaji wa viwanja vya ndege vya Mafia, Arusha,
     Mpanda, Sumbawanga Bukoba, Kigoma, Tabora na Shinyanga.
(viii)
(j)
Kuanza ujenzi wa kiwanja kipya cha Kimataifa cha ndege cha
Msalato (Dodoma).
Kuunda upya Shirika la Ndege la Taifa kwa kushirikisha sekta
binafsi.
Kupunguza Msongamano wa Magari katika Jiji la Dar es Salaam kwa
kufanya yafuatayo:
(i)
Kujenga barabara za juu (fly overs) kwenye makutano ya barabara
maeneo ya Ubungo na TAZARA,
(ii) Kupanua mtandao wa barabara za Jiji za Dar es Salaam kwa kujenga
na kukarabati barabara zifuatazo:-
• Mbezi (Morogoro road)-Malambamawili-Kinyerezi-Banana (Km
14.0);
• Tegeta Kibaoni-Wazo-Goba-Mbezi Mwisho (Km 20.0);
• Tangi Bovu-Goba (Km 9.0);
• Kimara Baruti-Msewe-Changanyikeni (Km 2.6);
• Kimara-Kilungule-External Mandela road (Km 9.0);
• Ubungo Bus Termanial-Mabibo-Kigogo Round about (Km 6.4);
• Kigogo Round About-Bonde la Msimbazi-Twiga/Msimbazi Junction
(Km 2.7);
• Tabata Dampo-Kigogo- Ubungo Maziwa External (Km 2.25);
• Old Bagamoyo-Garden Road (Km 9.1); na
• Jet Corner-Vituka-Devis Corner (Km 6.0).
(iii) Kuanzisha mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART).
43
Kuimarisha uwezo wa Utabiri wa Hali ya Hewa
68.
Kuimarisha Uwezo wa Utabiri wa Hali ya Hewa Nchini kwa kutekeleza yafuatayo:-
(i) Kukamilisha na kutekeleza Sera ya Taifa ya Hali ya Hewa,
(ii) Kuiongezea uwezo Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ili iweze kutekeleza
    majukumu yake ipasavyo,
(iii) Kuendelea kutanua mtandao wa rada hadi kufikia rada saba nchi nzima,
(iv) Kuboresha miundomblnu ya kutoa utabiri na mawasiliano katika kituo
    kikuu cha Utabiri wa hali ya hewa, na
(v) Kuboresha mfumo wa kutoa taarifa za hali ya hewa mapema na
   kuhakikisha kuwa taarifa hizo zinafika kwa watumiaji mapema.
Sayansi na Teknolojia
69. Mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda ambayo Taifa linataka yafanyike
   ili tuweze kuleta modenaizesheni ya uchumi wetu, yatawezekana na kasi yake
  itakua kwa njia ya nchi kuwekeza vema katika ujenzi wa msingi imara wa
 maendeleo ya sayansi na teknolojia (building a solid scientific and technical
base). Msingi imara wa sayansi na teknolojia katika uhandisi wa chuma na
madawa (kemikali) utaiwezesha nchi kupanua haraka matumizi ya sayansi na
teknolojia katika shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma katika sekta
mbalimbali za uchumi wetu.
70. Katika kipindi hiki ambacho nchi imeamua kwa dhati kujenga uchumi wa kisasa
   na kuutokomeza umaskini, ni lazima sasa tulipatie kipaumbele cha kwanza suala
  la maendeleo na matumizi ya sayansi na teknolojia ili tuweze kuondokana na
 uchumi ulio nyuma na pia uchumi tegemezi.
71. Hivyo, katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010-2015, Chama Cha
   Mapinduzi kitazielekeza Serikali kuweka msisitizo mkubwa katika suala la
  maendeleo na matumizi ya sayansi na teknolojia kwa kuchukua hatua
 zifuatazo:-
44
(a) Kutenga kila mwaka kiasi kisichopungua asilimia 1.0 ya pato ghafi la Taifa
   (GDP) kwa ajili ya Utafiti, Maendeleo na Maonyesho ya Matokeo ya Utafiti
  (R,D&D).
(b) Kuchukua hatua za makusudi za kuimarisha Tume ya Sayansi na
   Teknolojia ili kiwe chombo kinachowaunganisha watafiti na wagunduzi
  wote nchini ili waweze kukaa kubadilishana uzoefu na kuwa na msukumo
 wa pamoja katika ujenzi wa msingi wa sayansi na teknolojia tunaouhitaji.
(c) Kuishirikisha sekta binafsi katika kuchangia maendeleo na matumizi ya
   sayansi na teknolojia kwenye uzalishaji mali na utoaji wa huduma.
(d) Kuandaa programu mahusus ya wataalamu wa kada mbalimbali kama vile
   za uhandisi, uganga wa binadamu na wanyama, madini, jiolojia na kilimo
  n.k. watakaojaza nafasi ambazo ni muhimu na za lazima katika kuyafikia
 malengo hayo ya dira.
(e) Kufufua, kupanua na kuanzisha viwanda ili kukuza uzalishaji viwandani na
   kuongeza ajira ya wanasayansi.
(f) Kuimarisha shughuli za kuatamia teknolojia (technology incubation) kabla
   ya kuzipeleka sokoni.
(g) Kuandaa mazingira bora ya kusambaza teknolojia kwa watumiaji.
(h) Kutumia vyombo vya habari kutoa taarifa muhimu za sayansi, teknolojia
   na ubunifu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
(i) Kuwatambua wagunduzi wetu na kuwapa rasmi hakimiliki za ugunduzi
   wao.
45
(j)
Kuboresha kwa kiwango kikubwa mishahara, marupurupu na mafao ya
watafiti na wagunduzi wetu.
Sekta ya Fedha
72. Sekta ya Fedha ndicho kipimo kinachoweza kuonesha viwango vya uchumi wa
   nchi vilivyofikiwa katika vigezo mbalimbali kama vile pato la Taifa, ukuaji wa
  uchumi, mfumko wa bei n.k.
 Maendeleo ya haraka katika nyanja hizo
yanategemea uimara na uwezeshaji wa Sekta ya Fedha.
73. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010 - 2015, Chama kitaielekeza
   Serikali kuimarisha Sekta ya Fedha kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuweka akiba na
   kutumia huduma za benki katika shughuli zao za kila siku za kifedha.
(b) Kuendelea kupanua huduma za benki ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
(c) Kuendelea kuwahamasisha wananchi ili waone umuhimu wa kujiunga na
   huduma za bima mbalimbali ili zitumike pamoja na mifuko ya hifadhi ya
  jamii katika kukuza uwekezaji katika uchumi.
(d) Kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala la riba za mabenki ili kuondoa tofauti
   iliyopo baina ya riba za mikopo na riba za amana na kuhakikisha kwamba
  mikopo ya muda mrefu ina riba ndogo.
SURA YA TANO
SERA YA UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI
74.
Sera yetu ya Msingi ni kwamba wananchi wenyewe wamiliki na kuendesha
uchumi wa nchi yao. Lakini ili wananchi wa Tanzania waweze kumiliki uchumi
lazima wawe na maarifa ya kisasa. Watanzania walio wengi wanapungukiwa na
maarifa ya uchumi wa kisasa, hawana mitaji na mazingira ya jamii yenye vikwazo
46
vingi vinavyowafanya washindwe kushiriki katika uchumi wao. Ndio maana
ukabuniwa mkakati wa kuwawezesha wananchi kiuchumi ili nao waweze kushiriki
katika uendeshaji wa uchumi wa kisasa.
75.
Kwa kutambua kwamba kila raia wa Tanzania anayo fursa ya kumiliki ardhi na
kuendesha shughuli za maendeleo pale anapoishi, Chama Cha Mapinduzi
kinaendelea kutoa wito kwa wananchi kwamba sera ya uwezeshaji itafanikiwa tu
katika maisha yao kama kila mwenye uwezo wa kufanya kazi atatekeleza mambo
yafuatayo:-
(a) (b) Kutambua kwamba ardhi, cherehani, mgahawa, duka, mashine ya
       kufyatulia matofali anayomiliki n.k. ni msingi imara wa maendeleo yake na
      kwamba uwezeshaji ni njia ya kumuunga mkono. Kila mwananchi
     mwenye shughuli halali ya kufanya azame katika kujiletea maendeleo kwa
    kuendeleza shughuli hiyo.
(c) Kukubali kwamba kufanya kazi kwa bidii na kwa maarifa, pamoja na
   kutumia kwa busara mapato yatokanayo na kazi, ni msingi bora wa kuishi
  kwa kujitegemea. Kazi ni uhai na pia ni chimbuko la mali au utajiri ambao
 mwananchi anauhitaji.
(d)
76.
Kutambua kwa dhati kwamba uwezo wa kufanya kazi alio nao mwananchi
ni nguvu na mtaji wake namba moja katika kujiletea maendeleo yake pale
alipo. Mtaji huu utumike kama sharti la kujikwamua na umaskini.
Wananchi ambao wanajishughulisha na kilimo na ufugaji wanatakiwa
kulima kila zao kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo ili wapate mavuno
mengi kwa kila eneo wanalolima. Aidha, anayefuga ng’ombe, mbuzi,
 kondoo na kuku anatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia kanuni bora za
ufugaji ili aweze kupata faida kubwa hata kabla ya kupanua shughuli zake.
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010-2015, Chama kitaielekeza
Serikali kuendelea kutekeleza sera ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kwa
kuchukua hatua zifuatazo:-
(a)
Kufufua kwa nguvu zote elimu yenye manufaa ya watu wazima nchini
kote ili masomo ya ujasiriamali, uwezeshaji, urasimishaji wa biashara,
kilimo, ufugaji na uvuvi yaweze kutolewa kwa wananchi wengi.
Maandalizi kamili yafanyike ili elimu itakayotolewa iweze kuziingiza
kwenye mfumo rasmi rasilimali na biashara za wanyonge ambazo bado
ziko nje ya mfumo huo. Mafunzo hayo yalenge katika kuutokomeza
umaskini wa wananchi walio wengi.
47
(b) Kuhamasisha uanzishwaji wa ushirika wa kuweka na kukopa (SACCOS na
   VICOBA), wa mazao, ujenzi, uvuvi, biashara na aina nyingine za ushirika ili
  wananchi wengi zaidi wajiunge na ushirika na wawezeshwe kimtaji
 kupanua shughuli zao za uzalishaji mali. Serikali izingatie kwa ukamilifu
uzoefu ambao umepatikana katika eneo hili la ushirika na iandae
wataalam wengi wa ushirika ambao wataajiriwa kuimarisha na kuboresha
sekta ya ushirika nchini kote.
(c) Kuandaa mpango maalumu utakaowezesha utekelezaji makini wa Mkakati
   wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) kwa
  kuhakikisha kwamba upatikanaji wa hatimiliki za ardhi, leseni za biashara
 na mikopo ya kupanulia shughuli za wanyonge, unakuwa mwepesi ili
shughuli za kuinua mapato ya wananchi na kupambana na umaskini
zisicheleweshwe wala kukwamishwa na taratibu za mikopo.
(d) Kukuza mifuko ya uwezeshaji, kuboresha usimamizi wake na taratibu za
   kutoa mikopo ya riba nafuu ili walengwa wengi zaidi waweze kunufaika
  nayo.
 Serikali iunde chombo cha wataalam makini na waaminifu
watakaokabidhiwa jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli hizo nchini
kote ili ionekane wazi kwamba lengo la uwezeshaji kimitaji linazaa
matunda yanayoboresha maisha ya wanyonge.
(e) Kuimarisha Benki ya Rasimali Tanzania (TIB) kwa kuongeza mtaji wake
   kwa kiwango kikubwa ili kuongeza nguvu ya uwekezaji katika kilimo.
(f) Kuhamasisha wananchi kutumia fursa zinazotokana na kupitishwa kwa
   sheria zifuatazo:-
(i) Sheria ya Mikopo na Karadha inayowawezesha wananchi kupata
   zana bora za kufanyia kazi.
(ii) Sheria ya Dhamana ya Mikopo ya Nyumba inayowawezesha
    wananchi kujenga nyumba bora, na
(iii) Sheria ya Umilikaji wa Sehemu ya Nyumba inayowawezesha
     wananchi kumiliki sehemu ya jengo kwa ajili ya makazi au shughuli
    mbalimbali.
AJIRA NA UWEZESHAJI WA WANANCHI
77.
Chama Cha Mapinduzi kinatambua kwamba katika kipindi hiki suala la ajira, na
hasa ajira ya vijana, limekuwa nyeti. Hii ni kwa sababu idadi ya vijana
wanaofuzu elimu ya msingi, sekondari, vyuo na vyuo vikuu kila mwaka ni kubwa
48
sana. Idadi hiyo inakuzwa pia na vijana wanaomaliza mafunzo ya JKT. Vijana
hawa wote ni nguvu kazi ya Taifa ambayo inaweza kutumika katika kazi na
shughuli halali za ujenzi wa nchi.
78.
Ili kujenga fursa za ajira hasa kwa vijana, katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani
ya 2010 – 2015, Chama kitaitaka Serikali ishughulikie mambo yafuatayo:-
(a) Kuimarisha na kupanua mafunzo ya vyuo vya maendeleo ya wananchi ili
   vipokee vijana wengi zaidi na kuwapatia mafunzo ya maarifa ya kisasa
  katika fani za kilimo, biashara, ufundi stadi na ujasiriamali.
(b) Kufanya utafiti wa kina wenye lengo la kuandaa mpango wa muda mrefu
   utakaowashirikisha vijana katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ili
  kuwajengea uwezo wa kujitegemea.
(c) Kuimarisha Shirika la Tija la Taifa (NIP) ili kuongeza ufanisi na tija katika
   utekelezaji wa shughuli za uendeshaji wa uchumi nchini.
(d) Serikali kuibua Mpango Kabambe wa kuwawezesha kiuchumi vijana
   wasomi waliotayari kujituma kwa kujiajiri ili watumie nguvu na maarifa
  waliyonayo katika kilimo, ufugaji, uvuvi n.k. wa kisasa. Mpango huo
 utawawezesha vijana hao kwa:-
(i) Kuwaandalia na kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na yanayohusu
   shughuli wanazokusudia kuzifanya;
(ii) Kuweka utaratibu mwepesi wa kupata mikopo nafuu;
(iii) Serikali kutenga maeneo makubwa ya ardhi kwa ajili ya mpango wa
     aina hii kwenye maeneo yanayozunguka miji, majiji na kwingineko.
Wafanyakazi
79.
Katika kipindi cha 2010-2015, CCM itaendelea kuwa karibu na wafanyakazi na
kuhakikisha kuwa Serikali zinayatambua na kuyashughulikia kwa ukamilifu na
kwa wakati muafaka matatizo yao. Miongoni mwa hatua zitakazochukuliwa na
Serikali zitakuwa pamoja na hizi zifuatazo:-
(a) Kuendelea kuboresha mishahara ya wafanyakazi kwa kadri hali ya uchumi
   wa nchi utakavyoruhusu.
(b) Kuimarisha na kufanya kaguzi za kazi, ikiwa ni pamoja na masuala ya afya
   na usalama mahali pa kazi.
49
(c) Kusuluhisha na kuamua kwa wakati migogoro yote ya kikazi na kuimarisha
   ushiriki na ushirikishwaji wa wafanyakazi mahali pa kazi.
(d) Kuhakikisha kwamba mishahara ya wataalamu wa ndani na nje wenye sifa
   na kazi zinazofanana wanalipwa mishahara inayolingana.
(e) Serikali kuanzisha mchakato utakaohakikisha kwamba pamoja na
   kuthamini mchango wa kila mfanyakazi na kufanya kazi katika taaluma
  zao na kuziheshimu ni muhimu ione tofauti kubwa iliyopo kati ya malipo
 ya wafanyakazi wa ngazi za juu na wale wa ngazi za chini.
Vijana
80.
Chama Cha Mapinduzi kinatambua umuhimu wa vijana ambao ni kundi kubwa la
nguvukazi. Changamoto zinazowakabili ni pamoja na ukosefu wa ajira, elimu na
maarifa ya kisasa katika uzalishaji mali, biashara na ujasiriamali. Katika kipindi
cha utekelezaji wa Ilani hii Chama kitazihimiza Serikali zake kutekeleza
yafuatayo:-
(a) Kupanua mafunzo ya VETA yaweze kuchukua vijana wengi zaidi
   wanaofuzu elimu ya msingi ili waandaliwe kujiajiri wenyewe.
(b) Kuwahamasisha vijana kuanzisha miradi ya kiuchumi na kujiunga katika
   vikundi vya ushirika wa kuweka na kukopa (SACCOS) na VICOBA na
  kuziwezesha kimitaji.
(c) Kuwahamasisha vijana kujiunga na vituo vya ufundi stadi ili wapate stadi
   za kuwawezesha kujiajiri wenyewe.
(d) Kuimarisha usimamizi na matumizi ya fedha za Mfuko wa Maendeleo ya
   Wanawake na Vijana katika Halmashauri zote ili uweze kuwanufaisha
  vijana wengi zaidi kupitia SACCOS zao.
(e) Kushirikiana na wadau wengine katika kuimarisha vyama vya vijana vya
   ushirika wa akiba na Mikopo (SACCOS) ili viweze kutoa mikopo yenye
  masharti nafuu kwa vijana. Umuhimu wa kulipa mikopo kwa wakati
 utasisitizwa.
(f) Kushirikiana na wadau wengine katika kufanya utafiti juu ya maeneo
   mengi ya ajira na kupanua wigo wa harakati za kiuchumi zinazozalisha
  ajira nyingi kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara na viwanda vidogo
 vidogo ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana.
50
(g) Kuandaa na kuboresha mikakati na mipango mbalimbali ya malezi na
   makuzi bora kwa vijana yakiwemo mafunzo ya uraia mwema, maadili
  mema na uzalendo kwa nchi yetu.
(h) Kutekeleza mipango endelevu ya kuwaandaa vijana wataalamu katika fani
   mbalimbali za maendeleo. Mkazo mkubwa wa maandalizi utawekwa
  kwenye ajira binafsi.
(i) Serikali kuandaa mafunzo maalum kwa vijana ya kupenda kufanya kazi na
   kuwa waadilifu ili waweze kuajirika.
(j) Serikali isimamie kikamilifu sheria ya ajira kwa wageni.
(ki) Kuhamasisha ushiriki wa vijana katika ngazi mbalimbali za maamuzi ikiwa
    ni pamoja na kukamilisha uanzishaji wa Baraza la Vijana.
Hifadhi ya Jamii
81.
Ili kuimarisha na kuendeleza hifadhi ya jamii Chama Cha Mapinduzi katika kipindi
cha utekelezaji wa ilani hii kitazielekeza Serikali zake kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kufanya tathmini ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kurekebisha viwango
   vya mafao vinayotoa ili visipishane mno.
(b) Kuanzisha na kuimarisha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya
   Hifadhi ya Jamii.
(c) Kuchukua hatua za makusudi za kupanua wigo wa kinga ya Hifadhi ya
   Jamii, ili Watanzania walio wengi waweze kufaidika na huduma za mifuko
  ya jamii.
(d) Kuelimisha jamii ya wafanyakazi na waajiri juu ya umuhimu wa Hifadhi ya
   Jamii kwa maendeleo ya wafanyakazi na ya nchi kwa ujumla.
(e) Kuendelea kutumia uwezo wa kifedha uliopo katika kila Shirika la Hifadhi
   ya Jamii, kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya nchi.
51
SURA YA SITA
SEKTA YA HUDUMA ZA JAMII
82. Sekta ya huduma za jamii inayojumuisha huduma za elimu, afya na maji ni
   muhimu sana katika maendeleo ya nchi maana ubora wake ni kielelezo cha
  maisha yenye neema yaliyofikiwa. Aidha, katika kila Taifa la kisasa, ustawi wa
 jamii una sura mbili zinazotegemeana za maendeleo ya vitu kwa upande mmoja
na maendeleo ya watu kwa upande mwingine. Huduma za jamii ndiyo
maendeleo ya watu wenyewe.
83. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010 – 2015, Chama Cha Mapinduzi
     kitaitaka Serikali iyalinde mafanikio yaliyopatikana katika kila sekta na
    kuyaendeleza ili wananchi waendelee kufurahia matunda ya uhuru wa nchi yao.
ELIMU:
84.
Serikali itachukua hatua za kuboresha, kuimarisha na hata kupanua elimu ya
Awali hadi ya Chuo Kikuu na kuhakikisha kwamba elimu ya ngazi zote
itakayotolewa nchini tangu sasa iwe ya ubora utakaowawezesha vijana wetu
kuchukua nafasi zao stahiki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na dunia kwa
ujumla. Hivyo, lengo hilo litafikiwa kwa kuishirikisha sekta binafsi kwa ukamilifu
katika kutekeleza yafuatayo:-
52
(a)
Elimu ya Awali
(i) (ii) Kujenga vyoo kwa ajili ya watoto wa Elimu ya Awali ili wasiingiliane
        na wale wa shule za msingi.
(iii)
(b)
Kuhakikisha kwamba kila shule ya msingi ina darasa la Elimu ya
Awali lenye madawati yanayolingana na hali ya watoto wa elimu
hiyo.
Kuandaa walimu wengi wa Elimu ya Awali na kuwapanga katika
shule zinazohusika.
Elimu ya Msingi
Kusimamia kwa ukamilifu utekekezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu
ya Msingi awamu ya pili (MMEM II – 2007 – 2011) na kuandaa na
kutekeleza awamu ya tatu (MMEM III):-
(i)
Kununua na kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika
shule zote.
(ii) Kuimarisha Vituo vya Walimu (Teacher Resource Centres) katika
    Kanda na Halmashauri zote ili viweze kutoa mafunzo ya walimu
   kazini.
(iii) Kuimarisha utoaji wa mafunzo kwa walimu wa masomo ya Hisabati,
     Kiingereza na Sayansi.
(iv) Kuendelea kuweka msukumo katika uandikishaji wa watoto wote
    wa rika lengwa katika ngazi ya Elimu ya Msingi kufikia asilimia 100
   mwaka 2015.
(v) Kuinua kiwango cha uandikishaji wa watoto wenye ulemavu na
   wenye mahitaji maalumu.
(vi) Kuendelea kuratibu na kusimamia upatikanaji wa maslahi ya
    walimu wa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ualimu na
   kuyaboresha ili kuhakikisha kwamba mishahara itolewayo
  inazingatia hali halisi ya maisha na ya soko.
(vii) Kuendelea kuimarisha ukaguzi wa shule na kuhakikisha kuwa kila
     shule inakaguliwa angalau mara moja kwa mwaka na taarifa za
    ukaguzi kufanyiwa kazi.
53
(viii) (xv Serikali Kuu ihakikishe kwamba kila Manispaa au Halmashauri ya
          Wilaya inajenga vyoo vya kisasa na vya kutosha katika shule zote
         za msingi ambazo ziko chini yake. Sekta binafsi ishirikishwe katika
        utekelezaji wa mradi huu.
(x) Kuanzisha mradi kabambe wa ujenzi wa nyumba nyingi za walimu
   wa shule za msingi za vijijini kwa kuwashirikisha wadau wote.
  Utekelezaji uanzie katika Wilaya ambazo zina uhaba mkubwa wa
 nyumba za walimu.
(xi) Kuongeza idadi ya wanafunzi watakaochaguliwa kuendelea na
    elimu ya sekondari kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2015.
(xii)
(c)
Kuhakikisha kwamba kila shule ya msingi ina walimu, madawati,
vitabu vya kiada kwa kila somo vya kutosha. Uwiano wa mwalimu
mmoja kwa kila wanafunzi 60 ufanyiwe kazi.
Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti
ya programu za elimu katika ngazi zote.
Elimu ya Sekondari
Kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu
ya Sekondari awamu ya pili (MMES II – 2010 - 2014), kuandaa na
kutekeleza awamu ya tatu (MMES III):-
(i) Kuendelea kutekeleza azma ya kuwa na angalau shule moja ya
   kidato cha tano na sita kwa kila tarafa.
(ii) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa kidato cha 4 kwenda kidato cha 5
    kufikia asilimia 50 ya watoto wanaofaulu ifikapo mwaka 2015.
(iii) Kuendeleza na Kuimarisha mafanikio tuliyofikia katika ujenzi wa
     shule za sekondari kwa kuongeza idadi ya walimu, kununua vifaa
    vya maabara, vitabu, kuimarisha Maktaba na kukabiliana na jambo
   lolote litakalopunguza ufanisi wa kiwango cha elimu katika shule
  hizo.
(iv) Kuendelea kutekeleza mpango wa kujenga maabara ya Sayansi na
    ya Lugha katika kila Shule ya Sekondari ili kuboresha ufundishaji.
(v) Kuendelea kutekeleza Programu ya kufundishia na kujifunzia kwa
   kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Shule za
  Sekondari.
54
(vi) (vii) Kuendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba za walimu hasa
          sehemu za vijijini na maeneo magumu kufikika.
(viii) Kuendelea kusimamia na kuimarisha michezo shuleni.
(ix) Kupitia na kuimarisha mitaala ya elimu ya sekondari kulingana na
    mahitaji.
(x) Kusimamia ubora wa miundombinu ya shule za sekondari ili kuleta
   ufanisi katika utoaji wa elimu.
(xi) Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti
    ya programu za elimu katika ngazi zote.
(xii) Kurudisha utaratibu wa kuzipelekea shule vitabu na vifaa ili
     kuhakikisha kwamba shule hazitofautiani katika upatikanaji na
    utumiaji wa vifaa hivyo.
(xiii) Kuimarisha na kuboresha kwa kiwango kikubwa shule za vijana
      wenye vipaji maalumu ili lengo la kuzianzisha liweze kufikiwa kama
     lilivyokusudiwa tangu mwanzo.
(xiv)
(d)
Kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi,
Hisabati na Lugha na kuinua ufaulu wa masomo hayo.
Katika shule za sekondari, uwiano wa mwalimu mmoja kwa
wanafunzi 45 uzingatiwe kama hatua ya kuinua ubora wa elimu
hiyo.
Elimu ya Ualimu
Kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo na
Menejimenti ya Ualimu (Teacher Development Management Strategy -
TDMS) katika utoaji wa mafunzo ya ualimu:-
(i) Kuanzisha mafunzo ya walimu wa shule za msingi watakaoandaliwa
   kufundisha masomo mawili tu ambayo kila mmoja anayamudu ili
  kuinua ubora wa elimu ya msingi.
(ii) Kuandaa na kuendeleza walimu wanaofundisha masomo ya
    Sayansi, Hisabati na Lugha katika Shule za Msingi na Sekondari.
55
(iii) (iv) Kutoa mafunzo kwa walimu kazini ili kuimarisha na kuendeleza
          mbinu za ufundishaji kwa walimu.
(v) Kutoa mafunzo ya TEKNOHAMA katika kufundishia na kujifunzia
   katika Vyuo vya Ualimu.
(vi) Kuendelea kusimamia na kuimarisha michezo katika vyuo vya
    ualimu.
(vii) Kuimarisha miundombinu ya vyuo vya ualimu ili kuleta ufanisi
     katika utoaji wa elimu.
(viii) Kuboresha maabara ya vyuo vya ualimu vyenye mchepuo wa
      sayansi na kuvipatia vifaa na kemikali zinazotakiwa kwa ajili ya
     mafunzo ya vitendo katika vyuo hivyo.
(ix) Kuandaa mitaala wa mafunzo yatakayojumuisha masomo ya
    mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda ili kupata
   wataalamu wa kufundisha masomo hayo. Uandishi wa vitabu vya
  masomo hayo yaende sambamba na maandalizi ya mtaala huo.
(x)
(e)
Kuongeza udahili wa wanachuo katika mafunzo ya Ualimu tarajali
ngazi ya Cheti na Stashahada.
Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti
ya programu za elimu katika ngazi zote.
Elimu ya Juu
Kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu
ya Juu:-
(i) Kuboresha utaratibu wa utoaji na urejeshwaji wa mikopo kwa
   wanafunzi wa Elimu ya Juu.
(ii) Kupanua wigo wa utoaji wa mikopo ili kila mwanafunzi aliye na sifa
    ya kuingia chuo kikuu apate mkopo.
(iii) Kukarabati, kupanua na kuimarisha miundombinu ya vyuo vikuu na
     vyuo vikuu vishiriki ili iweze kuhimili ongezeko kubwa la wanafunzi
    watakaomaliza elimu ya sekondari.
(iv) Kuongeza udahili wa wanafunzi kwenye vyuo vya elimu ya juu.
56
(v) (vi) Kuandaa wahadhiri wa kutosha na wenye sifa za kufundisha
        kwenye vyuo vya elimu ya juu.
(vii) Kuunganisha vyuo vikuu na taasisi za utafiti kwenye mtandao ili
     kuimarisha utafiti wa pamoja, kupanua elimu kiwango cha uzamili
    na uzamivu.
(viii) Kuratibu na kusimamia utoaji wa Elimu ya Juu iliyo bora na
      kufanyika kwa utafiti ili ziweze kutatua matatizo ya kijamii na
     kiuchumi.
(ix) Kuimarisha mazingira ya utoaji wa Elimu ya Juu na maslahi
    yanayoendana nayo ili wahadhiri wavutiwe kujiunga na kubaki
   katika vyuo vya Elimu ya Juu na Vyuo Vikuu.
(x) Kuimarisha utoaji wa Elimu ya Juu kwa njia ya Masafa na Elimu
   Mtandao.
(xi)
(f)
Kuongeza idadi ya wanafunzi wa kike vyuo vikuu ili ifikie angalau
asilimia 40 ya wanavyuo wanaodahiliwa kila mwaka.
Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti
ya programu za elimu katika ngazi zote.
Mafunzo ya Ufundi
Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya
Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi:-
(i) Kuongeza kasi ya upanuzi wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi
   stadi kwa kushirikisha sekta binafsi.
(ii) Kuanzisha vyuo vya Ufundi Stadi angalau kimoja kwa kila wilaya
    ifikapo mwaka 2015.
(iii) Kuendeleza mafunzo ya ufundi na kada za kati za fani mbalimbali.
(iv) Kuongeza idadi ya wahitimu wa vyuo vya ufundi stadi wenye sifa za
    kuendeleza progamu za elimu ya ufundi kuanzia ngazi ya ufundi
   sanifu hadi ngazi za juu.
(v) Kuendelea kuhamasisha wanafunzi wa kike kujiunga na Elimu ya
   Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
57
(vi) (vii)
(g)
Kuimarisha miundombinu ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo
ya Ufundi Stadi.
Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti
ya programu za elimu katika ngazi zote.
Elimu ya Watu Wazima Yenye Manufaa
(i) Kuandaa na kutekeleza mpango kabambe wa Elimu ya Watu
   Wazima Yenye Manufaa nchini kote.
(ii) Kuimarisha Mipango ya Elimu ya kujiendeleza ikiwa ni pamoja na
    Elimu Masafa na Ana kwa Ana.
(iii) Kuimarisha utoaji wa Elimu Nje ya Mfumo Rasmi kupitia Mpango
     wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA) kwa
    kushirikiana na wadau wengine.
(iv) Kuinua ubora wa utoaji elimu ya watu wazima kupitia Mpango wa
    Uwiano Kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA).
(v) Kuimarisha uwezo wa watendaji katika usimamizi na menejimenti
   ya programu za elimu katika ngazi zote.
SEKTA YA AFYA
85.
Maendeleo ya Taifa letu yataletwa na wananchi wenye afya bora
inayowawezesha kuzalisha mali na kutoa huduma mbalimbali. Katika miaka
mitano ijayo, Serikali itatekeleza na Chama kutoa kipaumbele katika maeneo
yaliyoainishwa katika MKUKUTA na Malengo ya Milenia kwa kutekeleza
yafuatayo:-
(a)
Kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM), ambao
unazingatia na kutoa kipaumbele katika maeneo yafuatayo:-
(i) Upatikanaji wa rasilimaliwatu wenye ujuzi na wa kutosha katika
   Sekta ya Afya,
(ii) Uwepo wa miundombinu ya huduma za afya na ustawi wa jamii
    kwa kukarabati na kujenga vituo vya kutolea huduma katika Afya
   na Ustawi wa Jamii hasa ngazi ya kijiji na kata,
58
(iii) Kuongeza upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitenganishi
     katika vituo vya kutolea huduma; na
(iv) Kuimarisha mfumo wa rufaa toka ngazi ya kijiji hadi Taifa.
(b) Kuimarisha usafiri wa wagonjwa, vifaa vya huduma za afya na ustawi wa
   jamii, njia za mawasiliano ya simu, “redio call na Internet”, katika ngazi
      zote za utoaji wa huduma za afya na ustawi wa jamii, ili kuwezesha
     upatikanaji wa huduma za kawaida za dharura za rufaa, zilizo bora,
    pamoja na upatikanaji wa vifaa vya kuwawezesha watu wenye ulemavu
   kumudu maisha ya kila siku.
(c) Kuhakikisha vituo vyote vinapata dawa muhimu na vifaa vya teknolojia ya
   kisasa, ya kuchunguza na kutibu magonjwa ili kuboresha utoaji wa
  huduma za kinga, tiba na utengemao.
(d) Kuimarisha nyenzo, vifaa na Mfumo wa ufuatiliaji na ukaguzi wa Huduma
   za Afya na Ustawi wa Jamii, pamoja na upatikanaji wa Taarifa na
  takwimu za Uendeshaji ikiwemo ufanyaji tathmini na utafiti, wa huduma
 za Afya na Ustawi wa Jamii.
(e) Kuhakikisha kuwa, huduma za Bima ya Afya zinaboreshwa na kuungana
   na Mfumo wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na Tiba kwa Kadi (TIKA), ili
  ziwafikie Wananchi na kuongeza asilimia za wanachama kutoka 7.7 hadi
 30 ifikapo mwaka 2015.
(f) Kuendeleza jitihada za kujenga uwezo wa ndani wa kutoa huduma ya
   matibabu ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa
  matibabu hususan kwa maradhi ya moyo, figo, mishipa ya fahamu na
 saratani.
(g) Kuboresha huduma za Ustawi wa Jamii, Serikali inatarajia kufanya
   yafuatayo:-
(i) Kutafsiri sheria 3 zifuatazo, Sheria ya Mtoto Na. 21 ya 2009, Sheria
   ya usafirishaji Haramu wa Binadamu ya 2009 na Sheria ya Wenye
  Ulemavu ya 2010.
(ii) Kutengeneza kanuni za utekelezaji wa sheria hizo.
(iii) Kuhuisha miongozo iliyopitwa na wakati ili kuendana na mabadiliko
     ya kiuchumi na kijamii.
59
(iv) Kufanya utambuzi wa watoto walio katika mazingira hatarishi katika
    wilaya 48 ambazo hazijafanya utambuzi.
(v) Kupeleka huduma za ustawi wa jamii kwenye Halmashauri.
(vi) Kutoa mafunzo kwa Maafisa Ustawi wa Jamii kwa ngazi za Shahada
    30, Stashahada 20 na Udaktari 5.
(vii) Kununua magari kwa makazi ya wazee 10 na vyuo 4 vya ufundi
     kwa watu wenye ulemavu.
(viii) Kufufua vyuo 4 vya watu wenye ulemavu na kuvipatia rasilimali
      watu na fedha.
(ix) Kuboresha Chuo cha Walezi wa Kulelea Watoto mchana Kisangara
    na Ilonga ili kutoa Wataalamu ngazi ya Cheti na Diploma.
(x) Kujenga vyuo 2 vya Ustawi wa Jamii na Jengo la Ofisi ya Ustawi wa
   Jamii.
(xi) Kuanza ujenzi wa Chuo Kikuu kipya cha Udaktari pamoja na
    hospitali ya kufundishia katika eneo la Mloganzila, Dar es Salaam
   ambacho kitakuwa na kitivo cha matibabu ya moyo, saratani na
  mishipa ya fahamu. Aidha, katika Chuo Kikuu cha Dodoma
 kinajengwa Chuo kishiriki cha Udaktari.
(h) Kuimarisha huduma ya matibabu ya wazee nchini kwa kuwapatia
   vitambulisho na kuyatungia sheria matibabu yao ya bure ili waweze
  kutibiwa hivyo katika vituo vyote vya matibabu bila ya usumbufu wowote.
(i) Kuimarisha huduma za mama Wajawazito, Watoto Wachanga na Watoto
   walio chini ya umri wa miaka mitano, ili kuendelea kupunguza idadi ya vifo
  vyao kwa kutoa mafunzo ya huduma ya uzazi wa dharura na kuimarisha
 huduma za “EMOs” katika vituo vyote vya afya nchini.
(j) Kuwajengea uwezo na kuimarisha ujuzi wa watumishi wa Sekta ya Afya
   na Ustawi wa Jamii, katika ngazi zote za kutolea huduma.
(k) Kuvijengea uwezo vituo vinavyotoa huduma za afya na Ustawi wa Jamii
   nchini.
(l) Kuimarisha udhibiti wa magonjwa yanayoambukiza, yasiyoambukiza na
   yale yaliyosahaulika.
60
Sekta ya Maji
86.
Kutokana na umuhimu wa Sekta ya Maji kwa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na
hifadhi ya mazingira Chama kitaielekeza Serikali kuendeleza
Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji na kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kufikia asilimia
   65 vijijini na mijini asilimia 75 ifikapo mwaka 2015.
(b) Kuandaa na kutekeleza mipango shirikishi ya usimamizi na uendelezaji wa
   rasilimali za maji katika mabonde yote tisa kwa kuimarisha uwezo wa Ofisi
  za Mabonde hayo na Maabara za Maji. Mabonde hayo ni ya Mto Pangani,
 Rufiji, Wami/Ruvu, Ruvuma na Bubu; Maziwa ya Victoria, Nyasa na
Tanganyika na Bonde la Kati (Ziwa Eyasi na Manyara).
(c) Kuendelea kushirikisha kwa ukamilifu nguvu za wananchi katika hatua
   zote za kutoa huduma ya maji ikiwa ni pamoja na kupanga, kujenga,
  kuendesha na kumiliki miradi yenyewe kwa njia ya kueneza Kamati za
 Maji za Vijiji sambamba na kuimarisha mifuko ya maji.
(d) Kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika matumizi na usimamizi wa maji
   shirikishi.
(e) Kuimarisha utunzaji
   mazingira.
(f) Kuendeleza utekelezaji wa ujenzi wa malambo na mabwawa mapya,
   kukarabati na kufufua malambo ya zamani ili maji mengi zaidi yaweze
  kupatikana kwa ajili ya matumizi ya wananchi na mifugo.
(g) Kutunga sheria itakayoiwezesha Serikali kuhakikisha kwamba upatikanaji
   wa maji unaongezeka nchini kwa njia ya kila shule, chuo, taasisi, wizara,
  hoteli, kiwanda, kata, vijiji na mtu binafsi atakayejenga nyumba ya kisasa
 mjini au kijijini anajenga miundombinu ya kuvuna na kutumia maji ya
mvua.
(h) Kutekeleza mradi mkubwa wa kufikisha maji katika miji ya Igunga, Nzega
   hadi Tabora kutoka mkoa wa Shinyanga.
(i) Kuboresha huduma ya maji katika miji mikuu ya mikoa na wilaya kwa
   kukarabati na kujenga miundombinu ya maji safi na majitaka.
wa vyanzo vya maji na kudhibiti uchafuzi wa
61
(j) Kuimarisha na au kuikarabati miradi ya kitaifa ya Wanging’ombe, Maswa,
     Mugango – Kiabakari, Handeni Trunk Main (HTM), Chalinze, Makonde na
      Kahama – Shinyanga ili iwe endelevu.
(k) Kuhakikisha kwamba kila mamlaka ya maji mjini inadhibiti upotevu wa
   maji katika eneo lake lote kwa kukagua na kukarabati mara kwa mara
  miundombinu ya maji ili huduma itolewe kwa gharama nafuu.
(l) Kujenga uwezo wa kuhudumia miradi ya maji vijijini kwa kutoa mafunzo
   ya wataalamu na mafundi wa maji.
SURA YA SABA
62
MAZINGATIO MAALUMU YA ILANI
KUHUSU ZANZIBAR
Utangulizi
87. Sura hii ya Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka 2010-2015, inatafsiri na
   kuainisha maeneo muhimu ya sera za CCM kwa kuzingatia mazingira maalumu
  ya Zanzibar. Ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, 2000 na
 2005 kwa upande wa Zanzibar, kimsingi ulitokana na ridhaa ya wananchi baada
ya kuridhishwa na sera zake zenye kutekelezeka na kuweka mbele maslahi ya
wananchi, Uhuru wa taifa letu, umoja na mshikamano wa kitaifa na kuongozwa
na misingi ya usawa, uadilifu, uwazi, na uwajibikaji.
88. Katika kipindi cha mwaka 2005–2010, ambacho ni cha pili na cha mwisho kwa
     Awamu ya Sita ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, yapo mafanikio makubwa
    yaliyopatikana chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Dk. Amani Abeid Karume, Rais
   wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
89. Katika kutekeleza azma yake ya kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar pamoja
   na sera zake za umoja, amani na mshikamano CCM imeendelea kuimarisha
  umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania
 kwa jumla.
MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM YA UCHAGUZI MKUU WA
MWAKA 2005-2010
90. Chini ya uongozi wa CCM na Rais Karume, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
   imetekeleza kwa mafanikio makubwa Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya
  2000-2010, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar (2020), Malengo ya Milenia na Ilani
 ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005-2010.
91. Katika kipindi hiki, Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuendeleza na
   kuimarisha huduma za kiuchumi na kijamii ikiwemo miundombinu ya barabara,
  bandari, viwanja vya ndege pamoja na huduma za jamii hususan elimu na afya.
 Baadhi ya mafanikio hayo yanajidhihirisha katika sekta zifuatazo:-
Uchumi
92.
Mafanikio yaliyofikiwa katika kukuza Uchumi ni kama yafuatayo:-
63
(a) Ukuaji wa pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 4.9 mwaka 2004 na
   kufikia wastani wa asilimia 6.7 mwaka 2009.
(b) Kasi ya mfumko wa bei imeendelea kushuka kutoka asilimia 18.5 mwaka
   2004 na kufikia asilimia 8.9 mwaka 2009.
(c) Pato kwa kila mwananchi limeongezeka kutoka kiwango cha Tshs.
   325,000 mwaka 2004 na kufikia Tshs. 726,000 mwishoni mwa mwaka
  2009.
(d) Nakisi katika mizania ya biashara nayo inaonesha kupungua kutoka
   kiwango cha 115,233.0 milioni mwaka 2004 na kufikia kiwango cha Tshs.
  92,137.5 milioni mwaka 2009.
(e) Ukusanyaji wa mapato ya ndani kwenye Pato la Taifa nao umeongezeka
   kutoka asilimia 13.5 ya mwaka 2004/2005 na kufikia asilimia 18.5 mwaka
  2009/2010.
Sekta za Uzalishaji Mali
Mapinduzi ya Kilimo
93.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Kilimo ni kama yafuatayo:-
(a) Kutekeleza miradi ya jamii inayohusu kilimo, mifugo na utunzaji rasilimali
   za baharini (ASSP/ASDP-L, PADEP na MACEMP).
(b) Kuanzisha Skuli za wakulima (mashamba darasa) ili kutoa mafunzo ya
   kilimo bora na ufugaji wa kisasa kwa wakulima. Jumla ya Skuli 186,
  zimeanzishwa kupitia mpango wa ASDP-L Unguja na Pemba.
(c) Kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji maji na kutoa mafunzo kwa
   wakulima. Jumla ya hekta 300, visima 6 na pampu 6 zimeimarishwa na
  kuwekwa katika mabonde ya Kibokwa, Bumbwisudi, Mchangani na Cheju.
(d) Kununua zana za kisasa za kilimo yakiwemo matrekta 27 na matrekta
   madogo “power tillers” 20.
(e) Kufufua kituo cha kuzalisha mbegu bora za nafaka – Bambi.
(f) Kufanya utafiti wa mbegu bora za mazao ya chakula na kufanikiwa
   kupata mbegu 3 za mpunga (NERICA) na 4 za muhogo (Machui,
  Kizimbani, Mahonda na Kama) zenye sifa na ubora unaohitajika.
64
(g) Kuimarisha vituo vya utafiti na mafunzo na kufanya ukarabati wa
   miundombinu ya utafiti zikiwemo maabara 2, visima 3 vya maji na ujenzi
  wa barabara za ndani katika Kituo cha Kizimbani.
(h) Kuanzisha ujenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Usarifu wa Mazao ya wakulima
   huko Kizimbani.
(i) Kuendeleza udhibiti wa wadudu waharibifu wa mazao na kuandaa mpango
   madhubuti wa matumizi ya mbinu za uwiano (Intergrated Pest
  Management).
Mapinduzi ya Ufugaji
94.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Mifugo ni kama yafuatayo:-
(a) Kununua mtambo mpya wa “Liquid Nitrogen” ili kuendeleza kazi ya
       upandishaji ng’ombe kwa sindano na kupata mbegu bora ya ng’ombe wa
          maziwa.
(b) Kuwaendeleza wafugaji wadogo kwa kuwapatia ng’ombe wa maziwa kwa
     njia ya mkopo (kopa ng’ombe ulipe ng’ombe). Zaidi ya wafugaji 400
        walifaidika na mpango huu kupitia Mfuko wa OPEC. Aidha, wafugaji
       2,373 walipatiwa ng’ombe bora na wafugaji 3,666 walipatiwa mbuzi wa
        maziwa kwa kupitia mradi wa PADEP.
(c) Kuanzisha vituo vya Huduma za Ufugaji (Farm Service Centres) na
   kuendeleza huduma za kinga na tiba ya mifugo.
Mapinduzi ya Uvuvi na Mazao ya Baharini
95.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Uvuvi na Mazao ya Baharini ni kama
yafuatayo:-
(a) Kuwaendeleza wavuvi wadogo wadogo kwa kuwapatia mafunzo ya
   kudhibiti uharibifu wa mazingira ya baharini na kuwapatia vifaa vya kisasa
  vya uvuvi zikiwemo boti na mashine, nyavu, mishipi, madema pamoja na
 majokofu ya kuhifadhia samaki.
(b) Kuanzisha na kutekeleza mradi wa MACEMP pamoja na kuendeleza
   maeneo ya hifadhi ya ukanda wa pwani ya Mnemba-Chwaka, Mkondo wa
  Pemba na kuongeza maeneo mapya ya Tumbatu, Bawe na Menai.
65
(c) Kuwaendeleza wakulima wa mwani kwa kuwapatia vifaa vya kulima
   mwani.
(d) Kukamilika kwa utafiti wa viumbe hai adimu vya baharini ulioainisha
   kuwepo kwa pomboo 136, aina ya Bottleneck na pomboo 63 aina ya
  Humback.
Maliasili
96.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Maliasili ni kama yafuatayo:-
(a) Kuwahamasisha wananchi ili kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali
ikiwemo misitu na bahari pamoja na kusimamia ulinzi na utunzaji wa misitu
katika maeneo yao.
(b) Kuwaelimisha wananchi juu ya sheria mbalimbali
kuhamasisha upandaji miti na uhifadhi wa misitu.
(c)
za
maliasili
na
Kuendeleza utunzaji wa wanyama pori walio katika hatari ya kutoweka
kama vile kima punju, popo wa Pemba na paa nunga na kuwatumia kama
vivutio vya utalii. Idadi ya kima punju wa Jozani imeongezeka kutoka 2,500
hadi 5,000, kima punju wa msitu wa Masingini nao wameongezeka kutoka
500 hadi 21,700.
Mazingira
97.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Mazingira ni kama yafuatayo:-
(a) Kuendeleza kazi ya udhibiti wa uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya
   kazi, viwanda na mahoteli.
(b) Kufanya mapitio ya miradi ya vitega uchumi na kutoa mapendekezo kwa
   wahusika. Jumla ya taarifa za miradi 107 zilifanyiwa mapitio na maeneo
  485 ya miradi ya vitega yalifanyiwa ukaguzi.
66
Utalii
98.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Utalii ni kama yafuatayo:-
(a) Kutengeneza tovuti kwa lugha ya Kichina ili kuitangaza Zanzibar kwa
   wawekezaji kutoka Jamhuri ya Watu wa China.
(b) Kuziingiza hoteli ndogo hasa zinazomilikiwa na wananchi katika mtandao
   maalumu wa “World Hotel Link” ili kuziwezesha kuingia katika
      mashindano ya soko la kimataifa.
(c) Ushiriki wa Zanzibar katika maonyesho 40 ya Kimataifa katika kuitangaza
   kiutalii na kutoa matangazo katika jarida maalumu la TANZANIA na
  UNESCO.
(d) Kuchapisha jarida la “The Ultimate Indian Ocean Experience” kwa
       lugha za Kiingereza, Kihispania, Kifaransa na Kujerumani pamoja na Jarida
      la vivutio vya Utalii vya Zanzibar kwa lugha ya Kirusi na Kichina. Harakati
     hizo za utangazaji zimeiwezesha Zanzibar kutembelewa na watalii 670,231
    katika kipindi cha mwaka 2005-2009.
(e) Kuingiza taswira ya Zanzibar katika tiketi za kampuni za boti ziendazo kasi
   za Azam Marine Ltd. na Farst Ferries Ltd.
(f) Kupitishwa kwa Sheria Namba 7 ya Mwaka 2008 ya Chuo cha Maendeleo
   ya Utalii na Sheria Namba 6 ya Mwaka 2009 ya Kamisheni ya Utalii.
(g) Kukamilisha tafiti 4 kubwa juu ya Sekta ya Utalii (Tanzania Tourism Sector
   Survey) zilizopelekea uwekaji wa viwango vya kutoza kodi kwa huduma za
  mahoteli.
(h) Kukamilisha Mpango wa Uendelezaji Utalii wa baharini na Sera ya Utalii
   wa Utamaduni pamoja na kufanyika kwa utafiti wa kuzitambua rasilimali
  za Utalii ambazo hazijatumika ipasavyo kwa lengo la kuongeza idadi ya
 siku kwa watalii na kuondokana na utalii wa msimu.
(i) Kujengwa kwa hoteli 11 za daraja la 5, 11 za daraja la 4 na 12 za daraja
   la 3 ambazo zimeanza kutoa huduma.
(j) Kuimarishwa kwa Mitaala ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii hadi kufikia
   kiwango cha Diploma katika somo la “Tourism and Hospitality
67
Management” pamoja na kuhitimu kwa jumla ya wanafunzi 891 katika
ngazi ya cheti na diploma.
(k)
Kukamilisha ujenzi wa vituo viwili vya Polisi (Nungwi na Kiwengwa) kwa
mashirikiano na wawekezaji katika Sekta ya Utalii na ununuzi wa vifaa vya
mawasiliano (redio calls 10) ili kuimarisha ulinzi na usalama wa watalii na
mali zao.
Viwanda na Biashara
99.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Viwanda na Biashara ni haya yafuatayo:-
(a) Kuandaa na kupitisha Sera ya Biashara na Sera ya uendelezaji wa
   biashara/viwanda vidogo vidogo na vya kati (SMEs) na kutafsiriwa katika
  lugha nyepesi.
(b) Kukamilisha Mpango Mkakati wa Usafirishaji wa Bidhaa na kuanza
   utekelezaji wake.
(c) Baraza la Biashara la Zanzibar lenye wajumbe kutoka sekta ya umma na
   sekta binafsi limeundwa na linafanyakazi zake.
(d) Kuwapatia mafunzo wajasiriamali 250 katika fani zifuatazo:-
(i) Uzalishaji na kuongeza thamani hasa kwa mazao ya Kilimo.
(ii) Elimu ya ujasiriamali
(iii) Usindikaji wa mazao ya Kilimo
(iv) Huduma za maendeleo ya biashara (BDS).
(v) Uzalishaji wa mafuta ya majani ya mikarafuu na utumiaji wa vinu
   vya uzalishaji.
(e) Kujenga vituo viwili vya majaribio vya kukaushia mazao ya kilimo/bahari
   Unguja na Pemba.
(f) Kununua vinu vinane vya kuzalisha mafuta ya majani ya mkarafuu na
   kuvigawa kwa wajasiriamali ambavyo vimetoa ajira kwa watu 2,052.
(g) Kuwapatia mafunzo wajasiriamali 60 katika fani zifuatazo:-
68
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
(vi)
Utengenezaji nguo
Ufugaji bora
Maandalizi ya Mpango wa Biashara
Utafutaji masoko
Ubora wa bidhaa
Tathmini ya ujasiriamali ( SWAOC analysis).
(h) Kiwanda cha mafuta ya karafuu na makonyo kimefanikiwa kupeleka
   bidhaa zake katika soko la Marekani chini ya utaratibu wa AGOA.
(i) Kituo cha taarifa za biashara kimeendelezwa kwa kupatiwa vifaa na
   kuanzishwa kwa mtandao wa taarifa za biashara (database).
(j) Usafirishaji wa bidhaa umeongezeka kutoka T.Sh. 15.0 bilioni mwaka
   2006 hadi kufikia T.Sh. 30.0 bilioni mwaka 2010 sawa na ongezeko la
  asillimia 100.
(k) Jumla ya tani 32,910 za karafuu zenye thamani ya US$ 99.16 milioni
   zimesafirishwa kwenda nje ya nchi.
(l) Jumla ya vikundi 159 vya wajasiriamali vilishiriki katika maonyesho tofauti
   yakiwemo ya Sabasaba, Juakali na Kilimo.
(m) Jumla ya viwanda vidogo vidogo na vya kati 10 (SMEs) vimeanzishwa au
   kufufuliwa vikiwemo vya maji, vyakula, nguo, mbao, ukamuaji wa mafuta
  na sukari na kutoa ajira kwa wafanyakazi wapatao 2,334.
(n) Jumla ya miradi ya Uwekezaji 192 yenye thamani ya dola 2.2 bilioni
   imeidhinishwa. Katika miradi hiyo ni Utalii (115), Biashara (17), Viwanda
  (15), Kilimo (6), Mawasiliano (11) na mingineyo 28.
(o) Miundombinu ya maji, umeme, na barabara imefikishwa katika maeneo
   huru ya uchumi ya Fumba na Uwanja wa Ndege ambapo Wawekezaji
  1,010 wameweza kutumia huduma hizo.
(p) Muundo wa Mamlaka ya Uwekezaji umekamilishwa ili kukidhi masharti ya
   Sera na Sheria ya Uwekezaji.
Vyama vya Ushirika
100.
Kusajili SACCOS 313 na vyama vya Ushirika wa uzalishaji 544 pamoja na kutoa
mafunzo ya uendeshaji kwa wanachama 13,790.
69
MIUNDOMBINU YA KIUCHUMI
Barabara
101.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Miundombinu ya barabara ni haya
yafuatayo:-
Mtandao wenye urefu wa kilomita 136.10 za barabara kwa Unguja na Pemba
umekamilika ambazo ni:-
(a)








(b)
Mazizini
Tunguu
Paje
Paje
Mkwajuni
Pongwe
Donge
Mkoani
-
-
-
-
-
-
-
-
Fumba
Kinyasini
Makunduchi
Pingwe
Nungwi
Matemwe
Mkokotoni
Makombeni
Km
Km
Km
Km
Km
Km
Km
Km
18.0
26.8
17.3
16.6
18.4
20.2
12.8
6.0
Mtandao wenye urefu wa kilomita 102.9 za barabara umeanza kujengwa kwa
upande wa Pemba, barabara hizo ni:-










Kengeja
-
Kenya
-
Mizingani
-
Chanjamjawili-
Chanjaaani -
Mtambile
-
Chake
-
Wete
-
Wete
-
Mgagadu
-
Mtambile – Mwambe
Chambani
Wambaa
Tundaua
Pujini
Kangani
Wete
Konde
Gando
Kiwani
Km
Km
Km
Km
Km
Km
Km
Km
Km
Km
9
3.2
10
10
5
6.2
30
15
13
5
(c) Jumla ya kilomita 375.2 za barabara za mjini na vijijini zimefanyiwa
   matengenezo kwa Unguja na Pemba.
(d) Barabara za Mfenesini – Bumbweni Km. 13.2 na Welezo – Dunga Km. 12.7
       kwa upande wa Unguja ujenzi wake umeaanza.
Bandari
102.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Miundombinu ya Bandari ni haya
yafuatayo:-
70
(a) Kukamilisha Mradi wa ujenzi wa gati ya Malindi Unguja, ujenzi wa gati ya
   abiria pamoja na ununuzi wa vifaa vipya vya kubebea makontena (Reach
  Stacker 2 na Terminal Tractor 2).
(b) Kukamilisha ujenzi wa chelezo cha Malindi na kuongeza urefu wake kutoka
   mita 100 hadi mita 140 kuelekea baharini.
(c) Bandari ya Mkoani Pemba imeimarishwa na kutangazwa kuwa ni Mlango
   Mkuu (Entry Point) wa kuingilia meli za kigeni.
(d) Kuifanyia matengenezo gati ya Wete Pemba, na kuongeza urefu wake hadi
   kufikia mita 125 kutoka mita 114; na upana wa mita 6 pamoja na
  kukamilisha ujenzi wa jengo la abiria.
(e) Kukamilisha ujenzi wa ukuta wa kuzuia mmong’onoko wa ardhi ili
     kuimarisha gati ya Wesha-Chake Chake Pemba.
Usafiri wa Baharini
103.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Usafiri wa Baharini ni haya yafuatayo:-
(a)
Shirika la Meli pamoja na Makampuni Binafsi 8, yameendelea kutoa
huduma ya usafiri wa baharini.Makampuni 7 kati ya hayo yanamilikiwa na
Wazanzibari.
(b)
Jumla ya vyombo vya baharini 49, hutoa huduma ya kusafirisha abiria na
mizigo. Kati ya hivyo 21 ni vya abiria, 25 vya mizigo na 3 vya mafuta.
Usafiri wa Anga
104.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Usafiri wa Anga ni haya yafuatayo:-
(a) Kukamilisha maandalizi na kuanza kutekeleza Mpango Mkuu
   Uendelezaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Zanzibar.
wa
(b) Matengenezo ya barabara ya kurukia na kutulia ndege (runway) ya
   Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Zanzibar kilicho na urefu wa mita
  3,022 na upana wa mita 45 na ujenzi wa uzio yamekamilika.
(c) Ununuzi wa mtambo mpya wa kuongozea ndege, magari 2 ya kisasa ya
   zimamoto na gari la kufanyia doria za kiwanja umefanyika.
71
(d) Kukifanyia matengenezo kiwanja cha ndege cha Karume-Pemba, na
   kupatiwa gari la zimamoto.
(e) Kukamilika kwa matayarisho yote ikiwa pamoja na mikataba ya ujenzi wa
   jengo jipya la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Zanzibar.
Umeme
105.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Umeme ni haya yafuatayo:-
(a) Kukamilisha kwa rasimu ya Sera ya Nishati.
(b) Kukamilika kwa Sheria na Kanuni za Uanzishwaji wa Shirika la Umeme.
(c) Kufikisha huduma ya umeme katika vijiji 141, kikiwemo kisiwa kidogo cha
   Kojani Pemba na Uzi Unguja.
(d) Kufikisha huduma ya umeme wa jua katika Kisiwa cha Tumbatu na Uzi
   pamoja na vijiji vya Cheju, Charawe na Matemwe Unguja.
(e) Taaluma ya matumizi ya nishati mbadala imetolewa kwa wananchi wa
   vijiji vya Kiembesambaki, Donge na Bububu.
(f) Kisiwa cha Pemba ambacho kwa muda mrefu kilitumia umeme wa
   “generator” kimeweza kuunganishwa na Gridi ya Taifa na kupata umeme
      wa uhakika kutoka Tanga. Hatua hii imewezesha visiwa vya Unguja na
     Pemba kuwa na umeme wa uhakika wa gridi.
(g) Kazi ya uwekaji wa njia ya pili ya umeme kupitia baharini kutoka Ubungo
   hadi Mtoni chini ya Mradi wa “Millenium Challenge” umewekwa saini.
(h) Kununua magenereta 32 yenye uwezo wa kuzalisha 25 MW kwa ajili ya
   umeme wa akiba.
Ardhi
106.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Ardhi ni haya yafuatayo:-
(a) Kukamilisha maandalizi ya Mpango Mkuu wa Kitaifa wa Matumizi bora ya
   Ardhi.
(b) Kufanya mapitio ya Sheria za Ardhi, ikiwemo Sheria ya Mahkama ya Ardhi
   (Land Tribunal Act) na Sheria ya Uhaulishaji wa Ardhi (Land Transfer Act)
  ya Mwaka 1994.
72
(c) Kufanya usajili wa ardhi katika eneo la Mji Mkongwe ambapo Viwanja 795
   vimesajiliwa na kupatiwa hati rasmi.
(d) Kuanzisha Mahkama ya Ardhi, ili kutatua migogoro ya ardhi na kupunguza
   msongomano wa kesi za ardhi katika mahkama za kawaida.
(e) Kupima viwanja katika maeneo ya Tunguu, Kiwengwa na Nungwi Unguja,
   Tumbe na Ole-kianga kwa Pemba, kwa ajili ya makaazi bora na kilimo.
  Jumla ya viwanja 4,181 vimepima na kugawiwa kwa wananchi kwa ajili ya
 makazi, vikiwemo viwanja 308 kwa ajili ya shughuli za uwekezaji hususan
ujenzi wa hoteli za kitalii, viwanda, kilimo na shughuli za kijamii.
SEKTA YA HUDUMA ZA JAMII
Elimu
107.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Elimu ni haya yafuatayo:-
(a) Sera ya Elimu imepitishwa. Elimu ya lazima sasa ni miaka 12 ambapo
   elimu ya maandalizi ni miaka 2, msingi miaka 6 na sekondari miaka 4.
(b) Uandikishaji wa watoto waliofikia umri wa kuanza darasa la kwanza
   umeongezeka kutoka asilimia 100 mwaka 2005, hadi asilimia 106.8
  mwaka 2010. Mafanikio haya yameiwezesha Zanzibar kuvuka kiwango cha
 lengo la Milenia kabla ya mwaka 2015.
(c) Wananchi wamehamasishwa kuchangia ujenzi wa skuli mpya na kuongeza
   madarasa katika maeneo yao. Jumla ya madarasa 910 yamejengwa
  katika maeneo mbalimbali Unguja na Pemba.
 Ujenzi wa kituo cha Elimu Mbadala kiliyopo Rahaleo Unguja, umekamilika.
Kituo kimefunguliwa tarehe 6 Juni 2006, na kuanza kutoa mafunzo ya
kompyuta, uchongaji, upishi na ushoni.
(d)
(e) Ujenzi wa kituo cha Mafunzo ya Amali cha Mkokotoni Unguja na Vitongoji
   Pemba, umekamilika. Vituo hivi vinatoa mafunzo ya
  fani za ufundi,
 ufugaji, ushoni, useremala na kilimo.
(f) Ujenzi wa Maktaba Kuu ambao ulisimama kwa kipindi kirefu umekamilika.
   Maktaba hiyo imeanza kutoa huduma.
(g) Mafunzo ya Diploma ya Msingi yamenzishwa katika Vyuo vya Ualimu
   (badala ya cheti). Hatua hii imeimarisha ufundishaji katika ngazi ya Elimu
  ya Msingi na kutayarisha walimu bora.
73
(h) Vituo vya ualimu vimeimarishwa na kupatiwa vifaa vya kufundishia
   vikiwemo vitabu pamoja na kompyuta, ili viweze kutoa huduma kwa
  walimu kwa ufanisi.
(i) Chuo cha Ufundi cha Karume-Mbweni, kimepandishwa hadhi na kuwa
   “Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia”.
(j) Ujenzi wa majengo mapya ya Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) umeanzishwa
   huko katika eneo la Tunguu mkoa wa Kusini Unguja.
Afya
108.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Afya ni haya yafuatayo:-
(a) Kuifanyia mapitio Sera ya Dawa (National Drug Policy) na kuanzisha
   Sheria ya Dawa (Pharmaceutical Act) pamoja na Baraza la Tiba Asili na
  Tiba Mbadala.
(b) Kuimarisha Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwa kuzifanyia ukarabati
   sehemu muhimu na kuanzisha huduma ya Matibabu ya Haraka (Fast
  Track) pamoja na kuipatia vifaa vya kisasa (Mashine za X-Ray, CT Scan,
 Fluoroscopy, Ultra Sound, na Echo- Cardiography).
(c) Kuimarisha sehemu ya matibabu ya macho kwa kuifanyia ukarabati na
   kuipatia vifaa vya kisasa (AB Scan, automatic Torometer, Slit Lamp
  Machine, Electronic Operation Microscope na Phaco Emulsification
 Machine).
(d) Kujenga maabara mpya ya damu salama katika eneo la Sebleni Unguja.
(e) Kujenga jengo jipya la huduma kwa waathirika wa UKIMWI VCT (Gold
   Standard) na kuanza kutoa tiba ya ARV kwa waathirika wa UKIMWI katika
  vituo vya Kivunge, Bububu, Mwembeladu na Alrahma kwa Unguja na
 Chake Chake, Wete na Micheweni kwa Pemba.
74
(f) Kuimarisha huduma za hospitali ya Chake Chake na kuipatia mashine za
   kuchunguza VVU, ECG pamoja na vifaa vya upasuaji. Aidha, hospitali ya
  Wete imepatiwa “Solar Power” pamoja na sehemu ya kuhifadhia damu.
(g) Kuanzisha Mpango Maalumu wa huduma za afya na tiba ya macho, koo,
   pua na masikio vijijini kwa kutumia basi maalumu (mobile theatre).
(h) Kuanzisha chanjo ya kipindupindu katika Shehia ya Mtopepo, Chumbuni
   na Karakana kwa Unguja na Mwambe, Kengeja na Kojani kwa Pemba.
  Jumla ya wananchi 33,898 sawa na asilimia 65.2 ya wakaazi wa Shehia
 hizo wamepatiwa chanjo hiyo.
(i) Kuendeleza mapambano dhidi ya malaria kwa kufukiza dawa ya mbu
   majumbani na kugawa vyandarua vyenye dawa kwa watoto walio chini ya
  umri wa miaka mitano. Hatua hii imeiwezesha Zanzibar kuudhibiti
 ugonjwa huo kwa kiwango cha asilimia 98.
(j) Kuanzisha Mpango Maalum (Road Map) kwa ajili ya kupunguza idadi ya
   vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na vituo vya Afya ya msingi
  vya daraja la pili (PHCU+) kuanza kutoa huduma za uzazi salama. Vituo
 hivyo ni Fuoni, Jambiani, Muyuni, Uzini, Nungwi, Bumbwini Misufini,
Tumbatu kwa Unguja na Bogoa, Pujini Wesha na Makangale kwa Pemba.
(k) Kuendeleza Kampeni ya chanjo ya surua kwa watoto wenye umri wa miezi
   6 hadi miaka 10 na utoaji wa matone ya Vitamin A kwa watoto wenye
  umri wa kati ya miezi 6-59 kwa kiwango cha asilimia 95%.
(l) Kujenga vituo vipya vya afya 43 vya daraja la kwanza, kuvifanyia
   matengenezo makubwa vituo 10 vya daraja la pili na kuvijenga upya vituo
  11 vya daraja la pili, Unguja na Pemba.
(m) Kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya daraja la pili ya Jimbo la Mpendae.
(n) Kupitisha Sheria ya Mdawa ya Kulevya ili kudhibiti uingizwaji na utumiaji
   wa madawa hayo nchini, na kulinda afya za wananchi hususan vijana.
75
(o)
Kukiimarisha Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni. Aidha, kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha Matansas cha Cuba, madarasa mawili
ya madaktari wanafunzi yameanzishwa (darasa la wanafunzi 38 Unguja na
wanafunzi 13 Pemba).
Maji
109.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Maji ni haya yafuatayo:-
(a) Kukamilisha maandalizi ya Sera ya Maji inayozingatia dhana ya
   ushirikishwaji wa wananchi katika kuchangia huduma za maji pamoja na
  Sheria ya Maji ya Mwaka 2007.
(b) Kuanzisha Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA).
(c) Kukamilisha Awamu ya Kwanza ya Mradi wa Usambazaji Maji katika mkoa
   wa Mjini Magharibi kwa kuchimba visima 11, kujenga matangi 4 ya
  kuhifadhia maji na miundombinu mipya ya usambazaji maji.
(d) Kukamilisha Mradi wa Usambazaji Maji Vijijini na kufikisha huduma ya maji
   safi na salama katika kijiji cha Kigongoni, Kilimani Tazari, Kilindi, Dunga,
  Kikungwi, Mfumbwi, Kidimni, Ubago,
 Mfenesini, Bumbwini, Kitope,
Melinne, Welezo, Koani na Dungabweni kwa Unguja.
(e) Kukamilisha Mradi wa Usambazaji Maji Vijijini na kufikisha huduma ya maji
   safi na salama kijiji cha
  Pondeani, Gombani, Maziwang’ombe,
   Kiuyumbuyuni, Kwa Pweza, Kwa Bi Mtumwa, Kwale, Michungwani,
  Kiguuni, Shamiani, Kengeja, Mwambe, Mlindo, Mgelema, Mkungu,
 Kijichame Ngwachani, Kiuyu Momongawa, Nyali Shumbamjini,Wete Mjini,
Bagamoyo, Kiuyu Penjewani, Mtambwe Kaskazini, Mtambwe Kivumoni,
Ole kianga, Junguni na Gando kwa Pemba.
(f) Kufikisha huduma maji safi na salama kwa wananchi waishio mijini kwa
   kiwango cha asilimia 75 na wananchi wa vijijini kwa kiwango cha asilimia
  60 Unguja na Pemba.
Makazi
110.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Makazi ni haya yafuatayo:-
76
(a) Kuandaa Sera ya Taifa ya Nyumba, ambayo inazingatia tasnia ya ujenzi
   na kuanzisha Bodi ya Kusajili Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji wa
  Majengo na Bodi ya Kusajili Wakandarasi.
(b) Kukamilisha ujenzi wa Nyumba Namba 9 na 10 Michenzani zenye jumla ya
   fleti 166 (24+142) na kuzigawa kwa wananchi wanaostahiki.
(c) Kuanza ujenzi wa nyumba moja ya Maendeleo huko Bambi,
   kukwama kwa muda mrefu.
baada ya
MAENEO MENGINE YA KIPAUMBELE
Utamaduni na Michezo
111.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Utamaduni na Michezo ni haya yafuatayo:-
(a) Kuifanyia mapitio Sheria ya Baraza la Taifa la Michezo.
(b) Kuajiri walimu wa kigeni ili kufundisha na kukuza vipaji vya wanamichezo
   hasa wa mipira wa miguu, mpira wa kikapu, riadha na judo.
(c) Kuufanyia matengenezo makubwa uwanja wa Amani na kuimarisha
   miundombinu ya umeme katika uwanja wa Gombani Pemba.
(d) Kuanzisha ujenzi wa kituo cha michezo huko Dole.
(e) Kuandaa na kuendesha Matamasha ya Utamaduni kama vile ZIFF, SAUTI
   YA BUSARA, MKONGWE HAGEWA, MWAKA-KOGWA na “ZANZIBAR MUSIC
    AWARDS”.
(f) Kuvipatia fursa vikundi vya utamaduni hasa ngoma na taarabu asilia,
   kutumbwiza kwenye hoteli mbalimbali za kitalii, ili kukuza na kuendeleza
  utalii wa kiutamaduni.
Vyombo vya Habari
112.
Mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Vyombo vya Habari ni haya yafuatayo:-
77
(a) Kuaandaa Sera ya Habari na Utangazaji, Shirika la Magazeti ya Serikali na
   Tume ya Utangazaji.
(b) Kuimarisha Studio za TVZ na Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) kwa
   kuzipatia mitambo mipya na vifaa vya kisasa.
(c) Kupitisha Sheria ya kuanzisha Chuo cha Uandishi wa Habari na kuanza
   kutoa mafunzo ya Diploma ya Uandishi wa Habari.
(d) Kuanzisha vituo 4 vya Televisheni na 8 vya Radio vya binafsi.
Majanga na Huduma za Uokozi
113.
Mafanikio yaliyofikiwa katika kuimarisha udhibiti wa Majanga na Huduma za
Uokozi ni haya yafuatayo:-
(a) Kukiimarisha Kikosi cha Zimamoto na Uokozi kwa mafunzo ya kazi na
   uongozi nje ya nchi (Uingereza, China na India) na vifaa vya kisasa
  zikiwemo gari 12. Kati yake 10 za zimamoto na 2 za kubebea wagonjwa.
(b) Kuanzisha Kitengo cha Taifa cha Maafa na Kamati za Maafa za Mikoa na
   Wilaya.
Demokrasia na Utawala Bora
114.
Mafanikio yaliyofikiwa katika kukuza Demokrasi na Utawala Bora ni haya
yafuatayo:-
(a) Kuridhia Sheria ya Bunge ya Uanzishwaji wa Tume ya Haki za Binadamu
   na Utawala Bora na kuiwezesha Tume hiyo kufanya kazi zake Zanzibar.
(b) Kuanzisha ujenzi wa ukumbi mpya wa Baraza la Wawakilishi.
(c) Kukamilisha ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar.
(d) Kuanzisha Kitengo Maalumu cha kupokea malalamiko ya wananchi.
(e) Kuanzisha Kamati ya pamoja ya viongozi wa dini tofauti ili kujenga
   mshikamano miongoni mwa viongozi na waumini wa dini ya Kiislamu na
  wa dini nyingine.
(f) Kuanzisha kanuni ya adhabu ya kutumikia jamii kwa wahalifu wa makosa
   madogo madogo, ili kupunguza msongamano katika Vyuo vya Mafunzo.
78
Serikali za Mitaa
115.
Mafanikio yaliyofikiwa katika kuimarisha Serikali za Mitaa ni haya yafuatayo:-
(a) Kukamilisha ujenzi wa majengo mapya ya ofisi za Mabaraza ya Miji ya
   Chake Chake, Wete, Mkoani pamoja na Halmashauri za Wilaya.
(b) Kukamilisha ujenzi wa soko la Wafanyabiashara wadogo wadogo la
   Saateni-Unguja.
(c) Kukamilisha ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua katika Manispaa ya
   Zanzibar.
(d) Serikali Kuu kuendelea kutoa ruzuku kila mwezi kwa Baraza la Manispaa
   ya Zanzibar (Tshs. 100.6 milioni), Baraza la Mji wa Chake, Wete, Mkoani
  (Tshs. 59.25 milioni) na Halmashauri za Wilaya (Tshs. 15.66).
(e) Wananchi wamehamasishwa kushiriki katika ulinzi wa maeneo yao kwa
   njia ya ulinzi wa umma na Polisi Jamii. Aidha, Kamati za Ulinzi na
  Usalama za kila Shehia zimeundwa.
Vikosi Maalumu vya SMZ
116.
Mafanikio yaliyofikiwa katika kuimarisha Vikosi Maalumu vya SMZ ni haya
yafuatayo:-
(a) Vikosi vyote vya SMZ vimeimarishwa kwa kupatiwa mafunzo ndani na nje
   ya nchi katika fani ya utawala na uongozi, sheria, fedha, mawasiliano ya
  kompyuta, ufundi na afya.
(b) Aidha, vikosi vimeimarishwa kwa kupatiwa zana na vifaa vya kisasa.
KUYAENDELEZA MAKUNDI MBALIMBALI
Watoto
117.
Kwa upande wa maendeleo ya watoto mafanikio yafuatayo yamefikiwa:-
(a) Kuandaa Sera ya Uhai, Hifadhi na Maendeleo ya Watoto.
(b) Kuifanyia marekebisho Sheria ya Ajira ili kuwalinda watoto dhidi ya ajira
   mbaya.
79
(c) Kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Ajira Mbaya kwa Watoto
   na kuanzisha Kamati za Kupambana na Ajira Mbaya katika maeneo
  yaliyoathiriwa na tatizo hilo. Hatua hii imewezesha zaidi ya watoto 1,000
 kuondolewa katika ajira mbaya.
(d) Kuanzisha Sera ya Elimu ambayo inayoanzisha Elimu ya Awali (Elimu ya
   Msingi) ya miaka 6 na umri wa watoto kuanza darasa la kwanza ni miaka
  6 badala ya miaka 7.
(e) Huduma za chanjo ya surua kwa watoto wanaoanzia umri wa mia 6 hadi
   miaka 10 na kiwango cha utoaji wa matone ya Vitamin A kwa watoto
  wenye umri wa kati ya miezi 6–59 nacho kimefikia asilimia 95.
(f) Kuanzisha mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Watoto yatima Mazizini Unguja.
Vijana
118.
Kwa upande wa maendeleo ya Vijana mafanikio yafuatayo yamefikiwa:-
(a) Kuandaa Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2005, Sera ya Ajira
   pamoja na Sheria ya Kazi, ambayo inatoa mwongozo kwa vijana
  kuunganisha nguvu zao na kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali ili kuweza
 kujiajiri wenyewe.
(b) Kutoa mafunzo ya ujasiriamali ndani na nje ya nchi pamoja na kupatiwa
   vijana fursa ya kushiriki katika maonyesho ya Kimataifa yanayohusu
  biashara na kilimo.
(c) Kutenga maeneo maluumu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafunzo ya
   ujasiriamali kama vile ushonaji, kilimo, uvuvi, useremala na utalii.
Wanawake
119.
Kwa upande wa maendeleo ya Wanawake mafanikio yafuatayo yamefikiwa:-
(a) Serikali imeendelea kupiga vita mila na desturi zinazowabagua wanawake
   pamoja na kusimamia Sheria na Mikataba ya Kimataifa inayohusu ustawi
  wa wanawake kwa kuifanyia marekebisho Sheria Namba 4 ya Mwaka
 1995 ya kuwalinda wari, wajane na vizuka. Lengo la Sheria hiyo ni
kulinda haki zao.
(b) Kuwapatia mafunzo Waratibu wa Maendeleo ya Wanawake na Watoto wa
   Wilaya yanayohusu sheria, haki za binadamu, mkataba wa kimataifa wa
  kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake na UKIMWI.
80
(c)
Vikundi mbalimbali vya wanawake vimepatiwa mikopo kupitia Mifuko ya
Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi pamoja na mafunzo ya ujasiriamali.
CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA
120.
Mbali na mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii, uchumi wa Zanzibar ulipata
pigo kutokana na kuchakaa kwa njia ya umeme chini ya bahari inayounganisha
Zanzibar na gridi ya Taifa kutoka Tanzania Bara na kusababisha kukatika kwa
umeme mwezi Machi, mwaka 2008 na mwezi Novemba 2009. Aidha, ukame na
hali ya kudorora kwa uchumi wa dunia mwanzoni mwa mwaka 2009 ni miongoni
mwa changamoto kubwa zilizojitokeza katika kipindi hiki na kudhoofisha uwezo
wa Serikali katika kuendeleza huduma muhimu za kiuchumi na kijamii kwa
wananchi.
MALENGO YA ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA
2010-2015
121.
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM ikipata ridhaa ya
wananchi itaiongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kuhakikisha kwamba,
inatekeleza kikamilifu malengo ya Ilani hii na kuaandaa mipango mbalimbali ya
maendeleo kwa kuzingatia Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2010 hadi
2020, Malengo ya Maendeleo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar (2020)
na Awamu ya Tatu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini
Zanzibar (MKUZA).
SEKTA YA KIUCHUMI
Kukuza Uchumi
122.
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015), CCM itahakikisha kwamba
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, inaendeleza mafanikio yote ya kiuchumi
yaliyofikiwa hadi sasa zikiwemo Sera na Sheria za Uwekezaji, ili kuchochea kasi
ya uwekezaji na ujenzi wa msingi wa uchumi endelevu unaokua na kuendeshwa
kwa nguvu ya soko na kutekeleza hatua zifuatazo:-
(a) Kujenga mazingira yatakayowezesha uchumi wa Zanzibar kufikia kiwango
   cha ukuaji wa asilimia 10, mfumko wa bei kufikia kiwango cha chini cha
  asilimia 7 na pato la kila mwananchi kuongezeka kutoka Tsh. 726,000/=
 za sasa hadi Tsh. 884,000/= ifikapo mwaka 2015.
(b) Kuimarisha udhibiti wa mapato na matumizi ya Serikali, kuziba mianya ya
   uvujaji wa mapato ya Serikali na kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa
81
mapato ya ndani kwa uwiano wa asilimia 22 ya pato la taifa na kushusha
kiwango cha nakisi ya Bajeti ya Serikali kutoka uwiano wa asilimia 9.2 ya
pato la taifa (mwaka 2007/2008) na kufikia asilimia 8.0 ifikapo mwaka
2014/2015.
(c) (d)
123.
Kusimamia utekelezaji wa sheria za fedha ikiwemo Sheria ya Kodi na
Makampuni na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi.
Kuendeleza juhudi za kuimarisha maeneo huru ya kiuchumi ya Fumba na
Micheweni pamoja na Bandari huru.
Kuendeleza jitihada za kuimarisha sekta binafsi ili kuongeza mchango wake
katika uwekezaji kutoka asilimia 45 mwaka 2009 hadi asilimia 75 mwaka 2015.
Hatua zifuatazo zitatekelezwa:-
(a) Kufanya mapitio ya sheria na kanuni za biashara ili kuimarisha uwazi,
   kupunguza urasimu na vikwazo katika biashara ukiwemo mlolongo wa
  Leseni na Mamlaka za kodi.
(b) Kuwa na uwakilishi wa sekta binafsi kwenye vikao vya baadhi ya Bodi za
   Mashirika na Taasisi za Serikali zenye kutoa huduma za kiuchumi na
  kupanga kodi mbalimbali za biashara, ili kujenga mahusiano mema, kuleta
 ufanisi na tija katika makusanyo ya kodi na kukuza uchumi wa nchi kwa
ujumla.
(c) Kuandaa mazingira bora ya kiuchumi yatakayoweza kuvishawishi vyombo
   vya fedha kutoa mikopo yenye masharti na riba nafuu kwa wawekezaji wa
  ndani.
(d) Kuendeleza utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi (Zanzibar Growth
   Strategy), Awamu ya Tatu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
  Umasikini Zanzibar (MKUZA) pamoja na kutekeleza mageuzi ya kiuchumi
 hususan sera ya Fedha, Kilimo, Viwanda vidogo na Biashara.
Kupambana na Umasikini
124.
Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2010-2020 unabainisha kuwa,
mkakatia wa kuwawezesha wananchi kiuchumi umelenga katika kuhakikisha
kwamba wananchi wenyewe wanamiliki na kuendesha uchumi wa nchi yetu ama
mmoja mmoja kwa kupitia vyama vyao huru vya ushirika wa aina mbalimbali au
kwa kupitia makampuni ya wananchi ya ubia ambamo maelfu ya wananchi
watanunua hisa na kwa kupitia umilikaji wa dola kwa mashirika yote
yatakayoendelea kuwa mikononi mwake.
82
125.
Kwa kutambua kwamba, wananchi walio wengi bado ni masikini na wanakabiliwa
na tatizo la ukosefu wa maarifa, ujuzi na mitaji katika kilimo, biashara na
ujasiriamali hali ambayo ni kizuizi cha maisha bora na mapambano dhidi ya
umasikini, CCM itaielekeza Serikali (SMZ) kuendeleza jitihada za kuwawezesha
wananchi kiuchumi kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendeleza mafunzo na elimu ya ujasiriamali kwa wananchi na
   kuhamasisha matumizi ya kanuni za kilimo bora na Sayansi na Teknolojia
  rahisi katika uzalishaji mali.
(b) Kuendeleza utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi
   na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA).
(c) Kuimarisha Mifuko ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi ili kukuza
   uwezo wake wa kutoa mikopo kwa wananchi na kuwawezesha kutumia
  fursa zilizopo katika maeneo wanayoishi ili kujiendeleza kiuchumi.
(d) Kuendelea kuunga mkono juhudi za uanzishwaji wa vikundi vya ushirika
   na SACCOS hasa kwa vijana na akina mama.
  Kuyaendeleza maeneo maalumu ya kufanyia shughuli za biashara ndogo
 ndogo hasa mijini na kuimarisha mfumo na taratibu za utoaji wa leseni za
biashara wenye kuzingatia usafi wa miji na hifadhi ya mazingira.
(e)
(f)
Kutilia mkazo dhana ya kujitegemea kwa kuzitambua rasilimali na biashara
za wanyonge ambazo ziko kwenye sekta isiyo rasmi ili waweze
kuziendeleza kuboresha maisha yao.
KUHUSU SEKTA ZA UZALISHAJI MALI
Mapinduzi ya Kilimo
126. Sekta ya kilimo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi na maendeleo ya
    Zanzibar. Kilimo ndio chanzo kikuu cha ajira kwa wananchi walio wengi hasa
   vijijini, na huchangia asilimia 27.3 ya Pato la Taifa (GDP) katika uchumi wa
  Zanzibar na kutoa ajira kwa asilimia 44 ya wananchi wa vijijini.
127. Kwa kutambua umuhimu na mchango wa sekta ya kilimo katika kujenga msingi
    wa uchumi wa kisasa, katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2010-2015) Serikali
   ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa CCM, itaendelea kuimarisha
  Mapinduzi ya kilimo kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a)
Kusimamia utekelezaji wa Sera na Programu mbalimbali za Kilimo na
kuzifanyia mapitio kwa lengo la kuziimarisha. Aidha, Sera ya Chakula na
Lishe na Sera ya Mifugo zitaanzishwa.
83
(b) Kuendelea kuhimiza na kutilia mkazo mafunzo na matumizi ya kanuni za
   kilimo bora kwa mazao ya chakula, biashara na matunda, huduma za
  ugani na zana za kisasa wakiwemo wanyamakazi, matrekta makubwa na
 madogo.
(c) Kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji maji na kuhamasisha uvunaji wa
   maji ya mvua, ili yatumike katika kuzalisha mazao mengi ya chakula na
  mboga mboga kwa njia ya umwagiliaji maji.
(d) Kuihamasisha sekta binafsi kutoa huduma ya pembejeo katika maeneo ya
   kilimo.
(e) Kuendelea kukiimarisha Chuo cha Kilimo Kizimbani na kuendeleza utafiti
   wa mbegu bora za mazao ya chakula, biashara na mboga mboga. Njia ya
  utafiti shirikishi itatumika kwa lengo la kuwawezesha wakulima kushiriki
 kikamilifu katika kutoa mawazo yao kuhusiana na matatizo
yanayowakabili.
(f) Kuanzisha mradi maalumu wa kuwawezesha wananchi na sekta binafsi
   kuingia katika kilimo cha kisasa na cha kibiashara cha mazao ya viungo na
  matunda.
(g) Kuendeleza vituo vya huduma na udhibiti wa maradhi ya mazao, wadudu
   waharibifu na elimu kwa wakulima kuhusu hifadhi ya mazao na utafutaji
  wa masoko ya ndani na nje kwa kutumia Nembo ya Zanzibar.
(h) Kuendeleza uzalishaji wa mazao ya biashara hasa karafuu, matunda na
   viungo na kutilia mkazo kilimo hai na kilimo mseto, ili kuhifadhi mazingira
  na kupunguza matumizi ya kemikali zenye sumu kali kwa lengo la
 kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo hadi kufikia asilimia nne (4%)
ifikapo 2015.
(i) Kuendeleza kazi ya ukaguzi na karantini dhidi ya maradhi na wadudu
   waharibifu wa mimea na mfugo ili kudhibiti uingiaji nchini wa maradhi
  hayo.
Mapinduzi ya Ufugaji
128.
Kuleta mapinduzi ya ufugaji Zanzibar si tu kunazingatia tija na ubora wa mazao
ya mifugo, bali vile vile tatizo la uhaba wa ardhi, ongezeko la idadi ya watu na
kupanuka kwa shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika
ardhi ambayo ukubwa wake hauongezeki.
84
129.
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
chini ya uongozi wa CCM itaendelea kuimarisha ufugaji wa kisasa wa ng’ombe
wa maziwa, mbuzi na kuku wa nyama na mayai ili kuongeza tija na kipato cha
wafugaji, kwa kutekeleza hatua zifuatazo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Mifugo pamoja na programu
   za miradi mbalimbali itakayowawezesha wafugaji wadogo kuendeleza
  ufugaji wa kisasa (Zero-grazing) na kuongeza uzalishaji wa nyama,
 maziwa, ngozi na mayai kwa ajili ya mahitaji ya soko la ndani na nje ya
Zanzibar.
(b) Kuendeleza kazi za utafiti na upandishaji wa ng’ombe kwa njia ya
     sindano, ili kupata mbegu bora ya ng’ombe wa maziwa na nyama na
      kuwagawia wafugaji wadogo kwa njia ya mkopo.
(c) Kuendeleza Vituo vya Huduma za Ufugaji na huduma za kinga na tiba ya
   mifugo na kuihamasisha sekta binafsi kutoa huduma za afya na pembejeo
  za mifugo.
Mapinduzi ya Uvuvi na Mazao ya Baharini
130. Kwa kuzingatia maumbile na jiografia ya Zanzibar, uvuvi ni shughuli muhimu ya
    kiuchumi miongoni mwa wananchi wengi wanaoishi pembezoni mwa mwambao
   wa bahari. Kutokana na ukosefu wa zana bora za uvuvi, wavuvi wadogo wadogo
  wamekuwa wakitumia zana duni ambazo husababisha uharibifu mkubwa wa
 mazingira.
131. Ili kuimarisha uvuvi wa kisasa ambao ni endelevu na unaozingatia uhifadhi wa
    mazingira ya bahari na kukuza kipato cha wavuvi, CCM kupitia Ilani hii itaielekeza
   Serikali kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuandaa Sera ya Uvuvi na kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Uvuvi kwa
   lengo la kuimarisha uvuvi na uhifadhi wa mazingira ya bahari.
(b) Kuendelea kuwahamasisha wavuvi juu ya uanzishaji wa vikundi vya
   ushirika na matumizi ya maarifa ya kisasa na zana bora za uvuvi na
  kuwapatia misaada na mikopo ya zana hizo, ili uvuvi uwe wa kisasa zaidi
 utakaokidhi mahitaji ya soko la ndani.
(c) Kusimamia mpango shirikishi wa kuyaendeleza maeneo ya hifadhi ya
   bahari yakiwemo maeneo mapya ya Tumbatu, Chumbe-Bawe, Menai,
  MIMCA na PECCA.
(d) Kujenga mazingira ya kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika uvuvi wa
   bahari kuu, ujenzi wa kiwanda cha samaki na zana za kisasa za uvuvi.
85
(e) Kufanya utafiti juu ya uwezekano wa kulima mwani aina ya “cottonii”
       kwenye kina kirefu cha maji na kuwahamasisha wananchi kuanzisha
      vikundi vya ushirika ili kurahisisha upatikanaji wa nyenzo za uzalishaji na
     soko la uhakika. Aidha, wananchi watahamasishwa kuanzisha vikundi vya
    ufugaji wa chaza ili kupata lulu na kuongeza kipato cha kuwawezesha
   kupambana na umasikini.
(f) Kuendeleza uhifadhi wa viumbe hai na adimu vya baharini (pomboo, kasa
   n.k) na kuvitumia kama vivutio vya utalii.
Maliasili
132.
Maumbile ya Visiwa vya Unguja na Pemba yamesheheni utajiri mkubwa wa
maliasili ambao ni kivutio cha watalii. Ili kuiendeleza zaidi sekta ya misitu, katika
kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM itaielekeza Serikali kutekeleza
yafuatayo:-
(a) Kusimamia ulinzi na udhibiti wa maeneo ya hifadhi ya misitu ya Taifa ya
   Jozani, Unguja na Ngezi, Pemba pamoja na misitu ya asili kwa
  mashirikiano na wananchi na wadau mbalimbali.
(b) Kuendeleza utunzaji na hifadhi ya wanyama pori walio katika hatari ya
   kutoweka hasa kimapunju, popo wa Pemba na paa nunga na kuwatumia
  kama vivutio vya utalii.
(c) Kuendelea kuwahamasisha wananchi na kuwahimiza wajiunge pamoja
   kuanzisha vikundi vya jamii vitakavyopatiwa mafunzo ya utunzaji na
  upandaji miti katika maeneo wanayoishi na pembezoni mwa barabara,
 ufugaji wa nyuki na uvunaji wa asali.
Mazingira
133. Mazingira ni suala mtambuka ambalo linagusa sekta zote za kiuchumi na kijamii.
    Hivyo, uharibifu wa mazingira ni tishio la taifa zima na mazingira endelevu ni
   muhimu kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.
134. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM kupitia Ilani hii
    itahakikisha kuwa, Serikali inatekeleza yafuatayo:-
(a) Kuandaa Sera ya Mazingira na kusimamia utekelezaji wa Mpango wa
   Hifadhi ya Mazingira katika maeneo ya ardhi, bahari na ukanda wa pwani.
(b) Kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa hifadhi ya
   mazingira na kuimarisha ukaguzi katika maeneo ya makazi na sehemu za
  kazi, viwanda na mahoteli.
86
(c)
Kufanya mapitio ya miradi ya vitega uchumi ili kuangalia masuala ya
mazingira na kupendekeza hatua za utekelezaji.
Utalii
135. Zanzibar ni miongoni mwa Visiwa vyenye historia na vivutio vingi vya utalii.
    Fukwe mwanana, misitu ya asili, wanyama, magofu na urithi wa Kimatifa wa Mji
   Mkongwe wa Zanzibar ni miongoni mwa vivutio hivyo.
136. Ili kuendeleza sekta ya utalii na kuifanya itoe mchango mkubwa zaidi katika
    uchumi wa Zanzibar na maendeleo ya wananchi kwa jumla, katika kipindi cha
   miaka mitano ijayo (2010-2015), Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi
  wa CCM, itatekeleza yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Mpango Mkuu wa Utalii na
   kufanya mapitio ili kuziimarisha kwa kuandaa kanuni za utekelezaji wake.
(b) Kuendeleza jitihada za kuitangaza Zanzibar katika masoko mapya hasa ya
   Asia, ili kuongeza mapato ya utalii na kuchukua hatua za kudhibiti mianya
  ya uvujaji wa mapato, yakiwemo mapato ya utalii wa vikundi (package
 tourism).
(c) Kuendeleza na kuimarisha utalii wa kumbukumbu za kihistoria, utalii wa
   kiutamaduni na utalii wa ndani wenye kutunza mazingira.
(d) Kuibua maeneo mapya ya vivutio vya utalii yakiwemo mapango, michezo
   ya asili, matamasha, maeneo ya hifadhi ya wanyama (Zoo), “Aquarium”
      na kijiji kilichozama Mkumbuu kisiwani Pemba na kuongeza idadi ya
     watalii na muda wa kukaa nchini.
(e) Kufanya uhakiki wa hoteli ili kubaini hali halisi ya kila hoteli, kupanga
   madaraja yake, kuzisajili na kuanzisha mfumo wa mawasiliano ya
  komputa kwa lengo la kuimarisha huduma, gharama na mapato ya
 Serikali.
(f) Kuimarisha huduma za utalii kwa kuziendeleza Jumuiya za watoa huduma
   kama vile watembezaji na wasafirishaji watalii wakiwemo “Tour
    Operators”, wenye gari za Taxi na boti ziendazo kasi.
(g) Kuhamasisha wananchi kuendeleza miradi ya uzalishaji mali, hususan
   kilimo cha kisasa cha mboga mboga na matunda ili kuhudumia sekta ya
  utalii na kujiendeleza kiuchumi.
87
(h) Kupunguza idadi ya vituo vya ukaguzi katika maeneo wanayopita watalii ili
   kuwaondolea usumbufu na kuandaa vijarida vya taarifa za watalii na
  maelekezo katika maeneo ya kuingilia “Entry Points”.
(i) Kukiimarisha Chuo cha Maendeleo ya Utalii kwa kuboresha miundombinu
   yake, kuandaa Dira ya Chuo, kuboresha viwango vya elimu ya wakufunzi
  na huduma kwa wanafunzi.
Mapinduzi ya Viwanda na Biashara
137. Sekta ya Viwanda na Biashara ni yenye umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya
uchumi na ustawi wa wananchi. Ili kuendeleza shughuli za viwanda na biashara
na kuinua uchumi wa Zanzibar, CCM katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-
2015) itaielekeza Serikali kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Uendelezaji wa Viwanda Vidogo na vya
   Kati na kufanyia mapitio Sheria ya Biashara ya Mwaka 2006 ili kubaini
  mapungufu na kuchukua hatua zinazopasa pamoja na kuweka mfumo
 bora zaidi wa utoaji wa leseni za biashara .
(b) Kuwaendeleza wawekezaji, wazalishaji wa ndani na wajasiriamali wadogo
   na wa kati (SMEs) kwa kuwapatia fursa za mafunzo, mikopo ya fedha na
  vifaa vya kisasa vya uzalishaji mali ili kuzalisha bidhaa bora kwa ajili ya
 soko la ndani na nje ya nchi.
(c) Kufanya mapitio ya vivutio vya uwekezaji ili kuviendeleza na kuimarisha
   mtandao wa usambazaji wa habari za biashara kwa wafanyabiashara.
  Wawekezaji wenye mitaji mikubwa hasa kutoka nje watahamasishwa
 kuwekeza katika miundombinu na viwanda vinavyozalisha ajira nyingi
vikiwemo vya nguo na usindikaji wa mazao.
(d) Kufanya mapitio ya Sheria Namba 2 ya Kusimamia Mwenendo wa Biashara
   na Kumlinda mlaji ya Mwaka 1995, Sheria Namba 4 ya Mizani na Vipimo
  ya Mwaka 1983 na Sheria ya Biashara Namba 4 ya Mwaka 1989.
(e) Kuanzisha Taasisi ya Viwango ya Zanzibar.
(f) Kufanya utafiti ili kubaini maeneo ambayo wawekezaji wageni watavutiwa
   kuingia ubia na wafanyabiashara wa ndani na kuwawezesha
88
wafanyabiashara wazalendo kupata mitaji kutoka katika vyombo vya
fedha kwa riba nafuu.
(g) Kufanya utafiti utakaowezesha usarifu wa zao la karafuu kutengeneza
   dawa na aina nyingine za matumizi ya zao hilo kwa kukitumia Kiwanda
  Cha Makonyo kilichoko Pemba.
(h) SMZ kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na sekta
   binafsi, itaanzisha mchakato wa kujenga viwanda vinavyotumia malighafi
  inayopatikana hapa nchini hususan viwanda vya nguo, samaki, sukari,
 viwanda vya kuunganisha mitambo ya aina mbalimbali na vya kusindika
mazao ya kilimo na matunda ili kuyaongezea thamani katika soko na
kukuza uchumi.
(i) Kuanzisha na kuendeleza eneo la Uwanja wa Maonesho ya Biashara ya
   Kimataifa na kuwahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali na
  wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kutumia fursa za masoko ya EAC, SADC,
 AGOA na EU.
(j) Kuimarisha shughuli za bandari huru katika maeneo ya Maruhubi na
   Uwanja wa Ndege – Zanzibar na kuanzisha maeneo mapya.
Vyama vya Ushirika
138. Vyama vya Ushirika ni chombo cha kuwaunganisha na kuwawezesha wananchi
    kubadili hali ya maisha yao na kujiendeleza kiuchumi. Aidha, vyama vya ushirika
   wa kuweka na kukopa (SACOSS) ni nyezo ya kuwapatia wananchi mitaji
  kutokana na michango yao na mikopo kutoka katika vyombo vya fedha.
139. Ili kuendeleza ushirika, katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM
    itaielekeza Serikali kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na programu
   mbalimbali za kuendeleza sekta ya ushirika.
(b) Kuendelea kusajili vyama vipya vya ushirika na kuendeleza ukaguzi wa
   vyama vya ushirika.
(c) Kuendeleza mafunzo kuhusu uendeshaji na uongozi wa vyama vya
   ushirika, uzalishaji mali, utunzaji wa rasilimali na hesabu za ushirika.
89
Sekta za Miundombinu ya Kiuchumi
140. Maendeleo endelevu ya uchumi yanategemea sana ubora wa miundombinu ya
    kiuchumi ambayo hujumisha barabara, bandari,viwanja vya ndege na umeme.
   Katika kipindi kilichopita Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa
  CCM, imepata mafanikio makubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi,
 kuimarisha ustawi wa jamii na kuvutia uwekezaji na biashara.
141. Ili kuendeleza kazi ya kuimarisha miundombinu ya kiuchumi, katika kipindi cha
    miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM itahakikisha kuwa SMZ, inatekeleza kazi
   zifuatazo:-
Barabara
(a) Kuendeleza kazi ya utunzaji na matengenezo ya barabara zilizokwisha
   jengwa, ili ziendelee kuwa imara kwa kiwango kinachokubalika.
(b) Kukamilisha ujenzi wa barabara ya Mfenesini hadi Bumbwini (Km.13) na
   Welezo hadi Dunga (Km.12.75) kwa Unguja na Km. 108.9 za barabara za
  Pemba.
(c) Kujenga jumla ya Km. 119.9 za barabara Unguja, na kilomita 76.6, Pemba
   kama ufuatavyo:-
Unguja
(d)
Kujenga kilomita 152.9 za barabara za:-














Matemwe
-
Muyuni
-
Kichwele
-
Pangeni
-
Kizimbani
-
Kiboje
-
Njianne
-
Umbuji/Uroa -
Fuoni
-
Kombeni
-
Koani
-
Jumbi
-
Jendele
-
Cheju-Kae bona
-
Jozani - Ukongoroni Charawe- Bwejuu
-
Mkwajuni
-
Kijini
-
Pale
-
Kiongele
-
Fumba ring road
-
Bububu
-
Mtoni - Kinazini - Malindi -
Creek road -
Mkunazini
- M’moja -
Funi
-
Magomeni-Kariako-Mkunazini -
Km. 6.5
Km. 4.0
Km. 6.0
Km. 11.0
Km. 6.7
Km. 6.0
Km. 6.0
Km. 15
Km. 5.5
Km. 11
Km. 8
Km. 9
Km. 1.2
Km. 8.3
90










Welezo
-
Amani
-
U’ndege
-
Nyumba mbili -
Mahonda
-
Fukuchani
-
Utambi
-
Oshora
-
Donge-Mtambile
Amani-Freshi -
Amani-Ng’ambo - Kariakoo -
Mtoni
-
K’samaki- Kilimani - M’moja -
Maili Nne
-
Donge
-
Kigongoni
-
Tazari
-
Kilimani
-
-
Mwanda
-
Mboriborini
-
Km. 3.5
Km. 4
Km. 7
Km. 1.2
Km. 14
Km. 8
Km. 3
Km. 4
Km. 3
Km. 1
Pemba
(e)
Kukamilisha ujenzi wa kilomita 108.9 za barabara za:-










Mtambile – Kengeja - Mwambe
Kenya
-
Chambani
Mizingani
-
Wambaa
Chanjamjawiri-
Tundaua
Chanjaani
-
Pujini
Mtambile
-
Kangani
Chake
-
Wete
Wete
-
Konde
Wete
-
Gando
Mgagadu
-
Kiwani
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
9
3.2
10
10
5
6.2
30
15
13
7.5
Pemba
(f)
Kujenga kilomita 94.5 za barabara za:-










Ole
-
Kengeja
Bahanasa-Daya
-
Mtambwe
Mzambarau takao -
Pandani Finya
Mzambarau Karim-Mapofu
Chwale
-
Kojani
Kipangani
-
Kangagani
Mkanyageni -
Kangani
Finya -
Kicha
Shumbaviamboni - Tumbe
Kuyuni
- Ngombeni
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
Km.
35
13.6
8
8.6
2
3
6.5
8.8
5
4
91
(g)
Aidha, Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria zinazohusiana na
usafiri na kukamilisha maandalizi ya kanuni za Sheria ya Usalama Barabarani
pamoja na kuimarisha Karakana Kuu ya Serikali.
Bandari
142.
Huduma za bandari zinao mchango mkubwa katika kukuza uchumi na ustawi wa
jamii. Ili kuendeleza miundombinu ya bandari na kuimarisha uchumi wa
Zanzibar, katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM itaielekeza
Serikali kutekeleza hatua zifuatazo:-
(a) Kujenga majengo mapya ya kuhudumia abiria katika bandari ya Malindi
   pamoja na matengenezo ya maeneo ya kuhifadhia makontena bandarini
  na kuimarisha vifaa katika bandari hiyo.
(b) Kuifanyia matengenezo bandari ya Mkoani kwa kurekebisha sehemu ya
   gati iliyodidimia pamoja na kuipatia vifaa vya kuhudumia mizigo.
(c) Kuiendeleza zaidi gati ya Wete kwa kuongeza urefu na upana wake,
   kuipatia vifaa vya kuhudumia mizigo na kujenga ramp ya kuhudumia
  vyombo vya aina ya “Land Craft”.
(d) Kuimarisha gati ya Mkokotoni kwa kujenga jeti kwa ajili ya majahazi na
   usafiri wa wananchi hasa wa Tumbatu.
(e) Kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkuu (Master Plan) wa bandari ya
   Malindi, ikijumuisha huduma za bandari huru na kuendelea kutafuta
  uwezo wa kujenga Bandari Mpya ya Kibiashara ya Mpiga Duri.
Usafiri wa Baharini.
143.
Ili kuimarisha huduma za usafiri wa baharini, katika kipindi cha miaka mitano
ijayo (2010-2015) CCM itahakikisha kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
inatekeleza hatua zifuatazo:-
(a) Kuliimarisha Shirika la Meli la Zanzibar, ili liweze kujiendesha kibiashara.
(b) Kubadili mfumo wa uendeshaji wa Afisi ya Mrajis wa Meli na kuwa
   Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Usafiri wa Baharini ‘Maritime
    Authority.
92
(c)
Kuendeleza mazingira ya kuvutia wawekezaji wa nje na ndani ili kuwekeza
zaidi katika sekta ya usafiri wa baharini na kuboresha huduma ya usafiri
kwa wananchi na wageni hususan watalii wanaotembelea Zanzibar.
Usafiri wa Anga:
144.
Usafiri wa anga ni moja ya nyenzo muhimu katika kukuza uchumi na kichocheo
cha kuendeleza Sekta ya utalii. Ili kuiendeleza zaidi Sekta ya Usafiri wa Anga,
katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM itahakikisha kuwa SMZ,
inatekeleza kazi zifuatazo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Uendelezaji wa Kiwanja cha
   Ndege cha Kimataifa cha Zanzibar na kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la
  abiria.
(b) Kukamilisha kazi ya ujenzi wa uzio, uwekaji wa taa katika barabara ya
   kurukia na kutulia ndege na uimarishaji huduma za umeme kwa kukipatia
  “generator” la akiba Kiwanja cha Ndege cha Karume Pemba.
(c) Kuwapatia mafunzo na vifaa vya kisasa wafanya kazi wa Kiwanja cha
   Ndege cha Zanzibar na Karume Pemba pamoja na kuimarisha huduma za
  zima moto na usalama wa viwanja vya ndege.
Umeme:
145.
Nishati ya umeme ni muhimu katika kujenga Msingi wa Uchumi wa Kisasa wa
Taifa linalojitegemea. Ili kuendeleza kazi ya usambazaji wa nishati ya umeme na
kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii, CCM katika kipindi cha miaka mitano
ijayo (2010-2015) itahakikisha kuwa, kazi zifuatazo zinatekelezwa na Serikali:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Nishati na kuendeleza juhudi
   za utafiti wa vyanzo mbadala vya nishati ya umeme, ukiwemo umeme wa
  jua, upepo, mawimbi ya bahari, mafuta na gesi asilia.
(b) Kukamilisha utekelezaji wa mradi wa kujenga njia ya pili ya umeme
   inayopita chini ya bahari kutoka Ras Kiromoni Tanzania Bara hadi Fumba
  Unguja (Mradi wa MCC).
(c) Kuendeleza kazi ya usambazaji umeme mijini na vijijini, vikiwemo visiwa
   vidogo vidogo vinavyoishi watu katika maeneo mbalimbali Unguja na
  Pemba.
93
(d) Kuwahamasisha wananchi juu ya matumizi ya majiko sanifu, gesi asilia na
   umeme unaotokana na vyanzo mbadala kwa ajili ya matumizi ya
  nyumbani, hotelini na sehemu zote za majeshi na daghalia.
(e) Kuimarisha mazingira ya kuwavutia wawekezaji wa nje na ndani ili
   kuwekeza katika sekta ya nishati ya umeme.
(f) Kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Sekta ya Nishati kwa kuwapatia
   mafunzo ya fani mbali mbali za Nishati na Madini.
(g) Kuliimarisha Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), kwa kulijengea mazingira
   bora zaidi ili liweze kujiendesha kibiashara.
(h) Kusimamia utekelezaji wa Sheria na Kanuni za Uendeshaji wa Bohari,
   ‘Depot’ na usambazaji wa nishati ya mafuta kwa wananchi na
      kuhakikisha kuwa zinachangia katika mapato ya nchi.
Ardhi:
146. Ardhi ni rasilimali namba moja katika Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa kisasa na
    kichocheo cha maendeleo ya wananchi. Umiliki wa ardhi pia ni moja ya malengo
   ya Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12, Januari1964.
147. Ili kuendeleza na kusimamia matumizi bora ya ardhi, katika kipindi cha miaka
    mitano ijayo (2010-2015), CCM itahakikisha kuwa SMZ inatekeleza yafuatayo:-
(a) Kukamilisha maandalizi ya Sera ya Ardhi ya Zanzibar na kusimamia
   utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Matumizi bora ya Ardhi.
(b) Kuendeleza kazi ya kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa matumizi bora ya
   ardhi na kuongeza kasi ya upimaji wa viwanja katika maeneo mbalimbali
  kwa ajili ya makazi na shughuli nyingine za maendeleo.
(c) Kuendeleza kazi ya usajili wa ardhi katika maeneo mbalimbali hasa yale
   yasiyopimwa na kuwapatia wahusika hati za umiliki wa ardhi hiyo kwa
  mujibu wa sheria.
94
(d) Kuziimarisha Mahakama za Ardhi na kuanzisha Mahkama za Ardhi katika
   kila mkoa ili kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi na kupunguza
  migogoro ya ardhi.
(e) Kupanua shughuli za usajili wa ardhi kwenye
   maeneo ya miji yaliyopangwa na yasiyopangwa.
(f) Kufanya mapitio ya ramani zote na kuzifanyia marekebisho kwa mujibu wa
   mabadiliko yanayojitokeza, kuhuwisha ramani za miji ya Zanzibar (Unguja
  mjini, Chake chake, Wete, na Mkoani) vikiwemo visiwa vidogo vidogo na
 kuchapisha ramani mpya za visiwa vya Unguja na Pemba.
maeneo ya fukwe na
Sekta za Huduma za Jamii
Elimu
148. Elimu ya kisasa na hasa Sayansi na Teknolojia ina nafasi ya pekee katika
    kufanikisha ujenzi wa msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegema. Kwa
   kutambua ukweli huu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa CCM
  imetoa kipaumbele cha kwanza kwa sekta ya elimu.
149. Ili kuiendeleza sekta ya Elimu, katika kipindi cha mwaka cha miaka mitano ijayo
    (2010-2015), CCM itahakikisha kuwa SMZ inatekeleza yafuatayao:-
(a)
Elimu ya Maandalizi
(i) Kuendeleza juhudi za kuongeza ushiriki wa wanafunzi katika ngazi
   ya Elimu ya Maandalizi kutoka 18% hadi 50% ifikapo mwaka 2015.
(ii) Kutoa mafunzo kwa walimu wa Skuli za Maandalizi na kutayarisha
    vifaa vya kufundishia na kujifunzia (vikiwemo vitabu) vya Elimu ya
   maandalizi kulingana na mihutasari mipya.
(iii) Kukamilisha maandalizi ya Sera ya Makuzi na Malezi ya Mtoto
     (Integrated Early Childhood Care and Development Policy),
    na
(iv) Kuongeza idadi ya madarasa ya Elimu ya Maandalizi na
    kuwahasisha wananchi na sekta binafsi kujenga Skuli za Maandalizi.
95
(b)
Elimu ya Msingi
(i) (ii) Kuimarisha ufundishaji katika madarasa ya awali ya Msingi (Std 1 –
          4) na kusambaza vitabu na vifaa vyengine vya kufundishia na
         kujifunzia kwa Elimu ya Msingi kulingana na mihutasati mipya ya
        masomo, na
(iii)
(c)
Kuhamasisha wananchi kushiriki katika ujenzi wa skuli mpya na
kuongeza idadi ya madarasa katika skuli zilizopo kwenye maeneo
yao. Lengo ni kwenda sambamba na ongezeko la watoto
wanaohitaji kuandikishwa katika Elimu ya Msingi.
Kuimarisha mazingira ya skuli za Msingi ili ziwe zenye kumjali mtoto
(child friendly schools) pamoja na kukamilisha maandalizi ya Sera
ya Elimu Mjumuisho.
Elimu ya Sekondari
(i) Kuendeleza juhudi za kukarabati Skuli za Sekondari zilizopo,
   kuongeza idadi ya madarasa na kujenga skuli mpya za Sekondari ili
  kuongeza ushiriki wa wanafunzi katika ngazi ya Sekondari.
(ii) Kununua vitabu vya masomo ya Hisabati, Jiografia, Elimu ya uraia,
    Historia, Sayansi, Biashara, Ufundi, Dini, Kiingereza na Kiswahili
   kwa Elimu ya Sekondari pamoja na vifaa vya maabara na
  kuvisambaza katika skuli za sekondari.
(iii) Kuimarisha Elimu ya Sayansi na Hisabati kwa kuendesha kambi za
     Sayansi kwa walimu na wanafunzi katika Vituo vya Walimu na
    maskulini.
(iv) Kuendelea kuwashajiisha wanafunzi wa kike kupenda masomo ya
    Sayansi na Hisabati kwa kuwashirikisha kwa wingi katika kambi za
   Sayansi na kufungua madarasa zaidi ya watoto wa kike.
(v) Kuimarisha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na ufundishaji wa
   somo la kompyuta katika skuli kwa kuzipatia kompyuta. Aidha,
  tovuti ya Wizara itaanzishwa ili kuhifadhi taarifa muhimu na
 kuzisambaza kwa wadau mbali mbali wa elimu.
(vi) Kuimarisha uendeshaji wa masuala ya elimu katika ngazi mbali
    mbali kwa kutoa mafunzo kwa walimu wakuu, maafisa wa elimu
   wa wilaya, mikoa, idara pamoja na kuendelea kufanya ukaguzi na
96
kutoa ushauri kwa walimu juu ya mbinu bora za ufundishaji
madarasani.
(vii) Kujenga skuli mpya 21 za sekondari Unguja na Pemba. Skuli hizo
     zitajengwa katika vijiji vya Muanda, Matemwe, Chaani, Dole, Uzini,
    Paje (Mtule), Tunguu, Dimani, Kiembesamaki, Kibuteni, Mpendae
   kwa Unguja na Pandani, Chwaka Tumbe, Konde, Wawi, Kiwani,
  Mauani, Ngwachani, Shamiani, Utaani na Mkanyageni.
(viii) Kujenga nyumba 41 za waalimu Unguja na Pemba. Nyumba hizo
      zitajengwa kwa mpango ufuatao:-











Kibuteni
Muanda
Uzini
Paje (Mtule)
Mkanyageni
Pandani
Chwaka Tumbe
Kiwani
Wawi
Utaani
Matemwe
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
7
3
3
3
7
3
3
3
3
3
3
(ix) (x)
(d)
Kujenga Chuo cha Ualimu, Mchangamdogo Pemba pamoja na
nyumba 3 za Walimu.
Kuzifanyia ukarabati mkubwa skuli sita za sekondari skuli hizo ni
Uweleni, Utaani na Fidel Castro kwa Pemba na Forodhani,
Tumekuja na Hamamni Unguja.
Elimu Mbadala na Elimu ya Watu Wazima
(i) Kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Elimu Mbadala cha Wingwi
   Micheweni na kuanzisha vituo vya Elimu Mbadala katika Mikoa
  mengine ya Unguja na Pemba.
(ii) Kufanya mapitio ya mihutasari na vitabu vya Elimu Mbadala na
    kutayarisha mihutasari na vitabu vipya kulingana na Sera Mpya ya
   Elimu.
(iii) Kuendeleza mafunzo kwa walimu wa Elimu Mbadala na Elimu ya
     Watu Wazima, kuwahamasisha vijana kujiunga na madarasa ya
97
Elimu Mbadala na kuanzisha elimu endelevu (Continuing Education)
kwa watu wazima.
(e)
Kuimarisha Huduma za Maktaba:
(i) (ii) Kujenga Maktaba Kuu mpya Pemba na kuimarisha Maktaba za
        Wilaya, vituo vya Walimu na za skuli.
(iii) Kuendeleza mafunzo ya Ukutubi, kuongeza idadi ya vitabu kwa rika
     mbali mbali katika maktaba zote.
(iv)
(f)
Kuandaa Sera ya Maktaba Zanzibar.
Kuhamasisha wananchi kupenda kutumia maktaba na kuendeleza
matumizi ya “Mobile Libraries” kwa Skuli za Vijijini zisizokuwa na
   maktaba.
Kuendeleza na kuimarisha fursa za Elimu ya Juu:
(i) (ii) Kuimarisha Elimu ya Sayansi na Teknolojia ya kisasa katika vyuo
        vikuu, sambamba na upatikanaji wa Wakufunzi katika Chuo Kikuu
       cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
(iii) Kuwaendeleza wakufunzi waliopo.
(iv) Kuanzisha Diploma ya Sayansi kwa Walimu na Diploma ya Uongozi.
(v)
(g)
Kukamilisha ujenzi wa majengo mapya ya Chuo Kikuu cha Taifa cha
Zanzibar (SUZA) huko Tunguu.
Kuendeleza mazingiza ya kuwahamasisha wawekezaji na sekta
binafsi kuendelea kuwekeza katika elimu ya juu.
Kuimarisha Mafunzo ya Ualimu
(i) Kuandaa Sera ya Mafunzo ya Ualimu Kazini na kuendelea kutoa
   mafunzo kazini kwa walimu kuhusiana na masomo wanayofundisha
  na mbinu bora za kufundishia masomo hayo.
(ii) Kupitia mitaala ya Diploma ya Ualimu Msingi, Sekondari, Lugha na
    Dini na Kiarabu na kuifanyia marekebisho na kuanza kutoa mafunzo
   ya ualimu kwa Walimu wa Skuli za Maandalizi.
98
(iii) (iv)
(h)
Kuendelea kutoa mafunzo ya ualimu katika Vyuo vya Ualimu na
kuendeleza mafunzo ya ualimu kwa walimu wasiosomea kwa njia
ya Elimu Masafa.
Kuendelea kutoa mafunzo kwa Walimu wa Sayansi na Hisabati
kupitia Mradi wa Teacher Advancement Programme (TAP) katika
vituo vyote vya Walimu na kuendeleza mafunzo ya kompyuta kwa
Walimu 170.
Kuimarisha Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Amali:
(i) (ii) Kuimarisha Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia kwa
        kuifanyia matengenezo makubwa na kuongeza madarasa pamoja
       na kuanza kutekeleza mpango wa utekelezaji wa Taasisi wa miaka
      mitano.
(iii) Kununua vifaa vya kisasa vya kufundishia na kujifunzia kwa
     masomo ya Ufundi katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia na Skuli
    za Ufundi za Mikunguni na Kengeja.
(iv) Kupanua na kuimarisha Skuli ya Ufundi Kengeja kwa kuyafanyia
    matengenezo majengo yaliyopo, na
(v)
(i)
Kujenga Ofisi ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali na kuimarisha
matumizi ya teknolojia ya kisasa katika elimu.
Kujenga vituo vipya vya Mafunzo ya Amali katika Mikoa ya Kusini
Unguja, Kaskazini Pemba na Mjini Magharibi.
Kuhifadhi Kumbukumbu za Kihistoria na Mambo ya kale:
(i)
Kuandaa mpango wa miaka mitano (Master Plan) wa Uhifadhi wa
Mambo ya Kale, uanzishaji wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu
za Kale na vituo vya kuhifadhi kumbukumbu (Records Centres)
katika kila Mkoa.
99
(ii) Kuendeleza matengenezo ya Makumbusho ya Mnazi Mmoja, Beit –
      Ajab, jengo la Kale la Mtoni na Makumbusho ya Kasri Forodhani.
(iii) Kuendelea kukusanya kumbukumbu na nyaraka kutoka ofisi za
     Serikali na kuzihifadhi kumbukumbu hizo kwa kutumia kompyuta.
(iv) Kuendelea kufanya tafiti za kiakiolojia na hifadhi za Urithi katika
    Mapango ya kale na Baharini na kuanzisha Kituo cha Uhifadhi wa
   vitu vya baharini
(v) Kukamilisha upimaji wa maeneo ya Kihistoria na kuyapatia hati
   miliki.
Afya
150. Huduma bora za afya kwa wananchi wote bila ya ubaguzi ni miongoni mwa
    malengo makuu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12, Januari1964.
151. Ili kuendeleza uimarishaji wa sekta ya afya kwa maendeleo na ustawi wa
    wananchi, katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015), Serikali ya
   Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa CCM itatekeleza hatua zifuatazo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Afya na ushirikishwaji wa wananchi na
   sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya afya, kwa kuzingatia
  malengo ya Milenia, Dira ya 2020 na MKUZA.
(b) Kuendelea kuimarisha huduma za Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, ili ifikie
   hadhi na kiwango cha Hospitali ya Rufaa, Hospitali ya Abdalla Mzee na
  Wete Pemba zifikie hadhi na kiwango cha Hospitali za Mkoa na “Cottage
   Hospital” ya Michweni na Vitongoji Pemba na Makunduchi na Kivunge
    Unguja, zifikie hadhi na kiwango cha Hospitali za Wilaya.
(c) Kuendelea kuimarisha huduma za kinga na tiba katika hospitali na vituo
   vya afya na kuendeleza elimu ya afya kwa wananchi ili kudhibiti maradhi
  hasa yale ya kuambukiza.
(d) Kuendeleza mapambano dhidi ya malaria, UKIMWI pamoja na maradhi
   mengine ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.
(e) Kuendeleza huduma za tiba asili katika sehemu zote za Unguja na Pemba.
100
(f)
Kuendelea kukiimarisha Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya pamoja na
watumishi wa sekta ya afya kwa kuwapatia mafunzo ya ndani na nje ya
nchi.
Maji
152. Maji ni uhai, hasa maji safi na salama. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya
    uongozi wa CCM imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji maji
   mijini na vijijini.
153. Ili kuendeleza kazi ya usambazaji wa huduma ya maji safi na salama kwa
    wananchi, CCM katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) itahakikisha
   kuwa, SMZ inatekeleza yafuatayo:-
(a) Kufanya mapitio ya Sera na Sheria ya Maji ili kuzihuwisha kwa kuzingatia
   haja na umuhimu wa usimamizi na udhibiti wa maji machafu, ambayo ni
  matokeo ya matumizi ya maji safi pamoja na hifadhi ya mazingira.
(b) Kukamilisha Awamu ya Pili ya Mradi wa usambazaji maji safi na salama
   katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
(c) Kuendelea kusambaza huduma ya maji safi na salama kutoka asilimia 75
   mwaka 2010 hadi asilimia 95 mwaka 2015 mjini na kusimamia huduma
  hiyo kutoka asilimia 60 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 80 mwaka 2015
 vijijini kupitia mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika (ADB) ambao utajenga miundombinu ya maji kwa
miji mitatu ya Pemna (Chake-Chake, Wete na Mkoani) pamoja na maeneo
ya vijiji ambavyo kwa upande wa Unguja ni Nungwi, Matemwe, Machui na
Dunga/Tunguu. Maeneo ya Vijiji vya Pemba ni Mizingani, Wambaa,
Vitongoji, Ndagoni na Kambini-Mchangamdogo. Aidha, Serikali itaendelea
kupeleka maji katika maeneo ambayo hayajafikiwa na miradi mikubwa
iliyojengwa.
(d) Kuendelea kuhamasisha wananchi ili kukuza kiwango cha uelewa na
   mwamko wao katika kuchangia huduma za maji ili ziwe endelevu na kutoa
  kipaumbele katika kulinda, kuhifadhi na kutunza rasilimali maji hasa katika
 vyanzo na makinga-maji (Catchment areas) dhidi ya uvamizi kwa shughuli
za ujenzi na kilimo.
(e) Kupunguza kiwango cha upotevu wa maji(Non revenue water) kwa
   kufunga mita za maji na kuwaelemisha wateja wa maji jinsi ya kutumia
  maji vizuri ili kuyahifadhi.
101
(f)
Kuandaa Sera ya Usafi wa Mazingira (Sanitation Policy) ili kuweza kudhibiti
kwa kiwango kikubwa usafi wa mazingira ikiwemo kusimamia vyema
shughuli za maji machafu.
Makazi
154. Kuwapatia wananchi maakazi na nyumba bora ni miongoni mwa malengo ya
    Mapinduzi matukufu ya tarehe 12 Januari, 1964. SMZ chini ya uongozi wa ASP
   na sasa CCM imefanya juhudi kubwa kuendeleza ujenzi wa nyumba bora kwa ajili
  ya makaazi ya wananchi Unguja na Pemba.
155. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM itaendeleza juhudi za
    kuimarisha makaazi ya wananchi na kuhakikisha kwamba, SMZ inatekeleza
   yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Nyumba na kuandaa Sheria ya
   “Condominium” ili kuwawezesha wananchi waliopangishwa katika
      nyumba za maendeleo mijini na vijijini kuuziwa sehemu ya majengo hayo
     (fleti).
(b) Kuandaa taratibu za kuwashirikisha wananchi wanaoishi katika Nyumba za
   Maendeleo mijini na Vijijini, kuchangia gharama za matengenezo na
  utunzaji wa nyumba hizo.
(c) Kuanzisha maeneo maalumu ya ujenzi wa nyumba za ghorofa hususan
   mijini, ambako idadi ya wakaazi na tatizo la uhaba wa ardhi ni kubwa
  zaidi.
(d) Kukamilisha ujenzi wa Nyumba moja ya Maendeleo huko Bambi.
Uendelezaji wa Mamlaka ya Mji Mkongwe
156.
Mji Mkongwe wa Zanzibar ni hazina kubwa na kivutio cha historia ya Zanzibar.
Mji Mkongwe pia ni Urithi wa Kimataifa, ambao unapaswa kulindwa,
kuhifadhiwa na kutumika kama kivutio cha utalii. Katika kipindi cha miaka
mitano ijayo (2010-2015), CCM itaielekeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
kutekeleza yafuatayo:-
(a)
Kusimamia utekelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Mji Mkongwe na
kuimarisha kitengo cha sheria, ili kutoa ushauri kwa wananachi na
wakaazi wa Mji Mkongwe.
102
(b) Kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe kwa
   kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi na mafunzo ndani ya kazi.
(c) Kuandaa Mpango wa Matumizi Endelevu ya Eneo la Mji Mkongwe na
   kuimarisha mashirikiano na Mamlaka nyingine za Miji iliyoko katika
  orodha ya UNESCO na Urithi wa Kimatifa.
(d) Kuhamasisha ukarabati wa majengo yanayomikiwa na watu binafsi na
   Taasisi za Serikali na kupunguza wingi wa majengo yaliyo katika hali
  mbaya.
(e) Kujenga ukingo wa ukuta wa barabara ya Mizingani, ili kuzuia athari za
   mmong’onyoko wa ardhi unaosababishwa na bahari.
(d) Kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Matumizi ya Magari na Vyombo vya
   Moto (Traffic Plan) ndani ya eneo la Mji Mkongwe.
Maeneo Mengine ya Kipaumbele
Utamaduni na Michezo
157. Utamaduni ni nyenzo muhimu katika kulinda na kudumisha mila na silka njema
    za jamii. Michezo huimarisha afya na kujenga udugu na mashirikiano miongoni
   mwa wananchi na mataifa mbalimbali.
158. Ili kuiendeleza zaidi sekta ya Utamaduni na Michezo, katika kipindi cha miaka
    mitano ijayo (2010-2015), CCM itaielekeza SMZ kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria za Michezo na Utamaduni na
   kuhimiza matumizi ya sanaa katika kuhamasisha na kuelimisha jamii
  kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo na kampeni za kitaifa.
(b) Kuandaa Sera ya Utamaduni na Michezo na kuendeleza utalii wa
   kiutamaduni na wa kimaumbile.
(c) Kujenga kiwanja cha kisasa cha michezo ya ndani katika eneo la kiwanja
   cha Amaani na kukamilisha Ujenzi wa Kituo cha Michezo Dole (Akademia).
(d) Kuanza maandalizi ya ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa wa michezo
   ambao pia utatumika kwa maadhimisho ya sherehe mbalimbali za kitaifa.
(e) Kuanza matengenezo ya kuboresha uwanja wa Gombani Pemba.
103
(f) Kuendeleza na kuimarisha vipaji vya wanamichezo kwa kuwapatia fursa za
   kushiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa kwa njia ya ziara za
  kimichezo nje ya nchi na mafunzo.
(g) Kuendeleza juhudi za kulinda, kuhifadhi na kudumisha mila, silka na
   maadili mema ya Wazanzibari.
Vyombo vya Habari
159. Vyombo vya Habari vinalo jukumu kubwa la kuburudisha, kuelimisha
    kuhamasisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya maendeleo, demokrasia
   Utawala Bora. Kwa kutambua wajibu huo wa vyombo vya habari, Serikali
  Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa CCM, inao wajibu wa kusimamia
 kuendeleza uhuru wa Vyombo vya Habari.
na
na
ya
na
160. Ili kukuza na kuendeleza Uhuru wa Vyombo vya Habari, katika kipindi cha miaka
    mitano ijayo (2010-2015), CCM itahakikisha kuwa, hatua zifuatazo zinatekelezwa
   na Serikali:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera
   Vyombo vya Habari.
ya Habari na kuendeleza Uhuru wa
(b) Kusimamia utekelezaji wa Miongozo, Kanuni na Sheria ya Vyombo vya
   Habari ili kuongeza ufasini na kasi ya mageuzi ya Utangazaji.
(c) Kuendeleza mafunzo kwa watendaji wa Vyombo vya Habari na Utangazaji,
   ili kujenga weledi na vipaji vyao.
(d) Kuviimarisha Vyombo vya Habari ikiwemo TVZ na STZ, kwa kuvipatia
   vifaa na mitambo ya kisasa ili viweze kurusha matangazo yake kwa
  ufanisi, kuonekana na kusikika katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya
 Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
(e) Kuendelea kukiimarisha Chuo cha Uandishi wa Habari ili kiwe chombo cha
   kujenga na kutoa mwelekeo wa matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili kwa
  Vyombo vya Habari.
(f) Kusimamia na kudhibiti uingizaji wa vifaa vya utangazaji na kuhakikisha
   kwamba, Zanzibar haigeuzwi kuwa jaa la kutupia vifaa visivyotumika vya
  televisheni, redio na utangazaji kwa ujumla.
(g) Kukiimarisha kiwanda cha uchapaji kwa kukifanyia matengenezo
   makubwa na kukipatia mitambo mipya ya uchapaji na vifaa vya kisasa.
104
Majanga na Huduma za Uokoaji
161.
Huduma za uokoaji ni muhimu kwa jamii hasa pale yanapozuka majanga ya
kimaumbile na yale yanayosababishwa na binadamu. Ili kuimarisha huduma za
Uokoaji, katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015), CCM itahakikisha
kuwa Serikali inatekeleza yafuatayo:-
(a) Kuimarisha uwezo wa Kikosi Cha Zimamoto na Uokozi (KZU) kwa mafunzo
   na vifaa vya kisasa na kuanzisha vituo vipya katika kila wilaya.
(b) Kukiimarisha Kitengo cha Taifa cha Maafa na Kamati za Maafa za Mikoa na
   Wilaya kwa kuzipatia mafunzo na miongozo kuhusu kazi na wajibu wao.
(c) Kuanzisha kikosi maalum cha uokoaji wakati wa majanga ya baharini, ili
   kutoa huduma za uokoaji wa maisha na mali za wananchi wanaopatwa na
  ajali wakiwa baharini.
MADAWA YA KULEVYA
162. Madawa ya kulevya pamoja na maambukizi ya VVU ni miongoni mwa
    changamoto kubwa zinazowakabili vijana wa Zanzibar. Madawa ya kulevya
   huathiri afya za watumiaji ambao wengi wao ni vijana na kudhoofisha nguvu kazi
  na uchumi wa Taifa letu. Aidha, upo uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya
 madawa hayo na maambukizi ya VVU.
163. Ili kuendeleza mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na kudhibiti maambukizi
    ya VVU, CCM katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) itahakikisha
   kwamba, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatekeleza hatua zifuatazo:-
(a) Kuendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Kudhibiti Madawa ya
   Kulevya.
(b) Kuendelea kushirikiana na Asasi za kijamii katika kuhamasisha na
   kuelimisha vijana athari za madawa ya kulevya na kuwashawishi
  waachane na matumizi ya madawa hayo.
(c) Kuendelea kuchukua hatua thabiti za kuimarisha ulinzi na udhibiti wa vituo
   vya kuingilia nchini zikiwemo bandari na viwanja vya ndege.
105
(d) Kuhamasisha wananchi kushiriki katika ulinzi shirikishi na polisi jamii ili
   kudhibiti uingizaji, usambazaji na matumizi ya madawa ya kulevya katika
  maeneo yao.
(e) Kuanzisha Kituo Maalumu cha Kurekebisha Vijana walioathirika na
   madawa ya kulevya.
Demokrasi na Utawala Bora
164.
Demokrasi na Utawala Bora ni hatua muhimu katika ujenzi wa jamii yenye
umoja, mshikamano, uadilifu na uwajibikaji. Ili kuendeleza ujenzi wa demokrasia
na utawala bora katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM
itaendeleza azma yake ya kuimarisha na kukuza demokrasia na utawala bora na
kuhakikisha kwamba SMZ inatekeleza yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa kazi na majukumu ya Serikali kwa kuzingatia
   misingi ya demokrasia na utawala bora kama ilivyoainishwa katika Katiba
  ya nchi, kuimarisha uwazi na uwajibikaji na kulifanya suala la maadili
 kuwa agenda ya kitaifa.
(b) Kuendeleza kazi ya utekelezaji wa mkakati wa elimu ya uraia, ikiwemo
   elimu ya demokrasia, haki za binadamu na utawala bora kwa viongozi,
  watendaji na wananchi kwa jumla.
(c) Kukamilisha kazi ya kuandaa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
   na kusimamia utekelezaji wake, ili kuimarisha mapambano dhidi ya
  rushwa.
(d) Kuimarisha ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar na kukamilisha
   hatua za wanasheria wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kuendesha
  mashtaka katika ngazi zote za mahakama.
(e) Kukiimarisha kitengo cha kupokea malalamiko kwa kuyapokea, kuyafanyia
   kazi na kuyapatia ufumbuzi wa haraka.
(f) Kuimarisha ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa kuwapatia
   watendaji wake elimu ya kada mpya za ukaguzi, ukiwemo Ukaguzi wa
  Thamani (Value for Money Auditing), Ukaguzi wa Komputa (Computerize
 Auditing) na Ukaguzi wa Mazingira (Enviromental Auditing).
(g) Kuimarisha Mahakama kwa kujenga majengo mapya, nyumba za
   Mahakimu katika vituo vya kazi Unguja na Pemba, kuzipatia vifaa vya
  kisasa na kufanya marekebisho ya sheria na kanuni za utendaji kazi wa
 Mahakama.
106
(h) Kuanzisha Mahakama ya Biashara Zanzibar.
(i) Kufanyiwa mapitio ya Sheria ya Asasi za Wananchi (NGO’s) na kuweka
     mfumo wa kisasa utakaorahisisha usajili wa Jumuiya hizo.
(j) Kukamilisha ujenzi wa ukumbi mpya wa Baraza la Wawakilishi.
Serikali za Mitaa
165.
Serikali za Mitaa ni chombo muhimu cha kuwawezesha wananchi kushiriki katika
Utawala wa nchi yao. Serikali za Mitaa ni kichocheo cha maendeleo na ustawi wa
wananchi, ujenzi wa domokrasi na utawala bora. Ili kuziendeleza Serikali za
Mitaa katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM itahakikisha
kwamba, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatekeleza hatua zifuatazo:-
(a) Kuifanyia mapitio Sheria ya Serikali za Mitaa na Mamlaka ya Tawala za
   Mikoa na Miji na kuandaa Mpango wa Mageuzi ya Tawala za Mikoa na
  Serikali za Mitaa ili kuimarisha uwajibikaji na ufanisi.
(b) Kuendelea kuziimarisha Serikali za Mitaa kwa kuzipatia ruzuku, wataalamu
   wa fani mbalimbali, vifaa vya kisasa na vitendea kazi, ili kuendeleza
  utendaji wake wa kazi na huduma bora kwa wananchi.
(c) Kuimarisha mahusiano kati ya wananchi na Madiwani na watendaji wa
   Halmashauri za Wilaya, Mabaraza ya Miji na Baraza la Manispaa kwa
  kuwapatia mafunzo na miongozo mbalimbali Madiwani ili kuimarisha
 uwajibikaji wao kwa wananchi.
(d) Kuwahamasisha wananchi kuunda Kamati za Maendeleo katika maeneo
   yao, ili kusukuma kasi ya maendeleo yao kiuchumi na kijamii na kudhibiti
  aina zote za uhalifu ukiwemo wizi wa mazao na mifugo na kupiga vita
 vitendo vya ukahaba na madawa ya kulevya kupitia mfumo wa Ulinzi
Shirikishi na Polisi Jamii.
(e) Kuzihimiza Serikali za Mitaa kusimamia suala la usafi wa miji, hifadhi ya
   mazingira na kuhakikisha kuwa kila mwenye uwezo wa kufanya kazi
  anafanya kazi.
Vikosi Maalumu vya SMZ
166.
Vikosi Maalumu vya SMZ kama vilivyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar, kwa
ujumla wake ni vyombo muhimu vya utekelezaji wa Sera za CCM kuhusu Ulinzi
107
na Usalama na hususan dhana ya Ulinzi wa Umma, ambao unawashikisha
wananchi wote.
167.
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2010-2015), Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
chini ya uongozi wa CCM itaendelea kuviimarisha Vikosi Maalumu vya SMZ, na
kutekeleza hatua zifuatazo:-
(a) Kuvijengea uwezo na mazingira mazuri ya kazi kwa kuvipatia mafunzo na
   vifaa vya kisasa ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.
(b) Kuendeleza juhudi za kukiimarisha Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo
   (KMKM) kwa kukipatia mafunzo na zana za kisasa, ili kuongeza uwezo na
  mbinu za kuweza kukabiliana na kudhibiti aina mpya za uhalifu unaoanza
 kujitokeza katika maeneo ya ukanda wa pwani, ukiwemo uharamia na
utekaji nyara wa vyombo wa baharini.
(c) Kuendeleza juhudi za kuliimarisha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na
   kuimarisha miundombinu ya kambi zake, ili kuwavutia vijana wengi zaidi
  na kuwa vituo vya kuwajenga vijana katika uzalendo, ukakamavu, usawa
 na umoja wa kitaifa na kuwaandaa katika stadi mbalimbali za maisha.
(d) Kukiimarisha zaidi Kikosi cha Valantia (KVZ) kwa kukamilisha ujenzi wa
   majengo yake ya Makao Makuu huko Mtoni na maeneo mengine ya mikoa
  na wilaya, na kukiwezesha kutekeleza jukumu lake la msingi la kuendeleza
 mafunzo ya Ulinzi wa Umma miongoni mwa wananchi hasa vijana
(ambao ni nguvu kubwa), ili kushiriki katika ulinzi wa maeneo yao
wanayoishi chini ya mfumo wa Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii.
(e) Kuendeleza na kudumisha mashirikiano mema yaliyopo baina ya Vikosi
   vya SMZ na vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini.
Kuwaunganisha Wananchi wa Zanzibar
168. Hoja ya kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar, kimsingi inatokana na sera za
    CCM za kujenga Umoja wa taifa, Amani na Utulivu. Mazingira ya amani na
   utulivu ndio zana ya kwanza inayohitajika ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani hii
  ya CCM ya mwaka 2010-2015 na kufikia azma ya Chama ya kujenga msingi wa
 uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea. Nchi yenye fujo na vurugu haiwezi
kujenga uchumi imara na kuwaletea maendeleo ya maana wananchi wake.
Hakuna mwekezaji atakayekubali kuja kuwekeza na wananchi hawatapata fursa
ya kujiendeleza kiuchumi na kupambana na umasikini.
169. Hii ndio sababu siku zote CCM imekuwa ya kwanza kutetea na kusimamia
    amani, umoja na utulivu miongoni mwa wananchi. Kufikiwa kwa Muafaka wa
108
kisiasa wa mwaka 1999, 2001 na Maridhiano ya kisiasa juu ya mustakabali wa
Zanzibar ya Novemba 2009, ni uthibitisho thabiti wa ukweli huu.
170.
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015), CCM itaendelea kuimarisha
jitihada za kusimamia amani, utulivu na kuwaunganisha Wananchi wa Zanzibar
na Tanzania kwa jumla na kuhakikisha kuwa SMZ inatekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendeleza na kuimarisha amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa
   miongoni mwa Wazanzibari na Watanzania kwa jumla.
(b) Kuendelea kupiga vita, kudhibiti na kutoruhusu vitendo vya ubaguzi wa
   aina yoyote ile kujitokeza katika sehemu za utoaji wa huduma au fursa
  mbalimbali za kiuchumi na kijamii miongoni mwa wananchi.
(c) Kuendeleza umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi kwa
   kuwapatia elimu ya uraia na kuwajengea mazingira ya kuaminiana,
  kuvumiliana na kushirikiana kama dhana na silaha muhimu ya kuharakisha
 maendeleo yao, kuboresha huduma za kijamii na kupambana na
umasikini.
Kuyaendeleza Makundi Mbalimbali
Watoto
171. Watoto ndio chanzo cha rasilimali watu na mrithi wa taifa la kesho. CCM inaamini
kuwa, watoto wanayo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa kwa kupewa elimu
na afya bora na kutobaguliwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi.
172.
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM itaendelea kuimarisha
haki na maendeleo ya watoto na kuhakikisha kwamba, SMZ inatekeleza hatua
zifuatazo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Uhai, Hifadhi na Maendeleo ya Watoto,
   kupiga vita ajira kwa watoto na kusimamia utekelezaji wa sheria na
  mikataba ya Kimataifa inayohusu haki, usawa na hifadhi ya watoto.
(b) Kupitisha Sheria ya Mtoto na kusimamia utekelezaji wake.
109
(c) Kufuatilia na kusukuma kasi ya upatikanaji wa huduma za tiba, kinga na
   afya ya mama na mtoto katika Hospitali na vituo vyote vya afya mijini na
  vijijini kwa kiwango na ubora unaokubalika.
(d) Kusimamia na kuratibu ubora wa huduma zinazotolewa na Mashirika ya
   hiari na yasiyokuwa ya Serikali yanayojishughulisha na huduma
  zinazomgusa mtoto, vikiwemo vituo vya malezi na Skuli za awali.
(e) Kukamilisha ujenzi wa Nyumba ya Watoto yatima – Mazizini Unguja
(f) Kujenga Nyumba ya Watoto yatima Pemba.
Vijana
173. Vijana walioandaliwa vyema na kujipanga vizuri wanao mchango mkubwa katika
    kukuza uchumi na maendeleo ya jamii. Ukosefu wa ajira, kukosa ujuzi na maarifa
   ya kisasa pamoja na mitaji ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazowakabili
  vijana wengi mijini na vijijini na kuwafanya washindwe kujiendeleza na
 kutekeleza wajibu wao wa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa kisasa.
174. Katika kipindi cha mwaka 2010-2015, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya
    uongozi wa CCM itaendeleza juhudi za kuzipatia ufumbuzi changamoto za vijana
   na kahakikisha kuwa, SMZ inachukuwa hatua zifuatazo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Vijana, Sera ya Ajira na
   Sheria ya Kazi na kuendelea kuwahamasisha vijana ili kuunda vikundi vya
  uzalishaji mali.
(b) Kuimarisha mashirikiano na Asasi zisizokuwa za Serikali (NGOs) zenye
   kushughukia maendeleo ya Vijana ili kuanzisha vituo vya ujasirimali kwa
  vijana, kuwaendeleza na kuwapatia elimu ya stadi mbalimbali
 zitakazowawezesha kujiajiri wenyewe.
(c) Kuanzisha Mfuko Maalumu wa vijana utakaotoa mikopo nafuu ili
   kuwasaidia kujiendeleza kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.
110
(d)
Kukamilisha uanzishaji wa Baraza la Taifa la Vijana ili kuimarisha ushiriki
wa vijana katika ngazi mbalimbali za maamuzi na kupiga vita UKIMWI na
kuendeleza mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
Wanawake
175. CCM inatambua uwezo na nguvu kubwa ya wanawake katika kusukuma kasi ya
    maendeleo na kuleta mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa na kwamba:
   “Wakiwezeshwa, Wanaweza”.
176. Ili kuendeleza juhudi za kuwawezesha wanawake kiuchumi, kijamii na kisiasa,
    CCM katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) itahakikisha kwamba
   Serikali inatekeleza yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Hifadhi na Maendeleo ya Wanawake na
   kuhakikisha kwamba, haki za wanawake zinaimarishwa na kulindwa kwa
  mujibu wa Katiba na Sheria za nchi.
(b) Kuendelea kupiga vita mila na desturi zinazowabagua na kuwadhalilisha
   wanawake na kusimamia utekelezaji wa sheria na mikataba mbalimbali ya
  Kimatifa inayohusu haki na ustawi wa jamii.
(c) Kuendeleza juhudi za kuwahamasisha wanawake kujiendeleza kielimu na
   kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wa kike.
(d) Kuendeleza juhudi za kuwapatia mafunzo na elimu ya uraia ili kujenga
   uelewa wao na nguvu za kutetea haki zao na kushiriki kikamilifu katika
  shughuli za kijamii.
(e) Kuimarisha uwezo wa Mifuko mbalimbali ya Kuwawezesha Kiuchumi
   Wanawake na kujenga mazingira yatakayowawezesha kuanzisha Benki ya
  Wanawake.
Wazee
177.
Wazee ni hazina na chemchem ya busara katika jamii. Wazee ndio chimbuko la
familia na wametoa mchango mkubwa katika ujenzi na maendeleo ya taifa letu.
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM itahakikisha kwamba,
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kuchukua hatua thabiti za kuwatunza
na kuendeleza ustawi wa maisha yao na kutekeleza yafuatayo:-
111
(a) Kuendeleza juhudi za kuwapatia hifadhi ya makazi, huduma za afya na
   misaada ya kijamii kwa wazee wasiojiweza pamoja na kuzifanyia
  matengenezo ya mara kwa mara nyumba za wazee zilizopo Sebleni
 Unguja na Limbani Pemba.
(b) Kuihamasisha jamii kuendeleza utamaduni wa kuwaheshimu, kuwaenzi
   na kuwatunza wazee wetu pamoja na kuwapa nafasi wanayostahiki
  katika jamii.
Walemavu
178. CCM inaamini katika usawa wa binadamu na kwamba, watu wenye ulemavu
    wanayo haki kwa mujibu wa Katiba ya kutambuliwa utu wao, kuendelezwa,
   kuheshimiwa na kutokubaguliwa. Aidha, Chama kinatambua uwezo mkubwa
  walionao watu wenye ulemavu katika kujiendeleza na kuchangia katika uchumi
 na maendeleo ya taifa letu.
179. Ili kuwaendeleza watu wenye ulemavu, katika kipindi cha miaka mitano ijayo
    (2010-2015) CCM itahakikisha kuwa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendeleza
   jitihada za kuimarisha hali ya ustawi wa watu wenye ulemavu na kutekeleza
  yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Watu wenye Ulemavu na kuendelea
   kuwapatia huduma zote za msingi hasa elimu, afya pamoja na vifaa
  muhimu vinavyoendana na mahitaji yao maalumu.
(b) Kuunga mkono na kushirikiana kwa karibu na Jumuiya ya Watu wenye
   Ulemavu katika kuhamasisha na kuelimisha jamii iondokane na mtizamo
  hasi dhidi ya watu wenye ulemavu.
(c) Kuendelea kuwapatia watu wenye ulemavu fursa za mafunzo ya stadi
   mbalimbli za ufundi, misaada, mikopo ya fedha na vifaa vya kisasa.
Wafanya Kazi
180.
Wafanyakazi ni rasilimali watu na ndio msingi wa mageuzi yote ya kiuchumi na
kijamii. Wafanyakazi huchangia katika kukuza uchumi na maendeleo ya nchi
yetu. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) CCM itahakikisha kuwa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaimarisha jitihada zake katika kuwaendeleza
wafanyakazi na kutekeleza yafuatayo:-
112
(a) Kuandaa Sera ya Hifadhi ya Jamii na kufanya mapitio ya Sheria za Kazi.
(b) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Ajira, Mpango wa Kuzalisha Ajira,
   Sheria za Kazi na Kanuni za Utumishi, ili kulinda na kuendeleza haki na
  wajibu wa wafanya kazi.
(c) Kuimarisha mashirikiano kati ya Serikali na wafanyakazi kupitia chombo
   chao “Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi” kwa lengo kukuza
      mahusiano mema na kujenga “Utatu”.
(d) Kuendelea kuimarisha mazingira bora ya kazi na maslahi ya wafanyakazi
   kwa kadri hali ya uchumi wa Zanzibar utakavyoimarika.
113
SURA YA NANE
MAENEO MENGINE MUHIMU
Kuimarisha Muungano
181. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ni wa kipekee katika Bara la Afrika,
sasa umefikisha umri wa miaka 46, tangu kuasisiwa kwake hapo tarehe 26, Aprili
1964. Katika kipindi hiki Muungano wetu umezidi kuimarika na kupiga hatua
kubwa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Sambamba na mafanikio
hayo, zipo changamoto nyingi ambazo bado zinahitajika kufanyiwa kazi.
182.
Hii ni pamoja na kujenga mazingira endelevu na kuimarisha fursa za kiuchumi
miongoni mwa wananchi wa kila upande, ili waone na kuamini kwamba,
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sio tu ni ngao madhubuti ya Umoja,
Amani na Mshikamano wao, bali pia ni daraja lisilotetereka la kuwafikisha katika
azma yao ya kuondokana na umaskini na kuharakisha maendeleo yao na Taifa
kwa jumla. Hii ndio changamoto kubwa inayo ukabili Muungano wetu, ambayo
Serikali zetu zinapaswa kuivalia njuga.
183. Katika kipindi cha Ilani hii, Chama kitazielekeza Serikali zake kuimarisha zaidi
Muungano kwa faida ya pande zote mbili kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kukamilisha ujenzi wa majengo na taasisi za Muungano ambazo
   zimeanzishwa Tanzania Zanzibar.
(b) Kuimarisha utendaji wa Kamati ya Pamoja ya kutatua kero za Muungano
   kwa kuandaa utaratibu madhubuti wa vikao vya Kamati na utekelezaji wa
  haraka wa maamuzi yanayofikiwa.
(c) Kuboresha uchangiaji na mgawanyo wa mapato ya Muungano.
(d) Kuzifanyia mapitio na uboreshaji Sheria na Kanuni za Fedha zinazotawala
   ukusanyaji wa mapato chini ya TRA na ZRB upande wa Tanzania Zanzibar
  kwa lengo la kukuza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato hayo.
(e) Kuboresha Sheria, Kanuni na taratibu za ajira ya watumishi katika Taasisi
   za Muungano ili utumishi huo uwe na sura muafaka ya ki - Muungano.
114
(f) Kuimarisha utaratibu wa kuandaa na kutekeleza mikakati na mbinu za
   pamoja zenye lengo la kuinua uchumi wa pande zote mbili za Muungano.
(h) Kuendeleza miradi ya pamoja ya kiuchumi, miundombinu na ya kijamii
   iliyokwishaanzishwa ikiwemo ya TASAF, MACEMP n.k.
184. Aidha, CCM inatambua kuwa, Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964,
ndilo tukio kubwa na muhimu la kihistoria kwa Visiwa vya Zanzibar lililowakomboa
Wazanzibari wote kutoka makucha ya ukoloni na kujenga mazingira muafaka ya
Zanzibar huru kuungana na Tanganyika huru na kuunda Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii, CCM itahakikisha kwamba
Serikali zake zinaendelea kuchukua hatua za kuyalinda, kuyaenzi na kuyaendeleza
mafanikio yote yaliyopatikana kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuyalinda Mapinduzi hayo ikiwa ndio msingi wa maendeleo
   kamili, uhuru, haki, usawa wa binadamu na heshima ya kweli kwa
  Wazanzibari.
(b) Kuendelea kuyalinda kwa nguvu zote na kuchukua hatua za kuyaendeleza
   mafanikio mbalimbali yaliyoletwa na Mapinduzi hayo, hususan ardhi,
  huduma za jamii (elimu, afya, maji) pamoja na kupiga vita aina zote za
 ubaguzi au upendeleo miongoni mwa wananchi.
(c) Kuendelea kuheshimu Haki za Binadamu Demokrasia na Utawala Bora.
UTAWALA BORA
185.
Chama Cha Mapinduzi kinatambua kwa dhati umuhimu wa utawala bora na
katika kipindi cha Ilani hii ya 2010-2015, kitaielekeza Serikali kuendelea
kudumisha utawala bora nchini kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuwahamasisha viongozi wa vyama vya siasa kuendesha shughuli za
   kisiasa kizalendo, wakizingatia wakati wote kwamba na wao ni wadau wa
  mstari wa mbele wa maendeleo ya Taifa letu.
(b) Kujenga na kuimarisha zaidi matumizi ya dhana ya utatu baina ya Serikali,
   mwajiri na wafanyakazi katika kuleta utendaji kazi uliotukuka nchini
  mwetu.
(c) Kuendelea kuimarisha utoaji wa elimu ya demokrasia katika ngazi zote na
   kujenga uvumilivu wa kisiasa nchini.
115
(d) Kuhakikisha kwamba kuna usimamizi madhubuti wa matumizi ya fedha na
   rasilimali nyingine za umma kwa kusimamia ipasavyo uwajibikaji wa wote
  wanaohusika. Maadili ya viongozi wa umma yafuatwe kwa ukamilifu.
(e) Kuendesha Serikali kwa kufuata Katiba ya Nchi, Sheria, Kanuni na
   Taratibu zilizowekwa.
(f) Kutoa mafunzo ya Utawala Bora na Demokarasia.
(g) Kusimamia utekelezaji wa Haki za Binadamu kama zilivyoelezwa katika
   Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya Serikali ya
  Mapinduzi Zanzibar, Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Afrika na
 Tamko la Umoja wa Mataifa.
(h) Kuifanyia marekebisho Sheria ya Manunuzi ya Vifaa kwa kupunguza
   urasimu ili kuharakisha uamuzi juu ya vitu vinavyotakiwa kununuliwa na
  kuchochea maendeleo ya nchi.
(i) Kuona kuwa Serikali inateua Watendaji ambao ni wazalendo, waaminifu
   na waadilifu.
(j) Kuimarisha nidhamu, uwajibikaji na kupiga vita urasimu katika maeneo
   yote ya uongozi na utendaji Serikalini.
Sekta ya Sheria
186.
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010-2015, Chama kitaitaka Serikali
iendelee kuimarisha Sekta ya Sheria kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Pamoja na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Nne kwa kuteua Majaji wengi
   wakiwemo Wanawake, jitihada hizo za Serikali ziendelee pamoja na kuona
  kwamba Mahakama zote zinajengewa mazingira yatakayowawezesha
 kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.
(b) Kuhakikisha kuwa wanakuwepo pia wataalamu waliobobea katika Sheria
   za Mikataba na kwamba wanatumika ipasavyo wakati Serikali inapoandaa
  mikataba mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
(c) Kuyatafutia ufumbuzi endelevu masuala ya mlundikano
   mahakamani na la msongamano wa wafungwa magerezani.
(d) Kupanua mafunzo ya Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na kuwapangia
   kazi ili utoaji wa haki katika ngazi za chini usicheleweshwe.
wa
kesi
116
(e) Kuboresha posho za Wazee wa Mahakama na kuhakikisha kwamba
   zinatolewa kwa wazee wote kwa wakati unaotakiwa.
(f) Kuzifanyia marekebisho sheria
   kuwakandamiza wanawake.
(g) Kuanzisha na Kutekeleza Mpango maalum wa kuanzisha Ofisi za
   Mahakama Kuu katika kila Mkoa ili kusogeza huduma kwa wananchi.
(h) Kukamilisha Mchakato wa kutenganisha shughuli za upelelezi na
   uendeshaji mashtaka.
(i) Kutekeleza Mpango wa Uboreshaji wa Mfuko wa Sheria hususan ujenzi wa
   majengo ya Mahakama ya ngazi zote na kuajiri Majaji na Mahakimu wa
  kutosha. Mfumo wa elektroniki katika kuendesha mashauri na kuhifadhi
 nyaraka za mashauri utaanzishwa.
(j) Kuweka mfumo wa Kuwasaidia wananchi wasiojiweza kupata msaada wa
   Kisheria.
(k) Kupeleka huduma za Mahakama karibu na wananchi ikiwa ni pamoja na
   kujenga masjala ya Mahakama ya Biashara Dodoma.
(l) Kuendelea kuimarisha na kuongeza kasi ya usikilizaji wa migogoro ya
   nyumba na Ardhi ili kuwezesha wananchi kuendelea na shughuli za
  uchumi.
(m) Kuyawekea mfumo wa sheria maagizo mbalimbali ambayo hutolewa kama
   amri halali na viongozi wakuu wa nchi yetu kuhusu maendeleo yetu ili
  utekelezaji wa maagizo hayo upate nguvu ya sheria.
(n) Kuendelea kupunguza mlundikano wa mahabusu katika magereza.
za
mirathi
na
zile
zinazoonekana
Demokrasia na Madaraka ya Umma
187.
Katika jitihada za kukuza na kuendeleza demokrasia nchini na kuimarisha
madaraka ya umma, Chama Cha Mapinduzi kitaitaka Serikali kutekeleza
yafuatayo:-
(a)
Kuhakikisha kwamba NGOs kutoka nje zinajishughulisha na majukumu
ambayo zimeandikishwa kufanya na kwamba hazipati nafasi ya
kujiendesha kinyume na makusudi hayo.
117
(b) (c) Kuhimiza utekelezaji wa Sheria ya Ardhi namba 4 na 5 ya mwaka 1999
       katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
(d)
188.
Kuendelea kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika
kusimamia rasilimali watu na fedha ili zitumike kuharakisha maendeleo ya
Wilaya au Manispaa inayohusika.
Kuboresha usimamizi na udhibiti wa fedha katika Mamlaka ya Serikali za
Mitaa.
Mapambano Dhidi ya Rushwa
Rushwa ni kikwazo cha
Usipodhibitiwa kwa dhati,
unaweza kuenea katika
mmomonyoko mkubwa wa
189.
maendeleo ya Taifa na utoaji wa haki nchini.
uovu unaotendwa na watoaji na wapokeaji rushwa
sekta zote za maisha ya jamii na kusababisha
uwajibikaji na maadili ya uongozi.
Ili kukomesha madhara ya rushwa, Chama Cha Mapinduzi katika kipindi hiki cha
2010-2015 kitaitaka Serikali kuimarisha na kuendeleza mapambano dhidi ya
rushwa kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuimarisha na kuboresha kwa kiwango kikubwa mfumo wa
   upelelezi wa makosa, uendeshaji wa kesi na utoaji wa haki mahakamani
  kwa lengo la kudhoofisha vishawishi vya rushwa.
(b) Kuendesha mafunzo ya elimu ya uraia kwa wananchi ili kuwahamasisha
   wajue madhara ya rushwa na kuwataka waichukie rushwa katika sura
  zake zote.
(c) Kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma juu ya maadili ya kazi na mbinu
   za kupambana na rushwa ili waweze kujiepusha na rushwa katika ofisi
  zote za umma.
(d) Kuendelea kuimarisha uwezo wa vyombo vyote vya dola vinavyopambana
   na rushwa ili viweze kutoa mchango mkubwa zaidi.
Ulinzi na Usalama
190.
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinavyojumuisha JWTZ, JKT, JKU, Polisi na
Magereza ni vyombo vyenye dhima na jukumu kubwa la kulinda uhuru na
mipaka ya nchi yetu, usalama wa raia na mali zao. Aidha, vinadumisha
mazingira ya amani na utulivu yanayovutia wawekezaji wa ndani na nje na
118
kuwezesha utekelezaji ulio kamili wa mipango ya maendeleo toka ngazi ya
familia hadi Taifa.
191.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita 2005 – 2010, Vyombo hivi vilitekeleza
majukumu yake kwa ujasiri, uzalendo na uadilifu wa hali ya juu. Katika kipindi
cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010-2015, Chama Cha Mapinduzi kitazitaka
Serikali zetu kulinda mafanikio yaliyopatikana na kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuimarisha na kuboresha zaidi mafunzo ya aina zote ya
   vyombo vya ulinzi.
(b) Kuwapatia wananchi mafunzo juu ya ulinzi shirikishi ili wawe tayari
   kujilinda katika maeneo yao.
(c) Ili kukabiliana na tatizo linalowafanya wanajeshi wetu kuishi uraiani,
   mpango maalumu unaolenga katika kulitatua tatizo hili utaanzishwa.
(d) Halmashauri za Majiji, Manispaa na Miji zitakiwe kuanzisha vikosi vyao
   rasmi vya usalama wa raia ili kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo.
(e) Kujenga vituo vya Polisi katika kila Tarafa nchini.
(f) Kuimarisha shughuli za uzalishaji mali na wa mbegu bora za mazao na
   mifugo katika maeneo ya Magereza na JKT.
(g) Kuendelea na mpango wa kuimarisha na kupanua mafunzo ya JKT na JKU
   kwa vijana wa mujibu wa sheria ili kuwapatia fursa ya kujifunza juu ya
  ulinzi, kujenga Taifa, uzalendo na umoja wa kitaifa.
Hifadhi ya Mazingira
192. Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi aliwahi kusema,
    “Umaskini na uharibifu wa mazingira ni watoto pacha na mama yao ni
     ujinga” Tamko hilo linaashiria siyo tu umuhimu wa jukumu la kuhifadhi
      mazingira ya hewa, maji, udongo na uoto wa asili wa nchi yetu bali pia hatari
     zinazosababishwa na uchafuzi wa mazingira tunamoishi. Hatari kubwa zaidi ni
    umaskini wa wananchi.
193. Katika kipindi cha miaka ya 2010-2015, Chama Cha Mapinduzi kitaitaka Serikali
    iendelee kufanya yafuatayo ili kuhakikisha kazi iliyoanza ya hifadhi ya mazigira
   inakuwa endelevu:-
119
(a) Kuimarisha zoezi la kitaifa la kupanda miti na miti ya asili kila mwaka
   katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili hiyo. Viongozi wa Vitongoji, Mitaa,
  Vijiji na Kata watakiwe kukagua mara kwa mara miti iliyopandwa ili
 kuhakikisha inakua.
Aidha, miti ipandwe katika maeneo ya shule,
barabara, zahanati ya kijiji, Kituo cha Afya na makazi ya watu. Wakuu wa
maeneo hayo wahakikishe lengo la kupanda miti linafanikiwa.
(b) Serikali za Vijiji na Halmashauri za Wilaya na Manispaa zitunge sheria
   ndogo za hifadhi ya misitu.
(c) Kusimamia utekelezaji wa sheria ya hifadhi ya mazingira katika vyanzo vya
   maji na kusimamia utekelezaji wa mkakati wa usafi katika fukwe.
(d) Serikali ichukue hatua ya kuandaa sera na kutunga sheria itakayosimamia
   matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza uharibifu wa mazingira.
(e) Kupunguza gharama ya vifaa vya nishati mbadala ili wananchi
   wanaojenga nyumba za kisasa vijijini watumie nishati hiyo badala ya kuni
  na mkaa wa miti.
(f) Kuhimiza na kuhamasisha ufugaji wa kisasa vijijini ili uwe kichocheo cha
   hifadhi ya mazingira.
(g) Serikali iimarishe
   mazingira.
(h) Kutekeleza mradi wa vijiji vya mfano vya hifadhi ya mazingira (eco
   village).
(i) Vipeperushi vyenye mafunzo rahisi ya hifadhi ya mazingira viandaliwe,
   vichapishwe kwa wingi na vitumike kwenye mafunzo ya Elimu Yenye
  Manufaa nchini kote.
(j) Kufanya tathmini ya athari za kimazingira katika miradi ya ujenzi.
usimamizi
wa viwanda
na biashara kutochafua
Kujenga Uwezo wa Kukabili Majanga
194.
Majanga ni matukio yenye uwezo mkubwa wa kuhatarisha maisha ya watu,
mifugo, mazao, barabara, reli, madaraja na makazi ya watu mijini na vijijini.
Majanga makubwa husababishwa na vimbunga, mafuriko, matetemeko ya ardhi,
volkano, ukame, nzige, kwelea-kwelea, mioto mikubwa, kuvuja kwa mafuta
mengi, kuzama kwa meli, kupasuka kwa tenki au bomba la gesi, n.k.
120
195.
Kwa kuwa tunaishi katika kipindi ambacho janga lolote kati ya hayo linaweza
kuikumba nchi yetu wakati wowote, Chama Cha Mapinduzi kupitia Ilani ya 2010-
2015 kitaitaka Serikali ijizatiti katika kujenga uwezo mkubwa wa kukabiliana na
majanga kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuhakikisha kwamba wakati wote Taifa lina chakula cha kutosha kwenye
   hifadhi yake.
(b) Kuimarisha vikosi vya Zimamoto vyenye uwezo mkubwa wa wataalamu na
   zana za kisasa katika kukabiliana haraka na mioto mikubwa.
(c) Kuimarisha vikosi vya uokoaji majini vyenye zana bora za kazi na
   kuwapanga katika mikoa inayopakana na bahari na maziwa makuu tayari
  kwa kutoa huduma hiyo.
(d) Kuandaa vikosi vya wahandisi wa ujenzi jeshini na uraiani ambao
   watakuwa tayari wakati wa mafuriko kupambana ipasavyo na majanga
  mbalimbali.
(e) Kushirikiana na Halmashauri za Jiji, Manispaa, Miji na Wilaya kujenga
   uwezo wa vyombo vya dola katika kudhibiti na kukabiliana na majanga ya
  aina mbalimbali.
(f) Kuimarisha Idara ya Maafa iwe na uwezo mkubwa wa kushughulikia
   maafa nchini kwa kuiwezesha iwe Taasisi inayojitegemea na yenye ofisi za
  Kanda.
(g) Kuimarisha ushirikiano baina ya nchi yetu na nchi nyingine katika
   kupambana na maafa hususani katika nchi za Afrika Mashariki.
(h) Kuanzisha utaratibu wa kawaida wa kuuza nchini maboya madogo
   yanayovaliwa ili wavuvi na wananchi wanaosafiri kwa mitumbwi waweze
  kuyanunua kwa ajili ya usalama wa safari zote za majini.
Vyombo vya Habari
196.
Vyombo vya Habari vina jukumu la kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha
wananchi kuhusu kuhusu masuala muhimu kwa jamii. Chama Cha Mapinduzi
katika kipindi cha Ilani hii ya 2010-2015 kitasimamia Serikali kulinda mafanikio
yaliyopatikana na kuendeleza uhuru wa vyombo vya habari kwa kutekeleza
yafuatayo:-
(a)
Kuhakikisha kwamba matangazo ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
yanasikika nchini kote.
121
(b) Kuandaa Sheria ya kusimamia Vyombo vya Habari ambayo pamoja na
   mambo mengine itaondoa mianya inayosababisha ukiukwaji wa maadili ya
  uandishi wa habari.
(c) Kutilia mkazo mafunzo kwa Maafisa wa Habari na Wasemaji wa Wizara na
   Taasisi nyingine za Serikali.
(d) Kuendelea kuimarisha uwezo wa Idara ya Habari (MAELEZO) kama
   Msemaji Mkuu wa Serikali.
(e) Kuendelea kuhamasisha Halmashauri kuanzisha Vituo vya Radio na
   Televisheni.
Mambo ya Nje
197. Mwelekeo wa sasa wa Sera ya CCM ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
    Kimataifa, unaendelea kuongozwa na Sera ya Diplomasia ya Uchumi. Hivyo
   ofisi zetu za Ubalozi zitaendelea kuimarishwa kwa ajili hiyo.
198. Katika kipindi cha miaka ya 2010 -2015, Chama kitaielekeza Serikali iendelee
    kuboresha utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi kwa kuchukua hatua
   zifuatazo:-
(a) Kuendelea kuitangaza nchi yetu kama moja ya nchi duniani zenye
   mazingira muafaka kwa ajili ya uwekezaji kutokana na historia yake ya
  miaka mingi ya amani, umoja, utulivu na mshikamano wa kitaifa.
(b) Kuendelea kutangaza na kutetea utajiri mkubwa wa vivutio vya utalii
   tulivyonavyo na kuvutia watalii wengi kutoka mabara yote ya dunia waje
  kuviona.
(c) Kuendelea kuzitafutia masoko bidhaa zetu zenye ubora unaotakiwa katika
   nchi za nje kwa kushauriana na wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo.
(d) Kuendelea kuzielewa vema athari na fursa za utandawazi kwa nchi changa
   na kutoa ushauri kwa nchi yetu kwa kadri itakavyoonekana inafaa.
(e) Kuendelea kudai haki ya uwakilishi wa Afrika katika Baraza la Usalama la
   Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia hoja ya wingi wa agenda zinazojadiliwa
  na kuamuliwa na Baraza hilo bila ya uwakilishi wetu.
122
(f) Kuongeza uwakilishi wetu nje kwa kufungua Balozi mpya na kuongeza
   umiliki wa nyumba za makaazi na ofisi za Ubalozi katika Balozi zetu nje
  kwa kadri hali itakavyoruhusu.
(g) Kuendeleza Sera ya Ujirani Mwema na nchi jirani.
(h) Kujenga mahusiano ya kirafiki na ushirikiano wa kiuchumi na vyombo
   mbalimbali vya Kikanda na Kimataifa, unaozingatia maslahi makubwa ya
  Taifa letu.
(i) Kuendelea kuzishinikiza nchi tajiri kutekeleza ahadi yao ya kutenga
   asilimia 0.7 ya Pato la Taifa la nchi zao kwa ajili ya misaada kwa nchi
  maskini.
(j) Kuendeleza mchakato wa kuitambua Jumuiya ya Watanzania wanaoishi
   ughaibuni na kuweka utaratibu utakaowawezesha kuchangia maendeleo
  ya Taifa lao.
Utamaduni na Maendeleo ya Michezo
199. Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba vijana wa Tanzania wana vipaji vya
    michezo mbalimbali kama walivyonavyo wenzao wa mataifa mengine duniani.
   Mafanikio yaliyopatikana katika fani ya michezo yameonyesha wazi kwamba
  mbele ya safari nchi yetu itachukua nafasi yake stahiki katika michezo ya aina
 mbalimbali.
200. Katika miaka mitano ijayo ya utekelezaji wa Ilani hii, Chama kitaitaka Serikali
    kuweka msukumo mkubwa katika maendeleo ya utamaduni na michezo kwa
   kuchukua hatua zifuatazo:-
Utamaduni
(a) Kuona kwamba maeneo yote muhimu ya kihistoria nchini (historical sites)
   yanaimarishwa na kutunzwa ili kukuza utalii na maendeleo ya vizazi
  vijavyo.
(b) Kuendeleza utekelezaji wa uamuzi wa kuanzisha Makao Makuu ya”Urithi
     wa Ukombozi wa Bara la Afrika”.
(c) Kuhakikisha kwamba lugha ya Kiswahili ambayo ni kielelezo cha utaifa na
   utamaduni wetu, inaendelezwa nchini na kimataifa na kuona kwamba
  kinatumiwa kwa ufanisi.
(d) Kuendelea kufanya tafiti za amali za tamaduni na kusambaza matokeo.
123
(e) Kuanza mchakato wa kujenga Jumba la Utamaduni Kiromo (Bagamoyo).
(f) Kubaini wasanii mahiri na wenye vipaji na kuwaendeleza.
(g) Kufanya utafiti wa lugha za asili ili kuzihifadhi na kupata misamiati kwa
   kukuza Kiswahili pamoja na kusambaza istilahi za Kiswahili zinazokidhi
  mahitaji ya taaluma mbalimbali.
Michezo
(a) Kuonesha wazi kibajeti umuhimu wa michezo katika mipango yetu ya
   maendeleo ikizingatiwa kwamba zama hizi zimeufanya utamaduni na
  michezo kuwa sehemu ya Diplomasia ya Uchumi wa nchi inayohusika.
(b) Kuishirikisha kwa ukamilifu sekta binafsi katika kuendeleza fani mbalimbali
   za michezo.
(c) Kuweka mkakati endelevu wa kuinua na kuendeleza michezo ya riadha
   nchini.
(d) Kuandaa mkakati wa kuwatambua vijana wenye vipaji mbalimbali vya
   michezo na kuwaendeleza.
(e) Kuendelea kufundisha walimu wa michezo mbalimbali.
(f) Kuandaa mashindano ya michezo kwenye ngazi ya vijiji, kata, tarafa hadi
   Taifa.
(g) Kuendelea kutenga maeneo ya wazi kwa ajili ya michezo.
(h) Kuanza kutekeleza Awamu ya Pili ya Ujenzi wa Uwanja wa Taifa.
(i) Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi kutoa utaalamu na mafunzo ya
   miundombinu na vifaa vya michezo kwa Halmashauri na wadau
  mbalimbali.
(j) Kuendelea kukiimarisha Chuo cha Michezo Malya pamoja na kuendeleza
   michezo katika Shule na Vyuo.
(k) Kuitumia michezo kama nyenzo ya kuwaunganisha vijana wenye vipaji
   mbalimbali katika kufanya mambo makubwa ya kitaifa.
(l) Kulinda na kudumisha sheria ya viwanja vyote vya michezo nchini na
   kudhibiti uvamizi.
124
Kuyaendeleza Makundi Mbalimbali
201.
Makundi yatakayoendelezwa katika kipindi hiki ni ya watoto, wanawake, watu
wenye ulemavu na wazee.
Watoto
202. Kila mtoto wa Tanzania ana haki ya kuishi, kukua na kulelewa vema ili Taifa
    lipate kijana mwadilifu na raia mwema.
203. Katika kipindi cha Ilani hii ya 2010-2015, Chama kitaielekeza Serikali kuendeleza
    malezi ya watoto kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kukamilisha Sera ya Malezi na Makuzi ya Mtoto.
(b) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Mtoto (2009) kwa ajili ya ustawi na
   maendeleo ya mtoto.
(c) Kuwahamasisha akina Mama wajawazito kujifungulia kwenye Vituo cha
   Afya ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
(d) Kutilia mkazo matumizi ya vyandarua ili kuwalinda dhidi ya malaria na
   kupunguza vifo vya watoto.
(e) Kuimarisha huduma ya chanjo kwa watoto dhidi ya magonjwa. Vituo vya
   afya na zahanati viandaliwe kutoa huduma hiyo kwa watoto kwa
  kuzingatia umri unaokubalika kitaalamu.
(f) Kushirikisha sekta binafsi na mashirika ya hiari katika kuanzisha na
   kuendesha vituo vya kulelea watoto na shule za awali.
(g) Kuboresha viwanja vya kuchezea watoto katika ngazi za Mitaa, Vijiji na
   Vitongoji.
(h) Kupitisha Sera Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya
   Mtoto ili watoto wote nchini waweze kunufaika kutokana na utekelezaji
  wake.
(i) Kuendeleza vita dhidi ya ajira ya watoto.
(j) Kutekeleza mikataba ya haki za mtoto iliyoridhiwa na Bunge.
(k) Kuwahamasisha watumishi wa Afya juu ya kuwaelimisha Wazazi madhara
   ya madawa ya kulevya dhidi ya watoto.
125
Wanawake
204.
Chama Cha Mapinduzi kinatambua mchango wa wanawake katika ujenzi wa
Taifa letu. Katika kipindi cha Ilani ya 2010-2015, Chama kitaendelea kuitaka
Serikali iwahusishe wanawake katika siasa, uongozi na modenaizesheni ya
uchumi wetu kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuongeza nafasi na fursa katika kuwateua wanawake kushika nafasi
   mbalimbali za uongozi, utawala na menejimenti ndani ya Serikali na taasisi
  zake.
(b) Kuongeza nafasi za uwakilishi wa wanawake kwa lengo la kufikia asilimia
   50.
(c) Kuimarisha mifuko mbalimbali ya uwezeshaji wa wanawake
   kuhamasisha vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS na VICOBA).
(d) Kuendelea kuwahamasisha wanawake kutumia fursa za kiutendaji na
   kisiasa ambazo zipo katika nyanja mbalimbali kitaifa, kikanda na kimataifa.
(e) Kuimarisha mifuko iliyopo ya mikopo ili wanawake wengi zaidi waweze
   kufaidika kutokana na mifuko hiyo.
(f) Kuimarisha Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) kwa kuongeza mtaji ili
   iweze kutoa huduma zake katika maeneo mengi zaidi nchini.
(g) Kuendelea kupiga vita mila na desturi zinazowabagua wanawake na
   kutekeleza Mikataba ya Kimataifa inayohusu maendeleo ya wanawake.
(h) Kuendelea kuimarisha Vitengo vya Jinsia katika Wizara, Taasisi na Idara
   za Serikali.
na
Watu Wenye Ulemavu
205. Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba watu wenye ulemavu wanastahili
    kupata haki zote za kiraia na kibinadamu chini ya Katiba na Sheria za Nchi.
206. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010-2015, Chama kitaitaka Serikali
    kuendelea kuitafsiri imani hiyo kwa vitendo kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
126
(a) Kuendelea kupanua na kuimarisha fursa za kisiasa, kiuchumi na ajira kwa
   watu wenye ulemavu.
(b) Kuimarisha na kuboresha mbinu za ulinzi wa watu wenye ulemavu wa
   ngozi.
(c) Kuhakikisha kwamba ujenzi wa majengo yanayotoa huduma kwa umma
   yanajengwa kwa kuzingatia mahitaji ya raia hao.
(d) Kuendelea kuboresha shule za watu wenye ulemavu kwa kuwapatia
   walimu wenye taaluma ya kuwafundisha na zana za kufundishia.
(e) Kubaini watu wenye ulemavu wanaoweza kufanya kazi za uzalishaji mali
   katika maeneo wanakoishi na kuwawezesha ili waweze kujiajiri.
Wazee
207. Tangu nyakati za kupigania uhuru wa nchi yetu, TANU na ASP vilitambua na
    kuenzi ipasavyo nafasi ya wazee katika harakati hizo. Hekima na busara zao
   pamoja na mshikamano wa dhati uliokuwepo baina yao na vijana waliokuwa
  msitari wa mbele katika kudai uhuru wetu, viliijengea nchi mazingira ya ushindi
 wa uhakika. Wazee waliounda Baraza la Mapinduzi la Zanzibar baada ya
Mapinduzi ya Zanzibar, ni kielelezo hai cha umuhimu wa michango ya wazee
katika maendeleo ya nchi yetu. CCM imerithi hazina ya uzoefu huo.
208. Katika miaka ya 2010-2015, Chama Cha Mapinduzi kitazitaka Serikali ziendelee
    kuimarisha na kuboresha mipango na taratibu za utoaji wa huduma kwa wazee
   kwa kufanya yafuatayo:-
(a) Kutunga sheria itakayotawala utoaji wa haki ya matibabu bure kwa wazee
   wasiojiweza katika vituo vya matibabu huko wanakoishi. Chini ya sheria
  hiyo kila mzee apatiwe kitambulisho kwa ajili hiyo ili wazee waweze
 kutibiwa kwa uhakika bila ya usumbufu wowote.
(b) Kuendelea kuboresha mafao ya wazee wanaostaafu ili yaendane na hali
   halisi ya gharama za maisha na matakwa ya soko ili maisha yao tulivu
  yachangie vema katika amani ya nchi kwa ujumla.
(c) Kuendelea kutumia
   inavyowezekana.
(d) Kuendelea kuwawezesha kiuchumi kwa kiwango fulani wazee ambao
   wataonekana kuwa bado wana nguvu za uzalishaji mali.
uzoefu,
hekima
na
busara
zao
kwa
kadri
127
Kuhamia Makao Makuu Dodoma
209. Uamuzi wa kuhamishia Dodoma Makao Makuu ya Serikali ya Jamhuri ya
    Muungano wa Tanzania, uliotangazwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius
   Kambarage Nyerere mwaka 1973, ulifanywa kwa kuzingatia sababu za
  kudumu.
210. Pamoja na kwamba hatua za kutekeleza uamuzi huo zimekumbana na matatizo
    mbalimbali, yapo mafanikio yaliyopatikana. Mafanikio hayo ni: Makao Makuu ya
   CCM, Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya
  TAMISEMI tayari vimehamia Dodoma. Kujengwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma ni
 sehemu ya mafanikio ambayo yameongezea mazuri ya kuhamia Dodoma.
211. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2010-2015) Chama Cha Mapinduzi
    kitaitaka Serikali kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuandaa mpango thabiti wa kuhamia Dodoma hatua kwa hatua. Katika
   mpango huo, Mpango Mji wa Dodoma (Master Plan) utazamwe upya ili
  kuhakikisha kuwa majengo ya Serikali yanajengwa upya Chamwino kwa
 kuanzia na majengo ya ofisi na makazi ya Rais (Ikulu).
(b) Kuihamasisha Sekta binafsi kushiriki katika ujenzi wa hoteli za kisasa,
   viwanda, hospitali, n.k. katika maeneo ya Manispaa yaliyotengwa na
  yatakayoendelea kutengwa.
(c) Kutunga sheria ya kutambua mji wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi.
(d) Kuanzia sasa majengo mapya ya Wizara za Serikali yajengwe Dodoma
   badala ya Dar es Salaam.
128
SURA YA TISA
CHAMA CHA MAPINDUZI
212. Chama Cha Mapinduzi katika miaka mitano ijayo kinaelekeza nguvu kubwa katika
    kutimiza lengo la msingi la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 kwa kuendeleza
   jitihada za ujenzi wa uchumi wa kisasa na taifa linalojitegemea. Katika kuzingatia
  jukumu hilo Ilani hii ya CCM ya 2010 hadi 2015 inatangaza nia ya
 modenaizesheni ya uchumi. Modenaizesheni ya uchumi ndiyo njia ya uhakika
itakayobadili na kuleta mapinduzi katika uchumi wa nchi, kujenga msingi wa
uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda, kuondoa umasikini wa wananchi wetu
kwa kiwango kikubwa na hivyo kuwezesha nchi yetu kujitegemea. Ni ahadi ya
CCM kuwa ikichaguliwa tena itaongoza Mapinduzi hayo ya Kiuchumi kwa kutumia
Mkakati wa Kuwashirikisha Wananchi kupitia Sera ya Kuwawezesha Wananchi
Kiuchumi na Usimamizi wa Dola wa Mipango ya Uchumi wa Nchi.
213. Utekelezaji wa majukumu ya Ilani hii ni changamoto ya kihistoria kwa kizazi cha
    sasa cha viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Changamoto hii
   inahitaji viongozi na wanachama wanaoongozwa na nadharia ya mapambano,
  kutekelezwa kwa vitendo, kuhamasisha umma na kufanya tathmini ili kufikia
 malengo yaliyokusudiwa. Mtindo huu wa utekelezaji tunajifunza kutoka kwa
viongozi walioongoza harakati za ukombozi wa TANU na Afro katika kuung’oa
 ukoloni Tanganyika na kuupindua utawala wa Sultani Zanzibar. Waliongoza kwa
vitendo kwa kuhamasisha wananchi na kwa kupima matokeo yake.
214. Kizazi cha sasa cha viongozi wa Chama chetu lazima kibadilike kiutendaji, katika
    msimamo na mtazamo. Jukumu lililo mbele yetu ni hatua ya pili ya ukombozi wa
   nchi yetu na watu wake kiuchumi. Badala ya kulalamikia tu umasikini na
  utegemezi wetu, tuchukue hatua kivitendo, kimsimamo na kimtizamo. Jukumu la
 kujenga uchumi wa kisasa na taifa linalojitegemea linahitaji viongozi wa Chama
kuongoza kivitendo katika uhamasishaji wananchi na usimamizi madhubuti wa
Serikali katika utekelezaji wa Sera za Chama, Ilani na Mwelekeo.
129
215.
Katika kuzingatia usimamizi kivitendo Ilani ya Chama ya mwaka 2010-2015
inaainisha majukumu ya kimethodolojia yafuatayo:-
(a) CCM lazima kiongoze kwa kuonyesha njia na kwamba hii ni changamoto
   ya kihistoria kwa kizazi cha sasa cha viongozi wa Chama chetu;
(b) Wajibu wa kimsimamo na mtazamo wa viongozi na wanachama wetu
   wenye dhamira ya kupambana na umasikini mpaka watakapoushinda; na
(c) Wajibu wa vitendo kwa viongozi na wanachama wetu kwa kuwa mfano wa
   kuigwa kwenye utendaji na utekelezaji wa majukumu mbalimbali k.m.
  Wakulima bora, Wafugaji bora, Wavuvi bora n.k.
216. Hivyo, ni muhimu kwa Chama kudumisha na kuimarisha utaratibu wa kusimamia,
    kufuatilia na kusukuma utekelezaji wa Ilani kwa viongozi na wanachama wake na
   kwa upande wa pili kwa Serikali zake mbili. Chama chetu hadi sasa bado kipo
  imara na hakitayumba na kimejipanga vizuri katika kusimamia utekelezaji wa
 Ilani.
217. Malengo makuu ya Ilani ya miaka 2000-2010 yanatuunganisha na majukumu ya
    Ilani ya CCM ya 2010 hadi 2015. Katika kipindi hiki, Chama kitaendelea
   kusimamia na kuchochea utekelezaji wa malengo ya miaka mitano iliyopita kwa
  kuzingatia uzoefu uliopatikana ili ifikapo mwaka 2015 Sera ya Uwezeshaji wa
 Wananchi Kiuchumi iwe inashirikisha wananchi wengi zaidi katika ujenzi wa
uchumi wa kisasa nchini.
(a) Chama Cha Mapinduzi na Muungano
218. Zimeanza kujitokeza dalili kwamba wanasiasa wanapandikiza mbegu za udini,
    ukabila na hisia nyingine zinazowatenganisha Watanzania. Lengo lao ni kupata
   madaraka ya kisiasa bila kujali madhara makubwa kwa Taifa yanayoambatana na
  sera hizo za kibaguzi. TANU na ASP na sasa CCM chini ya uongozi wa waasisi
 wake vimefanya jitihada kubwa kujenga umoja wa Taifa. Wanachama ndio
wamekuwa kichocheo cha umoja, udugu na mshikamano wa Watanzania.
Katika kipindi cha Ilani (2010-2015) Chama Cha Mapinduzi kitahakikisha viongozi
wake wanakuwa mstari wa mbele katika kuongoza vita dhidi ya ubaguzi wa
Watanzania kwa misingi ya dini, kabila, eneo, jinsia n.k. ili kuendeleza ujenzi wa
misingi imara ya umoja, udugu na mshikamano wa kitaifa.
219. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sasa umefikisha umri wa miaka 46, tangu
    kuasisiwa kwake hapo tarehe 26, Aprili 1964. Katika kipindi hiki Muungano wetu
   umezidi kuimarika na kupiga hatua kubwa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na
  kijamii. Sambamba na mafanikio hayo, zipo changamoto nyingi ambazo bado
130
zinahitajika kufanyiwa kazi. Hii ni pamoja na kujenga mazingira endelevu na
kuimarisha fursa za kiuchumi miongoni mwa wananchi wa kila upande, ili waone
na kuamini kwamba, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sio tu ni ngao
madhubuti ya Umoja, Amani na Mshikamano wao, bali pia ni daraja lisilotetereka
la kuwafikisha katika azma yao ya kuondokana na umaskini na kuharakisha
maendeleo yao na taifa kwa jumla. Hii ndio changamoto kubwa inayo ukabili
Muungano wetu, ambayo Serikali zetu zinapaswa kuivalia njuga.
220.
Katika kukabiliana na changamoto ya kuulinda, kuuenzi na kuendeleza
Muungano wetu, sera za CCM katika miaka ya 2010-2015 zitaendelea kusisitiza
na kusimamia utekelezaji wa yafuatayo:-
(a) Kuendeleza muundo wa Serikali mbili zilizopo sasa na kudumisha
   ushirikiano mwema kati ya Serikali hizi.
(b) Kuendeleza dhamira ya kweli ya kujenga utamaduni wa kukaa pamoja ili
   kujadili changamoto mbalimbali za Muungano, kwa lengo la kuzipatia
  ufumbuzi wa haraka kwa faida na maslahi ya pande zote mbili za
 Muungano.
(c) Kuendelea kujenga na kukuza msimamo na uelewa wa pamoja wa
   wananchi (Watanzania) juu ya masuala ya Muungano, hususan historia,
  misingi, utaifa na malengo yake ili kuwawezesha wananchi kufahamu
 umuhimu na uhalali wa Muungano wetu pamoja na kuimarisha umoja wa
kitaifa na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
(d) Kuimarisha Taasisi zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria, za
   kushughulikia masuala ya Muungano pamoja na kuimarisha mkondo wa
  mawasiliano na urejeshaji wa taarifa kwa wakati ili kasi ya kuimarisha
 Muungano isipungue.
(b) Chama Cha Mapinduzi na Kutoa Uongozi kwa Taifa
221. Mwalimu J.K. Nyerere, Baba wa Taifa, aliwahi kusisitiza “Pasipokuwa na haki
      hapawezi kuwa na amani”. Tanzania imefanikiwa kuwa nchi yenye amani na
       utulivu kutokana na sera zake zinazoweka mbele uhuru, haki, usawa na utu.
      Lazima CCM iendeleze sera hizi kwa nguvu zote. Katika kipindi hiki ambapo
     uchumi wa soko ndiyo unaotawala dunia na kufanya watu wachache kupata
    nafasi ya kujilimbikizia mali na kuwaacha watu wengi kwenye kingo za umaskini,
   Chama Cha Mapinduzi kimekuwa mstari wa mbele kuendelea kuibua sera
  ambazo zinalenga katika kuwawezesha watu wake kiuchumi na kupambana na
 umasikini kama inavyoainishwa katika Mwelekeo wa Sera za Chama chetu wa
miaka 2010-2015. Chama Cha Mapinduzi kimekuwa wakati wote mstari wa
131
mbele katika kujali maslahi ya wanyonge ambao ndiyo wengi katika nchi hii kwa
kuweka wakati wote sera zinazozingatia maslahi yao.
222. Kwa mantiki hii Chama Cha Mapinduzi bado ndiyo Chama kinachotegemewa na
    watu wengi kuendelea kutoa uongozi unaozingatia maslahi yao. Na maslahi ya
   watu wengi yakilindwa na kutekelezwa, nchi inadumu katika amani na utulivu.
  Ilani ya CCM katika miaka ya 2010-2015 inakusudia kuendeleza amani na utulivu
 huo.
(c) Chama Cha Mapinduzi Kuongoza Ujenzi wa Uchumi wa Kisasa na
   Kuutokomeza Umaskini
223 Chama Cha Mapinduzi kitaongoza ujenzi wa uchumi na kutokomeza umaskini
   kwa kuchukua hatua madhubuti zifuatazo:-
(a) (b) Mafunzo ya siasa, itikadi, maadili na malengo ya Ilani hii yataimarishwa
       katika ngazi zote za uongozi wa Chama.
(c) Ngazi zote za uongozi wa Chama kufanya kazi ya Chama ndani ya Chama
   na kazi ya Chama ndani ya Umma kwa kuzingatia Kanuni ya kukosoa,
  kujikosoa na kukosoana kama njia ya kujijenga na kujiimarisha wakati
 wote. Vikao vya Chama vitatekeleza kanuni hii.
(d) Chama kutekeleza kwa ukamilifu Ibara ya 18 ya Katiba ya CCM kuhusu
   “Mwiko kwa Kiongozi” ili kuhakikisha kwamba ndani ya Chama na
      ndani ya Dola madaraka ya kiongozi hayatumiwi kinyume cha lengo
     lililokusudiwa madaraka hayo.
(e) Kuweka msukumo mkubwa katika ujenzi wa Chuo cha Chama
   kitakachotoa mafunzo kwa viongozi, watendaji, makada, makamisaa wa
  Chama na wanachama kwa jumla kama hatua ya uhakika ya kujenga
 uongozi na utendaji wa pamoja ndani ya Chama na dola.
(f) Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano
   mwema baina yake na vyama vingine vya siasa duniani kwa kadri
  itakavyoonekana inafaa.
(g)
(d)
Kuhakikisha kwamba, Chama na Serikali zina uelewa na msimamo wa
pamoja kuhusu utekelezaji wa Ilani na Sera hizi.
Chama kuendelea kuimarisha usimamizi wa kazi na shughuli za Serikali
kupitia Bunge, Baraza la Wawakilishi na Halmashauri zinazohusika.
Chama Kusimamia Utekelezaji wa Ilani
132
224. Mara kwa mara Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kinaelekeza vyema kazi ya
    Chama ya kuongoza na kusimamia kwa vitendo shughuli za Chama na Serikali.
   Pamoja na ukweli kwamba maelekezo yatolewayo ni mazuri, utekelezaji wake
  umekuwa ukilalamikiwa. Moja ya sababu ya mapungufu katika utekelezaji ni
 Chama kutotimiza jukumu lake la kuongoza kikamilifu kwa kuweka methodolojia
sahihi za kufuatilia, kudhitibi na kufanya tathmini. Mwelekeo wa Sera za Chama
Cha Mapinduzi katika Miaka 2010 hadi 2020 unaelekeza tuondokane na tatizo hili
kwa kuweka utaratibu wa ufuatiliaji. Kwa hakika jukumu la Chama ni pamoja na
kutoa lengo, lakini ili lengo hilo lifanikiwe Chama lazima kihakikishe uhamasishaji
umma, usimamizi wa utekelezaji na kufanya tathmini.
225. Katika kutekeleza jukumu la kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Ilani katika
    kipindi cha Ilani hii 2010 hadi 2015 Chama Cha Mapinduzi kitatumia utaratibu na
   methodolojia ifuatayo:-
(a) (b) Aidha kwa upande wa Chama mjadala wa Utekelezaji wa Ilani
       utaendeshwa kupitia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC),
      Halmashauri za Mikoa (REC), na Wilaya (DEC). Chama kitajadili programu
     ya utekelezaji wa Ilani na kazi ya kufanya na uhamasishaji wananchi
    katika ngazi zote.
(c)
226.
Viongozi wa Chama na Serikali watawezeshwa kupata uelewa wa pamoja
wa Sera na dhana husika. Chama kitasimamia suala hili kwa kuendesha
Mafunzo Elekezi na vikao kwa Watendaji Wakuu wa Serikali (Baraza la
Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Mikoa). Aidha, mara
baada ya uchaguzi Ilani itajadiliwa kwa kina na Serikali itaandaa programu
au ajenda ya utekelezaji wa Ilani.
Chama kitaweka utaratibu wa kufanya mapitio ya utekelezaji wa Ilani
mara moja kila mwaka, kwa Halmashauri Kuu (NEC) kujadili na kufanya
tathmini ya utekelezaji. Aidha Chama kitasimamia utekelezaji wa jukumu
la kikatiba la Serikali kutoa taarifa kila mwaka.
Kimsingi utekelezaji wa Ilani hii utafanikiwa kama Chama kitatekeleza jukumu
lake la kusimamia kwa kuhakikisha kuwa programu ya utekelezaji inaandaliwa na
kusimamiwa ipasavyo. Inawezekana kujenga Maisha Bora kwa kila Mtanzania na
Tanzania yenye Neema Tele kama Uongozi wa sasa wa Chama utabadilika
kiutendaji, kimsimamo na kimtazamo.
133
134

1 comment:

  1. This is a very valuable thing shared, I just want to thank for letting us know about this wonderful blog.
    https://blog.mindvalley.com/circle-of-concern/

    ReplyDelete