Thursday, September 30, 2010

IFUATAYO NI ILANI YA CUF

CUF
Rais makini, Serikali makini
Uchumi Imara, Mabadiliko Sahihi
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
The Civic United Front
(CUF-Chama Cha Wananchi)
Yaliyomo
1.     Utangulizi wa Prof Ibrahim Lipumba ........................ . . . . . . . . . . . . . . .     7
2.     Misingi mikuu ya uongozi wa nchi ........................ . . . . . . . . . . . . . . . . .     18
3.     Hali ya maisha ya mtanzania na sekta muhimu za uchumi .. . . . . . . . . . . .     50
4.    Elimu ....................... . . . . . . . . . . . . . . . . ....................... . . . . . . . . . . . . . .     60
5.    Afya ....................... . . . . . . . . . . . . . . . . ....................... . . . . . . . . . . . . . . .     64
6.     Ardhi na Maendeleo ya makazi . . . . . . . ....................... . . . . . . . . . . . . . . .     66
7.     Matumizi ya teknolojia za kisasa . . . . . . . ....................... . . . . . . . . . . . . .    
8.     Hifadhi ya jamii na maendeleo ya makundi ya wanawake,
H
     aki za watu wenye ulemavu, wazee, na vijana .......... . . . . . . . . . . . . . . .     73
9.     Utamaduni na Michezo .......... . . . . . . . . . . . . . .......... . . . . . . . . . . . . . ........     75
2
3
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
SEHEMU YA KWANZA
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
Katiba ya sasa haikidhi maendeleo ya demokrasia nchini mwetu. Chini ya Dira ya Mabadiliko
ya CUF – Vision for Change, Serikali ya umoja wa kitaifa itaandaa utaratibu unaofaa wa kupata
Katiba ya mpya ya wananchi yenye misingi imara ya demokrasia.
UTANGULIZI 2.  kutokomeza njaa na kuhakikisha lishe Bora kwa wajawazito na watoto;
Kwa mara nyingine tena ifikapo Oktoba 2010 wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na uwezo au kuwezeshwa kupata milo mitatu kwa
tutapiga Kura kuchagua Rais, Wabunge, na Madiwani wa nchi yetu. Huu utakuwa ni Uchaguzi siku. Hatua za makusudi zitachukuliwa kuhakikisha kuwa kinamama wajawazito na watoto
Mkuu wa nne kufanyika nchini chini ya mfumo wa vyama vingi. Tunaelekea kwenye uchaguzi wachanga wanapata lishe bora itakayowasaidia kujenga maungo, kinga ya mwili na ubongo ili
mkuu wakati nchi yetu ikiwa njia panda. Watanzania wamechoshwa na hadaa na ngulai za CCM. waweze kushiriki kikamilifu katika kujielimisha na kujiendeleza.
Umaskini unaongezeka, ajira zimetoweka, ufisadi na rushwa vimekithiri. Ahadi ya CCM ya mwaka
2005 ya “Maisha bora kwa kila Mtanzania” imeishia kuwa Maisha bomu kwa kila Mtanzania.
    Serikali ya CCM imeshindwa kuboresha maisha ya Mtanzania. Hali ya maisha imezidi kuwa ngumu.
    Mwaka 2005 kilo moja ya sukari iliuzwa shilingi 500/- lakini hivi sasa inauzwa shilingi 1800/- na
    vijijini ni zaidi ya shilingi 2000/-, mchele ulikuwa unauzwa kilo moja shilingi 450/- lakini hivi
    sasa unafika shilingi 1700/-, kilo moja ya sembe ikiuzwa shilingi 250/- lakini hivi sasa ni shilingi
    900/-, Wafanyakazi wanapodai kuongezewa mishahara kwa sababu ya kupanda kwa gharama za
    maisha wana sababu za msingi kabisa kufanya hivyo kutokana na hali halisi ya kupanda kwa
    gharama za maisha. Ufisadi na rushwa zinaendelea kuimarika nchini na CCM imegawika mapande
    mapande. Watanzania tutajuta ikiwa tutaruhusu wizi wa kura na kuipa fursa CCM kuendelea
    kutawala. CCM haina dira ya kuongoza nchi na kusimamia utawala bora. Imeshindwa kutumia
    utajiri mkubwa tulionao wa raslimali na maliasili ya Taifa kwa manufaa ya wananchi wote na
    badala yake leo Tanzania imegeuka kuwa omba omba na Matonya wa kimataifa.
Watanzania wameweka matumaini yao kwa Chama cha CUF na misingi yake ya sera ya kuleta Serikali inatakayoongozwa na CUF itatenga fungu maalum la kuwasaidia walemavu wapate elimu,
“Haki sawa kwa wananchi wote” na “Kujenga uchumi imara unaoongeza ajira na utakaoleta matibabu na vifaa vya kuwapunguzia dhiki ya ulemavu walionao na mafunzo stahiki waweze
      neema na tija kwa wote.” Chama chetu kimekuwa ni Chama kikuu cha upinzani nchini kwa muda kuajirika na kuajiriwa katika fani mbali mbali. Hii inatokana na ukweli kwamba Watanzania zaidi
        mrefu sasa na wananchi wanaendelea kuteseka kwa kuona matatizo yao yakizidi kuongezeka bila ya milioni 4.2 sawa na asilimia 10 ya Watanzania wote ni watu wenye ulemavu. Watu wenye
        kuchukuliwa kwa hatua za msingi kushughulikia matatizo yao. Hali hii inawafanya wananchi ulemavu wana mahitaji sawa na watu wengine lakini pia wanakuwa na mahitaji mengine zaidi
        wengi hasa vijana na wanawake kuwa katika shauku kubwa ya kuona utawala wa nchi yetu kulingana na aina ya ulemavu walio nao.
        unabadilishwa kwa amani kupitia karatasi za kura. CUF kwa kutambua nafasi yake katika
        kuyaongoza Mabadiliko yanayohitajika kikiwa siyo tu chama kikuu cha upinzani hapa nchini
        bali pia kutokana na mjengeko wake wa kuwa kweli ni chama cha kitaifa chenye kukubalika na
        chenye mtandao mpana katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano, imezindua DIRA YA
        MABADILIKO - VISION FOR CHANGE. Dira ya Mabadiliko ndiyo msingi wa ILANI yetu ya uchaguzi.
        Vision for Change chini ya Serikali ya CUF itatujengea Tanzania Mpya inayojali haki sawa kwa
        wananchi wote na itakayojenga uchumi imara unaoongeza ajira na utakaoleta neema na tija kwa
        wote. Mambo muhimu yaliyobebwa na Dira ya Mabadiliko ni haya yafuatayo;
1.  Kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa;
CUF itaunda serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kuimarisha Demokrasia ya kweli na ushindani
wa kisiasa kwa ajili ya kuwatumikia vyema wananchi wote katika misingi ya haki sawa kwa
washiriki wote, na uwepo wa uhuru wa kutosha wa vyombo na fursa ya kujieleza. Tunahitaji
kuwa na katiba nzuri inayompa kila mtanzania uhuru wa kweli wa kuchagua na au kuchaguliwa.
Tunahitaji kuwa na Muungano wa watanganyika na wazanzibari usio na mashaka ndani yake kwa
pande zote mbili. Tunahitaji Umoja wa kitaifa wa kweli ambapo hakutakuwa na ubaguzi wa aina
yeyote iwe ni wa jinsia, kabila, rangi, dini au ulemavu. Kuhakikisha kuwa serikali inaheshimu
dini zote na inajenga mazingira ya waumini wa dini mbali mbali kuheshimiana na kuvumiliana.
4
3.  kutoa huduma bora ya Afya na kudhibiti vifo vya wajawazito na watoto;
Kuhakikisha kuwa kila raia ana haki na anapata huduma za msingi za afya. Hatua maalum
zitachukuliwa kuhakikisha kuwa huduma za uzazi bila malipo anapatiwa kila mama mjamzito ili
kupunguza vifo vingi vinavyotokea ambavyo vinadhibitika.
4.  kuwahudumia wazee waliolitumikia Taifa letu;
kuweka utaratibu wa kitaifa wa hifadhi ya wazee itakayohusisha jamii kuwalea wazee wetu
ambao wengi wao baada ya kulitumikia Taifa letu kwa muda mrefu wanaishi katika dimbwi la
umasikini wa kutisha.
5.  kuwasaidia walemavu na kuwawezesha kupata elimu na ajira;
6.  Usimamizi wa elimu bora na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano;
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa watoto wote wa Tanzania wanakuwa na haki ya kupata elimu
bora ya msingi, elimu ya sekondari na elimu ya juu. kila raia ajiendeleze kielimu hasa kwa
kutumia vizuri teknolojia ya habari na mawasiliano. Serikali itakayoundwa na CUF chini ya Dira
ya Mabadiliko itatoa kipaumbele maalum katika kuwaendeleza kielimu wasichana na kujenga
misingi imara ya kuendeleza elimu ya hisabati, sayansi na teknolojia.
7.  Kusimamia maendeleo ya kiuchumi nchini;
Kujenga uchumi wa kisasa wenye ushindani kimataifa na utakaohimili misukosuko ya utandawazi,
unaokua kwa kasi bila kuharibu mazingira na wenye manufaa kwa wananchi wote. Kukua kwa
uchumi kunahitaji uongozi imara na utawala makini, mikakati na mipango mizuri ya maendeleo na
utekelezaji mzuri wa mikakati na mipango hiyo. Kuweka misingi ya utawala bora na utekelezaji wa
sera utakaohakikisha kuwa uchumi unakua kwa asilimia 8–10 kwa miongo mitatu (miaka 30) ijayo.
8.  Usimamizi makini katika sekta ya kilimo na maendeleo ya viwanda;
Dira ya Mabadiliko ya CUF inakipa kilimo nafasi ya pekee katika mikakati ya kukuza uchumi na
hivyo kuwaondolea umasikini wananchi wengi na hasa wa vijijini, kuhakikisha Taifa linakuwa
5
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
na chakula cha kutosha na ziada ya kuuza nje ya nchi. Katika miaka mitano ijayo, Bajeti ya
sekta ya kilimo chini ya serikali ya CUF itakuwa kati ya asilimia 10 – 15 ya bajeti yote na
italenga katika kuimarisha maeneo yafuatayo; utafiti na elimu kwa wakulima na huduma za
ugani, upatikanaji wa mbolea na pembejeo nyingine kwa bei nafuu, masoko ya uhakika, bei
nzuri kwa wakulima, kutengeneza barabara za vijijini, kusambaza umeme vijijini kwa kutumia
nishati mbadala kama vile biogas inayotokana na mabaki ya mimea na vinyesi vya mifugo, jua
na upepo. Dira ya Mabadiliko ya CUF inakusudia kuasisi Mapinduzi ya kweli ya kilimo nchini,
yatakayoongeza uzalishaji na tija kwa kuijenga upya sekta ya maendeleo ya viwanda. Serikali ya
CUF itaweka mkakati madhubuti wa kuanzisha na kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi ya
ndani na kuajiri watu wengi kama vile viwanda vya nguo na mavazi, viatu na bidhaa za ngozi,
vifaa vya matumizi ya nyumbani na vifaa vya umeme na elektroniki.
9.  kuimarisha miundo mbinu na kuhamasisha uwekezaji;
Mafanikio ya kiuchumi kwa Taifa lolote lile hutegemea mfumo wa kisera na uwekezaji wa serikali
katika sekta muhimu. Serikali ya CUF itawekeza kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha miundo
mbinu- barabara, reli, bandari, mawasiliano, nishati, maji, elimu na afya. Hii itasaidia kuvutia
sekta binafsi kuwekeza katika shughuli za uzalishaji na biashara.
10.  Usimamizi wa Rasilimali za Taifa na Nidhamu ya matumizi ya fedha za umma;
Kujenga mfumo mzuri wa usimamizi na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma. Kuondoa
misamaha holela ya kodi na ukwepaji wa kulipa kodi. Kuhakikisha kuwa sekta ya madini
inachangia asilimia 30 ya thamani ya mauzo ya madini kama mapato ya serikali. Kupambana
na rushwa na ufisadi kuhakisha kuwa maliasili na raslimali za taifa zinatumiwa kwa umakini
mkubwa na kwa manufaa ya wananchi wote.
Mathalani, Tathmini na uhakiki wa kina wa fedha za msaada wa dola milioni 60 uliotolewa na
serikali ya Norway katika Wizara ya Maliasili na Utalii katika kipindi cha miaka 12 uliofanyika
mwaka 2006 unaonyesha kuwa nusu ya fedha hizo, yaani dola milioni 30, ziliibiwa au kutumiwa
kifisadi. Tatizo la matumizi mabaya ya fedha haliko Wizara ya Maliasili na Utalii tu bali limetapakaa
serikalini kote. Mhe Rais Dk Jakaya M. Kikwete alipokuwa anafungua mkutano wa TAKUKURU
alieleza asilimia 30 ya matumizi yote ya serikali kila mwaka yanaibiwa au kutumiwa kifisadi. Hii ni
sawa na shilingi trilioni 11.8 kwa bajeti ya serikali ya mwaka 2006/7-2010/11, fedha inayotosha
kukamilisha mradi ya kufua umeme Mega watts 2000 na kujenga barabara za lami zenye urefu wa
kilomita 4000 na kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa serikali.
Mimi binafsi kama Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CUF nawaahidi Watanzania nikichagukliwa kuwa
Rais nitajiwekea lengo la kuijengea heshima nchi yangu kwa kuimarisha utawala bora na adilifu na
kukuza uchumi unaotoa ajira kwa wingi na kuleta neema kwa wananchi wote. Kazi hii nitaifanya
kwa uadilifu wa hali ya juu na kuhakikisha kuwa kwa mara ya kwanza Rais wa Tanzania atakapos-
taafu aweze kupata tuzo ya Mo Ibrahim ya kuongoza nchi vizuri kwa kuheshimu na kulinda haki za
binadamu, kupambana na ufisadi kwa mafanikio, kukuza uchumi na kuutokomeza umaskini.
ZINDUKA MTANZANIA, IPIGIE KURA CUF, ISIMAMIE MABADILIKO UYATAKAYO.
HAKI SAWA KWA WOTE
Prof Ibrahim H. Lipumba
6
SEHEMU YA PILI
MISINGI MIKUU YA UONGOZI WA NCHI
Katiba, Utawala wa Sheria, Mahakama, Haki za Binaadamu, Uongozi Madhubuti wa
Utumishi a Umma, Mapato wa kodi na Nidhamu na Matumizi ya Serikali, Mapambano
Dhidi ya Rushwa, Ulinzi na Usalama na Masuala ya Mambo ya Nchi za Nje.
KATIBA
•  Katiba ni SHERIA MAMA na ni mkataba maalum baina ya viongozi nchi na raia wake. Raia
wana jukumu la kuamua ni nani miongoni mwao akabidhiwe mamlaka ya kuongoza Serikali
kwa maslahi ya Taifa zima. Katiba inapaswa kukusanya na kuelekeza mambo yote ya msingi na
itakayodumu kwa muda mrefu bila ya kufanyiwa marekebisho kila uchwao.
•  Katiba inatakiwa kukusanya masuala yote yanayowaunganisha wananchi wote bila kujali
itikadi za vyama au namna nyingine yeyote ile na kuhakikisha inafumwa katika hali ya
kuzingatia kuboresha maisha ya watu wote na kulinda haki zote za raia na kuyapa fursa sawa
makundi yote na mtu mmoja mmoja aliyeko ndani ya nchi bila upendeleo.
Hali ilivyo sasa;
Katiba tuliyonayo haikidhi matakwa ya wakati wa sasa;
•     Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoandikwa mwaka 1977 ni katiba iliyotungwa
katika kipindi cha mfumo wa chama kushika khatamu na ilikuwa na malengo ya wakati huo.
Ni katiba ambayo haikuwahusisha wananchi wakati wa kuandaliwa kwake. Maoni ya tume ya
Jaji Nyalali na Jaji Kisanga hayakuzingatiwa na wenye nchi yao (watanzania) hawajapatapo
kutoa maoni yao na kuheshimiwa. Katiba tuliyonayo haikidhi matakwa ya demokrasia ya
wakati wa sasa na inawanyima raia haki za msingi za kugombea uongozi bila kupitia chama
chochote cha siasa. Katiba tuliyonayo ina mikanganyiko mingi kiasi cha kujitokeza haja na
ulazima wa kutakiwa kuandikwa upya.
•     Kumekuwepo na malalamiko kutoka pande zote mbili za Jamhuri juu ya Muundo na utekelezaji
wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Pamoja na jitihada zilizochukuliwa za kujaribu
kuyapatia ufumbuzi matatizo na kasoro au kero hizo bado hakujapatikana ufumbuzi wenye
kuleta tija na kuimarisha Muungano wetu bali kuongeza mashaka zaidi ya kustawi na kuimarika
kwa Muungano wetu. Hata hivyo marekebisho yote ambayo yamekwishafanyika hadi sasa kwenye
katiba iliyopo hayajazingatia uwepo wa tatizo hili. Kwa kiasi kikubwa katiba haiheshimiwi na
kufuata ipasavyo isipokuwa pale tu maslahi binafsi au ya makundi yanapojitokeza.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa;
Baada ya miezi mitatu ya kuingia madarakani, uongozi wa nchi utaanzisha mchakato wa
uandaaji wa katiba mpya ya wananchi itakayoandaliwa kwa kushirikisha wadau wote katika
mjadala wa kitaifa ikiwa ni pamoja na wataalamu wa katiba, vyama vya siasa, madhehebu
mbalimbali ya dini, wakulima, wafanyakazi, taasisi zisizokuwa za kiserikali, wanafunzi,
7
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
makundi mbalimbali ya jamii.
•     kama walemavu, vijana, wanawake, wazee, na kadhalika. Maoni yatakayokusanywa katika
mjadala huu ndiyo yatakayokuwa msingi mkuu wa maandalizi ya rasimu ya katiba mpya na
kuzingatia matakwa ya misingi ya demokrasia ya kweli na uendeshaji wa nchi hapo baadaye
kwa chama chochote kitakachopewa ridhaa ya kuongoza nchi. Katiba mpya itapatikana katika
kipindi cha Bunge la mwaka 2012 na uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka 2014 na
uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 utafanyika nchi ikiwa na katiba mpya.
•     Itaandaa utaratibu wa kushughulikia kikatiba masuala yote yanayohusiana na Muungano wa
nchi mbili kati ya Tanganyika na Zanzibar. Katiba mpya itabainisha wazi kuwa muundo wa
Muungano ni ule ulioainishwa katika madhumuni ya makubaliano ya Muungano ya mwaka
1964, yaani kuwa na Serikali tatu.
•     Utekelezaji wa mambo yote yaliyoongezwa katika orodha ya mambo ya Muungano baada ya
makubaliano ya awali ya mwaka 1964 yaliyounda Muungano, yatajadiliwa kwa kina mpaka
kufikia muafaka juu ya mambo hayo.
UTAWALA WA SHERIA
•     Utawala wa sheria ni kuendesha mambo kwa kuheshimu, kulinda na kufuata katiba na sheria
nyingine za nchi. Utawala wa sheria hauna huruma kwa mtu yeyote atakayekwenda kinyume
na matakwa ya sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria, utawala wa
sheria unamfanya kila mwananchi aziheshimu sheria na kuzifuata kwa ukamilifu wake.
Hali ilivyo sasa;
•     Kuna muonekano wa juhudi za kufuata utawala wa sheria kwa kiasi fulani kwa   ngazi za
kitaifa hata hivyo kwa ngazi za wilaya na vijiji hali bado ni mbaya mno. Matumizi ya vitisho,
mabavu, na ukatili wa hali ya juu na tabia ya kubambikizwa kesi na kukosa haki zote za
msingi za mtuhumiwa ni vitendo vya kawaida kufanywa na sehemu kubwa ya viongozi wa
ngazi za kata na vijiji.
•     Katiba na sheria nyingine za nchi zimekuwa zikifuatwa tu pale ambapo panaonekana kuna
maslahi binafsi ya wahusika, matumizi ya fedha yamekuwa ndio msingi wa kupata haki na
kama huna fedha hupati haki hata ikiwa haki hiyo ni stahiki yako.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•     Serikali ya CUF itahakikisha kuwa inafuta sheria zote kandamizi na kuhakikisha haki za kila
raia zinalindwa kikamilifu na kuheshimu utawala wa sheria na kulinda haki za binaadamu.
Serikali ya CUF itaongozwa kwa misingi ya kufuata kikamilifu katiba na sheria katika
utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku na si vinginevyo.
IDARA YA MAHAKAMA
Hali ilivyo sasa;
•     Idara ya mahakama imekuwa ikilalamikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa haki hazipatikani
kirahisi. Pamekuwepo ucheleweshwaji wa usikilizwaji wa kesi na watuhumiwa wamekuwa
wakikaa mahabusu kwa muda mrefu bila mashtaka yao kusikilizwa kwa haraka. Maslahi ya
8
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
watendaji wa idara ya Mahakama ni duni na mahakama zetu zimekuwa na tatizo la muda
mrefu la kuwa na vitendea kazi visivyotosha, majengo chakavu na kuwa makazi ya popo na
mvua ikinyesha hapakaliki na hakuna matumizi ya teknolojia ya kisasa ya usikilizaji wa kesi
na ufuatiliaji wa mwenendo wa mashtaka. Mahakama kutokana na muundo wake inakosa
uhuru kamili wa kuiendesha idara hiyo. Aidha, malalamiko ya wananchi ni kuwa vitendo vya
rushwa na ufisadi vimekithiri sana katika mahakama zetu.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
Serikali ya CUF itahakikisha unaandaliwa mfumo wa mahakama utakaompa haki kila
mwananchi;
•     Itaihakikishia idara ya mahakama uhuru wa kutosha katika kuendesha na kutoa maamuzi
yake. Ili suala hili liwe wazi na lisilo na utata wowote, katiba itatamka wazi kuwa Mahakama
ndio taasisi yenye uamuzi na usemi wa mwisho juu ya suala lolote la kisheria.
•     Itaandaa katiba itakayotamka wazi kuwa ni ukiukwaji wa Katiba kwa Serikali kuvunja agizo,
amri, au hukumu yoyote ambayo imeshapitishwa na Mahakama.
•     Itaanzisha utaratibu ambapo baada ya uteuzi wa majaji wote (ikiwa ni pamoja na Jaji mkuu)
na wasajili wa Mahakama Kuu na ile ya rufani watapaswa kuthibitishwa na Bunge.
•     Itaboresha maslahi ya watendaji wa idara ya mahakama kwa ujumla, kuongeza ajira ya
watendaji zaidi wenye uwezo na kuanzisha mfumo wa kisasa wa matumizi ya teknolojia katika
uendeshaji wa kesi.
•     Itafanya marekebisho ya sheria ili makosa madogo madogo yasiwe na hukumu za vifungo, na
badala yake yawe yanalipiwa faini tu au kufanya kazi yoyote ya maendeleo itakayoamuliwa
na mahakama iwapo mtuhumiwa atakuwa hana faini ya kulipa.
HAKI ZA BINADAMU
Uvunjifu na ukiukwaji wa Haki za binadamu ni tatizo kubwa nchini Tanzania. Hakuna chombo
huru chenye nguvu cha kusimamia haki za binadamu. Tume ya haki za binadamu haina nguvu
za kuweza kupambana na wavunjaji wa haki za binadamu wanaolindwa ambao miongoni mwao
ni watendaji wakuu wa Serikali.
Hali ilivyo sasa;
Kumekuwepo na mapungufu makubwa katika upatikanaji wa haki za binaadamu baadhi yake
ikiwa ni haki ya ajira mathalani; migogoro iliyodumu kwa muda mrefu sasa kati ya wafanyakazi
na waajiri katika mashirika kama TRL, TTCL na NBC iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki ni
kielelezo halisi cha hali hii. Na hata pale wanapodai maslahi yao wamekuwa wakikumbana
na vijembe vya kutolewa ng’eu, kupata kichapo cha mabomu ya moshi, na hata kubezwa kwa
kuambiwa kura zao hazihitajiki wapige au wasikipigie chama kinachoongoza Serikali kwa sasa.
Watanzania wengi wasio wanachama wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa hawana haki ya
kushiriki katika siasa kikamilifu kwa kuwa na haki ya kuchaguluwa kuwa viongozi.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
Ni dhamira ya dhati ya Serikali itakayoundwa na CUF kurejesha thamani ya utu na haki za kila
9
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
Mtanzania nchini, Serikali ya CUF; Itahakikisha kuwa inasimamia mchakato wa kuwa na katiba
mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwemo ndani yake kipengele kinachohusiana
na uwepo wa TUME HURU YA HAKI ZA BINADAMU na kwamba,
—    Tume itakuwa na jukumu la kuchunguza ukiukwaji wa maadili na haki za binadamu na
kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kurudisha haki hizo kwa walionyimwa na kuwafikisha
mahakamani wale wote watakaoonekana kuwa na makosa ya uvunjaji wa haki hizo.
—    Tume itakuwa na haki ya kuwaita na kuwahoji watuhumiwa wa uvunjifu wa haki za
binadamu, bila kuomba kibali kwa mtu au Taasisi yoyote, ikiwa ushahidi ulioko mbele
yake utaonyesha kwamba ni muhimu kufanya hivyo au baada ya kuombwa kufanya hivyo
na mwathirika au mwakilishi wa mwathirika.
—    Tume itakuwa huru – bila kuwa na mfungamano wowote wa kisiasa na wajumbe wake
watapatikana kwa kuteuliwa na Rais na kuidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
—    Tume itakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitano na kila mwaka itapeleka taarifa
ya kazi zake katika Bunge ambako zitajadiliwa. Wajumbe wa Tume ya Haki za Binadamu
watakaa madarakani kwa vipindi visivyozidi viwili.
•     Itaanzisha sheria itakayoibana Serikali juu ya mwenendo wa kujitwalia kwa nguvu maeneo
mbalimbali ya wananchi bila kuingia katika majadiliano ya kina na hatimaye kufikia
makubaliano na wananchi wa eneo husika.
•     Itaanzisha sheria inayokataza vyombo vya dola kutumiwa na wanasiasa au maafisa wenyewe
wa vyombo hivyo kushambulia wananchi wanaoandamana au kugoma kwa njia za amani,
aidha wananchi watakuwa na haki ya kulalamika kwa njia mbali mbali za amani ikiwemo
maandamano, mikusanyiko, na migomo.
•     Itaanzisha sheria inayowataka waajiri wote kuwa na mikataba huru na wafanyakazi wao.
•     Itahakikisha kuwa katiba mpya inaeleza wazi kuwa vyombo vya habari baada ya kujisajili
kama kampuni na kupata leseni ya biashara havitasajiliwa na taasisi nyingine yoyote ya
Serikali wala kuwekewa mipaka ya kijiografia katika utendaji na usambazaji wa shughuli zake
ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
•     Itahakikisha kuwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakuwa na kipengele
kinachoruhusu mtu yeyote kuwa mgombea katika nafasi yoyote ya uchaguzi bila kupitia
chama cha siasa.
•     Itahakikisha kuwa masuala ya haki za binadamu yanakuwa ni sehemu ya mitaala ya somo la
uraia mashuleni katika ngazi za elimu ya msingi na sekondari kwa madhumuni ya kukuza uelewa
juu ya haki za binaadamu tangu awali waweze kujua wajibu na haki zao na za watu wengine.
UONGOZI MADHUBUTI WA UTUMISHI WA UMMA;
Nchi ambazo zimefanikiwa kukuza uchumi kwa kasi ya juu na kuwa na maendeleo kwa muda
mrefu zimefanya hivyo kwa kuwa na uongozi adilifu wenye dira na ulio imara katika uamuzi,
utekelezaji na kujifunza kutoka kwenye makosa waliyoyafanya nyuma na kujirekebisha.
Uongozi wa nchi unawajibika kubuni sera kwa kuzingatia uhalisia na hali ya uchumi wa nchi,
fursa zilizopo na vikwazo vinavyoikabili nchi katika kukuza uchumi wake. Uongozi makini
utakaoweza kuchochea maendeleo ya muda mrefu unapaswa kuwa na subira, uwe na dira
na mipango ya muda mrefu na ujikite katika lengo la kukuza uchumi utakaoleta neema kwa
10
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
wananchi wote Imethibitishwa kwamba maendeleo ya nchi yetu yamekuwa yakiathiriwa mno
na matatizo ya wafanyakazi wa Serikali kutozingatia kwa kiasi kikubwa, kanuni, sheria na
uwajibikaji.
Hali ilivyo sasa;
Uwajibikaji na nidhamu kwa baadhi ya maofisa wa serikali viko chini na huduma inayoweza
kutolewa kwa saa chache inaweza kuchukua miezi kadhaa kupatikana. Matakwa ya kisiasa
yameingilia sana mfumo wa upatikanaji wa watendaji wakuu katika utumishi wa umma wa
serikali, na wizi na ubadhilifu wa fedha za umma vimekuwa vikiendelea kwa muda mrefu bila
kukemewa na kuchukuliwa hatua stahiki.
Dira ya Mabadiliko ya CUF
•     CUF Itaunda Serikali ya umoja wa kitaifa itakayoleta viongozi kutoka nyanja mbalimbali bila
kujali itikadi zao za kisiasa. Hili litafanyika ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania mwenye
uwezo anapewa nafasi ya kuiletea nchi yake maendeleo na kusimamia vyema nidhamu na
uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa manufaa ya Taifa letu.
•     Itaimarisha usimamizi. Ili kulifanikisha hili itaanzisha idara maalumu ya Msimamizi Mkuu wa
Huduma za Serikali (Inspector General of Government Services), ambayo itakuwa na jukumu
la kuchunguza na kufuatilia utendaji kazi wa vyombo vya Serikali, pamoja na kushughulikia
malalamiko ya wananchi ili kuhakikisha maafisa na vyombo vya Serikali wanatenda kazi zao
kwa ufanisi bila usumbufu kwa wananchi. Ofisi hii itafuatilia kila penye kulalamikiwa na
kuhakikisha kwamba kanuni za kazi zinafuatwa kwa ufanisi, hakuna upendeleo, na kwamba
maamuzi yanafanywa kwa kutumia vigezo kufanikisha malengo ya Taifa.
•     Itabadili mfumo wa kuwapata watendaji wakuu wa Serikali. Pamoja na kuweka utaratibu
wa usimamizi mzuri wa shughuli za Serikali itaweka utaratibu ambapo Serikali inapata
watendaji wakuu wenye uwezo na walio bora.
VIONGOZI WA KUCHAGULIWA;
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa ili kupata viongozi wazuri kuanzia Serikali kuu hadi Serikali
za mitaa. Katiba mpya itaweka bayana kuwa chaguzi zote zitakuwa huru na za haki na
zitasimamiwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa iliyo Huru na yenye kutenda haki. Wajumbe wa
Tume wapatikane kwa kupendekezwa na vyama vyote vya siasa vyenye uwakilishi bungeni
(kwa idadi sawa kwa kila chama) na baada ya hapo wathibitishwe na Bunge. Mwenyekiti wa
Tume achaguliwe kwa kura na Wajumbe wenzake kila baada ya miaka mitano.
VIONGOZI WA KUTEULIWA;
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa katiba inaweka bayana kuhusiana na Jukumu la uteuzi wa
viongozi waandamizi unafanywa na Rais na kuthibitishwa na Bunge kwa kufuata utaratibu
ufuatao:
•     Rais atakuwa na jukumu la kuteua Baraza la Mawaziri la Muungano, Makatibu Wakuu wa
Baraza hilo, Mwanasheria Mkuu, Msimamizi Mkuu wa shughuli za Serikali na Wakuu wa Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vya Jamhuri ya Muungano.
•     Rais ataendelea na uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wa Tanzania Bara hadi hapo Serikali
11
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
ya Tanganyika itakapoundwa ambapo jukumu la uteuzi wa Viongozi hao litahamia kwa Rais
wa Serikali hiyo mpya.
•     Tume ya Ajira Serikalini itatoa mapendekezo ya uteuzi wa watendaji wakuu wengine wote
katika idara, Mamlaka, na Tume za kudumu za Serikali baada ya nafasi husika kutangazwa
na usaili kwa waombaji kufanyika. Rais atateua watendaji kwa kuzingatia mapendekezo
ya Tume. Aidha Tume hii itahusika na kutoa mapendekezo ya uteuzi wa Bodi za Mashirika
mbalimbali ya Serikali kwa kuzingatia vigezo vya kitaalamu.
MATUMIZI YA SERIKALI.
Kasi ya maendeleo siku zote huamualiwa na mipango mizuri katika kuchagua vipaumbele
wakati wa kuwekeza mtaji uliopo.
Hali ilivyo sasa;
Matumizi mabaya ya fedha za umma;
Kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi (wananchi) zimekuwa zikitumiwa na Serikali kugharamia
matumizi ambayo hayana manufaa kwa Taifa. Wingi wa safari za viongozi nje ya nchi, matibabu
ya viongozi hao na familia zao nje ya nchi, na mafao makubwa yanayolipwa kila mwaka kwa
viongozi hao wanapostaafu, matumizi yasiyokuwa na uzingatiaji wa vipaumbele. Serikali ya
CCM ina maradhi sugu ya kushindwa kutambua maeneo ya kupewa kipaumbele kwenye matumizi
yake. Matahalani tukitaja maeneo machache;
•     Kitendo cha Serikali kutumia shilingi bilioni 46 kununulia ndege ya Rais, CUF tunaamini kuwa
haikuwa sahihi wakati idadi ya vitanda katika hospitali zetu haitoshelezi mahitaji na hakuna
huduma bora za afya kwa watanzania.
•     Kitendo cha Serikali kutumia zaidi ya shilingi bilioni 40 kununua Rada ni ukatili mkubwa kwa
wananchi masikini ambao wanakufa njaa ndani ya nchi. Fedha hizo zingeweza kununua matrekta
madogo “power tillers” zaidi ya 20,000 ambayo yangewasaidia wakulima wanaotaabika kwa
jembe la mkono, nah ii inamaanisha kuwa kila kijiji nchini kingeweza patiwa trekta moja na
zaidi ya asilimia 80 ya vijiji vingepata matrekta mawili.
•     Mhe. Kikwete akifungua Mkutano wa TAKUKURU alikiri kuwa asilimia 30 ya matumizi yote ya
Serikali yanaibiwa kifisadi. Hii ni sawa na zaidi ya shilingi trilioni 11.5 kwa kipindi cha miaka
mitano ya awamu ya nne. Fedha hizi zinatosha kutengeneza barabara za lami za kilomita
4000 na kujenga mitambo ya kufua umeme wa Mega watts 2000 kwa kutumia maporomoko
ya maji na gesi na kujenga hospitali yarufani ya kisasa na vyuo vikuu viwili vya sayansi na
teknolojia na na kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa Serikali.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•     Serikali ya CUF itatumia fedha za wananchi kwa umakini na imedhamiria kupunguza kwa kiasi
kikubwa gharama za kujiendesha ili fedha zitakazookolewa zielekezwe zaidi kwenye kujenga
miundombinu hasa barabara, reli, umeme, maji, bandari na mawasiliano ya kompyuta,
kuboresha huduma za jamii moja kwa moja na kuimarisha au kuanzisha miradi mipya ya
maendeleo. Pamoja na mambo mengine hatua zifuatazo zitachukuliwa ili kufanikisha malengo
haya kama ifuatavyo:
•     Kupunguza Ukubwa wa Serikali; marekebisho yatafanyika na kuwa na wizara 15-20 na baada
12
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
ya utafiti wa kina wafanyakazi watakaoonekana kuwa wa ziada watapewa mafunzo mapya na
ajira yao kuhamishiwa katika sekta nyingine.
•     Serikali Ya CUF katika mwaka wa kwanza itawekeza kwenye teknolojia ya kisasa ya kompyuta
na mtandao utakaounganisha idara zote za Serikali ili kuongeza ufanisi katika utendaji.
•     Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima; Ili kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima utaratibu wa
‘zero budgeting’ utafuatwa ambapo kila kipengele cha matumizi kinakuwa kimeelezwa uhalali
wake kabla ya kukubaliwa.
•     Kupunguza Marupurupu na Mafao ya Viongozi; Katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi
vya siasa, uwezekano wa kuwa na viongozi wakuu wengi wastaafu ni mkubwa sana, na hivyo
kulisababishia Taifa kuwa na mzigo mkubwa katika kuwahudumia. Mathalani, kwa sasa Serikali
za CCM (Muungano na Zanzibar) zinahudumia viongozi wakuu wastaafu wasiopungua ishirini
kwa gharama ya mabilioni ya fedha kila mwaka. Ili kupunguza mzigo kwa Wananchi katika
kuwahudumia wastaafu hao, Serikali ya CUF itaandaa sera mahsusi ya viwango (monitored
value) na muda maalum wa malipo usiozidi miaka 10 tangu kustaafu. Baada ya muda huo mfuko
wa kawaida wa huduma za jamii kwa wafanyakazi wa Serikali utatumika.
MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI NA RUSHWA;
Hali ilivyo sasa;
•     Ufisadi na Rushwa siyo tu kuwa ni adui wa haki, lakini pia ni adui mkubwa wa maendeleo.
Rushwa ni saratani (cancer) inayoua uchumi na kuwanyima wananchi haki ya maisha
na maendeleo. Rushwa katika Tanzania imekithiri na sasa Tanzania ni moja kati ya nchi
iliyokubuhu kwa rushwa duniani.
•     Serikali inapoteza mabilioni ya kodi ambazo hazilipwi na waagizaji wa bidhaa, Matengenezo
ya barabara na miundo mbinu ni hafifu mno japokuwa gharama inayotajwa ni kubwa, Madawa
yaliyomaliza muda wake wa kutumika yanaingizwa nchini kila kukucha na leo Tanzania ni
moja ya dampo la bidhaa bandia na visivyokidhi viwango vya kimataifa, Mitihani inavuja na
kwa hivyo haipimi uwezo wa wanafunzi wetu, Mabilioni ya fedha za walipa kodi yanafujwa
kila mwaka kwa matumizi yasiyofahamika mfano wizi wa shilingi bilioni 130 za akaunti ya
External Payment Arrears- EPA, Na Mamia ya Watanzania wanafungwa jela kila siku kutokana
na kushindwa kuinunua haki yao mahakamani kutokana na rushwa na ufisadi uliokithiri.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•     Seikali ya CUF na mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa nchini; Chanzo kikubwa cha rushwa
ni ukiritimba wa madaraka, mishahara midogo ya watendaji Serikalini, maamuzi yasiyofuata
taratibu na kutowajibishwa kwa wanaoshiriki katika vitendo vya rushwa. Vita dhidi ya rushwa
itafanikiwa ikiwa ukiritimba wa madaraka utaondolewa, maamuzi ya kiserikali yatafuata taratibu
zilizo wazi na zinazoeleweka na kuwaadabisha wanaoshiriki katika rushwa. Kupambana na
rushwa ni lazima tujenge mazingira ambayo yatatuhakikishia kuwa ‘MAPAPA na MANYANGUMI’ ya
rushwa na ufisadi yanashughulikiwa kwanza kabla ya kuwashughulikia ‘vijidagaa’. Ili kukabiliana
na ufisadi katika sura zake zote Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo;
•     Itaiongezea nguvu Taasisi ya Kupambana na Rushwa; Yatafanyika marekebisho ya kisheria
ili Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iwajibike kwa Bunge badala ya
Serikali. Mabadiliko haya yatalenga katika kuipa kinga dhidi ya hujuma inazoweza kufanyiwa
na Serikali kuvuruga shughuli zake za kiuchunguzi pale shughuli hizo zinapoonekana
kuwalenga baadhi ya maofisa wa Serikali au waliokaribu na maafisa wa Chama kinachotawala
13
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
pia TAKUKURU itapewa mamlaka ya kupeleka kesi mahakamani bila kuomba idhini toka kwa
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).
•     Itawatangaza wanaotiwa hatiani kwa vitendo vya Rushwa; Wahalifu wote wa vitendo vya rushwa
wanaotiwa hatiani watatangazwa hadharani kupitia vyombo vya habari vya Serikali.
•     Itabadili Muundo na Utendaji Serikalini; Mabadiliko ya muundo na utendaji Serikalini kama
yalivyoelezewa katika sehemu nyingine za ilani hii yamelenga katika kuondosha ukiritimba
wa madaraka na kuweka utaratibu wa wazi zaidi wa kiutendaji. Mabadiliko haya yatakuwa ni
silaha muhimu kabisa katika kubomoa mazingira ya rushwa.
•     Itaboresha maslahi ya Wafanyakazi. Marekebisho ya mishahara ya watumishi wa Serikali yatasaidia
kwa kiwango cha juu kufifisha rushwa katika ngazi za chini na kati za utendaji Serikalini.
•     Marekebisho ya kisera katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kuandaa mfumo
mzuri wa uchumi unaotoa tija na neema kwa wananchi wote kwa kuzingatia upunguzaji wa
gharama za maisha kwa kuwekeza katika sekta muhimu za maendeleo ya kiuchumi itakuwa
ni moja ya silaha ya CUF katika mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa nchini.
Makadirio ya Bajeti (Mapato na Matumizi) ya Serikali itakayoundwa na CUF 2010-2016
katika sekta za muhimu Kilimo, Miundo Mbinu, Elimu, Nishati, Afya, Maji, Na Mawasiliano
kwa mwaka wa fedha 2011-2016.
Halisi
Halisi
Pato la Taifa kwa Bei za Soko 26497.2 29764.3 37012.4
Mapato ya ndani
4293.1
4568.4
7217.4
Jumla ya Matumizi
6811.8
8639.1
9189.9
Matumizi ya Kawaida
4681.5
5813.7
5513.9
Matumizi ya Maendeleo
2130.4
2825.4
3676.0
Nakisi
-2518.8 -4070.7 -1972.5
Ukuaji halisi wa uchumi (%)
6.7
6.0
7.3
Mfumko wa bei wa PLT (%)
9.2
6.3
4.5
Mgao wa matumizi ya serikali Kisekta bilioni shilingi
Elimu
1341.9
1624.1
2021.8
Afya
790.2
898.5
1102.8
Kilimo
327.0
622.0
919.0
Miundombinu
1410.0
1606.9
2757.0
Jumla ndogo
3869.1
4751.5
6800.5
Mengine
2942.7
3887.6
2389.4
Mgao wa matumizi ya serikali Kisekta Asilimia (%)
Elimu
19.7
18.8
22
Afya
11.6
10.4
12
Kilimo
4.8
7.2
10
Miundombinu
20.7
18.6
30
Jumla ndogo
56.8
55
74
Mengine
43.2
45
26
14
Suala la Ulinzi na Usalama wa Taifa linapaswa kupewa uzito unaostahili, Kwa muda mrefu sasa
Serikali ya CCM imeshindwa kutekeleza wajibu wa kuhakikisha kuwa vikosi vyetu vya Majeshi ya
Ulinzi na Usalama – JWTZ, Polisi, Magereza, Zimamoto, Uhamiaji, na JKT vinaimarika na kuwa
vya kisasa zaidi.
Hali ilivyo sasa;
Vikosi vyetu vya majeshi hivi vimeathiriwa na ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi, mafunzo duni
na maslahi yasiyoridhisha. Makazi ya askari wetu ni ya udhalilishaji mkubwa na yanakwenda
kinyume na haki za msingi za binadamu. Mishahara na marupurupu mengine ya askari si yenye
kukidhi haja ukilinganisha na wito na maadili ya kazi zao. Askari wengi wastaafu wanaishi
maisha yanayokatisha tamaa uraiani kutokana na kutokuwepo na mipango madhubuti ya kuuenzi
muda walioutumia kulitetea Taifa letu. Huduma za uokoaji nchini ziko katika hali mbaya kabisa.
Udhaifu mkubwa uliojionyesha wakati wa kushughulikia majanga kama ya MV Bukoba, mafuriko
ya Mererani, maporomoko ya ardhi(land slide) Same, kuzama kwa boti kadhaa baharini na
kuungua kwa meli za abiria Zanzibar ni kielelezo halisi cha hali hii.
Dira ya mabadiliko ya CUF;
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa;
Makadirio ya Pato la Taifa na Bajeti 2008/09 – 2015/16 bilioni shilingi
2008/09 2009/10 2011/12
ULINZI NA USALAMA
2012/13 2013/14 2014/15 2015/16
Makadirio ya CUF
41551.7 46965.6 53430.8
8310.3
9862.8 11754.8
10295.2 11636.6 13238.4
6177.1
6981.9
7943.1
4118.1
4654.6
5295.4
-1984.8 -1773.8 -1483.7
7.8
8.5
9.3
4.5
4.5
4.5
61053.5
14042.3
15127.1
9076.2
6050.8
-1084.8
9.8
4.5
2470.8 2909.1 3309.6 3781.8
1441.3 1745.5 1985.8 2269.1
1235.4 1629.1 1985.8 2269.1
2573.8 2909.1 3309.6 3781.8
7721.4 9192.9 10590.8 12101.7
2573.8 2443.7 2647.7 3025.4
24 25 25 25
14 15 15 15
12 14 15 15
25 25 25 25
75 79 80 80
25 21 20 20
•     Vikosi vya ulinzi na usalama vinapatiwa mafunzo bora na vifaa vya kisasa ikiwa ni pamoja
na kuhakikisha kuwa vyombo vya usafiri, vyombo vya mawasiliano, na sare vinatosheleza
mahitaji ili viweze kukidhi haja ya ulinzi dhidi ya mashambulizi ya ardhini, baharini na
angani na viweze kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
•     Kikosi cha wanamaji cha polisi (police marine)
kinaimarishwa ili mbali ya kutoa msaada kwa kikosi
cha jeshi cha wanamaji dhidi ya mashambulizi ya
baharini pale yatakapotokea, kiweze kuboresha
doria katika ukanda wote wa pwani na kwenye
maziwa makuu kwa madhumuni ya kutoa msaada
kwa vyombo vya kiraia vya uvuvi na usafirishaji
wakati wa matatizo (Rescue Operations), na kuzuia
uharamia na wizi wa rasilimali za Taifa kwa kufanya
vitendo vya uvuvi haramu kama ilivyotokea hivi
karibuni kwa kukamatwa kwa meli ya uvuvi kutoka
nje ya nchi ikiwa na shehena ya samaki aina ya
Jodari tani 296 wenye thamani ya zaidi ya bilioni
21. Kuzuia magendo, biashara chafu kama za
madawa ya kulevya na uharamia wa majini.
•     Askari wa vikosi vyote nchini wanalipwa kima cha chini cha mshahara unaokidhi mahitaji ili
waweze kutekeleza majukumu na wajibu wao kwa ufanisi na kujituma na kuhakikisha askari
wetu wote wanapatiwa makazi ya kuheshimika na kupewa mafunzo ya kutosha juu ya wajibu,
sheria na maadili ya kazi yao ili matendo ya askari kuwaonea raia na kuvunja haki zao za
msingi yasijitokeze.
•     Inakihuisha, kukipanua na kukiimarisha kikosi cha Zima Moto ili kiweze kutoa huduma za
15
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
uokoaji kikamilifu. Hii itakuwa ni pamoja na kuongeza idadi ya askari, kutoa mafunzo ya kisasa
yanayohusiana na shughuli zote za uokoaji na kukipatia vifaa vya kisasa kabisa vya uokoaji.
•     Inapitia upya viwango vya pensheni za wastaafu kutoka vikosi vya ulinzi na usalama, na
kusimamia kuona kuwa wanapata haki zao stahiki bila ya kusumbuliwa.
•     Inaanzisha mafunzo ya kijeshi ya hiari kwa Wananchi wote watakaopenda ili wawe askari
wazuri pindi itakapohitajika.
•     Serikali ya CUF itasimamia kuongeza matumizi ya mawasiliano ya simu na teknolojia ya kisasa
ya kompyuta katika kupokea na kuweka kumbukumbu ya matukio ya uhalifu na kuyashughulikia
kisayansi zaidi.
•     Kuanzisha miradi mikubwa ya uzalishaji mali katika makambi ya vikosi vya majeshi ili
katika kipindi ambacho hakuna matushio ya kiusalama nguvu kazi hiyo iwe inatumika katika
shughuli za uzalishaji.
MAMBO YA NCHI ZA NJE
Hakuna Taifa duniani linaloweza kujitenga katika mashirikiano na mataifa mengine. Hili linatokana
na utegemezi na muingiliano wa masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, kibiashara,
maendeleo ya mwanadamu, ulinzi na usalama, na kusaidiana wakati wa majanga kunalifanya
kila Taifa lilazimike kuwa na mahusiano ya aina moja au nyingine na mataifa mengine.
Hali ilivyo sasa;
•     Baada ya miaka 49 ya uhuru wa taifa letu bado hakujakuwa na sera thabiti ya masuala
ya mahusiano ya mambo ya nchi za nje yenye kuleta tija na maslahi zaidi ya kiuchumi
kwa Watanzania. Jitihada za kujenga mahusiano ya nje zimejikita zaidi katika kufanikisha
upatikanaji wa misaada na mikopo na kukaribisha uwekezaji ambao wakati mwingine
unaonekana ni njia nyingine ya uwekezaji wa kifisadi wa kimataifa.
•     Utegemezi wa uendeshaji wa shughuli za serikali kutoka nchi “marafiki wa maendeleo” na
ukoloni mamboleo uliojikita katika kutafuta fursa za kuvuna utajiri wa rasilimali za asili
tulizonazo umeathiri sana uandaaji wa sera
za kitaifa zinazoendana na hali halisi ya
hatua ya maendeleo iliyofikiwa na kukidhi
matakwa na mahitaji ya watanzania.
•     Ushirikiano wa kimataifa limefanywa kuwa
ni suala la Muungano chini ya wizara ya
mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa
kimataifa na hivyo kuinyima Zanzibar fursa
na uhuru wa kujiendeleza kwa kuwa na
mahusiano ya kiuchumi na nchi na mashirika
ya mbalimbali ya kimataifa.
•     Baada ya miaka 49 ya kujitawala kumekuwepo
na ubadhirifu wa matumizi makubwa ya wizara
ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa
kimataifa yanayotokana na uendeshaji wa
ofisi zetu za kibalozi na kuwa na mabalozi ambao kimsingi wanaoshindwa kufanya ushawishi
16
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
mkubwa wa kisiasa na kiuchumi ili kulisaidia taifa letu kusonga mbele katika sekta mbalimbali.
Uteuzi wa mabalozi umekuwa wa kisiasa zaidi kuliko uzito na jukumu linalopaswa kufanywa
na wahusika. Jukumu ambalo kwa miaka mitano hii limeonekana kufanywa na Rais wa nchi
mwenyewe kwa kuwa na safari za nje kupita kiasi na kufuja fedha za umma.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•     Serikali ya CUF itaendeleza mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali kwa kushughulikia dosari
zilizopo na kujielekeza zaidi katika kuhifadhi na kulinda amani ya dunia na usalama wake,
kuhifadhi wa mazingira, kutumia fursa za kiuchumi kuiendeleza dunia na taifa kwa ujumla,
kujilinda na athari za mabadiliko ya tabia nchi, kuliendeleza taifa na dunia katika kunufaika
kiuchumi, kibiashara na utamaduni mwema.
•     Itaendelea na uungaji mkono na kushiriki kikamilifu katika Jumuiya na mashirika mbalimbali
ya kimataifa ikiwa ni pamoja na UN, AU, Commonwealth, nakadhalika kwa ajili ya kutekeleza
maamuzi ya pamoja yanayofikiwa na kufaidika na manufaa yatokanayo na uwepo wa jumuiya
hizi.
•     Itafanya maslahi ya kiuchumi kuwa nguzo muhimu ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania na
kwa hivyo mahusiano yetu na nchi nyingine kwa kiasi kikubwa yatalenga katika kuimarisha
uchumi na kukuza biashara ambapo siasa zitatumikia uchumi na siyo kinyume chake.
•     Itahakikisha kuwa kunakuwepo na uhusiano mzuri na nchi jirani bila ya kujali itikadi au
mfumo wa siasa na uchumi wa nchi hizo. CUF inaamini kwamba mustakabali wa Tanzania
utaendelezwa vizuri zaidi kwa kutilia mkazo ushirikiano na nchi jirani ikiwa ni pamoja na
kuunga mkono juhudi za kuimarisha na kuipanua Jumuiya ya Afrika Mashariki (East Africa
Community) kwa namna ambayo itakuwa na manufaa kwa Wananchi wote wa eneo lote la
maziwa makuu.
•     Itatoa ushirikiano wa kipekee na mafungamano ya karibu na nchi zote zitakazoonyesha nia
ya kweli ya kuisaidia Tanzania, pamoja na zile nchi zenye uhusiano wa kihistoria na nchi
yetu na kuyapa kipaumbele masuala ya usuluhishi na utatuzi wa migogoro katika nchi zote
zinazopakana na Tanzania. Mafanikio ya mpango huu siyo tu kwamba yatasaidia kudumisha
amani katika nchi zinazohusika, lakini pia yatajenga mazingira mazuri zaidi ya kiuchumi na
kisiasa kwa wananchi wa eneo lote hili, ikiwa ni pamoja na kuipunguzia nchi yetu mzigo
mkubwa wa wakimbizi wanaokimbia makwao kutokana na hali mbaya ya usalama.
•     Ushirikiano wa kimataifa katika nyanja za uchumi na biashara utaondolewa kuwa suala la
Muungano, ili kuziwezesha pande zote mbili za Muungano kunufaika kikamilifu na mikataba
inayogusa maeneo hayo.
17
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
SEHEMU YA TATU – UCHUMI
HALI YA MAISHA YA MTANZANIA KWA UJUMLA NA SEKTA MUHIMU ZA UCHUMI
•     Uchunguzi wa Bajeti za Kaya – Household Budget Survey(HBS) wa mwaka 2007 umeonyesha
kwamba umaskini umepungua kidogo sana toka asilimia 38.6 mwaka 1990, asilimia 35.7
mwaka 2001 mpaka asilimia 33.3 mwaka 2007. Kwa kuwa idadi ya Watanzania inaongezeka
kwa asilimia 2.9 kila mwaka. Idadi ya watu maskini imeongezeka kwa watu milioni 1.5 toka
watu milioni 11.4 mwaka 2001 na kufikia watu milioni 12.9 mwaka 2007. Izingatiwe kuwa
kigezo kilichotumiwa na HBS 2007 cha mtu mzima kutohesabiwa kuwa siyo maskini ni kutumia
shilingi 641/- au zaidi kwa siku ukiwa Dar es Salaam, shilingi 532/- au zaidi kwa siku ukiwa
katika miji mingine na shilingi 469/-au zaidi kwa siku ukiwa vijijini. Ni wazi kigezo hiki ni
cha chini mno na bado idadi ya watu maskini imeongezeka kigezo kilichokubaliwa kimataifa
kuwa matumizi ya chini kabisa kwa mtu mzima asihesabiwe kuwa ni maskini wa kutupwa ni
dola moja kwa siku.
•     Benki ya dunia inakadiria kwa kutumia kipimo hiki, umaskini Tanzania umeongezeka toka
asilimia 73 ya Watanzania wote mwaka
1990 mpaka kufikia asilimia 89 mwaka
2000. Kwa kutumia kigezo hiki cha
kimataifa na takwimu za uchunguzi
wa bajeti za kaya wa 2007, zaidi ya
Watanzania 90 katika kila Watanzania
100 ni masikini wa kutupwa. Hatuwezi
kuwa na mshikamano wa kweli wa kitaifa
ikiwa ukuaji wa uchumi unawanufaisha
watu wachache na kuwaacha zaidi ya
Watanzania milioni 36 wakiwa maskini
wa kutupwa. Kwa Watanzania walio
wengi kauli mbiu ya Maisha Bora kwa kila
Mtanzani ni kitendawili cha kejeli kwani
maisha yao ni ya dhiki kila kukicha.
•     Baada ya miaka 49 ya kujitawala pamekosekana Dira ya Taifa ‘National vision’ na kuangalia
vipaumbele matokeo yake mabilioni ya shilingi yamekuwa yakitumika katika semina, warsha,
na makongamano ya kuzungumzia umasikini bila kupatikana kwa suluhisho la uhakika zaidi
ya kutunisha mifuko ya washiriki.
•     Jitihada za kuiendeleza nguvu kazi ya wanawake kiuchumi ambao ndio wanachukua asilimia
zaidi ya 51 ya watanzania wote hazijazaa matunda yanayotakiwa. Sehemu kubwa ya njia
zote za uchumi zinashikiriwa na wanaume. Kundi kubwa la wanawake wako nyuma kielimu na
kitaaluma, matokeo yake wanaendelea kukaa majumbani na au kujishughulisha na shughuli
ndogo ndogo za uzalishaji zisizo na tija wakipambana na umasikini. Aidha, taasisi za fedha
nyingi ziko mijini na benki inayoitwa ya wanawake ipo Dar es Salaam pekee. Mikopo wanayopewa
inariba kubwa lakini pia hakuna mfumo sawia wa kiuchumi unaopelekea shughuli za kiuchumi
kuleta maslahi stahiki. Mwisho wa siku mikopo hiyo uwapelekea wengine kukimbia miji na au
kupokonywa mali zao (kufilisiwa).
18
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
•     Mfumo mbovu wa kodi unaowanyanyasa walipa kodi wadogo wadogo na kuwanufaisha zaidi
walipa kodi wakubwa unalipotezea Taifa mabilioni ya shilingi ambayo yangetumika katika
programu za kukuza uchumi wa Taifa. Sera mbovu ya ubinafsishaji imesababisha mashirika
mengi ya umma kuuzwa kwa bei ya kutupwa na kulipotezea Taifa mabilioni ya shilingi ambayo
yangetumika katika programu za kuinua hali za maisha ya watanzania.
•     Baada ya miaka 49 ya kujitawala thamani ya shilingi yetu imeporomoka kwa kiasi kikubwa
kilichokosekana udhibiti wake wa kisera. Mwaka 1964 dola moja ya Marekani ilikuwa sawa
na shilingi 7.14 za Tanzania, Mwaka 1990 shilingi 195, Mwaka 1994 shilingi 510, Mwaka
2005 shilingi 1129 na Mwaka huu 2010 Dola moja sawa na shilingi 1500. Hali hii inaathiri
sana mfumo wa ukuaji wa kiuchumi kutokana na kupanda kwa gharama za bidhaa mbalimbali
zinazoagizwa nje ya nchi ambapo mbebaji wa gharama hizo ni mlaji wa mwisho mtanzania
maskini. Leo Serikali ya CCM inakwenda kukopa katika benki za ndani fedha ambazo zilipaswa
kutumika kuwasaidia wajasiriamali wengi zaidi watanzania maskini.
•     Sera mbovu ya uwekezaji inatoa mwanya kwa wawekezaji kutoka nje kutorosha kutoka nchini
mabilioni ya shilingi ambayo yangetumika katika programu mbalimbali za kuinua hali za
maisha ya watanzania. Serikali ya CCM imeshindwa kutumia jiografia nzuri ya nchi yetu
kuinua uchumi wa nchi na kuliongezea Taifa mapato. Kilimo ambacho kimsingi ndio sekta
tegemezi kwa watanzania walio wengi hakijasimamiwa ipasavyo na badala yake kumekuwa na
kauli mbiu za kisiasa zaidi kuliko uhalisia kwa wakulima wenyewe. Juhudi za kuboresha sekta
ya kilimo kwa kauli mbiu ya kilimo kwanza bado haijitoshelezi kwani sekta hii inatozwa kodi
nyingi na haitengewe fedha za kutosha.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•     Chama cha CUF kinatambua kuwa zaidi ya robo tatu ya Watanzania wote ni wakaazi wa
maeneo ya vijijini. Hii ina maana kwamba kimsingi tunapozungumzia umasikini wa Mtanzania
kwa kiasi kikubwa mlengwa ni Mtanzania wa kijijini, kwa maana hiyo basi juhudi zozote za
kustawisha hali za maisha nchini haiwezi kufaulu bila kuyapa kipaumbele maeneo ya vijijini.
Serikali ya CUF itawekeza katika uboreshaji wa maisha kwa wakaazi wa vijijini kwa utaratibu
wa kuviwezesha vijiji 3000 kila mwaka kupata huduma za msingi za maendeleo ikiwa ni
pamoja na elimu, afya, miundombinu, nishati ya umeme wa Jua, kuiwezesha kikamilifu sekta
ya kilimo.
•     Watanzania wengi walioko vijijini au ni wakulima, wafugaji, wavuvi, au ni wenye kufanya
shughuli mchanganyiko. Sehemu kubwa ya shughuli zote hizi inahusu uzalishaji na kwa
hivyo basi kusudio la kukabiliana na kupunguza umasikini ni lazima lilenge kwanza kwenye
kuboresha uzalishaji; na pili, kutafuta masoko ya uhakika. Kuboresha uzalishaji kuna maana
ya kuboresha mipango, miundombinu, na ushauri wa kitaalamu, na kusimamia upatikanaji wa
masoko na bei nzuri ya bidhaa za wakulima. Serikali ya CUF itayasimamia ipasavyo maeneo
haya na Halmashauri za Wilaya zitakuwa ni vituo muhimu katika kufanikisha mkakati huu.
•     Kutafanyika Mabadiliko ya msingi ambapo Halmashauri zitabadili mwelekeo kutoka
kuwa ni asasi zinazoshughulikia zaidi masuala ya huduma za kiutawala na kuwa ni asasi
zinazoshughulikia zaidi mkakati wa kuinua hali za maisha.
•     Chini ya mwelekeo huu mpya kila halmashauri itawajibika kuweka mazingira yatakayovutia
uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vitakavyotumika kuongeza thamani ya mazao
mbalimbali yanayozalishwa vijijini.
19
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
Mathalani, badala ya muhogo kuuzwa kama muhogo unaweza kusindikwa na kuuzwa kama
wanga, badala ya asali kuuzwa kama asali inaweza kutiwa kwenye mchanganyiko wa mazao
mengine ya asili yanayopatikana katika maeneo husika na kutengeneza vipodozi vyenye ubora
wa juu, korosho zinaweza kubanguliwa na kufungwa vizuri badala ya kuuzwa nje zikiwa katika
hali ghafi, nakadhalika. Aidha ajira itakayopatikana kwenye viwanda hivi itaongeza mzunguko
wa fedha wa kudumu kwenye maeneo ya vijijini na hivyo kuchochea ukuaji wa ajira katika sekta
zingine zisizo rasmi.
•     Mfumo usioridhisha wa kodi utafanyiwa marekebisho ili mabilioni ya shilingi yanayopotea
hivi sasa kutokana na misamaha holela ya kodi yaokolewe na kuelekezwa kwenye kuinua hali
za maisha ya watanzania wanaogelea katika dimbwi la umasikini usio na dalili ya kumaliza
hata kwa miaka mia moja ijayo.
•     Jiografia nzuri ya nchi yetu inayoruhusu kuibua vyanzo vya mapato takriban katika kila
nyanja itatumika kukuza uchumi na kuliongezea Taifa mapato. Kilimo kitapewa msukumo
mkubwa ambapo kila mwaka wa bajeti lazima kilimo kipewe asilimia 15 ya bajeti nzima.
•     Serikali itakayoundwa na CUF itaanza utaratibu wa kuwalipa pensheni kila mwisho wa mwezi
na kuwatunza wazee wanaofikia miaka 70 na kuendelea kupitia idara ya ustawi wa jamii.
Chini ya Serikali ya CUF hakutakuwa na makundi ya wazee au watoto wanaopita mitaani
kuombaomba.
SEKTA MUHIMU ZA UCHUMI
KILIMO
Hali ilivyo sasa;
•     Kilimo chetu kimeendelea kuwa duni kwa sababu zisizokuwa na msingi. Tuna ardhi ya kutosha,
mito na maziwa makubwa. Jiografia ya Tanzania inafanya nchi yetu iwe na majimbo yenye
hali ya hewa tofauti. Mazao mbali mbali ya chakula na biashara yanastawi katika ardhi ya
Tanzania, nchi yetu ina uwezo mkubwa wa kuzalisha mazao ya chakula na biashara lakini
miaka 49 baada ya Uhuru, Tanzania haijitoshelezi kwa chakula. Wananchi vijijini wanakula
‘madaka’ na mizizi pori katika kila baadhi ya miezi kwa mwaka, wastani wa uzalishaji hapa
nchini kwa eka moja ni mdogo kuliko nchi nyingine zote za Kiafrika.
•     Hakuna ubunifu wa kuangalia ni mazao gani mapya ya kibiashara yanaweza yakakuzwa ikiwa
ni pamoja na michikichi, mawese, muarobaini, nakadhalika, nchi yetu imekuwa tegemezi
wa bidhaa hizo kutoka nchi za nje. Mazao ya nishati mbadala ya fueli ya mimea (petroli na
diseli) kama vile miwa na jatropha inastawi maeneo mengi. Petroli na dizeli mbadala yana
soko kubwa duniani na hasa Ulaya. Kuna fursa ya kuitumia vyema Jiografia nzuri ya nchi yetu
kukuza kilimo. Wakulima wamekuwa wakilazimishwa kulima mazao yasiyokuwa na tija na
hivyo kudidimizwa zaidi kwenye umasikini uliokithiri.
•     Tanzania imekosa sera sahihi ya kukuza kilimo na kuinua hali za maisha ya watanzania, zana
za kilimo na pembejeo haziwafikii wakulima na hata zinapowafikia huwa zimechelewa na
ufika nje ya wakati. Katika miaka mitano ya Serikali ya awamu ya nne matumizi ya mbolea
yamekuwa ndoto na yamepungua mwaka hadi mwaka, ilielezwa kuwa sababu kubwa ni kupanda
kwa bei yake na kutoweka mikopo kwa wakulima. Hata mikopo ya kununulia mazao imekauka
kabisa na kusababisha kuanguka kwa bei wanayolipwa wakulima na tena kwa utaratibu wa
mkopo na kwa mikoa ya kusini maarufu kama ‘Stakabadhi Ghalani’.
20
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
•     Pamoja kudaiwa kuwa kilimo kuwa ni uti wa mgongo wa Taifa letu, tangu tupate uhuru wa
Taifa letu bajeti ya kilimo ya kila mwaka haijawahi kuzidi asilimia nane (8%) ya bajeti yote
ya Serikali. Nchi yetu haina huduma bora kwa ajili ya kukuza kilimo cha kisasa na kwa ujumla
kumekuwa na udhaifu mkubwa hasa katika maeneo ya uwekezaji kwenye tafiti, motisha kwa
wakulima ili wajaribu mambo mapya, Ushauri na utaalamu kwa wakulima, mikopo ya zana za
kilimo na pembejeo, barabara na mawasiliano vijijini.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•     Serikali itakayoundwa na CUF itaasisi mapinduzi ya kilimo ya kweli na kukifanya kilimo kiwe
kweli ni injini ya maendeleo yetu. CUF Itayafanyia kazi mapendekezo ya Tume ya Prof Shivji
ya Ardhi kwa nia ya kuhakikisha kuwa sera bora ya Taifa ya ardhi inapatikana ambayo pamoja
na mambo mengine itatuhakikishia kuwa, ardhi yote ambayo iko kwenye milki za watu mbali
mbali muda wote inatumika kwa uzalishaji, kunakuwa na utenganisho na mipaka kati ya
ardhi inayomilikiwa kitaifa na ile inayomilikiwa na vijiji na kwamba Serikali iwe na mamlaka
na ardhi ya taifa tu. Umiliki wa ardhi kimila unapewa hadhi sawa na umiliki wa ardhi kwa
hati. Mashamba ya wananchi bila kujali kuwa yana mazao ya kudumu ama la yalipwe fidia
inayostahili na inayoendana na thamani ya pesa ya wakati husika pale Serikali inapoihitaji
ardhi hiyo kwa matumizi mengine.
•     Itahakikisha kwamba taaluma ya ubwana/ubibi shamba
inarejeshewa hadhi yake. Hii ina maana kuwa idadi ya
wanafunzi wetu wanaosomea taaluma hii itaongezwa
kwa kiasi kikubwa na wahitimu wote wa taaluma hii
(wa zamani na wapya) watapewa umuhimu mkubwa.
Kila bwana shamba/bibi shamba na maafisa ugani,
atapatiwa kila aina ya msaada ili aweze kuifanya kazi
yake katika kiwango kinachotakiwa.
•     Itaanzisha mfuko rasmi wa kulea na kukuza uzalishaji
kwa wakulima (Aglicultural Incubator Fund) kwa ajili
ya kilimo cha kibiashara. Mfuko huu ambao utakuwa
ni wa kudumu utalenga katika kuwasaidia wakulima
nchini kote kuanzisha kilimo cha kibiashara kwa
kuwapa uwezo wa kununulia matrekta, vifaa kwa
ajili ya kilimo cha umwagiliaji, ujenzi wa maghala,
pembejeo nakadharika.
•     Itaboresha ushindani wa soko la mazao ya wakulima.
Ili kufanikisha hili Serikali itawasaidia wakulima
kuanzisha makampuni yao ya mauzo ya bidhaa zao
nje ya nchi kwa kuwapatia utaalamu na ushauri wakati wote utakapohitajika. Makampuni haya
yatawasaidia wakulima kuondokana na adha ya kulazimika kuuza bidhaa zao kwa makampuni/
vyama vya ushirika visivyojali maslahi ya wakulima.
•     Serikali ya CUF itasimamia kuhakikisha kuwa wakulima wote waliokopwa mazao yao na
mpaka CUF inaingia madarakani hawajalipwa fedha zao, wahusika wote waliokopa mazao
hayo watasimamiwa na Serikali kulipa madeni yote haraka iwezekanavyo na atakayeshindwa
kufanya hivyo kwa muda uliowekwa watafikishwa mahakamani na kutaifishwa mali zao
ziwafidie wakulima.
21
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
•     Uboreshaji wa miundombinu na njia za mawasiliano itasimamiwa kwa haraka na serikali ya CUF,
Itahakikisha kuwa kila halmashauri inajenga mazingira ya kuanzishwa kwa viwanda vidogo
vidogo kwa ajili ya kusindika na kuyaongezea thamani mazao mbalimbali yanayozalishwa na
Wananchi katika maeneo ya halmashauri husika. Utaratibu huu siyo tu kwamba utawasaidia
wazalishaji vijijini kuwa na soko ambalo liko tayari, bali pia utasaidia sana katika suala zima
la kuongeza ajira nchini.
•     Kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa kama FAO, UNIDO, n.k. Serikali ya CUF itafanya
utafiti wa kina juu ya mazao mengine ya biashara yanayoweza kustawishwa nchini, na baada
ya kuyajua na kutambua maeneo ya nchi yanakoweza kukuzwa itatoa msaada kwa wakulima
wa maeneo husika ili waweze kuyakuza ikiwa ni pamoja na kuwatafutia wabia. Aidha kwa
kushirikiana na taasisi hizi, Serikali itaimarisha shughuli za utafiti katika vyuo na taasisi za
kilimo ili ziweze kutoa mchango mkubwa zaidi katika upanuzi na uimarishaji wa shughuli za
kilimo nchini.
•     Itarahisisha mfumo wa kodi na ushuru wa mazao ya kilimo; ikiwa ni pamoja na kufuta ushuru
na ada zote za mazao katika ngazi ya mkulima ili kuongeza motisha kwa wananchi kuwekeza
juhudi zaidi katika uzalishaji kupitia kilimo na kutoa uhuru kwa kila mkulima kulipia huduma
anayoihitaji. Vizuizi vyote visivyo na msingi katika biashara ya mazao yote ndani ya nchi
vitaondolewa.
•     Itahakikisha kuwa mazao yote yanalimwa kwa kuzingatia soko halisi ili kuongeza tija zaidi
katika kilimo. Katika kufanikisha jambo hilo maoni ya wakulima yatazingatiwa na kupewa
uzito mkubwa bila ya kutumia nguvu za dola kuwalazimisha wakulima kulima mazao kwa
mashinikizo ya serikali.
•     Serikali itaanzisha ruzuku maalum ili kulinda bei za mazao makubwa ya biashara kama
vile pamba, kahawa, tumbaku, na korosho yanayolimwa na wakulima wadogo wadogo; ili
kuwakinga wakulima hao na hasara ya kuanguka kwa bei za mazao yao kutokana na kuanguka
kwa bei katika masoko ya nje.
•     Maeneo ya mashamba na/au ardhi yaliyochukuliwa na watu/viongozi, isivyo halali
yaterejeshwa kwa wananchi na Serikali ya CUF itasimamia miradi mikubwa na midogo ya
kilimo cha umwagiliaji maji sanjari na ulinzi wa mazingira.
•     Itahakikisha wakulima na wafugaji wanaishi kwa amani bila migongano kwa kuwaandalia
mfumo mzuri wa mgawanyo wa maeneo kwa wafugaji na maeneo ya wakulima sanjari na
kuwachukulia hatua za haraka watendaji wote wa serikali wanaoshiriki kufanya hujuma
dhidi ya kundi moja kati ya haya kwa maslahi binafsi.
UFUGAJI
Tanzania ni nchi iliyojaliwa mifugo mingi kama vile ng’ombe, kondoo, mbuzi na kuku. Pamoja
na wingi wa mifugo yetu ukosefu wa huduma bora na miundo mbinu umeifanya sekta ya ufugaji
nchini kushindwa kutoa mchango mkubwa katika kuinua hali ya maisha ya wafugaji walio wengi
pamoja na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Hali ilivyo sasa;
Wafugaji kwa kipindi kirefu wamekosa kupatiwa huduma sahihi na kuandaliwa mazingira bora
yatakayowahakikishia wafugaji ubora wa mifugo yao, Viwanda vichache vya kusindikia nyama na
ngozi vilivyokuwepo miaka michache iliyopita vimeachwa vikafa hivyo kuwakosesha wafugaji soko
22
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
lenye uhakika zaidi la bidhaa zao. Upatikanaji wa masoko ya nje kwa ajili ya mifugo, au bidhaa zi-
nazotokana na mifugo halijapewa umuhimu unaostahiki. Ukosefu wa miundo mbinu imara baadhi
ya mifugo usafirishwa kwa njia ya kutembezwa maporini kwa muda mrefu na kupelekea kuathiri
ubora wa mazao ya mifugo. Kwa mfano kutokana na ukosefu wa njia ya reli Ng’ombe ulazimika
kutembezwa kilometa zaidi ya 500 kutoka Dodoma mpaka Ruvu Dar es Salaam.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•  Kuinua ubora wa mifugo inayozalishwa;
Serikali itafanya sensa ya mifugo kwa nia ya kujua uwiano uliopo kati ya idadi ya mifugo na
huduma zilizopo. Hii ni muhimu ili kuweza kupata takwimu sahihi za mahitaji ya madaktari wa
mifugo, idadi ya majosho, ukubwa wa maeneo ya malisho, na idadi ya manywesheo, na mahitaji
ya masoko na umbali wa soko na eneo la ufugaji nakadharika, kufuatia kujulikana kwa takwimu
sahihi za mahitaji halisi ya huduma kwa wafugaji, Serikali itaweka utaratibu madhubuti wa
kuimarisha na kuboresha usambazaji wa huduma hizo.
•  Kupanua shughuli za ufugaji na kuongeza ajira;
Pamoja na wingi wa mifugo iliyopo nchini bado kuna nafasi ya kuipanua sekta hiyo na kuongeza
ajira za wananchi wetu. Serikali ya CUF itaanzisha mfuko rasmi wa kulea na kukuza uzalishaji
(Livestock Incubator Fund) kwa wafugaji na wananchi wengine nchini kote wenye nia ya kujiajiri
kwenye sekta hiyo kwa ajili ya ufugaji wa kibiashara. Mfuko huu ambao utakuwa wa kudumu
utalenga katika kuwasaidia wafugaji kuanzisha ufugaji wa kibiashara kwa kuwapa uwezo wa
kununua mitamba bora, uanzishaji wa mashamba ya malisho, uchimbaji wa mabwawa, ujenzi
wa mabanda nakadharika.
•  Kuboresha huduma ya masoko;
—     Itahakikisha kuwa kila halmashauri inajenga na kumiliki viwanda vidogo vidogo kwa ajili
ya kusindikia na kuyaongezea thamani mazao mbalimbali yanayotokana na mifugo katika
maeneo ya halmashauri husika. Aidha Kwa kushirikiana na wafanya biashara wa ndani
na wawekezaji wa nje Serikali itahimiza ujenzi wa viwanda vya usindikizaji wa bidhaa za
mifugo kama vile Nyama, Maziwa, Jibini, Ngozi, vifungo vya mavazi kutokana na pembe,
gundi kutokana na kwato, mapambo mbalimbali kutokana na mifupa nakadharika.
—     Itawasaidia wafugaji kuanzisha makampuni yao kwa ajili ya uuzaji wa mifugo yao nchi
za nje kwa kutoa ushauri wa kitaalamu na misaada mingine itakayohitajika ikiwa ni
pamoja na kuwatafutia masoko.
MAENDELEO YA VIWANDA NA AJIRA RASMI;
•     Ukuaji wa uchumi unaambatana na Mabadiliko ya mfumo wa uchumi kutoka kutegemea sana
kilimo na kuelekea kwenye ongezeko la ajira viwandani, kutoka nguvu kazi inayoishi vijijini
kuelekea nguvu kazi inayoishi mijini. Mabadiliko ya mfumo wa uchumi husababishwa na
ushindani wa soko. Serikali zenye malengo ya kukuza uchumi endelevu zinawajibika kujenga
ushindani katika masoko yote kuruhusu makampuni mapya yenye tija kuanza na makampuni
yanayopata hasara kufilisika. Soko la Ajira liwe jepesi kuruhusu makampuni mapya kuajiri
wafanya kazi na makampuni yanayopata hasara kupunguza wafanyakazi. Sheria za kazi zijikite
katika kurahisisha uanzishwaji wa ajira. Ni muhimu sana kuwa na utaratibu wa hifadhi za
jamii kwa wafanya kazi wanaopoteza ajira ili kupunguza makali na kuwepo kwa soko la
23
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
ajira linalonyumbulika. Wanaopoteza ajira wapate kipato cha kuwawezesha kuishi wakati
wakitafuta ajira mpya.
•     Kwa kawaida kampuni yoyote ili iweze kusonga mbele na kupata mafanikio, ni sharti safu
yake ya uongozi ijazwe na watu wenye ujuzi wa hali ya juu, uzoefu wa kutosha na shauku ya
kuleta mafanikio. Kwa kuwa watu hawa ni wataalamu wanapaswa kuwa na uhuru wa kutosha
kufanya maamuzi bila kungoja ridhaa ya wanasiasa. Aidha mafanikio ya kukuza uchumi na
biashara yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na ubora wa miundo mbinu inayohitajika, kama
vile barabara, reli, bandari, mawasiliano, nishati, maji na huduma za fedha. Miaka 49 ya
UHURU tumeshuhudia kudidimia kwa kasi kwa sekta ya viwanda na mashirika/makampuni ya
huduma. Viwanda na mashirika/makampuni mengi yamekufa sio kwa sababu nyingine yoyote
zaidi ya kuwa na uongozi mbaya wa mfululizo ulioteuliwa toka Ikulu na udhaifu wa miundo
mbinu iliyohitajika.
•     Maendeleo ya viwanda ni madogo sana nchini. Pamoja na madeni makubwa tuliyolimbikiza
katika uwekezaji wa rasilimali katika viwanda, uzalishaji wa bidhaa za viwanda haukuongezeka
kwa kasi iliyotarajiwa. Ajira viwandani ni ndogo sana. Katika nchi yenye nguvu kazi ya watu
milioni 21 ni Watanzania 92,034 ndio wenye ajira rasmi katika sekta ya viwanda.
•     Kuongezeka kwa ajira rasmi ni kigezo muhimu cha uchumi unaokua na kupunguza umasikini.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba shughuli nyingine zote za kujiajiri zinategemea matumizi
ya vipato vya wale wenye ajira rasmi. Mkulima, Seremala, Fundi Cherehani, Kinyozi, Muuza
Duka nakadharika. Wote wanategemea mzunguko wa fedha ambao chanzo chake ni yule
mwenye ajira rasmi. Mathalani, kikijengwa kiwanda mahali kinachoajiri wafanyakazi 1000
ambao kwa wastani kila mmoja wao analipwa shilingi 300,000/= kwa mwezi, kila mwisho wa
mwezi kutakuwa na jumla ya shilingi milioni 300 kwenye mikono ya wafanyakazi hao ambazo
ziko tayari kutumiwa.
Dira ya mabadiliko ya CUF;
•     Kuweka mkakati madhubuti wa kuanzisha na kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi ya
ndani na kuajiri watu wengi kama vile viwanda vya nguo na mavazi, viatu na bidhaa za ngozi,
vifaa vya matumizi ya nyumbani na vifaa vya umeme na elektroniki.
•     Kuweka ubinafsishaji wenye mwelekeo mpya;
Serikali ya CUF itaipitia upya mikataba yote ya ubinafsishaji wa viwanda, mashirika, na
makampuni na kuiboresha upya ili iendane na matakwa ya wakati tulionao na kuzingatia
maslahi ya Taifa na watanzania kwa ujumla.
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa shirika la umeme na mamlaka za maji zinapewa kipaumbele
maalumu na kuingia ubia na makampuni binafsi yenye utaalamu na huduma hizo ili ziwafikie
watanzania walio wengi.
•  Upanuzi wa ajira na kutofautisha maeneo ya kuwekeza;
—     Ili kuwasaidia wananchi wetu mbali mbali na hususani vijana wetu wanaohitimu katika
vyuo vya elimu ya juu na wananchi waliopunguzwa makazini–walio wabunifu na wenye
mawazo mapya–kujiingiza katika shughuli za kujiajiri kupitia biashara na uzalishaji,
Serikali itaanzisha mfuko rasmi wa kulea na kukuza biashara na uzalishaji viwandani
(Trade and Manufacturing Incubator Fund)
—     Serikali itatenga maeneo ya ardhi ambayo yatapimwa mahsusi kwa ajili ya wawekezaji
24
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
wakubwa wa ndani na nje wanaotaka kujenga viwanda hasa kwa ajili ya masoko ya nje.
•  Sera za viwanda na mashirika ya huduma;
Serikali ya CUF itazindua sera mpya za kitaifa kusimamia viwanda na mashirika ya huduma
kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya kuvutia kwa wawekezaji wa ndani na nje. Sera hizi
zitalenga, kuimarisha na kuboresha miundo mbinu katika nyanja za usafiri, mawasiliano,
maji na nishati, kuweka mfumo wa kodi unaoeleweka na kutabirika ambao haubagui kati ya
wawekezaji wakubwa na wadogo, kuandaa nguvu kazi inayohitajika, na kuandaa mazingira
ya kuwawezesha watanzania wengi zaidi kujiingiza katika umiliki wa shughuli za uzalishaji,
biashara na utoaji wa huduma. Mazingira haya yatakuwa ni pamoja na kutoa ushawishi kwa
wawekezaji wa nje kuwa wale watakao ingia ubia na watanzania watapewa vivutio maalum.
Kuandaa mazingira ya kuwachochea wazalishaji wa ndani ya nchi kuimarisha viwango vya
ubora wa bidhaa zao ili ziwe na ushindani kwenye masoko. Na kuandaa mazingira yatakayoleta
unafuu wa kuridhisha katika gharama za uzalishaji.
SEKTA ISIYO RASMI
Hali ilivyo sasa
•     Wafanyabishara ndogo ndogo wanaojishughulisha na sekta hii wamekuwa wakipewa usumbufu,
vitisho visivyokwisha na unyang’anyi wa kimacho macho wa mali zao.
•     Hakuna mazingira muafaka ya kiutendaji kwa sekta isiyo rasmi.
•     Hakuna usalama wa mali ya wafanyabiashara katika sekta hii.
•     Sekta isiyo rasmi inaumizwa na mzigo mzito wa kodi isiyolipika
•     Serikali haijaonyesha kutambua na kuthamini sekta hii hadi kuonekana kama inaipiga vita.
Dira ya Mabadiliko ya CUF
•     Serikali ya itakayoongozwa na CUF itaheshimu na kuthamini sekta isiyo rasmi na kuwapa
nguvu wale walioamua kujiendeleza kwa kujiajiri na kujiongezea kipato kinachotokana na
jasho halali.
•     Itaweka mazingira mazuri na endelevu kwa sekta isiyo rasmi.
•     Itaweka na itasimamia taratibu za kisheria zinazosaidia kuongoza shughuli za sekta isiyo
rasmi sanjari na kuondoa urasimu na kupunguza mzigo wa kodi.
UVUVI;
Tanzania ina ukanda mrefu wa bahari na imejaaliwa vilevile kuwa ni mshirika katika maziwa
makuu matatu yaliyomo kwenye Bara la Afrika. Zaidi ya hayo ina maziwa mengine madogo
madogo mengi na mito kadhaa mikubwa. Maji yote haya yana utajiri mkubwa wa samaki na
bidhaa nyingine za majini. Bila shaka sekta ya uvuvi pekee ingeliweza kuchangia kiasi kikubwa
kabisa katika pato la Taifa na kupunguza kwa kiasi kikubwa kabisa umasikini unaoikabili jamii
ya wavuvi nchini.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya uvuvi nchini;
Wavuvi nchini ni mashahidi kwamba sekta ya uvuvi haijapata msukumo wa kutosha ili iondokana
25
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
na ukale, na kujiingiza katika uvuvi wa kisasa wenye tija na uhifadhi wa mazingira. Uharibifu
mkubwa kwa kutumia mabomu na sumu na nyavu za uvuvi zisizokidhi viwango ni miongoni mwa
matukio yanayoendelea hivi sasa nchini, siyo tu kwamba mabomu na sumu yanafanya uharibifu
mkubwa wa mazingira na kuhatarisha maisha ya walaji wa samaki, lakini ni wazi pia kuwa uvuvi wa
namna hii ukiendelea baada ya miaka michache ijayo hakutakuwa tena na sekta ya uvuvi nchini, na
wavuvi waliokuwa wanadhani wanaupiga vita umasikini watajikuta ni masikini maradufu zaidi.
Hapajafanyika Juhudi za kutosha za makusudi kuwasaidia wavuvi wetu kuingia katika uvuvi wa
kisasa. Hali hii imesababisha Taifa lishindwe kufaidika na utajiri mkubwa wa samaki tulionao
katika eneo letu la bahari. Wavuvi wa kizalendo kutokana na kuwa na vyombo duni wamekuwa
hawawezi kwenda katika maeneo ya mbali na mwambao yenye kina kikubwa cha bahari
wanakopatikana samaki wengi zaidi. Hali hii imesababisha uvuvi katika maeneo haya kuingiliwa
na wavuvi wa kigeni ambao wamekuwa wakiendesha shughuli za uvuvi kinyume cha sheria na
kuliibia Taifa letu utajiri wa rasilimali hii ya asili.
Pamoja na kuwa na utajiri mkubwa wa samaki, kutokana na uchache wa samaki wanaovuliwa,
bei ya samaki katika soko ni ya juu kuliko inavyopaswa kuwa na vilevile wakazi wa kandokando
na rasilimali hizi hawapati samaki wa kutosha kama chakula, Serikali imeacha wafanyabiashara
wakubwa kununua kila samaki anayevuliwa na hivyo wenyeji hawawezi bei ghali ya samaki
walioko katika ushindani wa bei na badala yake kuambulia kula ‘mapanki’
Dira ya Mabadiliko ya CUF katika sekta ya Uvuvi;
Serikali itakayoundwa na CUF;
•     Itaanzisha mfuko rasmi wa kudumu wa mikopo ya masharti nafuu kwa wavuvi na wananchi
wengine wenye nia ya kujiajiri kwenye sekta hiyo kwa ajili ya kununulia vifaa vya kisasa vya
uvuvi na hifadhi, na kuanzisha ufugaji wa samaki (fish farming).
•     Itatoa Huduma ya mafunzo kwa wavuvi kwa kiasi kikubwa italenga katika matumizi ya njia
bora za hifadhi ili kuhakikisha kuwa mavuno ya wavuvi hayapotezi ubora wake kabla ya kufika
kwenye soko.
•     itaimarisha Shughuli za doria katika maeneo ya uvuvi ili kuhakikisha kuwa wavuvi wachache
hawaendelei na utaratibu wa uvuvi unaoharibu mazingira na kuleta maangamizi makubwa
kwa samaki na viumbe wengine wa majini; na ambao una muelekeo wa kuhatarisha ajira
kwenye sekta ya uvuvi.
•     Serikali ya CUF itaweka utaratibu wenye tija kwa wavuvi wadogo na wasindikaji wa mazao
ya uvuvi kwa kuhakikisha kuwa wenye viwanda hawajishughulishi na shughuli za uvuvi na
badala yake watapaswa kununua samaki kutoka kwa wavuvi wadogo wadogo. Mgawanyo
huu utasaidia uwepo wa mzunguruko wa fedha kwa kutoa ajira kwa wananchi wetu. Wenye
viwanda watasaidia kununua zana za uvuvi za kisasa na kutoa mikopo kwa wavuvi.
•  Uboreshaji wa soko na upanuzi wa ajira.
—     Juhudi zitafanywa kuhakikisha kuwa wawekezaji zaidi wa ndani na nje ya nchi wanafungua
viwanda vya kusindikia minofu ya samaki katika maeneo yote yenye mavuno makubwa ya
samaki, hususan katika mwambao wa bahari ya Hindi.
—     Huduma za ukaguzi na uchunguzi zitaimarishwa ili kuhakikisha kuwa siku zote mavuno
yetu ya samaki yanakuwa katika kiwango cha juu cha ubora ili kujihakikishia mauzo
mazuri katika masoko, hususan ya nje.
26
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
—    Halmashauri za miji na wilaya zilizoko kwenye maeneo ya wavuvi zitahamasishwa
kuingia ubia na makampuni binafsi kujenga maghala ya hifadhi baridi (Cold Strorage
Facilities) kwa ajili ya kuwasaidia wavuvi kuhifadhi mavuno ya ziada kwa kulipa ushuru
kidogo.
MALI ASILI.
Misitu na mapori ya asili;
Tanzania imejaliwa misitu na mapori mengi ya asili yenye mchanganyiko mkubwa wa mimea.
Pamoja na kwamba mimea hii imekuwa ikichangia uchumi wetu kwa kiasi fulani, bado
mkazo wa kutosha haujawekwa kuhakikisha kwamba faida yote iliyomo kwenye mimea hii
inapatikana. Uvunaji wa Gum Arabica ambayo ni utomvi mgumu utumikao kuimarisha vinywaji
vya aina mbalimbali pamoja na uwepo wa soko kubwa la bidhaa hii duniani na bidhaa yenyewe
inapatikana kwa wingi nchini hasa katika mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, na Shinyanga
hapajapatapo kufanyika juhudi madhubuti za makusudi kukuza uzalishaji na mauzo yake.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya Mali Asili;
•     Juhudi za dhati hazijachukuliwa kuhakikisha kuwa uvunaji endelevu wa mali asili iliyoko
katika misitu na mapori ya asili yaliyoko nchini unatumika kunyanyua pato la Taifa.
•     Serikali kwa kiasi kikubwa imezitelekeza taasisi zetu zinazoshughulika na tafiti zinazohusu
mimea asilia hususan katika tafiti za madawa. Matokeo yake ni kwamba taasisi hizi zinafanya
kazi kikamilifu tu pale zinapopata wafadhili wa nje ambao huja kuhodhi matokeo na manufaa
yanayotokana na tafiti hizo.
•     Kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika maeneo yote yanayozunguka
hifadhi za Taifa. Wanavijiji wamekuwa hawana haki ya kulinda mazao yao dhidi ya wanyama
waharibifu, na pale wanapochukua hatua dhidi ya uharibifu wowote wamekuwa wakinyan-
yaswa, kupigwa na hata kufunguliwa kesi za kubambikizwa na askari wa wanyama pori.
Dira ya mabadiliko ya CUF
Ili kuhakikisha kuwa Taifa linanufaika kikamilifu kutokana na misitu na mapori yake, Serikali ya
CUF itachukua hatua zifuatazo:
•     Itafanya tathmini ya mimea asilia inayopatikana nchini.  Tathmini hii itafanyika kwa lengo
la kujua aina, wingi, mahali inapopatikana
na matumizi yake ya kijadi. Tathmini hii
itafanywa na idara husika katika chuo Kikuu
cha Dar-es-Salaam kwa kushirikiana na
chuo kikuu cha Dodoma kwa kusaidiwa na
Wananchi mbali mbali wenye ujuzi katika
fani hiyo. Aidha vitengo vya matumizi ya
miti asilia katika Taasisi ya Madawa Asilia
ya Chuo Kikuu kishiriki cha Tiba, na Idara
ya Kemia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
vitaimarishwa.
•     Itaanzisha benki maalum ya kuhifadhi viasili
27
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
(Gene Bank) kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimataifa na idara zinazohusika katika
vyuo vyetu vikuu vya Dar-es-Salaam, Sokoine na Dodoma, Serikali itaanzisha benki maalum
ya kuhifadhi kila aina ya mmea asili unaopatikana nchini, kama kinga endapo janga lolote
laweza kusababisha aina yoyote ile ya mmea kutoweka.
•     Itaandaa sera ya kitaifa kuhusu uvunaji endelevu wa mimea asilia. Sera hii itasaidia sana
katika kuweka taratibu za wazi na zinazotabirika za kusimamia uvunaji na biashara ya mimea
asilia, hususan kwa ajili ya masoko ya nje.
•     Itahakikisha kuwa wananchi wanalipwa fidia kwa mali na mazao yao yanayoharibiwa na
wanyamapori wanaotoroka kutoka katika hifadhi za taifa. Aidha elimu ya uraia itatolewa
kwa watendaji wote wa hifadhi za taifa ili waweze kuzingatia haki za binadamu.
MADINI
Nchi yetu ina utajiri mkubwa wa madini ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Dhahabu,
Almasi, Tanzanite, Bati, Chuma, Uranium, Phosphate, Makaa ya Mawe, Vito, Nickel, Chokaa,
Jasi, Jaribosi, Chumvi, Mfinyanzi, Gesi, Mafuta nakadharika. Nchi kama Ghana, Afrika kusini,
Botswana na nyinginezo zimetumia mapato toka sekta ya madini kujenga miundombinu na
kukuza uchumi wa nchi zao kikamilifu. CUF inathamini na kutambua umuhimu mkubwa wa
kuendeleza mahusiano mema kati ya Serikali na Wachimbaji wa ndani na nje ya nchi kwa
kukaribisha uwekezaji mkubwa na wa kiteknolojia za kisasa katika sekta ya madini.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya Madini;
•     Wachimbaji wadogo wadogo wa madini wamekuwa na wakati mgumu kutokana na maeneo
yao ama kuchukuliwa na wachimbaji wakubwa, ukosefu wa mitaji ya kutosha, zana za kisasa,
na masoko yenye tija ya bidhaa zao.
•     Kumekuwepo na malalmiko ya muda mrefu juu ya wananchi wanaozunguruka maeneo ya
uchimbaji wamekuwa hawanufaiki na rasilimali ya madini yaliyopo katika eneo lao na badala
yake kumekuwa na athari kubwa ya kimazingira na afya za wananchi kutokana na kemikali
zinazotumika katika migodi na kumwagwa katika mifereji ya maji ambayo hutumiwa na
wananchi. Mfano mzuri ni athari zilizopatikana hivi karibuni katika mgodi wa dhahabu wa
North Mara.
•     Mikataba isiyo na manufaa ya kuridhisha kwa Taifa ni mambo yanayolalamikiwa ikiwa ni
pamoja na udhibiti duni wa ukaguzi wa madini yanayovunwa ikilinganishwa na hali halisi
ya uendeshaji wa shughuli hizo.
Dira ya Mabadiliko ya CUF katika Sekta ya Madini;
Serikali itakayoundwa na CUF itachukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa utajiri mkubwa wa
madini unatumika kikamilifu kuinua uchumi wa nchi yetu na hivyo kuboresha hali ya maisha
ya wananachi. Itazindua sera mpya ya uwekezaji katika sekta ya madini, kwa lengo mahsusi la
kulinda maslahi ya wananchi, wachimbaji wadogo wadogo na wawekezaji kwa ujumla. Pamoja
na mambo mengine sera hii itaweka utaratibu ufuatao kwa wawekezaji wa ndani na nje:
•     Serikali ya CUF itapitia taarifa za Tume zote zilizowahi kuundwa ikiwemo Tume ya Jaji
mstaafu Paul Bomani na nyingine na kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na tume hizo na
kuyafanyia kazi maeneo ambayo bado hayajashughulikiwa kikamilifu na serikali ya awamu ya
28
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
nne na awamu tangulizi ikiwemo kufuta mikataba mibovu na kuweka saini mikataba mipya
yenye kuzingatia maslahi ya taifa.
•     Mjadala wa kina utafanyika kati ya Serikali na wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi ili
kufikia maridhiano muafaka juu ya namna gani ya kulinda maslahi yao wawekezaji kwa kupata
faida inayolingana na uwekezaji wao katika sekta hiyo na wakati huohuo kuzingatia maslahi
ya Taifa na watanzania ambao ni wamiliki wa utajiri huo waliopewa na Mwenyezi Mungu.
•     Tutafanya marekebisho ya utozaji wa mrahaba na kodi kwenye madini. Tutahakikisha kwamba
mapato ya serikali yanakuwa alau asilimia thelathini (30) ya thamani ya mauzo ya madini
badala ya asilimia 3 ya hivi sasa, ili kuwepo na uwiano wa mapato ya migodi yetu na ile ya
Kusini na Magharibi mwa Afrika.
•     Tutaimarisha udhibiti na ukaguzi wa mavuno ya madini. Aidha tutarekebisha mfumo wa
misamaha ya kodi na uagizaji wa bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi ili kuweka urari sawia
wa kukuza sekta ya biashara nchini.
•     Tutashirikiana na wawekezaji wa ndani na nje katika kuhakikisha kuwa makampuni yote
yanaweka na kutoa taarifa sahihi za mitaji yao na kuepuka kufanya udanganyifu wa kuongeza
thamani halisi ya mitaji yao (over invoicing of capital expenditure) kwa madhumuni ya
kukwepa kodi.
•     Migodi yote mipya itasamehewa ushuru wa forodha kwa asilimia 100 kuhusiana na mitambo
itakayoingizwa kabla ya kuanza uzalishaji, na baada ya kuanza uzalishaji itapata msamaha
wa kodi ya mapato wa asilimia 100 katika miaka miwili ya kwanza. Baada ya kipindi hicho
kila mgodi utalazimika kulipa kodi kamili ya Serikali kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa.
•     Ili kuweza kuwapatia huduma muhimu ikiwa ni pamoja na masoko mazuri na kuwaendeleza
kitaalam, Serikali itawasaidia wachimbaji wadogo wadogo wajisajili kama kampuni na kwamba
kampuni inayohusika ndio itakayomilikishwa mgodi unaohusika.
•     Vitalu ambavyo vimetelekezwa kwa muda mrefu bila kuendelezwa vitashughulikiwa kwa
mujibu wa sheria husika.
•     Itasimamia uanzishwaji wa viwanda vya kuboresha madini husika kabla ya kuuzwa nje
(polishing industries) ili kuyaongezea thamani na kuanzisha ajira rasmi mpya kwa watanzania.
Aidha maeneo yote yaliyo na utajiri wa madini yatapewa kipaumbele cha kipekee ili miji hiyo
iendane na hadhi na ulinganifu wa utoaji wa mchango mkubwa wa utajiri huo kwa taifa.
•     Serikali ya CUF itahakikisha kuwa wananchi kwa wingi zaidi wanajishughulisha na shughuli
za uzalishaji wa madini ya mfinyanzi na chumvi ambayo yanapatikana nchini kwa wingi na
hayana tatizo la soko. Madini ya chumvi yana soko kubwa katika nchi za jirani. Mfinyanzi
ni madini yenye soko kubwa katika viwanda vya petroli sehemu mbalimbali duniani.
UTALII
Ziko nchi nyingi duniani ambazo zinategemea kwa kiasi kikubwa biashara ya utalii kuweza
kufidia gharama za mahitaji ya wananchi wake. Nchi hizi zimefanikiwa kwa sababu zimewekeza
kwa dhati kwenye sekta hii, pamoja na kwamba baadhi yake hazina vivutio vingi vya watalii.
Bahari ya Hindi, Visiwa vya Zanzibar na Mafia, Delta ya mto Rufiji, mbuga za wanyama za
Serengeti, Ngorongoro, Lake Manyara, na Selous, milima Kilimanjaro na Meru na ukarimu wa
wananchi wetu na tamaduni zao, unaifanya Tanzania kuwa nchi ya pekee kwa mapumziko
murua kwa wageni watokao nchi za Ulaya, Marekani na Asia. Gazeti la Financial Times la
29
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
Uingereza katika moja ya matoleo yake limeelezea kuwa Tanzania “Offers one of the world’s
most complete holiday destinations”. (Ni moja ya nchi za dunia zinazofaa kutembelewa na
anayehitaji mapumziko murua ya uhakika). Hata hivyo hatujautumia urithi huu kikamilifu
kuinua hali ya maisha ya Watanzania tuliopo sasa na wale wa vizazi vijavyo.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya utalii;
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
wawe na taarifa kamili ya nchi yetu na sekta ya utalii.
•     Serikali ya CUF italinda mazingira ya hifadhi za Taifa kwa kuwashirikisha wananchi wanaoishi
kandokando ya hifadhi wanufaike na mapato ya hifadhi hizo. Serikali ya CUF itatengeneza
utaratibu ambapo kila kijiji au kata ambayo eneo lake lina kivutio chochote cha utalii
vinapewa sehemu ya mapato yanayotokana na utalii. Hii itawafanya wenyeji wa maeneo
husika wanufaike moja kwa moja na maeneo waliyoyatunza kwa karne kadhaa.
Hapajakuwepo na uwekezaji wa kutosha wa miundo mbinu inayohitajika kwa huduma ya utalii. •  Huduma kwa wafanyakazi wa idara ya wanyamapori;
Serikali kwa muda mrefu ilimejikita katika kuangalia utalii wa asili, yaani ule wa kuja kuangalia
mbuga za wanyama au kupanda mlima Kilimanjaro, na kusahau kuendeleza maeneo ya utalii
ya aina nyingine. Juhudi za kuhamasisha utalii wa ndani zimekuwa zikifanyika kwa msimu na
hazijitoshelezi inavyotakiwa.
Kuna tatizo katika utaratibu wa ugawaji wa maeneo maalumu ya uwindaji na kwamba imekuwa Serikali itachunguza tuhuma malimbali zinazoelekezwa katika maeneo haya na kuchukua hatua
ikilalamikiwa kuwa hauzingatii maslahi ya Taifa serikali ya awamu ya nne imechagua kukaa muafaka kurekebisha matatizo yaliyopo.
kimya.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•  Kuimarisha miundo mbinu;
—     Serikali itaimarisha mawasiliano ya aina zote katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu
ambayo kwa hivi sasa yako kwenye ukanda wa utalii.
—     Serikali itatafuta wawekezaji zaidi kuwekeza katika huduma za watalii kama vile hoteli,
usafirishaji, uandaaji wa ziara nakadharika.
—     Serikali italinda mazingira ya hifadhi za taifa.
•  Kupanua wigo shughuli za utalii;
Hivi sasa shughuli za kitalii nchini zimeelemea sana
kwenye utalii wa kiasili. Serikali ya CUF pamoja na
kuchukua hatua za kuimarisha utalii wa kiasili, pia
itasimamia kwa karibu uanzishwaji na uuzwaji wa
utalii wa kimazingira na kiutamaduni (eco-tourism
& cultural tourism). Utalii wa aina hii utawavutiwa
wageni wengi wenye nia ya kujua Watanzania
wanavyoishi na mazingira yao, hususan wanafunzi
na watafiti. Aidha Serikali itafanya juhudi kubwa
kuhamasisha na kutoa vichocheo kwa watalii wa
ndani. Matarajio ni kuongeza pato linalotokana na
utalii kutoka wastani wa dola za kimarekani milioni
2300 kwa mwaka za sasa hadi wastani wa dola
milioni 4200 kwa mwaka katika miaka 5 ijayo.
•  Kukuza na kupanua soko la utalii;
Pamoja na kuimarisha miundo mbinu ya kitalii na kupanua vivutio vya utalii, Serikali ya CUF
itafanya juhudi kubwa kuitangaza biashara yetu ya utalii nchi za nje, ikiwa ni pamoja na
kuanzisha kituo kikubwa cha utalii kwenye mtandao wa internet ambacho kitakuwa na habari
zote zitakazo kuwa zinaboreshwa mara kwa mara ili wageni wenye nia ya kuizuru nchi yetu
30
Zitaimarishwa kwa kiasi kikubwa kwa kuboresha maslahi zaidi na kuwapatia vitendea kazi.
Kuimarishwa huku kwa huduma kutakuwa ni motisha kwa wafanyakazi hawa kutoa huduma bora
na ya uhakika zaidi siyo kwa wanyamapori tu, bali pia na kwa watalii wanaouzuru maeneo yao.
•  Kusimamia maeneo ya uwindaji;
HUDUMA ZA KIBIASHARA.
Hali ya huduma za kibiashara nchini siyo ya kuridhisha hususani katika sekta ya benki, mitaji,
na huduma za Bima.
HUDUMA ZA BENKI
•     Benki ni Taasisi muhimu sana siyo tu katika kuhudumia biashara ila pia katika kurahisisha
mfumo wa malipo na utunzaji wa akiba. Kigezo kimojawapo muhimu cha uchumi imara katika
nchi yoyote ni umadhubuti wa mtandao wa kibenki uliopo. Katika nchi yetu taasisi za kibenki
zimekuwa na matatizo ya aina nyingi kwa muda mrefu. Kabla ya mfumo wa benki binafsi
kuruhusiwa nchini sekta ya benki ilikuwa chini ya ukiritimba wa benki chache za ‘Umma’
yaani NBC, CRDB, Benki ya Nyumba, na Benki ya Posta chini ya usimamizi wa lililokuwa
Shirika la Posta na Simu. Ukiondoa Benki ya Posta ambayo kimtaji na kwa aina ya wateja
iliyowahudumia ilikuwa ni benki ndogo tu, benki hizi hazikufanya kazi kibiashara, zilitawaliwa
na utoaji wa huduma mbaya, wizi na udanganyifu wa hali ya juu hadi kuilazimu Serikali mara
kwa mara kuzipa ruzuku ili kuzinusuru zisife.
•     Mabadiliko ya sheria yaliyoruhusu wawekezaji binafsi kuwekeza katika sekta ya benki nchini
yalisaidia zaidi kuzinusuru NBC na CRDB. Siyo tu kwamba mabadiliko haya yalizilazimisha
benki hizi kujifanyia marekebisho makubwa kiutendaji ili kukabiliana na ushindani, bali pia
yaliinufaisha CRDB moja kwa moja pale ilipoamua kuingia ubia na wawekezaji binafsi na
shirika la maendeleo la misaada la Denmark (Danida).
Hali ilivyo sasa katika Sekta ya Benki;
•     Pamoja jitihada za kueneza huduma za kibenki kwa kuanzisha matawi mengi zaidi na matumizi
ya mtandao wa mawasiliano ya simu kupata taarifa za kibenki na kulipia huduma mbalimbali
bado sekta ya benki imekuwa na mfumo usio sawa wa utoaji wa mikopo na utozaji wa riba
kwa asilimia kubwa ukilinganisha na hali ya mzunguruko wa fedha kiuchumi.
•     Kumekuwa na tatizo la kutokuwa na udhibiti wa idadi ya wateja katika matawi kiasi cha
kusababisha msongamano mkubwa kama ule wa magari barabarani katika kuwahudumia
31
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
wateja kwa haraka. Wakati mwingine umchukua mtu mpaka masaa matano akiwa katika foleni
ya kusubiri kuweka au kuchukua fedha.
•     Mashine za ATM zilizowekwa katika baadhi ya maeneo ni za mtumba ‘second hand’ na hivyo
kuzorotesha ufanisi wa utowaji wa huduma kwa wakati wote.
•     Mtandao wa kibenki umejikita zaidi katika maeneo ya mijini na hasa Dar es Salaam na
kuwatelekeza wananchi wengi wa maeneo ya vijijini ikiwa ni pamoja na wakulima kupata
huduma za kibenki kwa ukaribu. Mathalani Benki ya Rasilimali Tanzania (Tanzania Investment
Bank-TIB) benki iliyoelekezwa kupokea sehemu ya fedha za EPA zilizorejeshwa ambayo ina
dirisha la kilimo (Agriculture window) ipo Dar es Salaam.
•     Serikali wala Watanzania katika sekta binafsi hawamiliki benki kubwa ya biashara. Utendaji
wa mabenki haya unaongozwa na makao makuu yao nje ya nchi. Athari hizi zimeonekana
wakati wa mtikisiko wa uchumi duniani. Mabenki yalipunguza kasi ya kutoa mikopo sekta
binafsi wakati Tanzania haikuwa na matatizo kama yale yaliyotokea nchi za Marekani na Ulaya.
Serikali haikuweza kutumia benki hizi kupunguza athari za mtikisiko wa uchumi duniani.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
Sekta ya benki inahitaji kufanyiwa marekebisho ya msingi kuiimarisha ili kurejesha imani ya
wananchi kwa benki zilizopo na kujenga mazingira yatakayowahakikishia wawekezaji juu ya
uwezo wa mfumo wetu wa benki kukidhi mahitaji yao. Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo
ili kuhakikisha kuwa mfumo wa kibenki unaimarishwa na kuweza kutoa mchango mkubwa katika
kuinua hali za maisha ya watanzania:
•  Kuzilinda benki dhidi ya usimamizi mbovu;
Serikali ya CUF itafanyia marekebisho sheria ya Benki Kuu ili iweze kutumia mamlaka iliyopewa
katika mazingira ya uwazi na ithibati zaidi katika kutekeleza majukumu yake ya ukaguzi na
usimamizi. Aidha Mabadiliko hayo yatalenga kuziwezesha benki kuwa huru zaidi katika kuanzisha
huduma mpya katika utoaji wa mikopo kwa nia ya mikopo hiyo kuwafikia watu wengi zaidi.
Mfano mzuri wa huduma hizi ni utaratibu unaoruhusu benki kuwekeza katika miradi mbalimbali
itakayoona inafaa na kushiriki katika kugawana faida badala ya kutoza riba.
•  Serikali kuendelea kumiliki Benki ya Wananchi;
Serikali ya CUF itaendelea kuimiliki benki ya Posta Tanzania na kuiwezesha kimtaji kusudi iweze
kupanua mtandao wa huduma zake katika maeneo yote ya nchi yetu; na kuwahudumia wananchi
wanyonge walio wengi.
•  Riba katika amana na mikopo;
Sera ya benki itaangaliwa upya ili kuweka uwiano wa haki kati ya riba inayotolewa kwa amana
za wateja na riba inayotozwa katika mikopo ya wateja hii itasaidia wananchi wengi kukopa na
kuwa na uwezo wa kulipa bila kuhofia kuuzwa kwa amana zao.
•  Benki ya Raslimali ya Tanzania;
Tanzania Investment Bank itaongezewa mtaji na kuundiwa menejimenti na Bodi mpya ya watu
wenye ujuzi na uzoefu na wasio na shutuma za ufisadi na ubadhirifu ili iwe benki yenye uwezo
wa kutoa mikopo ya muda mrefu, na kuanzisha matawi katika kila mkoa na baadae kila wilaya
ili kuwafikia walengwa husika ikiwa ni pamoja na wakulima.
•     Utaandaliwa utaratibu wa kudhibiti ukomo wa idadi ya wateja katika matawi ili kuondokana na
32
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
msongamano mkubwa kama ule wa magari barabarani katika kuwahudumia wateja na hii itaweze-
sha uanzishwaji wa matawi mengi zaidi yatakayotoa ajira na kuharakisha maendeleo ya Taifa.
•     Mtandao wa kibenki utaenezwa mpaka maeneo ya vijijini ili wananchi wengi wa maeneo ya
vijijini ikiwa ni pamoja na wakulima waweze kupata huduma za kibenki kwa ukaribu.
•     Juhudi za makusudi zitafanyika kuhakikisha kuwa inauhishwa upya benki kubwa ya biashara
inayoongozwa na watanzania wenyewe ili iweze kusaidia ukuaji wa uchumi kwa kutoa huduma
za mikopo kwa wajasiriamali wetu waliowengi ambao mitaji yao ya biashara ni midogo na
haiimiri soko la ushindani wa kibiashara.
MASOKO YA MITAJI NA HISA
Dhana ya Masoko ya Mitaji na Hisa bado ni ngeni kwa Watanzania walio wengi. Ugeni huu
unatokana na historia ya nchi yetu kutoka katika
sera za ‘Ujamaa’ zilizoshinikizwa kwa Watanzania
kwa karibu miaka 35 ambazo hazikuwa zinaruhusu
kabisa kuwepo kwa aina hii ya masoko. Hata baada
ya Serikali ya awamu ya pili kuzitupilia mbali sera
hizo na kuruhusu uchumi wa soko huria, bado
taasisi hii haikupata kipaumbele kutokana na
ukweli kwamba mazingira halisi ya kiuchumi ya
wakati huo hayakuwa yanaruhusu. Soko kama hilo
wakati huo halikuwa na maana yoyote kwa sababu
hakukuwa na wanunuzi wala wauzaji. Wananchi
ambao mara nyingi ndio wanunuzi (wa hisa) katika
soko la aina hii walikuwa taabani kwa umasikini
na makampuni (ukiondoa machache sana) ambayo
ndio wauzaji yalikuwa katika hali mbaya mno.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya masoko na mitaji ya hisa;
•     Soko la Mitaji na Hisa la Dar-es-Salaam, maarufu kwa jina la kiingereza la The Dar-es-Salaam
Stock exchange (DSE), halina uchangamfu wa kutosha na uendeshaji wa shughuli zake ni
mdogo sana. Ni kweli kuwa moja ya sababu zinazofanya shughuli za soko hili kudorora ni
ugeni wa dhana hii kwa Watanzania. Lakini sababu kubwa zaidi ni umasikini wa Wananchi.
Ni vipi utarajie Wananchi kujiingiza katika biashara ya kununua na kuuza hisa ili hali walio
wengi hawana hata kipato kinachoweza kukidhi mahitaji yao ya kawaida ya mwezi? Umasikini
wa Watanzania umewafanya walio wengi wasiwe na shauku ya kuwekeza katika miradi ambayo
matunda yake yatachukua muda mrefu kuonekana, na si kwa sababu hawaelewi umuhimu wa
kuwekeza katika miradi hiyo. Tatizo lao ni kutomudu kusubiri kwa muda mrefu. Hii ndiyo
sababu michezo ya upatu kama DECI n.k pamoja na matatizo yake, ni maarufu na Wananchi
huichangamkia sana. Katika upatu faida haitarajiwi baada ya kipindi kirefu cha mwaka, bali
ni katika kipindi cha miezi au hata majuma machache tu. Mtu anajua kuwa akiwekeza huko
huo ni muda mfupi mno kiasi cha kutoweza kuathiri ulipaji wa karo za wanawe au kodi ya
pango kwa mwenye nyumba.
•     Hapajakuwepo na nia thabiti au mikakati sahihi mbadala ya kuwasaidia wananchi kuondoa
umasikini wao bila shaka yoyote wangegundua kwamba kipaumbele kilikuwa kiwekwe kwenye
aina zingine za Masoko ya Mitaji ambazo zingeendana na hali halisi iliyopo. Masoko ya aina
33
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
hii ni yale yenye mitaji inayotafuta wa kuitumia kwa kuingia ubia au kulelea mawazo mapya
ya kibiashara. Masoko haya kwa kiingereza yanajulikana kama Venture Capital Markets & Start
– up Incubators.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•     kuimarisha soko la hisa la Dar-es-Salaam (DSE).
—     Pamoja na mambo mengine Serikali itahamasisha makampuni zaidi yenye sifa kujiorodhesha
kwenye soko la hisa.
—     Serikali itaimarisha Kanuni zinazoyataka makampuni kuweka mahesabu sahihi na pia
itaimarisha huduma za ukaguzi.
—    Makampuni na mashirika yote ya Serikali yaliyobinafsishwa na ambayo yako kwenye
mpango wa kubinafsishwa yatahamasishwa yaorodheshwa kwenye soko hili.
—     Chini ya utaratibu mpya wa ubinafsishaji utakaowekwa na Serikali, Serikali kupitia soko
hili itawauzia wananchi asilimia 30 ya hisa zake kwenye shirika au kampuni yoyote
inayobinafsishwa.
•  Kupanua huduma za masoko ya mitaji;
—     Mbali ya kwamba Serikali ya CUF itaanzisha mifuko mahsusi ya mikopo ya masharti nafuu
(Incubator Funds) kwa ajili ya shughuli za uzalishaji kama ambavyo imekwishaelezwa
kwenye sehemu nyingine za ilani hii, Serikali pia itatoa leseni kwa makampuni binafsi
yatakayokuwa na nia ya kufungua mifuko ya aina hii kwa nia ya kuwawezesha wananchi
wenye mawazo mapya ya kibiashara lakini wasio na sifa za kukopa katika mabenki,
kufanikisha malengo yao.
HUDUMA ZA BIMA
Dhana ya Bima ni kutoa kinga ili kufidia madhara yanayoweza kutokea. Mbali ya kwamba nchini
Tanzania ziko bima za aina nyingi, ni aina chache tu (zile ambazo zinalazimishwa kwa mujibu
wa sheria) ndizo ambazo zimeshamiri. Bima nyingi muhimu, kama vile bima ya kinga dhidi ya
uharibifu kwenye biashara-mathalani kutokana na moto, bima ya kinga dhidi ya unyang’anyi,
n.k., bado haziwavutii wananchi wengi.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya Bima nchini;
kwa muda mrefu mno kulikuwa na usumbufu mkubwa kwa wananchi wengi ambao walikuwa
wakifuatilia malipo yao ya bima NIC – ambalo lilikuwa ndiyo shirika pekee la bima nchini. Wakati
mwingine kwa visingizio mbalimbali ilichukua hata zaidi ya mwaka mmoja kabla ya muathirika
kufidiwa. Hali hii imewafanya wananchi wengi wajenge utamaduni wa kutokuwa na imani na taasisi
za bima, japokuwa hivi sasa soko la bima ni huru na ufanisi umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
Utamaduni uliojengeka wa kulea rushwa iliyosababisha sekta ya bima kujaa uzembe na ubabaishaji,
imesababisha wananchi kuendelea kutokuwa na imani sana na sekta bima mpaka hivi leo.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•  Ubinafsishaji wa shirika la bima la Taifa (NIC);
Hatua za haraka zitachukuliwa kulibinafsisha shirika hili ili pamoja na mambo mengine lifanye
shughuli zake kwa ufanisi na kuzuia lisiendelee kuwa kisima cha Serikali kuchota fedha za
34
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
wanachama kufanyia ubadhirifu. Aidha Serikali itahakikisha kuwa ubinafsishaji wa NIC unaenda
sambamba na malipo halali ya mafao ya wafanyakazi wa shirika hilo na katika ubinafsishaji huo
wananchi wa kawaida wanakuwa na uwezo wa kumiliki hisa za kutosha.
•  Uimarishaji wa ushindani katika sekta ya bima;
Serikali ya CUF itahimiza makampuni binafsi zaidi kuwekeza katika sekta ya bima ili kuimarisha
ushindani na kupanua orodha ya huduma zinazotolewa. Aidha Serikali itayahimiza makampuni
ya bima kutoa elimu ya kina kwa wananchi kuhusu huduma zao ili zieleweke na wananchi wengi
zaidi waweze kushiriki.
HIFADHI YA JAMII.
Nchini Tanzania kuna mifuko kadhaa ya hifadhi ya jamii ambayo kila mfanyakazi kwenye sekta
rasmi ni lazima kisheria awe mwanachama wa mmoja wapo. Iliyo maarufu zaidi katika hii
ni ile ya PPF, PSPF, na LGPF. Mbali ya nia nzuri ya kuwepo kwa mifuko hii, uendeshaji wake
umekuwa na manufaa kidogo kwa wananchama wake na badala yake Serikali imekuwa ikitumia
fedha za wanachama kujinufaisha. Sheria iliyopitishwa hivi karibuni inayowazuia wanachama
wa PPF walioachishwa kazi kabla ya kufikia umri wa kustaafu kuchukua fedha zao ati mpaka
watakapofikia umri wa kisheria kuweza kustaafu, haikuwa na nia nyingine yoyote zaidi ya
kuiwezesha Serikali kupitia shirika hilo kujikopesha fedha za wanachama hao kwa nguvu.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya hifadhi ya Jamii;
Kwa muda mrefu sasa mifuko hii imekuwa ikiwekeza fedha za Wanachama wake kwenye vitega
uchumi mbalimbali lakini faida itokanayo na vitega uchumi hivi haigawiwi kwa wanachama.
Mifuko hii imekuwa ikikopesha fedha za wanachama kwa watu ambao siyo wanachama, na
kibaya zaidi haijaweka utaratibu wowote unaoeleweka kuwakopesha wanachama wake.
Mifuko hii imekuwa ikihodhi fedha za wanachama zinazotokana na michango ya mwajiri, pale
inapotokea mfanyakazi kufukuzwa kazi. Aidha kumekuwa na usumbufu mkubwa kwa Wanachama
wanaotaka kuchukua michango yao baada ya kuacha ajira zao.
Sera ya kukata kodi mafao ya wafanyakazi wanaostaafu au kuacha na kuachishwa kazi. Hii haina
mantiki hata kidogo ikizingatiwa kuwa muathirika anahitaji sana mafao haya kama mtaji wa
kujianzishia shughuli nyingine za kujiendeshea maisha yake.
Sera mbovu za huduma ya hifadhi ya jamii kuwalenga zaidi watumishi walio katika sekta rasmi
na kuwatelekeza kabisa wananchi wengi walio katika sekta isiyo rasmi; hususani wakulima,
wafugaji, na wavuvi.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•  Kuifanya mifuko hii iwajibike zaidi kwa wanachama;
—     Mgawanyo wa faida inayotokana na vitega uchumi. Mifuko hii itawajibika kugawa robo
tatu ya faida yote inayotokana na vitega uchumi vilivyotokana na kuwekeza fedha za
wanachama, kwa wanachama wa mifuko hiyo.
—     Malipo yote kwa wanachama wanaoacha ajira zao. Malipo yao yatakamilishwa katika
kipindi cha miezi mitatu (3) na mwanachama atakuwa na haki ya kuchagua utaratibu
wa malipo anaoutaka. Mathalani, tofauti na utaratibu wa sasa unaotumiwa na NSSF,
mwanachama atakuwa na haki ya kuchukua fedha zake zote kwa mkupuo mmoja iwapo
huo ndio utakuwa uamuzi wake.
35
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
Serikali ya CUF itaasisi sera ya taifa ya hifadhi ya jamii ili huduma hii iweze kuwanufaisha Uganda na Rwanda hupitia katika bandari ya Mombasa nchini Kenya.
wananchi walio wengi. •     Urasimu mkubwa katika kutoa makontena bandarini,inaweza kumchukua mfanyabiashara wiki
                       au miezi kadhaa kufanikiwa kupata mizigo yake kutoka bandari za Tanzania, kwa mfano
                      tangu Serikali iingie ubia na kampuni ya TICTS ili kupakua na kupakia mizigo bado hakuna
                     mabadiliko makubwa yaliyofanyika, mizigo inachukua miezi kupakuliwa bandarini,huu ni
                    uzembe mkubwa na unawafanya wafanyabiashara wengi wazikimbie bandari zetu.
                   •     Shehena iliyohudumiwa na bandari ya Dar es Salaam ilipungua toka tani milioni 6.32
                    mwaka 2006 mpaka kufikia tani milioni 2.32 mwaka 2008. Shehena katika bandari ya Tanga
                   imepungua toka tani 519,000 mwaka 2006 na kufikia tani 178,000 mwaka 2008. Bandari ya
                  Mtwara ilihudumia shehena ya tani 82,000 tu mwaka 2008 ukilinganisha na tani 519,000
                 mwaka 2006.
MATUMIZI YA BANDARI Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•     Ni nchi chache duniani zenye jiografia nzuri kama Tanzania lakini haziko katika matumizi Ni wazi kabisa kuwa kungekuwapo na njia za reli zinazounganisha bandari ya Mtwara na Mbamba
  ya jiografia hiyo. Tanzania ina ufukwe wa bahari upatao kilometa 1,424 na ndani yake kuna bay kwenye ziwa Nyasa, na miji ya Arusha na Mwanza kwenye ziwa Victoria, na hali ya ufanisi
  Bandari za Tanga, Dar-es-Salaam, Mtwara na Zanzibar kwa upande wa mashariki. Upande ikaingizwa katika utendaji wa bandari
  wa kaskazini, kaskazini magharibi, magharibi, na kusini magharibi inapakana na mataifa zetu, bila shaka bandari za Mtwara na
  ya Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Zambia na Malawi. Haya yote ni mataifa ambayo Tanga zingekuwa ni bandari chaguzi
  hayakujaliwa milango ya bahari, hivyo ni tegemezi kwa mataifa ya jirani ya Tanzania, Kenya, kwa nchi za Malawi na Uganda. Hali
  na Msumbiji kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa zao. hii ingepunguza msongamano kwenye
  •     Miongoni mwa nchi hizi tatu – yaani Tanzania, Kenya na Msumbiji, Tanzania ina nafasi bandari ya Dar-es-Salaam na kutoa
      ya kipekee kabisa. Tofauti na Kenya ambayo nchi pekee inayopakana nayo isiyokuwa na nafasi kwa bandari hii kutoa huduma
      bandari ni Uganda, au tofauti na Msumbiji ambayo nchi pekee inazopakana nazo zisizokuwa bora zaidi kwa nchi za Zambia, Congo,
      na bandari ni Swaziland, Zimbabwe, na Malawi, Tanzania kama ambavyo tumekwishaona Burundi na Rwanda.
      inapakana na mataifa sita yasiyo na bandari. Hii ina maana kwamba bandari zetu za Tanga,
      Dar-es-Salaam, na Mtwara ni maeneo ambayo yaliyotakiwa kuwa na pilika pilika nyingi
      katika harakati za usafirishaji wa bidhaa zinazoingia na kutoka katika nchi hizi za jirani. Kwa
      kifupi bandari hizi zilitakiwa kuwa ni chanzo kikubwa sana cha ajira na mapato ya nchi.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya Bandari nchini; •  Kuongeza ufanisi na tija kwenye
                                                    utendaji wa bandari zetu;
•  Kusitisha utaratibu wa kujimilikisha michango ya waajiri;
Utaratibu huu utasitishwa mara moja na michango ya mwajiri atakabidhiwa mfanyakazi
aliyefukuzwa kazi sambamba na michango yake.
•  Kusitisha utaratibu wa kukata kodi kwenye mafao ya wafanyakazi;
Serikali ya CUF itafuta mara moja utaratibu wa kukata kodi kwenye mafao ya wafanyakazi
wanaostaafu au kuacha kazi; ili kutoa fursa kwa wahusika kujianzishia shughuli za kuendeshea
maisha yao wakiwa na uwezo mzuri zaidi.
•  Kuasisi sera ya Taifa ya hifadhi ya jamii;
•     Huduma mbovu bandarini na mtandao mbovu wa njia za reli na barabara ni mambo ambayo
yamesababisha nchi jirani zisizo na bandari kutopendelea kuendelea kutumia bandari zetu
kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, Malawi na Zambia ziko karibu zaidi na bandari ya Mtwara kuliko
zilivyo karibu na bandari ya Dar-es-Salaam. Hata hivyo zinapoamua kusafirisha bidhaa zake
kupitia Tanzania zinalazimika kutumia bandari ya Dar-es-Salaam kwa sababu mawasiliano ya
barabara na reli ni rahisi zaidi. Hali kadhalika Uganda iko karibu zaidi na bandari ya Tanga
kuliko ilivyo karibu na bandari ya Dar-es-Salaam, lakini ni rahisi zaidi kupitishia bidhaa zake
Dar-es-Salaam kutokana na mawasiliano ya reli kuwa rahisi zaidi kwa njia hiyo.
•     Wizi na uzembe ni mambo ambayo yanawafanya wafanyabiashara wengi wa nchi jirani
kupendelea bandari za nchi nyingine kuliko zile za kwetu. Mathalani, Zambia ilishawahi
kutamka wazi kuwa pamoja na umbali kati ya Zambia na Afrika Kusini, na uhusiano wa karibu
kati yake na Tanzania, iko radhi ianze kutumia bandari za Afrika Kusini kusafirishia bidhaa
zake kwa sababu: mosi, itakuwa na uhakika wa usalama wa bidhaa hizo, na pili upotevu
wa muda utakuwa mdogo. Hali kadhalika kwa sababu hizo hizo sehemu kubwa ya bidhaa za
36
Serikali ya CUF itachukua hatua za
makusudi kabisa kuhakikisha kuwa
bandari zetu zinakuwa ni chanzo
kikubwa cha mapato ya nchi na ajira.
Hatua hizi ni pamoja na:
—     Ubinafsishaji wa baadhi ya shughuli za bandari utaendelezwa ili kuvutia teknolojia mpya,
mitaji, utaalamu na ufanisi – hususan katika usalama wa bidhaa za wateja.
—     Kutakuwa na utaratibu wa makusudi wa kujifunza kutoka kwa wenzetu waliopata
mafanikio makubwa kwenye matumizi ya bandari zao.
•  Kuzifanya bandari zetu ziwe ni chaguo la kwanza;
Ili kuzifanya bandari zetu kuwa ni chaguo la kwanza kwa wasafirishaji wa mizigo wa nchi jirani,
pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji tunahitaji pia kuangalia suala la gharama kwa
wasafirishaji hao. Kama ambavyo tayari imeshaelezwa, kuna wasafirishaji ambao wangevutiwa
zaidi na matumizi ya bandari za Tanga na Mtwara iwapo kungekuwa na usafirishaji mzuri wa reli
kuanzia kwenye bandari hizo. Serikali itachukua hatua za dharura kabisa kutafuta wawekezaji
watakaowekeza katika ujenzi wa njia hizo za reli.
•     Serikali ya CUF itahakikisha panakuwa na kampuni za uhakika za kupakua na kupakia mizigo
37
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
na itazisimamia ipasavyo ili kuondoa msongamano bandarini na kufanya muhusika kupokea
mzigo wake (kontena) kwa siku chache kabisa baada ya mzigo kuwasili bandarini. Kampuni
ambayo itashindwa kufanya kazi hii kwa haraka na ufanisi itaondolewa mara moja na kazi
kupewa kampuni nyingine.
MAPATO YA KODI
Kulipa kodi ni wajibu wa kila Mwananchi mwenye uwezo wa kiuchumi kufanya hivyo. Hata hivyo
mazingira ya ulipaji kodi yanatakiwa yaandaliwe vizuri kiasi kwamba wajibu huu ugeuke kuwa
ni utamaduni uliokumbatiwa na Wananchi na siyo jambo la kuchukiza.
Iwapo utamaduni wa namna hii utajengwa ni dhahiri kabisa kuwa mapato ya Serikali yatokanayo
na kodi yatakuwa ni makubwa na ya kuridhisha. Kwa bahati mbaya sana mazingira yaliyoko
nchini kwetu katika masuala ya kodi yamekuwa ni kizingiti dhidi ya kukua kwa utamaduni huu.
Hali hii imesababisha kuwe na udhaifu mkubwa katika ukusanyaji wa kodi.
Hali ilivyo sasa katika eneo la mapato ya kodi
•     Viwango vya kodi vimepelekea kujengeka kwa hisia kuwa ni vikubwa mno kiasi cha kutishia
uhai wa biashara au maendeleo ya mlipa kodi.
•     Hisia za matumizi mabaya na ufisadi wa fedha za walipa kodi yanayofanywa na Serikali
yamewafanya walipa kodi wengi kuwa na imani kuwa kodi inayokusanywa haitumiki kwa
maslahi ya Taifa.
•     Utaratibu wa kutoza kodi ambao unawapendelea walipa kodi wakubwa (kwa kuwapa misamaha
holela) na kuwakandamiza walipa kodi wadogo.
•     Chini ya nusu ya ushuru wa mafuta ya petroli na diseli unaostahiki kutozwa ndiyo unaokusanywa
na serikali.
•     Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imekuwa ikitumiwa na Serikali ya CCM kuwatisha walipa
kodi, na hususani wafanyabiashara wakubwa ili kuiunga mkono CCM na yule ambaye hafanyi
hivyo hupelekewa gharama kubwa za kodi au kufilisiwa kwa mlango wa nyuma.
•     Kumekuwa na mlundikano wa kodi (duplication of taxes) jambo ambalo linawaumiza walaji na
kuwakatisha tamaa wafanyabiashara, mathalan katika biashara inayofanyika kati ya Zanzibar
na Tanzania bara.
Dira ya Mabadiliko ya CUF
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 CUF- Chama cha Wananchi kilifanya kampeni kubwa
dhidi ya mwenendo mzima wa ukusanyaji kodi nchini. Kutokana na juhudi hizi kumekuwa na
mafanikio kiasi fulani. Mafanikio haya ni pamoja na kuondolewa kwa utaratibu uliokuwepo
uliokuwa unamshinikiza mlipa kodi kulipa sehemu ya kodi inayotarajiwa (provisional tax) kabla
hata ya kuanza kwa shughuli yenyewe inayotakiwa ije itozwe kodi, na kufutwa kwa kilichokuwa
kinaitwa kodi ya maendeleo. Hata hivyo bado kunahitajika marekebisho makubwa katika mfumo
wa kodi na jinsi inavyotumiwa ili kuwajengea watanzania utamaduni wa kuridhia kulipa kodi.
Serikali ya CUF inakusudia kuchukua hatua zifuatazo ili kufanya Mabadiliko ya kweli kwenye
mfumo wa kodi kwa ajili ya kuleta manufaa yanayotarajiwa na wananchi:
•  Kodi za Serikali kuu;
Kuangalia upya viwango vya kodi;
38
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
—     Serikali ya CUF itavipitia upya viwango vyote vya kodi zinazotozwa na Serikali kuu kwa nia
ya kuvirekebisha visiwe ni kero kwa wananchi walipa kodi. Viwango vya kodi vinavyohusu
vifaa vya elimu, vifaa vya afya, pembejeo za kilimo, maji, nishati, na mawasiliano ikiwa
ni pamoja na reli na barabara vitapewa upendeleo maalum kwa kipindi cha miaka kumi ili
kukuza uwekezaji katika maeneo haya.
—     Utaratibu mpya wa kuchukua kodi katika posho utaanzishwa, kila mtu apokeaye posho
katika vikao, semina, makongamano n.k atatozwa kodi. Hii itahusisha kwa dhati
posho wanazopokea wabunge, mawaziri na maafisa wa ngazi zote wanaopkea posho
wahudhuriapo shughuli yoyote.
—     Utaratibu wa kodi ya mapato kwa kampuni mpya;
Marekebisho yaliyofanyika yanawaruhusu wafanyabiashara wapya kufanya kazi kwa miezi
mitatu tu kabla ya kuanza kulipa kodi. Huu ni muda mfupi mno kwa biashara kuanza kuonyesha
mwelekeo. Pamoja na mambo mengine Serikali ya CUF itauondoa utaratibu huu na badala yake
wafanya biashara wapya waliosajiliwa kama kampuni watawajibika kulipa kodi ya mapato katika
faida halisi watakayopata baada ya kipindi kimoja cha biashara (mwaka mmoja) kumalizika.
•  Misamaha ya kodi;
Hakutakuwa na misamaha ya kodi. Iwapo itatokea kuwa kwa sababu za kistratejia kuna umuhimu
wa kutoa msamaha wa kodi fulani, basi Serikali italiomba bunge kuidhinisha msamaha huo
baada ya kuhakiki kuwa msamaha huo wa kodi utaongeza tija katika uchumi wa nchi.
•     Kodi za mauzo na VAT; Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) itashushwa kutoka asilimia ishirini
(18%) ya sasa hadi asilimia kumi na tano (15%). Hata hivyo wigo wa wafanyabiashara
wanaostahili kujiorodhesha kwa ajili ya kodi hii utapanuliwa na kuwaingiza wafanyabiashara
wote ambao mauzo yao kwa mwaka hayapungui shilingi milioni 20; tofauti na utaratibu wa sasa
ambapo wafanyabiashara wenye haki ya kuorodheshwa kwa ajili ya VAT ni wale wenye mauzo
yasiyopungua shilingi milioni 40 kwa mwaka hata hivyo, Utaratibu wa ushuru wa stempu kwa
wale wafanyabiashara wasio na sifa ya kujiorodhesha kwa ajili ya VAT utatumika.
•  Ushuru wa barabara;
Mianya ya kukwepa ushuru wa barabara unaotozwa mafuta ya petroli na dizeli itaondolewa.
•  Matumizi ya kodi maalum;
Hivi sasa kuna kodi kadhaa ambazo hutozwa maalum kwa ajili ya kuimarisha eneo fulani na
huduma, mathalani ushuru wa barabara. Hata hivyo matumizi ya kodi hizi yamekuwa hayaeleweki
vema na mara nyingi kisingizio kinachotolewa ni kwamba zimechotwa kugharamia masuala
fulani nje ya yale yaliyokusudiwa. Serikali ya CUF itapitisha sheria inayozuia matumizi ya kodi
hizi nje ya makusudio ya awali, na iwapo kutakuwa na dharura yoyote inayohitaji sehemu ya
kodi hizi kutumika nje ya makusudio yake, itabidi kwanza Serikali iombe idhini ya bunge.
•  Kodi katika mafao ya wastaafu;
Serikali ya CUF itafuta kodi yoyote inayotozwa kwenye mafao ya wafanyakazi wanaostaafu au
kupunguzwa makazini kwa sababu yeyote ile. Ufutaji wa misamaha holela ya kodi, kurahisisha
ukusanyaji wa kodi na kukusanya kodi toka sekta ya madini kutaongeza ukusanyaji wa pato la
Taifa kama mapato ya Serikali toka asilimia 16 za hivi sasa mpaka kufikia asilimia 20.
•  Kodi za Serikali za Mitaa;
Kutenganisha vyanzo vya kodi
—     Ni muhimu sana vyanzo vya kodi za Serikali kuu na zile za Serikali za mitaa vikatenganishwa
39
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
ili kuondoa uwezekano wa kuwatoza wananchi kodi ya aina moja mara mbili. Serikali za
mitaa zitatakiwa kuangalia upya kodi zinazotoza na pale ambapo itabainika kodi fulani
inayotozwa tayari inatozwa na Serikali kuu japo kwa jina tofauti.
—     Kodi na ada za mazao; Ili kuongeza motisha kwa wakulima kodi na ada za mazao zitafutwa
kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
—     Marekebisho ya sheria yatafanyika ili kuziwezesha ngazi za kata kusimamia maendeleo
ya maeneo yao kwa kurejeshewa nusu ya mapato yanayotokana na kata husika katika
kupanga na kusimamia miradi ya maendeleo.
MTANDAO WA MAWASILIANO
Moja ya mambo yanayochangia kuongezeka haraka kwa maendeleo katika nchi ni mtandao mzuri
wa mawasiliano. Barabara, reli, usafiri wa majini pale unapohitajika, usafiri wa anga, simu,
fax, na hivi sasa Intaneti. Kuwapo kwa njia za uhakika za usafiri ndani ya nchi kunarahisisha
sana usafirishaji wa idadi kubwa ya watu na kiasi kikubwa cha bidhaa toka pande moja ya nchi
hadi nyingine. Hili mbali ya kuokoa muda, lina mchango mkubwa katika kushusha gharama za
kibiashara na hatimaye bei ya bidhaa. Hali kadhalika linasaidia sana kukuza maingiliano ya watu
kwenye jamii na hivyo kufanya watu wa upande mmoja kujifunza kutoka kwa watu wa upande
mwingine. Kwa kifupi mtandao mzuri wa mawasiliano unaongeza tija kwa kiwango cha juu iwe
ni kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
RELI NA BARABARA
MTAZAMO WA CUF JUU YA USAFIRI WA RELI NA BARABARA NCHINI
Tanzania ina tatizo kubwa la mawasiliano ya ardhini kwa maana ya usafiri na usafirishaji.
Sehemu kubwa ya mtandao wa barabara uko katika hali mbaya kabisa. Kielelezo cha ubovu
wa barabara zetu si kigeni kabisa kwa wakazi wa miji yetu. Barabara takriban zote alizoziacha
mkoloni zikiwa na lami hivi sasa ni vumbi na makorongo matupu. Pamoja na tuhuma za uongozi
mbaya unaosimamia Mamlaka za Reli zilizoko nchini, mtandao wa reli uliopo mbali ya kwamba
ni chakavu, pia hauko kimkakati. Tanzania ina njia kuu za reli tatu. Kuna reli ya kati inayoanzia
Dar-es-Salaam hadi Kigoma na ambayo ina tawi linaloanzia Tabora hadi Mwanza. Kuna reli ya
Tanga inayoanzia Tanga hadi Moshi na Arusha na pia kuwa na matawi, moja linaloanzia Korogwe
hadi Dar-es-Salaam, na jingine linaloanzia Kahe (mkoani Kilimanjaro) hadi Taveta mpakani
mwa Kenya na Tanzania. Reli ya tatu ni ile ya TAZARA inayoanzia Dar-es Salaam hadi Tunduma
mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Reli za Tanga na ile ya kati zilijengwa na wakoloni wa Kijerumani kati ya mwaka 1896 na
1905. Baadaye wakoloni wa Kiingereza waliongeza matawi katika reli hizo yanayounganisha miji
tuliyoitaja. Wajerumani walipozijenga reli hizi kusudio lao kubwa lilikuwa kurahisisha usafirishaji
wa mazao (hasa katani, kahawa na pamba) kufika kwenye bandari za Tanga na Dar-es-Salaam.
Wakoloni wa kiingereza hali kadhalika nao walizitumia reli hizi kikamilifu kwa malengo hayohayo.
Kudidimia kwa kilimo cha mazao ya biashara baada ya uhuru na kuwepo kwa barabara nzuri
inayoiunganisha mikao ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Dar-es-Salaam kumepunguza kwa kiasi
kikubwa umashuhuri wa reli ya Tanga. Ili kuurejesha umaarufu wake inabidi juhudi zifanyike
kuongeza wingi wa mizigo inayohitaji kufikishwa bandarini Tanga. Ni dhahiri kabisa kuwa
kuhuishwa kwa shughuli za kilimo cha kibiashara katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, na Tanga
40
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
yenyewe kutatoa mchango mkubwa katika kufanikisha hili. Lakini huenda mchango mkubwa zaidi
ukatokana na kufanikisha juhudi za kuhakikisha kuwa bidhaa za Uganda, na pengine Rwanda
zinasafirishwa kupitia reli hii kwenda na kutokea bandarini Tanga. Ili suala hili lifanikiwe hata
hivyo itabidi kwanza lijengwe tawi la reli litakaloiunganisha miji ya Arusha na Mwanza. Umuhimu
wa reli ya kati hadi leo umekuwa ni wa kipekee kabisa ikizingatiwa kuwa kuanzia Dodoma hadi
Kigoma na Mwanza(tofauti na maeneo yanayounganishwa na reli za Tanga na TAZARA ambayo
vile vile yana barabara kuu za uhakika), huu ndio usafiri pekee wa uhakika unaotegemewa na
sehemu kubwa ya wananchi wa maeneo hayo ya kanda ya ziwa kwa hivi sasa.
Reli ya TAZARA ilijengwa kwa msaada kutoka China kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia
kati ya mwaka 1970 na 1975. Reli hii ilijengwa kwa kuzingatia zaidi hali ya kisiasa iliyokuwepo
kusini mwa Afrika katika miaka ya sabini, kuliko mahitaji ya kiuchumi ya Watanzania. Ujenzi
wa reli hii ulizingatia zaidi kuisaidia Zambia kufikisha bidhaa zake (na hasa hasa madini ya
shaba) katika bandari ya Dar es Salaam baada ya njia za kusini, kupitia Zimbabwe hadi Beira
nchini Msumbiji, au Zimbabwe hadi Afrika Kusini kuwa hazipitiki kutokana na vita vya ukombozi
vilivyokuwa vimeshamiri katika eneo hilo lote. Hata hivyo ilikuwa ni muhimu kwa wajenzi wa
reli hii kuzingatia ukweli kuwa kuna siku vita vya ukombozi vingemalizika, na Zambia ianze
kuvutika tena kutumia njia za kusini kwa usafirishaji wa bidhaa zake. Bila shaka wangelizingatia
hili wangehakikisha kuwa reli inajengwa kufuata maeneo yote yenye wingi wa watu (tofauti
na ilivyo sasa) ili ikitokea kuwa usafirishaji wa bidhaa za Zambia unadorora, reli hii iendelee
kuwa ni huduma muhimu kibiashara na kimawasiliano kati ya maeneo hayo. Hivi sasa reli hii
inakabiliwa na tishio la Zambia kukimbilia nchi za kusini mwa Afrika kwa usafirishaji wa bidhaa
zake. Migogoro ya mara kwa mara ya kiuendeshaji inayolikumba shirika la TAZARA ni kioo cha
hali hii. Ni wazi kabisa kuwa zinahitajika juhudi za makusudi kabisa kuiokoa reli hii kabla
haijafikwa na kile kilichovifika viwanda vyetu. Ujenzi wa matawi kati ya Tunduma na Rukwa,
Mbeya na mpaka wa Malawi kuunganisha na Songea, Tunduru hadi bandarini Mtwara kutatoa
uhai mkubwa sana siyo kwa TAZARA tu, bali pia kwa bandari ya Mtwara na shughuli za kiuchumi
kwa ujumla kwa eneo lote la kusini.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya mawasiliano ya Reli na Barabara;
•     Rushwa, ubadhirifu na kutojali ndani ya Serikali vimetoa mchango mkubwa katika
kusababisha hali mbaya katika sekta ya mawasiliano ya ardhini ambayo tunaishuhudia
hivi sasa. Makusanyo ya mapato ya mfuko wa barabara yamefikia shilingi bilioni 284.1 kwa
mwaka. Hata kama kila kilomita 1 ya barabara ya lami inagharimu shilingi 600 milioni, fedha
hizi zingetosha kutengeneza kilomita 470 za lami kila mwaka. Kama kwa miaka 10 iliyopita
fedha hizi zingetumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa, nchi yetu ingekuwa na barabara nzuri.
Isitoshe, fedha inayokusanywa ni nusu tu ya mapato ya mfukowa barabara yanayostahiki
kukusanywa.
•     Bado Serikali imeshindwa kuona kuwa matumizi ya vivuko katika maeneo ambayo hayana
madaraja katika barabara kuu na barabara zinazounganisha mikoa, kwa malengo ya muda
mrefu yana gharama kubwa zaidi kuliko kujenga madaraja katika maeneo hayo.
•     Kufa kwa kilimo cha kibiashara katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, na Arusha; na kutokuwa
na nia thabiti ya kupanua fursa za kibiashara na nchi ya Uganda kunakaribia kuididimiza
kabisa reli ya Tanga.
•     Uzembe wa kutoikarabati kikamilifu reli ya kati baada ya mvua za El-nino za 1998 umesababisha
reli kusimama kutoa huduma kwa kipindi kirefu mwaka 2010 baada ya mvua kubwa iliyopiga
41
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
katika wilaya ya Kilosa. Aidha ubinafsishaji usio makini wa uendeshaji wa Shirika la Reli
umeliongezea matatizo na kudidimiza ufanisi wa shirika hilo na kuathiri kwa kiasi kikubwa
juhudi za wananchi za kujikwamua kiuchumi. Malalamiko ya huduma mbovu katika mabehewa
ikiwa ni pamoja na kujaa wadudu kama kunguni, mende, panya, na uchafu wa kila aina.
•     Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita Serikali ya CCM imeingia katika mashindano na CUF
kuhusu kuweka mtandao wa barabara nchini, baada ya dhamira ya CUF juu ya suala hili kuwa
wazi. Wizara ya ujenzi imeanzisha miradi mingi ya barabara kama kielelezo cha jinsi Serikali
hiyo ilivyo livalia njuga suala hili, ukiwemo ujenzi wa barabara ya Kibiti-Lindi, na baadhi
ya vipande vya barabara inayotokea Dodoma hadi Mwanza. Hata hivyo kama ilivyo kawaida
ya jambo lolote ambalo halifanyiki kwa dhati kuna ushahidi kuwa barabara takriban zote
zinazojengwa chini ya miradi hii zina ubora ambao uko chini ya viwango vinavyotakiwa.
Katika baadhi ya miradi hii makandarasi wamekimbia baada ya kushindwa kuhimili vitendo
vya rushwa na ufisadi walivyohitajiwa kushiriki.
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
Serikali itakayoundwa na CUF – Chama Cha Wananchi itahakikisha mawasiliano ya barabara na yanatumia vivuko katika barabara kuu na mabarabara zinazounganisha mikoa, yatakuwa
  reli kuwa ni miongoni mwa mambo yanayopewa umuhimu wa kipekee kwa kutenga fedha za na madaraja ya uhakika na utumiaji wa vivuko kusitishwa. Kabla ya kufikia malengo haya
  kutosha kukarabati na kujenga barabara na reli mpya. uvushaji katika vivuko vyote utakuwa bila malipo.
                                                      •     Pamoja na kukarabati barabara zilizopo Serikali itajenga kilomita 500 za barabara kuu mpya
                                                       za lami kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano.
                                                      •     Sekta ya miundo mbinu na hasa ujenzi wa barabara imekuwa ikilalamikiwa juu ya uwepo wa
                                                       ubadhilifu na ufisadi kutokana na makandarasi kujiingiza au kulazimishwa kushiriki utoaji wa
                                                      rushwa na kuathiri ubora wa viwango vya barabara zinazojengwa. Serikali ya CUF itachukua
                                                     hatua maalumu za kuthibiti suala hili kwa kuzingatia na kuiboresha sheria ya manunuzi ya
                                                    umma na kuhakikisha kuwepo kwa utaratibu makini wa kuingia katika mikataba ya ujenzi.
                                                   •     Sanjari na kuthamini makandarasi wazalendo, suala la kuharakisha ujenzi wa miundo mbinu
                                                    ili kukuza uchumi wa taifa ni jambo linalohitaji kupewa msukumo wa kipekee. Serikali ya CUF
                                                   itahakikisha miradi mikubwa ya ujenzi inapewa makampuni yenye uwezo mkubwa kifedha,
                                                  kiutendaji (vifaa vya kutosha na vya kisasa), uzoefu, na utaalamu wa hali ya juu. Makampuni
                                                 haya yatapewa kazi hizo na kuweka utaratibu wa kuwashirikisha wazalendo (sub-contract)
                                                katika kutekeleza kazi za mradi husika. Lengo likiwa ni kuondokana na ucheleweshaji wa miradi
                                               ya barabara ambayo tumeshuhudia kutokana na mapungufu ya kiutendaji na kusababisha
                                              miradi kujengwa kwa mwendo wa konokono.
MKAKATI WA CUF KUBORESHA USAFIRI RELI; USAFIRI WA MAJINI
•     Serikali ya CUF itakaribisha wawekezaji wa kibiashara kwenye ujenzi wa matawi ya reli ambayo Ukiondoa hali ilivyo sasa kati ya Dar es Salaam na Zanzibar ambako wawekezaji kadhaa
  umuhimu wake tayari tumekwisha ueleza hapo juu. wanaendesha safari za maboti yaendayo kasi, hali katika maeneo mengine yanayohitaji usafiri
  •     Serikali ya CUF haitabinafsisha shirika la reli isipokuwa litapatiwa menejimenti makini na wa majini siyo ya kuridhisha. Usafiri wa baharini kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini, na
    bodi imara yenye uhuru wa maamuzi na kufanya kazi zake kitaalamu zaidi na kwa kuzingatia kati ya Dar es Salaam na kisiwa maarufu cha Mafia umedidimia kabisa. Usafiri katika maziwa
    maslahi ya Taifa. Menejimenti itapewa mkataba yenye viwango vinavyopimika (performance makuu unategemea meli chakavu za kizamani ambazo mbali ya kuhatarisha usalama wa abiria,
    management contract). kutokana na uchakavu unaozikabili zinashindwa kuwa na ratiba za uhakika. Kwa nyakati tofauti
    •     Pamoja na mambo mengine Menejiment itakuwa na wajibu wa kuhakikisha inaboresha tumeshuhudia maafa ya watu wengi yakitokea na bado hatujaweza kuitumia vizuri fursa hii ya
      huduma za usafiri wa reli kwa kuwa na vifaa vya kisasa vya utendaji kazi, mabehewa ya kuwa na bahari na maziwa makuu. Juhudi za watu mbalimbali kuwekeza katika usafiri wa majini
      abiria na mizigo yenye viwango na hadhi ya kimataifa kuweza kulinda usalama na afya za katika maeneo ambayo hivi sasa yana tatizo kubwa la usafiri huo zimekuwa zikikwama kutokana
      abiria na mizigo, kuwa na ratiba ya ukahakika ya usafiri na kuwajibika pale itakapozembea na sababu zisizokubalika zinazonasibishwa na ubinafsi na ufisadi.
      kutekeleza wajibu wake kwa wateja. Mathalani, abiria amepakia bidhaa kutoka Tabora kuleta
      Dar es Salaam, bidhaa inakadiriwa kusafirishwa kwa siku tatu na kubakia katika ubora wake,
      shirika la reli kwa namna yoyote ile kama bidhaa zitasafirishwa kwa siku nane na matokeo
      yake kuharibika, shirika litawajibika kulipa fidia juu ya uharibifu huo. Hali hii itasaidia sana
      kulifanya shirika kuwajibika kikamilifu katika kuyaendea majukumu yake.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
MKAKATI WA CUF KUBORESHA BARABARA NCHINI;
•     Serikali ya CUF itahakikisha kuwa ushuru wote wa barabara unaelekezwa kwenye ujenzi wa
barabara mpya na kurekebisha zile zilizoharibika, Asilimia 50 ya fedha za ushuru wa barabara
zitaelekezwa kwenye ujenzi wa barabara za vijijini. Aidha wawekezaji kwenye sekta ya barabara
(kwa ajili ya ujenzi wa barabara zitakazolipiwa ushuru, yaani Toll Roads) watatafutwa ili
pamoja na matumizi ya kodi ya Serikali na misaada tunayoweza kupata kutoka nchi mbalimbali
marafiki, kasi ya kuboresha usafiri wa barabara nchini kote iwe ya kuridhisha.
•     Katika kipindi cha miaka mitano Serikali itahakikisha kuwa maeneo yote ambayo hivi sasa
42
MKAKATI WA CUF KUBORESHA USAFIRI WA MAJINI
•     Serikali ya CUF itafanya juhudi kubwa kupata wawekezaji watakaowekeza katika maeneo yote
ambayo hivi sasa yanahitaji usafiri wa majini, na kwa sababu huduma hizi hazipo kabisa
katika maeneo mengi Serikali itaweka msamaha wa kodi wa miaka mitano mfululizo kwa
watakaokubali kutoa huduma ya usafirishaji katika sehemu zote ambazo zimekuwa hazina
usafiri wa majini kwa muda mrefu.
•     Serikali ya CUF itafanya kila linalowezekana bila kuathiri maslahi ya Taifa kuwasaidia
wawekezaji hao kufanikisha utoaji wa huduma hii muhimu.
•     Serikali ya CUF itasimamia mipango ya ujenzi wa ‘magati’ kwa maeneo mbalimbali ili kurahisha
huduma ya majini kuweza kuwanufaisha wanachi wengi zaidi.
USAFIRI WA ANGA
•     Usafiri wa anga siyo maarufu sana kwa Watanzania walio wengi, kwani wananchi wengi
43
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
wanahusisha gharama kubwa na usafiri huo. Pili, kuna mikoa michache tu ambayo ina
viwanja vya ndege vilivyochakaa vinavyoweza kuhudumia ndege kwa muda wote huku mikoa
mingine ikiwa haina viwanja vya ndege kabisa. Mtazamo wa Serikali juu ya aina hii ya usafiri
kuonekana kama anasa kwa wananchi wa kawaida na kuona kuwa ni haki ya wageni wa
kimataifa pekee. Ukosefu wa viwanja vya ndege katika maeneo mengi ya nchi vyenye uwezo
wa kuhudumia ndege muda wote kumesababisha wawekezaji wengi wasivutiwe kuwekeza
katika aina hii ya usafiri.
•     Viwanja vya ndege vidogo na vibovu vilivyoshamiri nchini vinawatia hofu abiria wengi na
kuwakatisha tamaa, kwa mfano pamoja na ukuaji na umaarufu wa mkoa wa Mwanza juhudi za
makusudi hazijachukuliwa kuboresha uwanja wa ndege.
MKAKATI WA CUF KUBORESHA USAFIRI WA ANGA;
•     Itakaribisha wawekezaji kuwekeze zaidi katika eneo hili, na hasa yale makampuni ya nje
ambayo yana uzoefu mkubwa katika
kutoa huduma za haraka kati ya mji
na mji (Shuttle service). Kwa kawaida
makampuni haya yanatoa huduma ya
usafiri wa anga kwa gharama nafuu sana
kiasi kwamba huduma zao zinavuta watu
wa aina zote wakiwemo na wananchi
wenye kipato cha chini.
•     Itahakikisha kuwa walau kila mkoa
nchini una kiwanja kimoja cha ndege
kinachoweza kuhudumia ndege muda
wote bila kujali majira ya mwaka na pia
kila kanda inakuwa na kiwanja cha ndege
kikubwa kimoja kinachoweza kuhudumia
ndege zenye ukubwa unaohitaji viwanja vikubwa, viwanja hivi vya kikanda vitasaidia pia
kuleta mashirika ya ndege ya kimataifa ambayo yatafanya biashara ya kubeba mizigo na
abiria kutoka kwa mfano; kanda ya ziwa kwenda nchi za nje n.k.
•     Itachambua kwa makini gharama za usafirishaji wa anga na hasa bei za mafuta ya ndege
kwa nia ya kuangalia jinsi ya kuzifanyia marekebisho yenye lengo la kushusha gharama za
uendeshaji na kwa abiria.
HUDUMA ZA SIMU, NUKUSHI (FAX), POSTA, NA MTANDAO (INTERNET)
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEKNOHAMA ni muundo mbinu muhimu katika mkakati wa
kukuza uchumi katika karne ya 21. Teknolojia hii imepunguza sana gharama za mawasiliano na
inaongeza tija katika uzalishaji na utoaji huduma katika sekta zote. Matumizi ya mtandao wa
kompyuta kupitia Internet yameleta mapinduzi katika sekta ya elimu, huduma za afya na burudani
za aina mbalimbali. Teknolojia ya simu za mkononi imeongeza utumiaji wa huduma za simu.
Hadi mwisho wa mwaka 2009, kampuni za simu za mikononi zilikuwa na wateja milioni 17.5
ukilinganisha na wateja 173,922 wa simu za mezani. Tatizo jingine kwenye eneo hili ni bei kubwa
mno zinazotozwa na makampuni ya simu kwa wateja. Pamoja na gharama za mawasiliano kuwa
juu, bado Watanzania walio wengi wanatumia muda mwingi kutafuta taarifa na kuingia gharama
kubwa zaidi za usafiri kwa sababu tu ya kukosa mawasiliano ya simu katika maeneo wanamoishi.
44
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
Hali ilivyo sasa katika sekta ya Mawasiliano ya Simu, Fax, Posta na Intaneti;
•     Mtazamo wa kuona kuwa huduma hizi ni anasa tu na mfumo wa siasa za Ujamaa zilizotufunga
katika kichumba kisicho madirisha ya kuona mambo ya maana na maendeleo yanayofanyika
katika maeneo mengine ya dunia ni jambo lililotuchelewesha sana watanazania kufika hapa
tulipo.
•     Uendeshwaji wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL) kisiasa zaidi kuliko kitaalamu pamoja
na kwamba kampuni hii ilikuwa ni moja ya makampuni machache sana ya umma nchini
yaliyokuwa yanajiendesha kwa faida na wakati inabinafsishwa ilikuwa na akiba ya mabilioni
benki, kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi viongozi wa Serikali ya CCM walilazimisha
kampuni hiyo ibinafsishwe.
•     Gharama za mawasiliano ya simu nchini, bila kujali kuwa ni simu za kawaida au za mkononi
ziko juu kupita kiasi. Kwa wastani bei zinazotozwa na makampuni ya simu yaliyoko nchini
ni mara tisa zaidi ya bei zinazotozwa na makampuni yanayotoa huduma hizo katika maeneo
mengine duniani, na hasa yale yaliyoko katika nje ya bara la Afrika. Inatia shaka mno kuona
kuwa baadhi ya viongozi wa umma ambao ndio wanashiriki vikao vya kupanga viwango
vya malipo ya gharma za simu nchini wakati huohuo ni wajumbe wa bodi katika baadhi ya
makampuni hayo ya simu nchini.
•     Eneo la matangazo (promotion and advertisement) kwa makampuni ya simu limechukua
sehemu kubwa mno na kuleta mkanganyiko kwa wateja na jamii kwa ujumla.
•     Serikali ya CCM imeshindwa kuelewa kuwa uchumi wa kisasa unatumia kompyuta na mtandao
(internet), na kuwa ili wananchi waweze kushiriki kikamilifu katika uchumi wa aina hii ni
lazima kuwe na juhudi za makusudi kabisa kuwafikishia huduma hii muhimu na kufanya
maandalizi ya kimfumo katika sekta ya elimu ili wanafunzi na walimu waweze kuingia moja
kwa moja katika matumizi ya teknolojia hii. Aidha kutokana na ujuzi mdogo, Watanzania
walio wengi hawajaweza kutumia teknolojia hii ya mawasiliano (hata simu za mkononi) kwa
kuwango cha juu kabisa yaani zaidi ya kutuma ujumbe mfupi kupiga na kupokea basi. Mbali
na simu kusheheni vifurushi-programu mbalimbali zinazoweza kusaidia kuratibu shughuli za
kila siku za mtumiaji wa simu.
Mpango wa CUF Katika Kuboresha Matumizi ya Huduma za Simu, Fax, Posta, na Intaneti;
•     Serikali ya CUF pamoja na mambo mengine itachukua hatua makhsusi kuhakikisha kuwa
huduma za simu, fax, na mtandao wa internet zinasambaa kwa haraka na kuyafikia maeneo
mengi nchini kote mijini na vijijini.
•  Gharama za mawasiliano;
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa gharama za mawasiliano zinashuka ili kuwiana na gharama
hizo kama ilivyo kwa mataifa mengine.
•  Kuwakaribisha wawekezaji zaidi;
Serikali itakaribisha makampuni zaidi ya ndani na nje kuwekeza kwenye sekta hii na yale
yatakayowekeza vijijini yatapewa motisha maalum.
•  Matumizi ya kodi;
Kwa muda wa miaka kumi ijayo, kodi yote ya mauzo inayotozwa na Serikali kwa watumiaji wa
simu, fax, na internet itarejeshwa tena kuwekezwa kwenye upanuzi wa huduma za mawasiliano
haya vijijini.
45
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
•  Kujifunza kwa wenzetu;
Pamoja na jitihada nyingine, Serikali pia itachukua hatua za kujifunza na kuiga kutokana na
uzoefu walioupata wenzetu wa nchi mbali mbali, hususan Bangladesh na kampuni yao ya
GrameenPhone, juu ya usambazaji wa huduma ya simu kwa malengo ya kupiga vita umasikini
vijijini.
•  Huduma ya mtandao(Internet);
Katika kipindi cha miaka 5 Serikali ya CUF itasambaza mkonga wa broadband ufike katika kila
Makao makuu ya mkoa na hatimaye katika kila makao makuu ya wilaya, kupunguza gharama
mkonga huu pia utatumiwa na TANESCO katika usambazaji wa umeme.
•     Pia Serikali itafanya mazungumzo na makampuni yanayosambaza huduma za internet nchini
ili makampuni hayo yasambaze huduma hizo hadi kwenye shule za msingi na sekondari na
vyuo kwa gharama nafuu. Gharama hizi zitakuwa zinafidiwa na Serikali kama punguzo la kodi
yake kwa serikali.
HUDUMA ZA UZALISHAJI MALI
NISHATI
Hatuwezi kuzungumzia uchumi wa kisasa iwapo hakuna nia ya kushughulikia suala la nishati na
maji. Hii ni kutokana na ukweli kwamba uchumi wowote wa kisasa unaoanishwa na matumizi ya
hali ya juu ya mashine – iwe ni mitambo ya viwandani, matrekta ya mashambani au vyombo vya
usafirishaji nakadharika, hutegemea nishati na maji kujiendesha. Hivyo basi ili uweze kupata
ufanisi wa juu kutoka kwenye mashine ni sharti kwanza kuwepo na uwekezaji wa kiasi cha
kutosha kwenye sekta za nishati na maji ili kuhakikisha kuwa siyo tu kuwa vitu hivi vinapatikana,
bali pia vinapatikana kwa bei ya kuridhisha. Hata hivyo Tanzania ni nchi ambayo imeonyesha
udhaifu mkubwa sana katika sekta za nishati na maji.
UMEME
Umeme ambao ndiyo nishati kuu kwa matumizi ya mitambo viwandani na ambayo pia inapaswa
kuwepo majumbani ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa lengo la kulinda mazingira,
unazalishwa kwa kiwango kidogo, kwa ufanisi mdogo na bei yake ni kubwa sana. Uzalishaji
umeme nchini Tanzania kwa asilimia 90 unategemea maji ya mvua. Hili lisingekuwa ni tatizo
sana kama hifadhi ya maji haya kwenye mabwawa ya kuzalishia umeme ingekuwa ni ya uhakika.
Kwa bahati mbaya sana uhakika huo haupo. Zaidi ya maji, TANESCO pia huzalisha umeme kwa
kutumia mafuta ya dizeli na hivi karibuni gesi ya Songosongo. Mitambo inayotumia dizeli ya
kampuni ya IPTL ambayo ilijengwa mwanzoni mwa miaka ya tisini kwa ajili ya kuzalisha umeme
wa kuiuzia TANESCO siyo tu kwamba haijasaidia kuondoa tatizo la umeme, lakini pia imekuwa ni
mzigo mkubwa kwa watumiaji huku Serikali ikipoteza mabilioni ya shilingi kutokana na ufisadi
mkubwa uliombatana na kampuni ya IPTL, RICHMOND na zinginezo. Ilitarajiwa kuwa tatizo la
umeme lingepungua sana baada ya TANESCO kuanza kutumia gesi ya songosongo. Hata hivyo
pamoja na kuanza kuitumia gesi hiyo matatizo ya umeme kwa wateja yamebaki palepale, kama
siyo kuongezeka. Pamoja na Serikali ya CCM kuifukuza menejimenti ya TANESCO na kuiajiri
kampuni ya NET GROUP SOLUTIONS katika mazingira yaliyojaa utata wakati ule, ili kuliendesha
shirika hilo. Net Group Solution wameiacha TANESCO katika hali mbaya zaidi kuliko walivyoikuta,
na kuwa ‘NET GROUP PROBLEM’
46
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
Hali ilivyo sasa katika sekta ya Umeme nchini;
Bila ya shaka makucha ya UFISADI ambayo yamejikita kila mahala chini ya Serikali ya CCM, hadi
kuteketeza takriban kila nyanja ya maisha ya Mtanzania yanaiparua na TANESCO pia:
•     Mitambo chakavu ya TANESCO inayosababisha umeme ukatike ovyo ni kielelezo tosha kuwa
siyo tu kuwa fedha za mfuko wa nishati zilikuwa zikitafunwa kwa miaka mingi bila kufanyia
kazi iliyokusudiwa, lakini pia kuwa kuna ubadhirifu mkubwa katika shirika hilo.
•     Uchambuzi unaonyesha kuwa pamoja na TANESCO kuwa na matatizo mengi tangu wakati
ikiwa chini ya menejimenti ya umma, matatizo hayo yameongezeka kwa kiasi kikubwa baada
ya menejimenti hiyo kufukuzwa na nafasi yake ikachukuliwa na menejimenti ya kigeni na
baadaye kurudisha menejimenti ya wataalam wa ndani ambayo nayo hadi leo haina jipya
zaidi ya kuongeza gharama za umeme kila kukicha.
•     TANESCO imekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuwa baadhi ya wateja wake wamekuwa
wakiliingizia shirika hilo hasara kwa kuwa na malimbikizo ya bili ya muda mrefu. Kwa upande
mwingine wateja nao wamekuwa wakilalamika kuwa bili wanazoletewa na TANESCO ni kubwa
mno na kuwa haziakisi matumizi halisi ya umeme. Suala hili bado halijapatiwa uchunguzi na
ufumbuzi sahihi na kulitolea kauli. Malalamiko ya TANESCO kwa upande mmoja, na malalamiko
ya wateja kwa upande mwingine yangeweza yakapatiwa suluhisho kupitia matumizi ya mita
za LUKU.
•     Gharama za kuunganisha umeme zimeendelea kuwa ghali, wananchi wengi hata walioko
maeneo ambayo nguzo zimebahatika kupita karibu wanaishia kuzitizama tu nguzo hizo kwani
hawawezi kumudu gharama kubwa za kuunganisha umeme na hata wale waliounganisha hivi
sasa wanashindwa kumudu malipo makubwa ya umeme yanayotozwa na TANESCO kwa mwezi.
•     Tatizo la kukatikakatika kwa umeme limekuwa halina tiba tena, wananchi wengi wamekwishapata
hasara kubwa baada ya umeme unaokatika kurudi kwa nguvu na kuunguza samani zao muhimu
huku hakuna wa kuwafidia hasara hizo zinazorudisha nyuma maendeleo yao.
•     Viwanda vingi na sehemu za uzalishaji hazifanyi kazi kutokana na ukatikaji wa umeme wa kila
wakati unaosababishwa na miundombinu mibovu ya TANESCO, wamiliki wa viwanda wamekuwa
wakipata hasara kubwa sana ya kuwasha majenereta yanayotumia dizeli ili kuendesha mitambo
yao hali hii inakatisha tamaa na kuua uchumi wa nchi.
Dira ya Mabadiliko ya CUF
•  Kuteua Menejimenti mpya;
Serikali italiimarisha shirika la TANESCO kwa kuteua menejimenti ya wataalam wenye uzoefu
katika shughuli za umeme na kuwapa mkataba wenye malengo yanayopimika (management
performance contract) sanjari na uboreshaji wa Menejimenti, Serikali ya CUF kwa kuzingatia
uzoefu na mafanikio yaliyopatikanwa kwa nchi zingine itaunda utaratibu wa kuwa na mgawanyo
wa makampuni yatakayosimamia Nishati ya Umeme kwa kuwa na mgawanyiko ufuatao; kuwepo
kwa kampuni inayoshughulikia uzalishaji pekee (electricity power generation). Kampuni
nyingine kushughulikia usambazaji (electricity power transmission). Na kampuni nyingine
kushughulikia na Masoko na Mauzo ya Nishati ya umeme (electricity power distribution) ili
kuleta tija na ufanisi zaidi.
•  Uanzishaji wa vyanzo vipya vya umeme;
Pamoja na Serikali ya CUF kuendelea na mpango wa kutumia gesi ya SongoSongo kufua
47
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
nishati ya umeme, Serikali pia itatafuta wawekezaji watakaowekeza kwenye ujenzi wa vinu
vya kuzalisha umeme kutokana na vyanzo vingine, hususan kwa kutumia malighafi ya makaa
ya mawe kutoka katika mgodi wa Kiwira na migodi mingine. Tathmini ya kina itafanywa
kuzingatia gharama na athari ya ajali mbaya na uchafuzi wa mazingira kabla ya kuamua
kutumia madini ya uranium kuzalisha umeme. Hili ni muhimu ili kutuhakikishia kuendelea
kupata umeme wa kutosha hata kama kutakuwa na tishio la ukame litakaloathiri uzalishaji
wa umeme wa maji.
•  Nishati ya jua na upepo;
Serikali itafuta ushuru wote kwenye vifaa vinavyotumika kuzalisha umeme kutokana na
nishati ya jua na upepo ili kuharakisha usambazaji wa umeme katika maeneo ya vijijini. Hali
ilivyo kwa sasa ni kwamba vifaa vya kuzalisha umeme kwa kutumia jua na upepo vimekuwa
ghali na Watanzania hawana pa kukimbilia ili kuwa na nishati bora ya umeme.
BIDHAA ZA PETROL
Baada ya mchakato wa ubinafsishaji wa biashara ya mafuta ya petroli, makampuni mengi binafsi
yamejitokeza kushiriki katika kufanya biashara ya bidhaa za petroli. Katika hali ya kawaida
ingetarajiwa kuwa ushindani baina ya makampuni haya ungepelekea kushuka kwa bei za bidhaa
za petroli na hivyo kuwa wa manufaa kwa wateja. Hali kadhalika ingetarajiwa kuwa Serikali
ingenufaika zaidi kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya walipa kodi katika sekta hiyo. Hata hivyo, hali
halisi ni tofauti kabisa kwani badala ya manufaa yaliyotarajiwa sekta hiyo imevurugika. Siyo tu
kwamba bei ya bidhaa za petroli imeongezeka kwa kiasi kikubwa bali inabadilika mara kwa mara.
Uzoefu unaonyesha kuwa kila uchaguzi mkuu unapokaribia makusanyo ya kodi inayotozwa kwenye
bidhaa za petroli yamekuwa yakishuka, ikiashiria kuwa kiasi kikubwa cha bidhaa hizi wakati huo
huingizwa nchini kwa magendo. Mwaka 1999, yaani mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2000, makusanyo ya kodi kwenye bidhaa za petroli yalishuka kwa asilimia 25. Wakati
tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010 mapato ya kodi inayotokana na bidhaa za
petroli tayari yamekuwa yakishuka ilhali matumizi ya bidhaa hizo yameendelea kupanda.
Moja ya sababu zinazochangia sana magendo na ukwepaji kodi katika biashara ya mafuta
nchini ni bei kubwa ya bidhaa za petroli. Sababu nyingine ni usimamizi dhaifu kwa mafuta
yanayoorodheshwa kuwa ni ya kusafirishwa kwenda nchi jirani. Kwa kutumia ujanja ujanja na
rushwa sehemu ya mafuta haya imekuwa ikiuzwa nchini bila kulipiwa kodi. Pamoja na kwamba
bei kwenye masoko ya dunia iliongezeka sana kabla ya mtikisiko wa uchumi wa dunia, bei ya
mafuta ilishuka sana wakati wa mtikisiko wa uchumi lakini bei za mafuta Tanzania hazikushuka
kwa uwiano wa kushuka kwa bei ya soko la dunia. Katika siku za hivi karibuni bei za mafuta
zimepanda kiasi, lakini ukweli wa mambo ni kwamba bei hizo hadi mafuta yanafika kwenye
bandari zetu na kuanza kupokelewa na waagizaji bado ziko chini sana ukilinganisha na bei za
kuuzia zinazotangazwa na makampuni ya mafuta.
   
Hali ilivyo kwa sasa;
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
•  TATIZO LA UCHAKACHUAJI WA MAFUTA;
Tatizo la baadhi ya wafanyabiashara kuchakachua mafuta ya taa na dizeli na bidhaa nyingine
limekuwa sugu na kukosa ufumbuzi sahihi kiasi ambacho mpaka magari ya Mhe Rais akiwa
ziarani mkoani Kilimanjaro yalifanyiwa uchakachuaji.
•  Kushindwa kukuza uchumi na kushuka kwa thamani ya shilingi;
Kushindwa kuendesha uchumi wa nchi vizuri na kuendelea kuporomoka kwa thamani ya
shilingi kila kukicha, kumetokana na mchango mkubwa wa kupandisha mara kwa mara bei ya
mafuta yanayonunuliwa na Tanzania kwenye masoko ya Dunia. Kati ya mwaka 1995 na mwaka
2010 shilingi ya Tanzania imepoteza thamani yake dhidi ya dola ya kimarekani ambayo bei
yake imepanda toka shilingi 575 mwaka 1995 mpaka kufikia shilingi 1500 kwa dola moja
mwaka 2010.
•     Ubinafsishaji holela wa sekta ya bidhaa za petroli umerutubisha rushwa katika sekta hiyo na
kuchochea kuongezeka kwa magendo ya bidhaa hizo kwa kiwango cha kutisha.
•     Serikali haikuwa makini wakati wa kusajili kampuni mpya za mafuta na kuzipa leseni za
kufanya biashara hiyo. Nyingi ya kampuni hizi hazina sifa zinazostahili kwa kampuni ya
mafuta kuwa nazo kwa sababu;
—     Nyingi ya kampuni hizi mpya hazina maghala ya hifadhi. Katika biashara ya mafuta
kampuni ambayo haina maghala ya kuhifadhia mafuta inayoyapokea kabla ya kuyasambaza
inakuwa ni vigumu kwa serikali kufuatilia kodi zake. Sababu ni kwamba kisheria maghala
haya yanakuwa chini ya uangalizi wa kudumu wa serikali na muda wote wanakuwepo
maafisa wa ushuru wa forodha kukagua mali inayoingia na kutoka. Haijulikani ni vipi
serikali ilitarajia kukusanya kodi zake kwa baadhi ya kampuni hizi mpya, ilihali ilijua fika
kwamba hazikuwa na maghala ya hifadhi.
—     Ukwepaji mkubwa wa kodi unaofanywa na baadhi ya kampuni hizi mpya umesababisha
mauzo ya makampuni makubwa yaliyokuwepo tangu zamani kushuka na hivyo basi
kupungua kwa kiasi cha kodi ambacho serikali imekuwa ikikusanya. Hata hivyo kuna
taarifa kuwa kuna baadhi ya vigogo serikalini wanahisa kwenye baadhi ya kampuni hizi
mpya na huenda hicho ndicho kilichokuwa kichocheo cha kukiuka taratibu.
—     Nyingi ya hizi kampuni mpya zinafanya shughuli zake katika mazingira ya hatari. Biashara
ya mafuta inahitaji uangalifu wa hali ya juu. Ni biashara ambayo inaweza kuzua janga kubwa
na kuleta madhara makubwa kwa maisha ya watu na mali zao. Kwa kawaida makampuni ya
mafuta yanatumia fedha nyingi kutoa mafunzo kwa wafanya kazi na makandarasi wao juu
ya kuchunga usalama. Aidha hutumia fedha nyingi kuweka miundombinu ya kinga dhidi
ya majanga ya moto. Kwa kuwa nyingi ya kampuni hizi mpya huingiza mafuta kwa njia ya
barabara kutokea nchi jirani, na hazina sehemu maalum za hifadhi, ni jambo la kawaida
kukuta magari yaliyobeba shehena ya mafuta yakiwa yameegeshwa sehemu mbalimbali
katikati ya makazi ya watu. Hali kadhalika, hata makampuni yaliyoweka vituo vya kuuzia
mafuta vya rejareja, vituo hivi mara nyingi vinakuwa havikujengwa kukidhi viwango vya
usalama vinavyotakiwa.
•  Viwango vya kodi; MKAKATI WA CUF KUBORESHA SEKTA YA BIDHAA ZA PETROL
Viwango vikubwa vya kodi vinavyotozwa kwenye bidhaa hizo za petrol imekuwa ni mzigo kwa Serikali ya CUF pamoja na mambo mengine itachukua hatua zifuatazo ili kuleta marekebisho
Watanzania na kusababisha ongezeko la gharama zinazozalishwa viwandani na gharama za yanayotakiwa katika sekta hii muhimu:
usafiri na usafirishaji wa bidhaa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
48
49
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
Makampuni yatakayofanya biashara ya mafuta nchini;
Serikali itaangalia upya usajili wa makampuni ya mafuta na yatakayoruhusiwa ni yale tu
yatakayotimiza masharti ya kuwa na maghala ya hifadhi yaliyojengwa kwa kuzingatia viwango
vya usalama vinavyokubalika. Na pili kuhakikisha kuwa mafuta yote yanayoingizwa nchini kwa
ajili ya biashara yatakuja kwa njia ya baharini, ila tu katika nyakati za dharura.
Mafuta yanayosafirishwa nje ya nchi kupitia Tanzania;
—     Serikali ya CUF itafanya mazungumzo na majirani zetu wanaopitishia mafuta yao nchini
kwetu ili kwa pamoja tukubaliane juu ya suala la kutia rangi mbalimbali kwenye mafuta
na mgawanyo wa rangi hizo kwa kila nchi. Mathalani, Tanzania pink na njano, Uganda
kijani na bluu, Rwanda, zambarau na hudhurungi nakadharika. Kwa utaratibu huu mafuta
yoyote yaliyoorodheshwa kuwa yanasafirishwa nje kisha yakauzwa nchini kwa magendo
bila kulipiwa kodi yatagundulika kwa urahisi na wahusika kudhibitiwa. Utaratibu wa sasa
wa kutumia BIOMARKER unakwepeka kirahisi kwa kuwa unahitaji utafiti wa kimaabara
kutambua mafuta ya magendo.
—    Pamoja na utaratibu wa kutia rangi Serikali pia itaweka sheria inayowalazimisha
wasafirishaji wote wa mafuta ya nchi jirani kutia sahihi dhamana inayolingana na kodi
yote ambayo Serikali ingelipwa iwapo mafuta haya yangeuzwa nchini. Dhamana hiyo
itafutika mara moja baada ya Serikali kuthibitisha kwamba mafuta hayo tayari yamevuka
mpaka na kuingia kwenye nchi yalikokusudiwa.
•  Suala la bei ya mafuta;
Serikali ya CUF itazipitia upya kodi zinatozwa kwenye bidhaa za petroli na kuzirekebisha ili
kushusha bei ya nishati hii muhimu. Marekebisho haya yatalenga kuzifanya bei za bidhaa
za petroli zinazouzwa nchini ziwe katika uwiano mzuri na bei ya bidhaa hizo katika nchi za
jirani; ili pamoja na kuwaletea wananchi unafuu na kupunguza gharama za uzalishaji katika
sekta mbalimbali zinazotegemea nishati ya mafuta, tuweze pia kuwa na silaha nyingine ya
kupigia vita ukwepaji kodi na biashara ya magendo katika mipaka yetu.
•     Itahakikisha kunakuwa na udhibiti wa juu wa mafuta ili kuwabana wafanyabiashara wote
wanaoingiza mafuta yaliyo chini ya viwango au yaliyochakachuliwa.
MAJI NA MAZINGIRA
Hali ya maji nchini kwa ajili ya matumizi ya viwandani na majumbani ni mbaya sana. Hali hii ni
ya kushangaza sana ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo Mwenyezi Mungu
amezijaalia sana wingi wa maji, kwani zaidi ya asilimia 6 ya eneo lote la nchi yetu ni maji.
Tukumbuke kuwa sehemu kubwa ya maziwa makuu matatu yaliyoko katika bara la Afrika yaani
Victoria, Tanganyika, na Nyasa, iko Tanzania, pia kuwa zaidi ya maziwa haya matatu, nchi yetu pia
imejaaliwa maziwa mengine madogo madogo na mito mikubwa na midogo kwa mamia. Tanzania
iko katika ukanda wa dunia ambapo mvua ni nyingi na kwa kiasi kikubwa ni za uhakika.
Tanzania ina bahati ya kuwa na maji ya kutosha kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya
uchumi na jamii. Raslimali ya maji tuliyonayo haijatumiwa vizuri ipasavyo kukuza uchumi na
kustawisha hali za maisha ya Watanzania kwa ujumla wake. Tanzania ina mabonde tisa ya
maji (water basins). Mabonde ya ziwa Victoria, ziwa Tanganyika, ziwa Nyasa, ziwa Rukwa, mto
Ruvuma, mto Rufiji, mto Pangani, mito ya Ruvu na Wami, na bonde la ndani (internal drainage
basin) la mikoa ya Arusha, Dodoma, Manyara, Singida na Shinyanga. Mwaka 2006, Tanzania
50
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
ilipata maji ya mvua ya wastani wa mita za ujazo 2467 kwa kila mtu. Kwa sababu la ongezeko la
watu, wastani wa maji ya mvua yanayoweza kutumiwa na kila mwananchi utapungua na kufikia
mita za ujazo 1500 mwaka 2025. Nchi inahesabiwa kuwa na upungufu wa maji ikiwa inapata
maji ya mvua chini ya mita za ujazo 1000. Hivi sasa Tanzania inatumia chini ya asilimia 1 ya
maji ya mvua. Hatuna utaratibu mzuri na endelevu wa kuvuna na kuhifadhi maji. Nchi nzima ina
mabwawa ya kuhifadhi maji 22 mengi yake ni madogo madogo isipokuwa mabwawa yanayohifadhi
maji ya kufua umeme kama vile mtera na nyumba ya Mungu. Ofisi tisa zinazosimamia mabonde
ya maji (Basin Water Offices) hazina uwezo wa kuratibu na kupanga matumizi ya maji katika
mabonde yao. Ofisi hizi hazina wataalam wa kutosha kupata taarifa ya haidrolojia ya mabonde
yao, matumizi halisi ya maji na kuwa na mipango ya maendeleo ya kuvuna na kuhifadhi maji.
Kwa muda mrefu nchi imekosa uratibu endelevu wa kulinda vianzio vya maji katika mabonde
yote na badala yake Serikali hukurupuka wakati maji yakipungua katika mabwawa ya kufua
umeme kuhamisha wafugaji na wakulima wanaofanya shughuli zao katika vianzio vya maji.
Hata hivyo pamoja na utajiri huu wa maji, tumekuwa na udhaifu mkubwa katika kuyaandaa
maji hayo yawe tayari kwa matumizi. Huduma za usambazaji ni mbaya mno kiasi kwamba
moja ya kero kubwa sana zinazowakabili wananchi wengi, bila kujali kuwa ni wa mjini au
vijijini, ni uhaba wa maji. Haishangazi basi kuwa uchimbaji wa visima – hata katikati ya miji –
miaka hii imekuwa ni biashara kubwa. Viwanda, makampuni, na watu binafsi - wote wanaponea
kwenye maji ya chumvichumvi ya visima. Lakini tujiulize, ni mwekezaji gani wa hadhi atawekeza
kiwanda muhimu nchini mwetu kwa kutegemea maji ya kisima? Hakuna shaka yoyote kuwa
baada ya miaka 49 ya kujitawala suala la maji linatakiwa lianze kupewa umuhimu unaostahili
kama kweli tuna nia ya kuboresha maisha ya Watanzania na kuwavutia wawekezaji wa uhakika.
Hali ya huduma ya maji ilivyo sasa;
•     Hazijafanyika juhudi za makusudi na za uhakika kuboresha miundombinu ya kusambazia maji
ambayo mingi ilirithiwa toka kwa wakoloni, na hakuna mipango endelevu ya kupanua huduma
ya maji kulingana na ongezeko la idadi ya watu.
•     Serikali haijaona umuhimu wa kuwa na mipango ya kuhifadhi maji ya mvua. Kila mwaka
mabilioni ya galoni yanapotelea baharini kupitia katika mito yetu inayofurika wakati wa
misimu ya mvua.
•     Pamoja na kubinafsisha baadhi ya mamlaka za maji ubinafsishaji huo mpaka sasa haujaleta
matunda yanayoonekana. Maji bado hayawafikii walengwa wengi kama ilivyotarajiwa na hata
hao ambao kwa kiasi fulani yanawafikia, maji wanayopata sio safi na salama. Wananchi bado
wanalazimika kuingia gharama kuchemsha maji hayo au kuyatia dawa ya kuulia vijidudu.
•     Maji ya visima yanayotumiwa na wananchi wengi siyo safi na salama kwani visima vingi ni
vifupi na vimechimbwa katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa makaazi. Kutokana
na kuwepo kwa miundo mbinu chakavu ya maji taka au kutokuwepo kabisa kwa miundo
mbinu hiyo maji mengi ya visima hivi yanachanganyika na vinyesi, hasa wakati wa misimu
ya mvua. Kutokana na hali hii kipindupindu kimekuwa ni ugonjwa wa kudumu hapa nchini.
Utafiti unaonyesha kuwa asilimia zaidi ya kumi ya magonjwa yote wanayoyapata wanaadamu
yanatokana na matumizi ya maji yasiyosalama kwa muda mrefu.
MKAKATI WA CUF KUBORESHA HUDUMA YA MAJI KWA MAENDELEO YA TAIFA
Serikali ya CUF italichukulia suala la usambazaji wa maji kuwa ni miongoni mwa majukumu ya
51
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
msingi ya kipekee ambayo yatashughulikiwa kwa haraka. Pamoja na mambo mengine Serikali
itachukua hatua zifuatazo:
•     Itaimarisha ofisi za mabonde ya maji zipate taarifa ya
haidrolijia ya mabonde yao, ziandae mipango endelevu ya
matumizi ya maji utakaozingatia matumizi ya maji ya binadamu
na mifugo, shughuli za viwandani, kufua umeme, kilimo cha
umwagiliaji maji na ulinzi wa mazingira kuzuia ukaukaji wa
maji unaosababishwa na binadamu na mifugo yake.
•     Itatekeleza mipango endelevu ya ujenzi wa mabwawa ya
kuvuna na kuhifadhi maji.
•     Itawahamasisha na kusaidiana na wanakijiji kuwa na miradi
midogo midogo ya kuvuna maji.
•     Itafungua mabonde ya chini (down stream basin) kwa kilimo
cha umwagiliaji maji baada ya maji ya bonde kutumiwa
katika kufua umeme. Kwa mfano kuna hekta zaidi ya milioni 1
zinazoweza kutumiwa kwa kilimo katika bonde la chini la mto
Rufiji.
•     Huduma za usambazaji maji zitabinafsishwa na kupewa
kampuni zenye uwezo, utaalamu na uzoefu wa kutoa huduma
bora kwa wananchi.
•     Katika kuimarisha utaalamu wa maji. Pamoja na kwamba nia ni kubinafsisha sekta ya maji,
bado tuna wajibu mkubwa wa kuwaandaa vijana wetu kufuzu kuchukua nafasi za ajira
zitakazojitokeza kwenye makampuni binafsi ya uzalishaji na usambazaji wa maji. Pamoja
na mambo mengine Serikali itakiimarisha zaidi Chuo cha Maji cha Rwegarulila na kuanza
kuchukua hatua za kukipandisha hadhi kuwa chuo kikuu kishiriki chini ya Chuo Kikuu cha
Dar-es-Salaam ambacho kitatoa wataalam wa viwango vya juu ambao wataisaidia sekta ya
maji kufikia malengo yake.
ELIMU
Kukua kwa uchumi wa kisasa wenye uwezo wa kuboresha maisha ya wananchi kunategemea
wafanyakazi wenye ujuzi na maarifa. Kwa hakika utafiti unaonyesha kuwa kukua kwa uchumi
wa taifa lolote kunashabihiana kwa karibu na kiwango cha kuwekeza katika sekta ya elimu.
Hivi sasa dunia inashuhudia mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA)
ambayo yanaleta mageuzi makubwa ya uchumi na biashara ya kimataifa. Ni dhahiri hatutaweza
kushindana kiuchumi na kibiashara katika ulimwengu tulionao leo iwapo hatutachukua hatua
za makusudi kuhakikisha kuwa watu wetu wengi na hasa wanafunzi na vijana wote wanapata
fursa kujifunza taaluma hii.
Elimu ya Chekechea
Serikali ya CUF itawahamasisha wananchi-ikiwa ni pamoja na watu binafsi, taasisi za kidini, na
mashirika yasiyo ya kiserikali kuwekeza kwenye nyanja hii chini ya utaratibu ufuatao:
—     Serikali itashughulika na kuweka viwango vinavyotakiwa na usajili.
—     Serikali itawasaidia wananchi wenye nia ya kuanzisha shule za chekechea kwa kuwapatia
52
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
viwanja vinavyotosheleza mahitaji kwa ajili ya kuzingatia viwango wakati wa ujenzi.
—     Kwa kuwa hivi sasa hakuna utaratibu wa kuwaandaa walimu wa chekechea kwenye vyuo
vyetu, Serikali ya CUF itauanzisha ili watakaowekeza kwenye shule za chekechea wasiwe
na shida ya kupata waalimu wenye sifa.
—     Shule za chekechea hazitatozwa kodi.
Elimu ya msingi
Pamoja na kwamba Elimu yetu kwa ujumla imeendelea kukumbwa na matatizo mengi, lakini hali
ni afadhali kidogo hivi sasa kuliko ilivyokuwa mwaka 2000. Mwaka 2000 kulikuwa na wastani wa
watoto milioni nane (8.07) waliokuwa wanapaswa kuwa katika shule za msingi, lakini katika hao
ilikuwa ni watoto milioni nne (4.37) tu ndio waliokuwa wanasoma katika shule zilizokuwepo, na
waliobaki milioni tatu (3.69) hawakuwa wakisoma kwa sababu mbalimbali. Aidha ilikisiwa kuwa
mpaka kufikia mwisho wa mwaka huo kungejitokeza kiasi cha watoto yatima laki nane (800,000)
kutokana na wazazi wao kufariki kwa ugonjwa wa Ukimwi, na hivyo kuzidisha uwezekano wa
ongezeko la watoto ambao wangekosa shule ya msingi.
Katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 CUF ililivalia njuga tatizo hili na kuifanya
CCM ije juu na kudai kuwa CUF ilikuwa inasema uongo. Hata hivyo pamoja na kuja juu, baada
ya chama hicho kurudi madarakani kilizikubali hoja za CUF, ikiwemo ya kufuta ada na michango
yote mashuleni, na kuanzisha operesheni kubwa ya kupunguza idadi ya watoto wenye umri wa
kwenda shule ambao walikuwa mitaani.
Pamoja na mafanikio haya kiasi yaliyokwisha patikana, sehemu kubwa ya watoto ambao wako
mashuleni wanasoma katika mazingira magumu yenye matatizo makubwa matatu ikiwemo
Msongamano kwenye madarasa, Njaa, na uhaba mkubwa wa waalimu na vifaa vya kufundishia.
Kutokana na matatizo haya na mengine, uwezo wa darasani wa wanafunzi umeendelea kuwa wa
chini.
Hali ilivyo sasa katika Sekta ya Elimu nchini;
•  Ukosefu wa mipango ya kisera tangu mwaka 1961;
Pamekuwepo utamaduni wa kutokuchukua hatua muafaka kwa wakati muafaka katika
kukabiliana na changamoto nyingi zinazoikabili sekta hii ya elimu nchini. Ukosefu wa mipango
ya kisera tangu awali hivi sasa taifa limejikuta likihitaji kufanya marekebisho makubwa katika
elimu ya msingi ili kurejesha hali ya kawaida katika ngazi hiyo ya elimu.
•  Ubora wa kiwango cha elimu;
Bado kiwango cha ubora ya elimu ya msingi inayotolewa nchini ni cha chini mno. Kwa
wastani kila mwaka, zaidi ya nusu ya wanafunzi wote hawapati alama za kufaulu.
•  Watoto wenye njaa ni vigumu kufundishika;
Tangu mwaka 2000 na kurejea tena mwaka 2005 Chama cha CUF imekuwa mstari wa mbele
kusisitiza kuwa lazima uwepo utaratibu wa kuhakikisha kuwa watoto mashuleni wanapatiwa
alau mlo mmoja kwa siku. Uzoefu unaonyesha wazi kuwa mototo mwenye njaa ni vigumu
kufundishika. Lakini suala hili halikupewa umuhimu unaostahiki kutokana na ama kutofahamu
au kutokuwa na dhamira ya dhati katika kupambana na adui ujinga, maradhi na umasikini,
53
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
na kumkomboa mtoto wa Tanzania kielimu. Wilaya zote zilizojaribu zimeshindwa kuendelea
na kutoa chakula kwa wananfunzi kutokana na njaa kubwa inayolikabili taifa kila kukicha na
maeneo mengine utaratibu huo umekuwa kero kubwa kwa wazazi/walezi wa watoto wasio na
uwezo wa kumudu kuchangia madebe ya nafaka mashuleni.
•  Kazi ya ualimu ni ya kitaalamu;
Mbali ya mwalimu kufundisha darasa zima katika ujumla wake, anatakiwa pia kumfuatilia
kwa karibu mwanafunzi mmoja mmoja ili aweze kutoa msaada wa ziada kwa wale wenye kasi
ndogo ya kujifunza (slow learners). Maslahi duni kwa walimu yamesababisha walimu wengi
walazimike kujikita zaidi katika kuhangaikia kujikimu kuliko kuzingatia kanuni za ufundishaji.
Pia malimbikizo ya mishahara kwa muda mrefu ni hali inayowamaliza walimu kwani wanajikuta
wanapaswa kukaanga vitumbua na maandazi ili kujikimu na ukata mkubwa.
•  Elimu ya chekechea;
Serikali haijawekeza kuhakikisha kuwa elimu ya chekechea inatolewa kwa watoto wote nchini.
Mathalan, vyuo vya ualimu vya Serikali havina utaratibu wa kuandaa walimu wa chekechea
na hivyo kusababisha waalimu wengi wa shule zilizopo kutokuwa na taaluma ipasayo. Aidha
Serikali haitoi msaada wowote, mathalan wa viwanja vya ujenzi wa shule hizo kwa wananchi
wenye nia ya kuanzisha mashule hayo, pamoja na kwamba inakataa kuzisajili nyingi ya shule
zilizopo kwa kisingizio kuwa nyingi ziko katika majengo ya nyumba za kawaida za kuishi na
hivyo kutofikia viwango vinavyotakiwa.
•     Watoto wanaohitimu elimu ya msingi wengi kati yao hawajui kusoma na kuandika kiingereza
na hata kiswahili japokuwa wanapelekwa sekondari;
Lugha ya kufundishia imekuwa ni tatizo kubwa sana.Vigogo wa CCM wanawapeleka watoto
wao shule za msingi zinazofundisha kwa kiingereza huku kiswahili kikiwa ni kama somo la ku-
jitegemea. Watoto wa makabwela (mahohehahe) wanapelekwa katika shule zinatumia kiswa-
hili kufundisha. Wakati haya yanatokea CCM wanajua kabisa kuwa mtoto yule anayepewa elimu
ya msingi kwa kutumia kiswahili atapaswa kupewa elimu kwa kutumia kiingereza katika hatua
zote za elimu zinazofuata ikiwa ni sekondari, vyuo na vyuo vikuu. Wanachofanya ni kuwadan-
ganya watanzania kuwa wanakienzi kiswahili huku wao wakiwaandaa watoto wao kukabiliana
na elimu za ngazi zinazofuata huku mtoto wa mtanzania wa kawaida akianza kujifunza upya
kiingereza wakati akiwa na akili isiyokomaa na isiyoweza kujifunza vizuri lugha ngeni-ndiyo
maana Taifa linaendelea kuzalisha wasomi wenye vyeti vya juu huku walikariri kila kitu daras-
ani bila kuelewa kutokana na kutoielewa vizuri lugha ya kufundishia waliyobadilishiwa ghafla
walipofika sekondari na ambayo hawakuanzishiwa mapema walipokuwa shule za msingi.
•     Walimu wa shule za msingi wamezidi kuwa masikini wa kutupwa, misharaha yao inalingana
na pesa ya posho ya siku moja anayopewa mbunge, walimu wamekuwa hawana hata nyumba
za kuishi na hii inapelekea wakae maeneo ya mbali na shule na hivyo kuondoa ufanisi wa
kazi zao shuleni. CCM waliahidi katika ilani yao ya uchaguzi ya mwaka 2005 kuwa chini ya
mpango wa MKUKUTA awamu ya kwanza ambao unakamilika mwaka huu, kuwa ifikapo mwaka
2010 itajenga nyumba za walimu 22,000. mpaka sasa kuna nyumba kama 360 zilizojengwa
kwa kiwango duni kabisa ambazo ni sawa na alilimia 1.6 ya asilimia 100 iliyoahidiwa.
•  Elimu kwa watoto wa kike(wasichana);
Ukimuelimisha mwanamke ndio umeielimisha jamii nzima. Hili linatokana na ukweli kuwa
wanawake wanajukumu la msingi la kimaumbile la ulezi wa familia. Kuporomoka kwa maadili
54
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
ya Taifa na ukosefu wa heshima na nidhamu na kujiingiza katika vitendo hatarishi kama
utumiaji wa madawa ya kulevya, uhasherati, ukahaba, nakadharika kunatokana na kukosekana
kwa kiasi kikubwa msingi wa awali wa malezi ya watoto. Watoto wa kike ndio walezi wa
familia watarajiwa wenye nafasi ya kipekee katika familia. Kutokana na ugumu wa maisha
wasichana walio wengi wamejikuta hawamalizi elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya juu
kutokana na kupata ujauzito kutokana na ‘MAFATAKI’ wakiwa mashuleni na hivyo kushindwa
kuendelea na masomo. Sera ya kuwataka wasichana wanaopata mimba kuendelea na masomo
na wenzao wengine darasa bado ni suala lenye utata linalohitaji umakini na uchambuzi wa
kina kuangalia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na hilo.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo kuhakikisha kuwa sekta ya elimu katika ngazi za
msingi na chekechea inaboreshwa:
•  Asilimia 25 ya Bajeti kila mwaka kutumika katika sekta ya ELIMU;
Itatumia si chini ya asilimia 25 ya bajeti yake kila mwaka kuboresha sekta ya elimu kwa
ujumla. Asilimia 50 ya bajeti yote ya elimu itaelekezwa kwenye kupanua na kuboresha elimu
ya msingi. Hili litasaidia kukamilisha marekebisho yanayotakiwa katika ngazi hii ya elimu
katika muda wa miaka mitano.
•  Kuhamasisha Ujenzi wa Shule binafsi na kufuta kodi katika vifaa vya elimu;
Serikali itafanya juhudi kubwa kuwahamasisha watu binafsi, mashirika ya dini na mengine
yasiyokuwa ya serikali, na makampuni ya biashara kujenga mashule zaidi ya msingi. Ili wananchi
walio wengi waweze kumudu gharama za kusomeshea watoto wao kwenye mashule haya,
Serikali haitayatoza kodi yeyote na itadhibiti viwango vya karo na michango vinavyotozwa.
Aidha Serikali itavifanyia marekebisho makubwa viwango vya kodi zote zinatozwa kwenye
vifaa vya elimu ili sekta ya elimu kwa ujumla inufaike na punguzo la gharama.
•  Marekebisho ya Mitaala;
Serikali ya CUF itafanya marekebisho ya mitaala kwa kuzingatia zaidi umuhimu (Relevance)
wa maudhui, muda wa kila somo, uwezo wa wanafunzi, na faida ya somo lenyewe:
—     Mitaala italenga kukuza lugha ya kiingereza na hivyo kuwaongezea wanafunzi uwezo wa
kumudu vizuri masomo ya sekondari.
—     Shule zisizomilikiwa na serikali zitakuwa na uhuru wa kufundisha masomo ya ziada kama
itakavyokubaliwa na bodi za shule zinazohusika.
—     Itakuwa ni marufuku kwa wanafunzi wa shule za msingi kutumiwa kwa ajili ya maandamano
ya aina yoyote zaidi ya yale yanayohusu siku ya mtoto duniani. Hii ina maana kwamba
watoto wa shule za msingi hawatahusishwa na vitu kama mbio za mwenge, mapokezi
ya wanasiasa, au kutumika katika shughuli za kuwachezea ngoma na kuwatumbuiza
wanasiasa hao.
—     Itakuwa ni marufuku kwa wanafunzi kujihusisha na aina yoyote ile ya biashara kwenye
maeneo ya shule.
•  Matumizi ya kompyuta mashuleni;
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa Serikali inajiunga na mpango wa kimataifa wenye lengo
la kumpatia kila mwanafunzi kompyuta (laptop) moja ya bei nafuu. Hatua kwa hatua shule
55
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
za msingi na sekondari zitaunganishwa na mtandao wa intaneti wanafunzi waanze mapema
kutumia kompyuta na mtandao wa mawasiliano (internet).
•  Lishe kwa wanafunzi;
Utafiti unaonyesha kuwa watoto wenye njaa hawafundishiki, na huu ndio msimamo na mtazamo
wa CUF siku zote. Serikali ya CUF kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya na kamati za shule
itahakikisha kwamba watoto wote wa shule za msingi wanapata walau mlo mmoja kamili wa
chakula kikuu kinachopatikana katika eneo husika, wakati wanapokuwa shuleni.
•  Elimu itatolewa bure na kupiga marufuku michango ya aina zote;
Hili ni eneo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na wazazi. Michango ambayo haitabiriki
imekuwa ni mingi na inavyoonekana siyo yote ambayo inachangishwa kwa nia njema. Serikali
ya CUF itahakikisha kuwa huduma zote zinazotakiwa katika elimu ya msingi zitakuwa ni
jukumu la serikali na kwa hivyo basi zitakuwa zinatolewa bure, mzazi atapaswa kumnunulia
mtoto wake nguo za shule na madaftari tu. Vitabu na na vifaa vingine vitagharamiwa na
serikali. Kamati za shule na mabaraza ya kata hayataruhusiwa kuirejeshe michango ya aina
yoyote ile kwa mlango wa nyuma. Chini ya serikali ya CUF mchango wowote ule utakuwa ni
suala la hiyari la muhusika.
•  Huduma za ukaguzi;
Huduma za ukaguzi ambazo hivi sasa zimedorora kwa kiasi kikubwa zitahuishwa na kuimarishwa.
Kila shule ni lazima ikaguliwe angalau mara moja kwa muhula.
•  Mishahara na Makazi ya walimu;
Serikali ya CUF itaongeza mishahara ya walimu kama ilivyo kwa watumishi wote wa umma ili
kukidhi mahitaji muhimu ya mwalimu wa shule ya msingi. Suala la makazi bora ya mwalimu
litakuwa ni jukumu la msingi kabisa kwa serikali ya CUF ambalo litaanzisha mradi mkubwa wa
ujenzi wa nyumba za walimu utakaosimamiwa na Serikali kwa haraka ndani ya miaka mitano
ya kwanza ya uongozi wa nchi.
ELIMU YA SEKONDARI
Tanzania ni nchi iliyoachwa nyuma sana duniani katika maendeleo ya elimu ya sekondari,
Chimbuko la Taifa letu kuwa nyuma mno katika elimu ya sekondari linaanzia katikati ya miaka
ya sitini pale serikali ilipotangaza kuwa elimu ya darasani (formal education) haina maana sana,
ati kwa kuwa ilikuwa inachukuwa miaka 20 hadi 30 mpaka matunda yake yaanze kuonekana na
taifa lisingeweza kusubiri na hivyo mkazo ungeelekezwa kwenye elimu ya msingi na ya watu
wazima, kutokana na msimamo huo athari zifuatazo zilijitokeza:
—     Elimu haikuonekana tena kuwa ni haki kwa kila mtoto kujiendeleza hadi mwisho wa upeo
wake.
—     Dhana ya kufaulu kwa ajili ya kujiunga na masomo ya sekondari iliuawa na sehemu yake
ikapandikizwa dhana ya kuchaguliwa.
—     Watu na taasisi binafsi, hata waliokuwa na uwezo, walikatazwa kuwekeza kwenye elimu
ya sekondari.
—     Serikali haikujihangaisha kuwekeza katika mashule mapya ya sekondari ukiondoa mawili
matatu ya mchepuo wa kilimo.
—     Serikali ya awamu ya nne imejenga sekondari za kata bila maandalizi ya walimu wa
kutosha na vifaa muhimu vya kufundishia kama vile mahabara na maktaba
56
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
—     Hivi leo elimu ya sekondari imekuwa ghali mno kulingana na uwezo mdogo wa wananchi
wengi walio masikini, japokuwa CCM inajisifia kuwa imeondoa ada na michango katika
shule za sekondari ukweli unabakia palepale kuwa maelfu ya watoto wanashindwa kujiunga
na sekondari kutokana na mzigo wa michango. Mathalani, ili mtoto ajiunge kidato cha
kwanza anahitaji aende shule na vifaa au mchango wa dawati, mwalimu, mlinzi, jembe,
panga, fyekeo, godoro, tahadhari na ada nakadharika hivi vyote vinaleta gharama kubwa,
wazazi wangapi wanamudu elimu hii ambayo serikali ya CCM wanasema ni bure?
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
Kama ilivyo kwa elimu ya msingi, elimu ya sekondari nayo inahitaji kupanuliwa na kuboreshwa.
Ongezeko la bajeti ya elimu kwa ujumla litatupa uwezo wa kufanya marekebisho yanayohitajika.
Serikali ya CUF inakusudia kutumia si chini ya asilimia 25 ya bajeti ya elimu kuimarisha na
kuboresha elimu ya sekondari. Pamoja na kusudio hili Serikali itachukua hatua zifuatazo ili
kuyafikia malengo haya:
•  Elimu ya sekondari bure;
Katika kuongeza nafasi za elimu ya sekondari Serikali ya CUF itahakikisha kuwa ada na
michango yote katika ngazi hiyo ya elimu vinafutwa; na nafasi za kutosha katika elimu ya
sekondari zinapatikana ili kila kijana aliyepata alama za kufaulu katika mtihani wa darasa la
saba aweze kuendelea na masomo ya elimu ya sekondari, bila kikwazo chochote.
•  Kuhamasisha ujenzi wa shule binafsi;
Serikali itafanya juhudi kubwa kuwahamasisha watu binafsi, mashirika ya dini na mengine
yasiyokuwa ya kiserikali, na makampuni ya biashara kujenga mashule zaidi ya sekondari.
Aidha Serikali itatoa kila aina ya msaada unaohitajika ili kufanikisha lengo hili ikiwa ni
pamoja na kuondoa vikwazo visivyo na sababu katika usajili wa shule binafsi. Ili wananchi
walio wengi waweze kumudu gharama za kuwasomeshea watoto wao kwenye mashule haya,
Serikali haitayatoza kodi yeyote.
•  Marekebisho ya mitaala;
Serikali ya CUF itafanya marekebisho kwenye mitaala inayotumiwa na shule za sekondari ili
pamoja na mambo mengine:
—    Kupunguza idadi kubwa ya masomo ya lazima ambayo kwa kiasi fulani yanachangia
mwelekeo uliopo hivi sasa wa wanafunzi kusoma kwa ajili ya kufaulu mitihani badala ya
kuwajengea uwezo wa kukuza uelewa.
—     Kuingiza elimu zaidi ya vitendo kuliko nadharia.
—     Kuingiza somo la kompyuta na matumizi ya mtandao wa internet.
—     Kuhamasisha wanafunzi kujifunza masomo ya hisabati na sayansi.
—     Somo la uraia liboreshwe ili kuwajenga vijana katika utamaduni wa kuthamini haki za
binadamu na kwa hivyo kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki hizo.
—    Ufundishwaji wa katiba ya nchi katika mashule ya sekondari itakuwa ni moja kati
marekebisho ya mtaala yatakayopaswa kuingizwa mashuleni.
•  Huduma za ukaguzi;
Kama ilivyo kwa shule za msingi, itakuwa ni lazima kwa shule za sekondari kukaguliwa angalau
mara moja kwa muhula.
57
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
•  Maslahi ya walimu na makazi bora;
Mishahara ya walimu na mazingira bora ya walimu wa shule za sekondari vitaboreshwa.
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa kila mwalimu wa shule ya sekondari ya umma anaishi katika
nyumba bora itakayojengwa na serikali na iliyo eneo lake la kazi isipokuwa atakavyopenda
mwenyewe kuishi eneo jingine bila kuathiri utendaji wa kazi yake.
ELIMU YA JUU
Elimu ya juu kwa Taifa lolote ni muhimu kwa sababu inalenga katika kuwaandaa wataalamu
mbali mbali kuja kukabidhiwa majukumu mbalimbali kwenye jamii. Kutokana na ukosefu wa
mipango makini tangu awali katika kuboresha elimu kwa ujumla, Tanzania tumekuwa na udhaifu
mkubwa katika suala zima la kuwaandaa wataalamu wetu. Siyo tu kwamba idadi ya wataalamu
wanaoandaliwa ni wachache ikilinganishwa na mahitaji halisi, lakini pia ubora wa maandalizi
yao hauridhishi. Waajiri wengi nchini, na hasa wale wa sekta binafsi wamekuwa na upendeleo
wa wazi wa wahitimu walioandaliwa kwenye vyuo vya nje kuliko wale walioandaliwa nchini. Ni
dhahiri kabisa kuwa kwa hali tuliyonayo nchi yetu itakwama katika juhudi za kuboresha uchumi
na kujiletea maendeleo iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa mapema siyo kuongeza tu
idadi ya wataalamu tunaowaandaa, lakini pia kuboresha utoaji wa taaluma katika taasisi zetu
za elimu ya juu.
Hali halisi ilivyo sasa katika sekta ya elimu ya juu nchini;
•     Tanzania pamoja na kwamba ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu kuliko nchi zote za Afrika
Mashariki, ndiyo ya mwisho kwa idadi ya wananchi wake wenye walau shahada moja.
•     Kumekuwa na wimbi kubwa la wahadhiri katika taasisi zetu za elimu ya juu kuondoka
na kwenda vyuo vya nchi zingine za kiafrika kutokana na maslahi duni wanayopata hapa
nchini.
•     Katika taasisi zetu nyingi za elimu ya juu huduma za kitafiti zinalegalega kwa kiasi kikubwa
kutokana na serikali kushindwa kutenga fedha kwa shughuli hiyo. Huduma hizi pale ambapo
zipo kwa kiasi kikubwa zinafadhiliwa na wahisani wa nje ambao mara nyingi wao ndiyo
wanaoamua ni aina gani ya utafiti wanataka ufanywe. Hali hii imesababisha taifa kutonufaika
kikamilifu na matokeo ya tafiti mbalimbali zinazofanyika kwenye taasisi hizi.
•     Bila kujali kwamba kimsingi Tanzania haijafikia wakati wa kuhitaji wanafunzi wetu wanaosoma
katika taasisi za juu za elimu kuchangia gharama, Serikali ya CCM imeulazimisha utaratibu
huo kutumika bila kuzingatia mizania ya faida na hasara zake kwa jamii yetu.
•     Kumekuwa na kulazimisha kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma katika taasisi za juu
kusikoendana sanjari na uboreshaji wa huduma za msingi zinazohitajika. Matokeo yake ni
kwamba mazingira ya wanafunzi wanaosoma miaka hii ni magumu kuliko ilivyokuwa miaka ya
nyuma.
•     Elimu ya juu imefanywa kama ni anasa na mzigo mkubwa kwa serikali, wanafunzi wa elimu ya
juu wananyanyasika vya kutosha kutokana na utaratibu wa utoaji mikopo, wanafunzi wengi
wanakopeshwa kwa madai ili waweze kuja kuitumikia nchi yao hali hii inaondoa uzalendo
kwa Taifa tunalolilea kwani iwapo vijana hawathaminiwi na serikali hawatakuwa na mchango
wowote kwa taifa baadaye.
•     Utoaji wa udhamini wa mikopo kwa madaraja; vigezo vya utoaji wa mikopo kwa wanafunzi
hauzingatii hali halisi ya maisha na uwezo wa kifedha za wazazi wa wanafunzi, mathalani wale
58
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
watoto waliosoma shule zisizo na walimu na wakapata daraja la tatu na la pili kwa wavulana
na la tatu kwa wasichana ndio wanaonyimwa mikopo.Wale watoto wa vigogo wanaosoma
shule nzuri na zenye walimu wa kutosha ambako ni rahisi kufaulu kwa kiwango cha daraja la
kwanza ndio CCM imewatengea mikopo.
•     Sehemu kubwa ya gharama za posho wakati wa mafunzo kwa vitendo yanayoenda kufanywa
na mwanafunzi wa chuo kikuu yanagharamiwa na mzazi na mwanafunzi peke yake. Serikali
haioni umuhimu wa mafunzo haya na ina mchango kidogo sana katika kuwezesha mafunzo
bora ya vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
•     Wanafunzi wa vyuo vikuu leo wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa makazi ya kuishi, Serikali
imeliacha suala hili kuwa mikononi mwa wanafunzi na wazazi. Kinachotokea ni kuwa
wanafunzi wengi wanaishi kwenye baadhi ya nyumba duni za kupanga zilizoko katika maeneo
ya mbali na vyuo vyao. Kwa mfano; kwa Dar es Salaam mwanafunzi kuishi Mbagala Chalambe
na kusoma Chuo kikuu cha Dar es Salaam humchukua masaa 4 kwa siku kwenda na kurudi
chuoni lakini pia hayo mazingira ya makazi ya Mbagala na kujisomea elimu ya juu ni mashaka
makubwa.
•     Kiwango cha mkopo wanachopewa wanafunzi kwa ajili ya kujikimu ni shilingi 5,000/- kwa
siku. Kiasi hiki ni kidogo na hakitoshelezi kumfanya mwanafunzi kuweza kulipia gharama za
chakula, malazi, anunue madaftari, sabuni, nauli, mawasiliano, matibabu, nakadharika.
•     Kushindwa kuviunganisha vyuo vikuu ndani ya nchi na huduma ya intaneti ya uhakika pamoja
na kuvipatia kompyuta za kutosha ni tatizo linaloathiri uharaka wa kujifunza na kuendana
na karne ya sayansi na teknolojia. Utafiti uliofanywa na serikali ya wanafunzi ya chuo kikuu
cha Dar es salaam (DARUSO) mwaka 2007 ulibainisha kuwa katika chuo kikuu hicho sehemu
ya mlimani kompyuta moja inatumiwa na wastani wa wanafuzi 400.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
Pamoja na kwamba Serikali ya CUF imedhamiria kutumia si chini ya asilimia 25 ya bajeti yote
yote ya elimu kuboresha elimu nchini, Serikali pia itachukua hatua zifuatazo kuhakikisha kuwa
malengo haya yanatimizwa;
•  Ugharimiaji (uchangiaji) wa elimu ya juu;
CUF inaamini kuwa Tanzania haijafikia wakati wa kuhitaji wanafunzi wa elimu ya juu kuchangia
gharama. Serikali ya CUF itaweka utaratibu utakaowawezesha vijana wote wenye sifa na
waliochaguliwa kujiunga katika chuo kikuu chochote ndani ya nchi kupata elimu ya juu bila
vikwazo. Serikali ya CUF itagharamia mahitaji yote ya msingi ya mwanafunzi wa elimu ya juu
bila MKOPO, ikiwa ni pamoja na kugharamia bima ya afya ya kila mwanafunzi. Uboreshaji wa
eneo hili la elimu ya juu utafanyika hatua kwa hatua kwa kuzingatia hali halisi ya ukuaji wa
uchumi na mahitajio mengine ya Taifa.
•  Posho za kujikimu vyuoni na wakati wa mafunzo kwa vitendo;
Serikali itakayoongozwa na CUF itatoa mchango wa kutosha na kuhakikisha kuwa wanafunzi
wa elimu ya juu wanapatiwa posho zinazokidhi mahitaji wanapokuwa vyuoni na wanapokuwa
katika mafunzo kwa vitendo, Serikali ya CUF itaongeza posho za kujikimu vyuoni kutoka
shilingi 5,000/- ya sasa na kuwa kuanzia shilingi 10,000/- wawapo vyuoni na shilingi
15,000/- wawapo katika mafunzo kwa vitendo ili wawe na uwezo wa kusoma kwa utulivu na
kujifunza mambo yote muhimu kwa ufasaha kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu.
59
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
•  Matumizi ya intaneti;
Serikali ya CUF itatengeneza mtandao mzuri wa matumizi ya intaneti katika vyuo vikuu vyote
vya Serikali na kuhakikisha kuwa panakuwa na kompyuta za kutosha kwa uwiano wa kompyuta
moja wanafunzi wawili au kila mwanafunzi na laptop yake. Hali hii itawafanya wanafunzi
wetu kujielimisha vizuri zaidi ili waendane na ushindani wa soko la taaluma na ajira kutoka
nchi nyingine zilizoendelea duniani.
•  Makazi ya wanafunzi wa elimu ya juu;
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa kila chuo kikuu cha umma kinakuwa na makazi thabiti
yatakayotosheleza wanafunzi wote. Makampuni makubwa ya ujenzi yatapewa tenda za kujenga
mabweni ya kisasa ya wanafunzi yaliyounganishwa na mtandao wa intaneti katika kila chuo.
Lengo la Serikali litakuwa kuwezesha kila mwanafunzi apate makazi rafiki kwa usomaji, isipokuwa
kwa yule ambaye kwa sababu binafsi atataka kukaa mahali pengine. Aidha uanzishwaji wa miji
mipya ya vyuo vikuu pembezoni mwa miji mikuu litazingatiwa ili kuandaa mazingira bora zaidi
ya kujifunza na kuondokana na msongamano wa vyuo kuwa katikati ya miji.
•  Mazingira ya kazi ya wahadhiri;
Serikali ya CUF itaandaa mpango maalum wa makazi na mishahara ya wahadhiri wa vyuo
vikuu vyote vya umma nchini ambapo kila mhadhiri atapewa nyumba maalum na kulipwa
mshahara unakidhi hali halisi ya maisha ya wakati husika.
•  Uboreshaji wa mitaala;
Serikali kwa kushirikiana na wataalamu mbali mbali toka kwenye vyuo vinavyohusika
itaanzisha programu ya kuifanyia mitaala inayotumika marekebisho ili ilenge zaidi kwenye
kuandaa wahitimu walio tayari kwa kazi.
•  Kuongeza nafasi zaidi za masomo ya Sayansi na Teknolojia;
Pamoja na kwamba Serikali ya CUF inakusudia kuipanua elimu ya juu nchini kwa ujumla,
ongezeko la nafasi kwa fani za sayansi na teknolojia litapewa kipaumbele. Chini ya mkakati
huu madaktari, mainjinia, wanasayansi na wataalamu wa kompyuta wengi zaidi wataandaliwa
kila mwaka. Serikali pia itaendelea kuziunga mkono juhudi za watu binafsi, mashirika ya dini,
na taasisi nyingine zenye malengo ya kuanzisha vyuo vikuu kwa ajili ya taaluma mbali mbali.
•  Kuimarisha huduma za kitafiti;
Ukiondoa maslahi madogo, udhaifu mkubwa katika huduma za kitafiti ni sababu nyingine
kubwa inayowafanya wataalamu mbali mbali kuzikimbia taasisi zetu za elimu ya juu. Serikali
ya CUF itajitahidi kuziimarisha huduma hizi kwa kutoa fedha zaidi kwa ajili ya vifaa na
masurufu. Aidha, itaanzisha kitengo maalumu cha uratibu wa kuzifanyia kazi tafiti/vumbuzi
mbalimbali zinazopatika kutokana na jitihada zilizofanywa katika vyuo vyetu.
•  Ujenzi wa miundombinu katika vyuo vikuu vyote;
Serikali ya CUF itatengeneza miundombinu ambayo itawezesha mazingira ya vyuo kuvutia
wanafunzi wa ndani na nje ya nchi. Vifaa vya kitaalam na kiteknolojia, vitabu vya kutosha,
kuboresha vyumba vya masomo, barabara, korido zenye mapaa juu yake kwenye kila njia
zinazounganisha darasa na darasa, ofisi za wahadhiri, sehemu za chakula, mabweni na
maeneo mengine. Mtandao huu utasaidia kurahisisha mawasiliano na kuendana na muda na
vipindi madarasani kutosimama hasa nyakati za mvua ambapo wanafunzi na wahadhiri wengi
hushindwa kufika madarasani.
60
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
•  Maktaba zenye uwezo mkubwa;
Miaka 49 sasa tangu tujitawale hali ya maktaba zetu imekuwa duni, Serikali ya CUF itahakikisha
kuwa maktaba zetu zinakuwa na uwezo mkubwa sawa na maktaba za nje, na kwa kutumia
mawasiliano ya intaneti wanafunzi wa vyuo vyetu wataweza muda wote kutumia TEKNOHAMA
itakayowaruhusu kusoma vitabu mbalimbali vilivyoko katika maktaba za vyuo vikubwa duniani
kwa njia za ki-elektroniki.
ELIMU MAALUM KWA WALEMAVU
Kwa bahati mbaya baadhi ya ndugu zetu wetu nchini ni walemavu na wana mahitaji ya elimu
maalum yanayohitajika kuweza kujiendeleza. Kwa kawaida watoto au watu wenye ulemavu kwa
ujumla wake huwa wana mahitaji maalumu ikiwemo ya uangalizi wa muda wote, hili upelekea
kuwepo kwa gharama za kuwahudumia waangalizi. CUF tunaamini kuwa kuzisaidia familia
zenye watoto wenye ulemavu kutasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na vikwazo vya kielimu
wanavyopata watoto wenye ulemavu.
Hali ilivyo sasa;
•     Kukosekana kwa sera ya elimu inayojumuisha mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu
kumesababisha idadi kubwa ya vijana wenye ulemavu kukosa fursa ya kupata elimu.
•     Huduma zilizoko katika taasisi mbalimbali za elimu kuanzia ngazi ya msingi, sekondari, na
vyuo hazijazingatia mahitaji maalum ya walemavu.
•     Hali duni ya maisha ya wazazi ni kikwazo kwa watoto wenye ulemavu kupata elimu bora.
•     Ukosefu mkubwa wa vifaa vya kujifunzia ni kikwazo kwa watoto wenye ulemavu kupata elimu
bora.
•     Ukosefu wa kupewa kipaumbele na kutozingatia kutenga bajeti ya kutosha ya taifa kusaidia
watoto wenye ulemavu ni kikwazo.
•     Ulaghai wa kisiasa unaofanyika kwa baadhi ya walemavu na kusahau kusimamia haki za
msingi za watu wenye ulemavu.
•     Mazingira hatarishi ya maisha ya watu wenye ulemavu.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
Kwa kutambua umuhimu mkubwa wa kuwaendeleza watoto wenye ulemavu na kuwapunguzia
wazazi mzigo wa ziada katika kuwahudumia, Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo:
•     Itazindua sera mpya ya elimu ambayo itakuwa imeyajumuisha kwa ukamilifu mahitaji maalum
ya wanafunzi wenye ulemavu.
•     Itafanya marekebisho mbalimbali ya kiufundi kwenye taasisi mbalimbali za elimu ili kuondoa
vikwazo mbalimbali vinavyowakwaza wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika taasisi
hizo.
•     Mahitaji maalum ya kielimu kwa watoto wenye ulemavu yatajumuishwa katika mitaala ya
vyuo vya waalimu ili kuongeza idadi ya waalimu wenye uwezo wa kutoa elimu kwa watoto
wenye ulemavu.
•     Serikali itagharamia kwa asilimia mia moja gharama zote zinazohusiana na masomo ya
wanafunzi wenye ulemavu katika ngazi zote za elimu.
61
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
ELIMU YA WATU WAZIMA
Hivi sasa inakadiriwa kuwa asilimia 27.4 ya Watanzania wenye umri wa zaidi ya miaka 15 sawa
na wananchi milioni 6.4 kati ya nguvukazi ya watu milioni 21 hawajui kusoma na kuandika.
Sehemu kubwa ya watu wanaohesabiwa wanajua kusoma na kuandika, uelewa wao ni mdogo
sana. Idadi hii ni kubwa mno katika nguvu kazi ya watu wasiozidi milioni 16.
Hali ilivyo sasa;
•     Kuupuza kwa muda mrefu umuhimu wa kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda
shule wameandikishwa shule kumechangia sana katika kuongeza idadi ya vijana wanaoingia
katika utu uzima ilhali hawajui kusoma na kuandika.
•     Kuanguka kwa ubora wa taaluma inayotolewa katika shule za msingi kumesababisha kundi
kubwa la watoto kumaliza darasa la saba wakiwa na uwezo kidogo sana wa kusoma na kuandika.
Wengi wa hawa hupoteza ujuzi huu baada ya miaka michache huko mitaani kwa sababu ya
kutoweka kwa kiasi kikubwa kwa utamaduni wa kujisomea miongoni mwa wananchi.
•     Hivi sasa maktaba mbalimbali za Serikali zinatoza ada kwa wanaotaka huduma ya kujisomea.
Hali hii inazidi kufifisha hamu ya wananchi kujifunza na kujiendeleza kielimu.
•     Mkazo uliokuwepo katika miaka ya 70 kuhusu elimu ya watu wazima uliachiwa taratibu
kufifia hadi hatimaye ukatoweka kabisa. Kwa hivi sasa fedha za bajeti ya elimu ya watu
wazima zinatolewa lakini haziwanufaishi walengwa.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
•     Serikali ya CUF itahuisha upya madarasa ya elimu ya watu wazima. Serikali itaandaa utaratibu
utakaowezesha kila shule ya msingi iliyoko nchini kuendesha madarasa ya elimu ya watu
wazima kila siku jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa. Kwa hali hii fedha za bajeti ya elimu
ya watu wazima zitatumika ipasavyo na hivyo kuwanufaisha walengwa.
•     Serikali ya CUF itafuta ada zote zinazotozwa na maktaba za Serikali hivi sasa na kuhakikisha
kuwa huduma katika maktaba hizi zinaboreshwa kwa kiwango cha juu ili kukidhi haja ya
wananchi kujiendeleza kielimu.
•     Maktaba zitaunganishwa na mtandao wa internet.
ELIMU YA UFUNDI
Kati ya mambo ambayo Serikali ya CCM haijafanikiwa ni kuimarisha vyuo vya elimu ya ufundi.
Nchi yoyote iliyowekeza katika elimu hii inajiweka katika mazingira mazuri ya kuleta maendeleo
haraka kwani vijana wengi wanapata ujuzi na kujiajiri katika sekta binafsi au zisizo rasmi.
Dira ya Mabadiliko ya CUF
Elimu ya Ufundi kuwa nyenzo muhimu ya maisha ya vijana;
•     Shule za ufundi zitaongezwa katika kila wilaya kwa kadri ambavyo uchumi wa nchi unavyokua
na serikali itazisimamia ipasavyo.
•     Kila mtoto asiyejiunga shule ya sekondari lazima apate nafasi ya kusoma masomo ya ufundi
ili ajijengee mazingira ya kupata ajira au kuwa na uwezo wa kujiajiri katika sekta binafsi.
•     Serikali itawapeleka walimu wengi zaidi katika mafunzo ya juu ya ufundi ili vyuo vya ufundi
62
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
viwe na wataalam wa kutosha watakaokuwa wakiwafundisha wanafunzi kwa kuzingatia
msisitizo wa mafunzo kwa vitendo kuliko nadharia.
AFYA
Katika Tanzania tatizo la afya za wananchi ni kubwa mno. Huduma za afya ziko katika hali
mbaya sana. Hospitali, vituo vya afya, na zahanati ni chache na zinakabiliwa na matatizo
mengi. Msongamano mkubwa wa Wagonjwa, uhaba wa madaktari na wauguzi, uhaba wa vitanda,
uhaba wa vifaa vya kazi, uchakavu wa majengo, na zaidi ya yote uhaba mkubwa wa madawa ni
baadhi tu ya matatizo haya. Utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya watoto wanaokufa
chini ya umri wa miaka mitano hufia majumbani bila kufikishwa hospitali au zahanati angalau
mara moja. Katika kila watoto 100 wenye umri
usiozidi miaka mitano, 44 wanakosa lishe bora na
kwa hivyo wameathirika kwa utapiamlo. Watoto
wanaokosa lishe bora hawajengi kinga ya mwili
na ubongo wao haukuwi vizuri. Ukimwi hivi sasa
ni tishio kubwa linaloashiria maangamizi kwa
taifa letu.
Ni lazima tuelewe kuwa maendeleo hayawezi
kupatikana kwenye taifa lenye idadi kubwa ya
watu ambao hawana afya nzuri, Tunawajibika
kujenga mazingira yatakayouhakikishia umma
kuwa kuna nia ya dhati ya kuifufua na kuiboresha
sekta ya afya. Tuandae madaktari na wauguzi
kwa wingi zaidi na wapewe motisha wa kutosha
ili wasilazimike kuikimbia nchi. Hospitali kuu zote kuanzia wilayani zipatiwe vifaa vya kisasa
vinavyohitajika kukidhi haja ya matibabu katika ulimwengu wa kileo. Madawa yapatikane kwa
gharama nafuu. Ni lazima uandaliwe utaratibu utakaotuhakikishia kwamba Mtanzania yeyote
hatakosa kupata matibabu kwa sababu tu ameshindwa kumudu gharama. Lakini lililo la msingi
kabisa ni kufufua na kuimarisha huduma ya afya ya kinga. Uboreshaji wa mazingira ni sehemu
muhimu kabisa katika utoaji wa huduma ya afya ya kinga. Ili kuzuia utapiamlo na maradhi
mengine serikali isimamie na kuratibu uwekaji wa virutubisho muhimu kama vile iodine kwenye
chumvi, vitamini A na D kwenye unga nakadharika.
Ni lazima tuondoe vyanzo vya maradhi; taka zizolewe na turejeshe utaratibu uliotoweka siku nyingi
zilizopita wa kudhibiti wadudu wanaobeba vimelea vya maradhi, hususan mbu. Ni lazima tuweke
utaratibu utakaotuhakikishia kuwa Wananchi hawaishi na kufanyia shughuli zao kwenye maeneo
yenye misongamano mikubwa. Ni lazima tufufue na kuimarisha huduma za ukaguzi za mabwana na
mabibi afya ili kuhakikisha kuwa migahawa, maduka, masoko, machinjio, makazi yetu nakadharika,
yanakuwa katika mazingira salama muda wote. Pamoja na haya yote ni lazima tuhakikishe kuwa
suala la uhaba wa maji salama kwa matumizi ya majumbani linapatiwa ufumbuzi wa haraka. Aidha
ni lazima kama Taifa kuliangalia upya suala la maambukizi ya UKIMWI kwa uzito unaostahili.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya Afya;
•     Utaratibu wa kinga ya msingi kwa maradhi umepuuzwa kwa kiwango kikubwa. Huduma ya
63
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
kuzoa taka na mfumo wa maji machafu ziko katika hali mbaya. Mkakati wa kuharibu vyanzo
vya maradhi umeachwa muda mrefu uliopita.
•     Wafanyakazi wa sekta ya afya wanafanyakazi katika mazingira ya hatari yanayoweza kuwaletea
maambukizi. Mishahara ni midogo ambayo hailingani kabisa na ugumu wa kazi. Wakilalamika
wanaitwa ‘wabinafsi’ wasiojali ‘wito’ wa kazi yao na kukumbushwa viapo walivyoapa. Matokeo
yake madaktari na wauguzi wamekuwa ‘ombaomba’ na wagonjwa wasio na chochote cha
kutoa wamejikuta wakitekelezwa. Nchi jirani zimekuwa ndiyo kimbilio kubwa la madaktari na
wauguzi wetu.
•     Zahanati, vituo vya afya na hospitali ni chache na hazikidhi hitajio la ukuaji wa idadi ya watu
Tanzania.
•     Huduma muhimu katika vituo vya afya na hospitali kama madaktari na wauguzi, madawa,
vitanda, na vipimo havitoshelezi mahitaji.
•     Serikali imeendelea kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kutoa huduma bora ya afya nje ya nchi
kwa kundi la watu wachache ambao ni viongozi waandamizi na familia zao.
•     Utaratibu wa kuwalazimisha wananchi kulipia gharama za matibabu umesababisha wananchi
wengi kuathirika kwa kushindwa kumudu gharama hizo.
•     Kuanzia mwaka 1985 hatua na mikakati kadhaa imechukuliwa yote ikilenga katika kuelimisha
na kuhamasisha jamii juu ya athari za maambukizo ya ukimwi na njia za kudhibiti kuenea
kwa maambukizi mapya. Hata hivyo pamoja na kampeni hizi, maambukizi ya ukimwi bado
yameshika kasi na wanaougua maradhi haya wanazidi kujitokeza. Pamoja na kujitokeza kwa
hali hii Serikali ya CCM imeshindwa kubadili mwelekeo wa kampeni hizi ili ziweze kutufikisha
kwenye malengo tuliyokusudia.
•     Mpango wa bima ya afya ulioletwa na Serikali ya CCM katika miaka ya hivi karibuni unafanya
kazi katika maeneo machache na hivyo kuwasababishia usumbufu mkubwa wanachama wa
mfuko huo.
Dira ya Mabadiliko ya CUF katika kuboresha sekta ya Afya nchini;
Kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo la afya kwenye jamii yetu, Serikali ya CUF itatenga asilimia 15 ya
bajeti yote ya Serikali kwa ajili ya kuboresha huduma za afya na kutekeleza mambo yafuatayo:
•  Huduma za afya ya msingi bila malipo;
Huduma za msingi za afya zitakuwa ni haki ya kila Mtanzania. Mkazo maalum utawekwa
katika tiba ya kinga ikiwa ni pamoja na chanjo za watoto na kuweka virutubisho katika
vyakula (food fortification). Tiba ya maradhi ya kuambukuza kama vile malaria, kifua kikuu,
UKIMWI, cholera (TB), typhoid, minyoo na kadharika zitapatikana bila malipo.
•  Huduma za upendeleo;
Kina mama wajawazito, wazee kuanzia miaka sitini, walemavu na watoto wadogo wote
walio na umri chini ya miaka mitano watapata matibabu yote bure. Aidha, Serikali ya CUF
itaendeleza utaratibu wa ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa kuongeza wigo zaidi kwa
kuhakikisha kila mtanzania anapata chandarua sanjari na kuwa na program endelevu ya
kuangamiza mazalia ya mbu.
•  Utaratibu wa kuchangia gharama;
Pamoja na ongezeko kubwa katika bajeti ya afya bado bajeti hiyo itakuwa haitoshelezi
64
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
kulinganisha na mahitaji halisi. Ili kufidia pengo kuna umuhimu mkubwa kwa vyanzo vingine
kuchangia katika huduma za afya. Uchangiaji huu utafanyika chini ya utaratibu ufuatao:
—    Mpango wa bima ya matibabu; Serikali itasimamia uboreshaji wa utaratibu wa bima
ya matibabu nchini ambapo waajiri wote katika sekta rasmi watatakiwa kuwakatia
wafanyakazi wao bima, na pia kuwawezesha wanachama wa mpango huo kupata huduma
hiyo mahala popote humu nchini. Bima hiyo itagharimia matibabu ya wafanyakazi na
familia zao, yasiyohusiana na huduma za msingi za afya au huduma za upendeleo. Bima
hii haitakuwa mzigo kwa waajiri kwa kuwa itamezwa katika marekebisho ya viwango vya
kodi yatakayofanywa na Serikali ya CUF.
—     Uchangiaji wa gharama wa moja kwa moja; Utaratibu wa kuchangia moja kwa moja gharama
za matibabu yaliyo nje ya huduma za msingi za afya, au zile za upendeleo utaendelezwa
kwa wananchi ambao watakuwa hawana bima na wenye uwezo wa kuchangia gharama.
Kwa wagonjwa ambao watakuwa hawana uwezo kabisa wa kujigharamia dawa, watapatiwa
matibabu kamili bila malipo na serikali.
•  Kuboresha miundo mbinu ya afya;
Serikali ya CUF itahakikisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo mazingira ya hospitali
zote nchini kuanzia wilayani yameboreshwa kufikia viwango vinavyokubalika. Fedha zaidi
zitatumiwa kuhakikisha kuwa ifikapo mwishoni mwa kipindi hicho hakuna mgonjwa anayelala
chini au kuchangia kitanda, vipimo vyote muhimu vinapatikana kuanzia wilayani, na kila
hospitali kuanzia wilayani ina madaktari na wauguzi wa kutosha kuweza kutoa huduma bora,
na kuwepo kwa huduma zote za msingi ikiwemo upatikanaji wa maji na umeme wa uhakika.
•  Kuboresha huduma ya matibabu;
Kila hospitali itabuni utaratibu wa kuongeza tija. Pamoja na mambo mengine utaratibu huu ni
lazima uhakikishe kuwa kila mgonjwa atakayelazwa wodini ataanza kupata matibabu mapema
iwezekanavyo. Kutafanyika ukaguzi wa mara kwa mara kwenye hospitali utakaohusisha
kuwasaili wagonjwa mbalimbali kwa siri ili kupima ni kwa kiwango gani mahospitali
yanazingatia utaratibu huu.
•     Kuimarisha huduma za kinga; Taifa linaweza kuokoa fedha nyingi sana zinazotumika kwa
matibabu iwapo watu watajikinga na maradhi. Ili watu waweze kujikinga na maradhi taifa
halina budi kuzingatia kanuni za afya ya msingi kama usafi wa mazingira na kuzuia vyanzo vya
maradhi. Serikali ya CUF itashirikiana na serikali za mitaa kuhakikisha kuwa katika kipindi cha
miaka mitano ijayo vyanzo vyote vya maradhi ya kuambukiza kama mrundikano wa takataka,
mazalio ya mbu, ujenzi wa vyoo bora nakadharika vinazingatiwa.
•  Nidhamu ya matumizi ya fedha za mfuko wa Afya;
Serikali itafanya utaratibu wa kupunguza idadi ya wafanyakazi wa maofisini katika sekta ya
afya na kuwahamishia katika ajira nyingine bila kuathiri huduma, na fedha zitakazookolewa
zitaelekezwa kwenye kuboresha miundo mbinu na maslahi ya madaktari na wauguzi.
—     Serikali itaboresha hospitali zetu kwa kuzipatia zana za kisasa, madaktari na wataalamu
wenye uwezo ili kupunguza uwezekano wa viongozi waandamizi kutumia fedha nyingi za
wananchi kwa ajili ya matibabu nje ya nchi.
—     Ili kuongeza ufanisi baadhi ya huduma kwenye mahospitali ambazo hazina uhusiano wa
moja kwa moja na tiba zitabinafsishwa.
•     Kupunguza gharama za madawa; Serikali itafanya mazungumzo na wawekezaji zaidi ili kujenga
65
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
viwanda vitakavyozalisha madawa ya kuiga (Generic Drugs) na vifaa vingine vya mahospitali
kwa gharama nafuu zaidi nchini mwetu. Aidha, baadhi ya madawa ya msingi yatatengenezwa
kwa wingi na kuwekwa nembo ya serikali ili kudhibiti matumizi mabaya ya dawa hizo.
•     Maslahi ya madaktari na wauguzi; Kwa kuzingatia kuwa madaktari na wauguzi ni watu ambao
wanafanya kazi ngumu na kwenye mazingira ya hatari ni lazima taifa lielewe kuwa maslahi
yao yanahitaji kuboreshwa zaidi. Serikali ya CUF itahakikisha kuwa maslahi ya wafanyakazi
hawa yanaboreshwa angalau kufikia viwango vya wenzao katika nchi jirani. Serikali ya CUF
itaongeza mishahara na marupurupu kwa madaktari na wauguzi kwa kadri uchumi wa nchi
unavyokua ili kuwafanya madaktari na wauguzi wajitume zaidi, wajiepushe na vitendo vya
rushwa na waokoe maisha ya Watanzania yanayopotea wakati mwingine kwa sababu tu ya
kushuka kwa ari ya kufanya kazi.
•     Mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI; Serikali ya CUF pamoja na mambo mengine itaweka
mkakati wa kitaifa utakaolenga kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa mtu ambaye hivi
sasa hana virusi vya ukimwi, kuambukizwa. Mkakati huu utalenga katika kuishirikisha jamii
katika mjadala wa kutunga sera mahsusi ya nchi itakayosimamia mapambano dhidi ya Ukimwi
kwa nia ya kufanikisha malengo yafuatayo:-
—     Kuondoa utaratibu wa sasa unaofanya taarifa za maambukizi ya Ukimwi kuwa ni siri na
badala yake taarifa hizi ziwe za wazi kama ilivyo kwa magonjwa mengine.
—     Kuweka utaratibu wa kutangazwa na kuchapishwa kila mwezi kwa takwimu za maambukizi
ya Ukimwi kuanzia katika ngazi ya kata ili kumwezesha kila mwananchi kuwa na taarifa
sahihi zinazohusu eneo analoishi.
—     Kufikia makubaliano ya kitaifa ni nini kifanyike ili kudhibiti kwa kiwango cha juu kabisa
uwezekano wa maambukizi kwa wananchi wetu ambao bado kuambukizwa.
—     Kuanzisha utaratibu wa makusudi wa kuziunga mkono na kutoa kila aina ya msaada
unaowezekana, juhudi za watafiti wa kizalendo ikiwa ni pamoja na waganga wa jadi
katika kutafuta tiba au kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya ukimwi.
—     Kuhakikisha kuwa waathirika wote wa UKIMWI wanapatiwa madawa ya kuongeza muda wa
kuishi ili waendelee kutoa mchango muhimu katika malezi ya familia zao na maendeleo
ya taifa kwa ujumla.
—     Kuendeleza na kuimarisha kampeni za kutoa elimu dhidi ya UKIMWI itakayoweka msisitizo
juu ya ukweli kwamba njia ya uhakika ya kujikinga dhidi ya maambukizo ni kuacha
kufanya vitendo vya uasherati.
—     Kujenga uchumi imara unaoongeza ajira, tija na neema kwa wote utakaopelekea jamii
kujishughulisha zaidi katika masuala ya msingi na kujiepusha na vitendo vya ukahaba na
uasherati.
MAKAZI
Pamoja na kwamba Tanzania ina wizara nzima inayoshughulikia masuala ya Ardhi, ina Chuo
Kikuu kishiriki kinachoshughulikia masuala ya Ardhi tu na kuna Idara za Mipango Miji katika
kila Halmashauri na Mabaraza ya Miji, hali ya makazi ya wananchi inazidi kuwa mbaya siku
hadi siku. Uhaba mkubwa wa viwanja vilivyopimwa umewalazimisha wananchi wengi kujenga
makazi kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu na ambayo hayana huduma za
msingi kama vile mitaro ya maji machafu, barabara zisizo na msongamano, vyoo vya umma,
barabara, viwanja vya kuchezea watoto na sehemu za kuzikia za uhakika. Inakadiriwa kuwa zaidi
66
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
ya asilimia 70 ya wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam wanaishi kwenye maeneo yaliyojengwa
kiholela na yenye msongamano mkubwa. Aidha hali hii imewalazimisha baadhi ya Wananchi
wengine kujenga sehemu za mabondeni na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha na mali zao
wakati wa kipindi cha mvua.
Ukosefu wa sehemu za uhakika wa wafanyabiashara ndogondogo ‘Machinga’ na uhaba wa vituo
bora vya mabasi, na maegesho rasmi kwa ajili ya vyombo vya usafiri - hususan magari, umetokea
kuwa ni kero kubwa kwa wananchi wengi hususan katika Jiji la Dar es Salaam. Pamoja na yote
haya pia kuna udhaifu mkubwa sana katika kusimamia sheria zinazotawala makazi.
Pamoja na matatizo haya, sheria ndogondogo zinazotungwa na halmashauri na mabaraza mengi
ya miji hazizingatii hali halisi ya kimaisha ya wakazi wa miji husika. Mathalani, katika baadhi
ya miji kuna sheria inayowakataza wakaazi kufanyia matengenezo nyumba zao zinazochakaa
kwa maelezo kwamba maeneo ziliko nyumba hizo yametengwa kwa ajili ya kujenga magorofa.
Matokeo ya sheria hii ni kwamba katika miji mingi kuna nyumba nyingi chakavu zinazokaribia
kuanguka huku wamiliki wake wakisubiri zianguke na wao kupoteza haki ya kumiliki viwanja
husika kwa sababu hawana uwezo wa kujenga maghorofa. Ni wazi kabisa kuwa sheria ya namna
hii siyo tu kwamba ni ya kikandamizaji, lakini pia ni yenye kuongeza kiwango cha umasikini
miongoni mwa wananchi.
Hali ilivyo sasa;
•     Shirika la nyumba la Taifa ambalo kinadharia lilianzishwa kwa malengo ya kutatua tatizo la
makazi kwa wananchi, hususani wale wanaoishi mijini limeshindwa kabisa kutimiza azma
hiyo. Kasi ya ujenzi wa majengo mapya imefifia kabisa, na majengo yake mengi ya zamani,
ikiwemo yale liliyoyarithi kutoka kwa wamiliki wake halali baada ya kutaifishwa, yako katika
hali mbaya sana kutokana na kutokuwa na uangalizi mzuri. Hivi sasa shirika hilo liko kwenye
mgogoro mkubwa na baadhi ya wapangaji wake kutokana na kupandisha kodi bila kuzingatia
hali halisi ya uboreshaji wa makazi hayo.
•     Pamoja na Serikali kubuni mradi wa viwanja elfu ishirini (20,000) katika jiji la Dar Es Salaam,
bei za viwanja hivyo ni za juu mno kwa watu wa kawaida kuweza kuzimudu. Matokeo yake
ni kwamba vingi kati ya viwanja hivyo vitaangukia katika mikono ya watu wachache wenye
uwezo, na wananchi wa kawaida (ambao ndiyo wengi) wataendelea na ujenzi holela katika
maeneo yasiyofaa.
•     Kasi ya kuboresha maeneo ya makazi amabayo hayajapimwa kwa kujenga barabara, kuweka
maeneo ya ujenzi wa shule, vituo nya afya, na viwanja vya kuchezea watoto ni ndogo mno.
Matokeo yake ni kwamba huduma muhimu, mathalan za magari ya zima moto na magari ya
wagonjwa bado ni vigumu kuwafikia wakazi walio wengi katika maeneo hayo.
•     Kuna udhaifu mkubwa katika kuandaa maeneo ya wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’
na maeneo mengine muhimu kama vituo vya mabasi ya daladala. Kutokana na hali hii kuna
baadhi ya mitaa ambayo wakazi wake wanapata adha kubwa kutokana na msongamano
mkubwa wa biashara hizo na wingi wa daladala zilizogeuza mitaa hiyo kuwa stendi za kupakia
na kushusha abiria.
•     Kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria ndogondogo zinazotawala makazi na hususan
katika maeneo ya mijini, bila ya hatua zozote kuchukuliwa.
•     Sheria katika baadhi ya miji na manispaa zinazokataza wakazi wa baadhi ya maeneo kufanyia
67
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
matengenezo nyumba zao kwa kisingizio kuwa maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi
wa maghorofa ni za udhalilishaji, zinalenga kuongeza umasikini katika jamii, na zinakiuka
haki za binadamu.
•     Serikali imeshindwa kabisa kukitangaza kitengo chake cha mradi wa utafiti wa nyumba za
bei nafuu na matokeo yake ni kwamba wananchi walio wengi hawanufaiki na kuwepo kwa
kitengo hicho.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
Ili kuboresha makazi, Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo:
•     Kubinafsisha shirika la nyumba la Taifa; Serikali ya CUF itaweka utaratibu wa kuwarejeshea
majumba yao wale wote waliokuwa wametaifishiwa na hawakulipwa fidia, na baada ya zoezi
hili italibinafsisha shirika la nyumba la Taifa.
—     Baada ya kuibinafsisha NHC Serikali ya CUF itaanzisha “Housing Banks” ili kuhamasisha
mifuko ya jamii kujiingiza katika sekta ya ujenzi wa nyumba za kuishi “ESTATE
DEVELOPMENT” kwa mikopo nafuu ya muda mrefu na mfupi kama ilivyo kwa nchi zingine
zinazoendelea kwa kasi duniani.
•     Upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa; Serikali itahakikisha kwamba katika kipindi cha miaka
miwili tu, katika miji yote nchini viwanja vilivyopimwa na vinavyopatikana kwa bei nafuu
ndivyo vitatafuta wajenzi; badala ya hivi sasa ambapo wananchi mbalimbali wenye nia ya
kujenga ndio wanaohaha kutafuta viwanja hivyo. Huduma za barabara, maji na umeme kwenye
makaazi zitakwenda sambamba na upimwaji wa viwanja vipya.
•     Uboreshaji wa mazingira ya miji; Serikali itasitisha mara moja ukiukwaji mkubwa wa sheria
za mipango miji uliopo hivi sasa. Aidha kwa kushirikiana na serikali za mitaa, serikali
itaweka mkakati imara wa kuhakikisha kuwa kila penye makazi na hasa kwenye maeneo
ambayo yamejengwa kiholela, barabara zinapitishwa, mitaro ya maji machafu inakuweko au
kufanyiwa ukarabati, vyoo vya umma vinasambazwa, taka zinazolewa kwa wakati na madimbwi
yanayotuama maji wakati wa mvua yanashughulikiwa. Serikali pia itahakikisha kuwa uhaba
wa sehemu za kuzikia, vituo bora vya mabasi, sehemu za uhakika kwa biashara za ‘Machinga’,
viwanja vya kuchezea watoto, na bustani za mapumziko unapatiwa ufumbuzi wa haraka.
•     Gharama za ujenzi; Gharama za ujenzi zitapungua kutokana na azma ya Serikali ya kurekebisha
viwango vya kodi. Serikali itakiimarisha na kukitangaza kwa nguvu zote kitengo chake cha
mradi wa utafiti wa nyumba za bei nafuu na kuwahamasisha wananchi wote- wa mijini na
vijijini – wakitumie kujengewa nyumba bora kwa gharama nafuu. Aidha katika maeneo ya
mijini makampuni zaidi yatahamasishwa kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu na
kuzigawa kwa wananchi mbali mbali kwa mikopo ya masharti nafuu.
•     Sheria ndogo iliyotungwa na baadhi ya manispaa inayowakataza wakazi wa baadhi ya maeneo
kufanyia matengenezo nyumba zao kwa madai kwamba maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya
maghorofa itafutwa.
•     Kuondoa msongamano wa magari; Kwa sababu wakazi wa miji mikubwa yote ndani ya nchi
na hasa Dar es salaam wanakumbana na tatizo kubwa la msongamano wa magari. Serikali
ya CUF itahakikisha msongamano unamalizwa kwa kuanzisha barabara mbadala (alternative
roads), kujenga madaraja ya juu (flying bridges) kwenye makutano muhimu katika miji yenye
msongamano pamoja na kupanua barabara zote za miji yenye msongamano kutoka kwenye
“single roads” njia moja hadi kuwa njia mbili.
68
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
•     Lakini kubwa zaidi ni kuhakikisha kuwa barabara zote za miji mikubwa zinawekewa mfumo
wa taa ili kuwawezesha watu kufanya shughuli zao muda wote bila kuhofia usalama wao.
MAENDELEO YA MAKUNDI YA KIJAMII
Wenye Ulemavu;
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya la Dunia, katika kila watu kumi ulimwenguni mmoja
ana ulemavu. Kwa kuwianisha, hii ina maana kwamba asilimia 10 ya Watanzania wote, yaani
watu 4,200,000 wana ulemavu wa aina moja ama nyingine. Kwa mtizamo wa aina yoyote ile
idadi hii ni kubwa mno kiasi cha kuhitajika mipango maalum ya kuwahudumia.
Hali ilivyo sasa;
—    Baada ya miaka 49 ya uhuru
taifa letu bado halina sera sahihi
inayowalenga wenye ulemavu
kuwahakikishia kuwa wanapata
fursa sawa katika masuala yote
yanayoihusu jamii.
—    Mchakato mzima wa uendeshaji
masuala mbalimbali ni wenye
kuwabagua na kuwapuuza wenye
ulemavu. Juhudi za makusudi
zinazofanywa kuwaondolea wenye
ulemavu vikwazo mbalimbali
wanavyokabiliana navyo hata
pale ambapo mazingira ya
kufanya
hivyo
yanaruhusu
hazijitoshelezi.
—   
Serikali imeshindwa kujenga
mazingira mazuri kushughulikia ulemavu unaoepukika na ule unaoweza kupunguzwa
makali yake.
—     Serikali imeshindwa kutekeleza sheria namba 2 na namba 3 za mwaka 1982 zinazolinda
ajira na matunzo kwa watu wenye ulemavu. Aidha Serikali ya CCM imeshindwa kutekeleza
maazimio mbalimbali likiwemo lile la Umoja wa mataifa namba 149 la mwaka 1982
linalohusu wenye ulemavu pamoja na Muongo wa watu wenye ulemavu 2000 - 2009
(African Decade). Ingawa Bunge la mwaka huu lilipitisha Sheria kwa watu wenye ulemavu
nchini lakini limeshindwa kukidhi mahitaji mengi muhimu kwa kundi hili ikiwemo
ushirikishwaji kamilifu katika maamuzi ikiwa ni moja ya mambo matatu yaliyoridhiwa na
Serikali katika (African Decade).
Dira ya Mabadiliko ya CUF kwa watu wenye ulemavu;
CUF inatambua kuwa ni vigumu kupata ufumbuzi muafaka wa matatizo ya wenye ulemavu
bila kuwashirikisha kikamilifu. Aidha inatambua kuwa ukiondoa ulemavu wa kuzaliwa, kuna
aina nyingi za ulemavu zinazoepukika iwapo hatua sahihi na za makusudi zitachukuliwa. Kwa
69
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
kuzingatia utambuzi huu Serikali ya CUF itafanya yafuatayo;
•     Kwa kushirikiana na wadau husika Serikali itaandaa na kupitisha sera ya kitaifa itakayojulikana
kama ‘EQUALISATION OF OPPORTUNITIES POLICY’ ambayo pamoja na mambo mengine
itasimamia kikamilifu ushiriki wa wenye ulemavu katika masuala yahusuyo Utawala, Siasa,
Ajira, Afya, Elimu, Na Michezo.
•     Serikali itahakikisha kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo watu wenye
ulemavu wenyewe kupitia upya sheria mbalimbali zinazokwaza haki za kundi hilo na kupitia
upya sheria namba 2 na namba 3 za mwaka 1982 kuhusu ajira na matunzo kwa watu wenye
ulemavu ili kuziboresha kabla ya utekelezaji kamilifu, na pia kuhakikisha maridhio yote ya
kimataifa ya haki za watu wenye ulemavu yanatekelezwa ipasavyo.
•     Serikali itasimamia kikamilifu kuhakikisha kuwa mazingira mbalimbali yanayosababisha
ulemavu unaoepukika yanadhibitiwa. Hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na:
—     Kudhibiti kikamilifu usalama katika viwanda, migodi, na maeneo mengine. Kutakuwa na
sheria inayoagiza kuwepo na sera ya ndani inayosimamia usalama ambayo pamoja na
mambo mengine itajumuisha na ukaguzi wa kila siku wa usalama wa mazingira ya kazi
(safety audits).
—     Kudhibiti kikamilifu ubora wa madereva na vyombo vya abiria, na njia vinakopita vyombo
hivyo ili kupunguza ajali.
—     Kutengeneza mazingira rafiki yatakayowasaidia sana wenye ulemavu kuzifikia huduma
bila kutegemea msaada, kwa mfano kutengeneza njia maalum wanazoweza kupita wakiwa
katika hospitali, shule, vituo vya mabasi na sehemu nyingine za utoaji huduma kwani
sehemu zote hizi zimejengwa bila kujali kuwa kuna walemavu, mfano mzuri ni pale
majengo yanapowekewa ngazi peke yake bila kukumbuka kuwa wenye ulemavu wa miguu
hawataweza kupita.
•     Serikali itasimamia kikamilifu kuhakikisha kuwa hatua muafaka za kitabibu zinachukuliwa
kushughulikia ulemavu unaopunguzika;
—     Utoaji bure wa viungo bandia, baiskeli za magurudumu matatu, vifaa vya kusikilizia
(hearing aid devices), miwani ya jua, mafuta maalumu ya ngozi na vifaa vingine.
—    Kupitisha sheria inayoelekeza kuwa watoto wote wanaozaliwa wakiwa na athari
zinazorekebishika wanapatiwa matibabu bila kuchelewa.
—     Kujenga makazi maalum ambapo wenye ulemavu wa ngozi wanaoishi katika familia au
maeneo yasiyo na ulinzi mzuri wa kijamii wataweza kuishi mahali salama kwa maisha yao.
Wanawake
Ingawa wanawake ni asilimia 51 ya wananchi wote wa Tanzania, mila na desturi, matatizo
ya kihistoria na uzembe wa muda mrefu wa Serikali vimesababisha kuwe na tofauti kubwa
ya kifursa kati ya Watanzania wanaume na Watanzania wanawake. Kipaumbele katika fursa
zinazogusa masuala mengi muhimu katika jamii kimekuwa kikitolewa kwa wanaume zaidi.
Hali hii imewajengea wanawake kutojiamini iwe ni katika masuala ya uongozi, elimu, kazi, na
hata katika masuala ya kifamilia. Kwa upande mwingine, hali hii imewajengea wanaume wengi
mtizamo hasi juu ya uwezo wa wanawake. Wanaume wengi waliokumbatia mila na desturi, na
hasa wale ambao hawakubahatika kupata elimu ya kutosha wamejenga mazoea ya kuwachukulia
wanawake kama viumbe duni na wasiokuwa na mchango wowote kifikra zaidi ya kuzaa watoto,
kutafuta mahitaji ya familia, na kuwatumikia wanaume. Kwa muda sasa kumekuwa na juhudi
70
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
za makusudi na hasa kutoka kwa kina mama wenyewe zenye kulenga kujaribu kurekebisha hali
hii. Sehemu kubwa ya juhudi hizi zimelenga zaidi katika kuhimiza kuwe na upendeleo maalum
kwa wanawake. Pamoja na uzuri wa jitihada hizi, ni dhahiri kuwa hazitoshi na bado kazi kubwa
inahitajika kufanyika ili hatimaye tofauti za kijinsia zisiwe ni tatizo tena katika upatikanaji wa
fursa za kujiletea maendeleo.
Maendeleo duni ya wanawake nchini;
•     Kuna mapungufu juu ya kubuni mbinu sahihi zitakazotuhakikishia kuwa matatizo ya ubaguzi
dhidi ya wanawake katika upatikanaji wa fursa yanapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
•     Kuna mapungufu juu ya kuielimisha jamii katika ngazi zote juu ya umuhimu wa kukumbatia
haki sawa kwa jinsia zote na hivyo kuwa ni kikwazo katika kuwaendeleza wanawake.
•     Pamoja na uwakilishi walionao hivi sasa wanawake katika bunge – ikiwa ni pamoja na kuwepo
kwa nafasi za viti maalumu za wanawake - ushiriki wao mdogo katika vyombo mbalimbali
vya kutoa maamuzi, unaonyesha kuwa bado hakuna nia ya dhati ya kuleta usawa wa kijinsia
katika jamii. Hali hii isingetarajiwa ikizingatiwa kuwa hivi sasa idadi ya wanawake wenye
elimu ni kubwa inayotosheleza kuweka uwiano mzuri wa kijinsia katika vyombo mbalimbali
vya maamuzi.
•     Pamoja na kuwepo kwa mifuko mbalimbali kwa ajili ya mikopo ya wanawake, uendeshaji wa
mifuko hiyo ni wa kisiasa zaidi na hivyo kufanya wanawake walio wengi, hasa wa vijijini
wasinufaike na mikopo hiyo. Benki ya wanawake ndiyo imezinduliwa mwaka huu 2010 na ipo
Dar es Salaam pekee.
•     Wanawake wanakabiliwa na tatizo kubwa mno la afya ya uzazi, huduma za uzazi kutozwa
fedha, ukosefu wa lishe bora wanapokuwa wajawazito na majukumu ya malezi ambapo vifo
vya akinamama na watoto limekuwa ni jambo lililozoeleka sana na kuonekana ni kitu cha
kawaida katika jamii ya watanzania.
•     Huduma duni ya maji. Wanawake wamekuwa wakitaabika sana katika kutafuta huduma ya
maji na kutembea kwa mwendo mrefu, katika maeneo ya vijijini wakati mwingine hulazimika
kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 10 kufuata maji baada ya miaka 49 ya uhuru.
•     Mfumo wa elimu uliopo nchini haumuandai mtoto wa kike kuweza kukabiliana na majukumu
ya kijamii.
Dira ya Mabadiliko ya CUF;
Msingi mkuu wa sera za CUF ni ‘Haki sawa kwa wote’. Hii inamaanisha kwamba pamoja na CUF
kutambua tofauti za makundi mbalimbali ya watu katika jamii, inayatambua makundi yote
kuwa ni sawa kutokana na uwananchi wa kila kundi. Wanawake na wanaume ni makundi yenye
kutegemeana na hakuna linaloweza kuwa endelevu bila ya jingine. Kwa maana hii basi mfumo
Dume uliojikita katika kila nyanja ya maisha nchini ni kikwazo cha maendeleo ya taifa letu. Sera
za chama chetu kuhusu elimu, afya, na kuondoa umasikini kama zilivyoainishwa katika ilani
hii ni kichocheo kikubwa katika suala zima la ukombozi wa mwanamke wa Kitanzania. Lakini
pamoja na sera hizi nzuri, Serikali ya CUF pamoja na mambo mengine itachukua hatua zifuatazo
ili kuboresha mazingira ya kujenga usawa wa kijinsia katika uwiano unaofaa:
—     Itatunga sheria itakayotoa adhabu kali kwa mtu yeyote atakayetumia mamlaka yake kumd-
halilisha kijinsia, na kumsababishia madhara ya namna moja ama nyingine Mtanzania mwe-
nye jinsia tofauti na ya kwake; ili kujinufaisha binafsi kwa njia moja ama nyingine. Pamoja
71
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
na manufaa ya sheria hii katika maeneo mengine, sheria hii itasaidia hasa katika suala zima
la kupambana na rushwa ya ngono, hususani kwa wanafunzi na waajiriwa wa kike.
—     Itauboresha utaratibu ulioko hivi sasa ambao unatoa nafasi maalum za upendeleo kwa
wanawake ili kuongeza ushiriki wao katika ngazi mbalimbali za maamuzi ya kisiasa,
utawala, menejimenti na uongozi.
—     Ili kuwanyanyua wanawake kiuchumi Serikali ya CUF itaiimarisha mifuko mbalimbali ya
mikopo na kuisimamia kusudi iwanufaishe wanawake walio wengi wa mijini na vijijini bila
kujali itikadi zao za kisiasa.
—     Serikali ya CUF itawaunganisha wanawake wote bila kujali itikadi zao, kuunda chombo
chao huru ambacho kitasimamia maslahi yao.
—     Hata hivyo kwa kuwa CUF inaelewa fika kuwa suluhisho la kudumu la matatizo ya kijinsia
nchini liko katika kubadilisha mitizamo ya jamii kuliko katika kuweka mashinikizo ya
kisheria na kutoa upendeleo, basi hatua zifuatazo za ziada zitachukuliwa:
•     Kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa wasichana wanaosoma katika shule za peke yao mara
nyingi wanajenga kujiamini kuliko wale wanaosoma katika shule mchanganyiko, Serikali
itahakikisha kuwa kunakuwa na marekebisho katika mashule ili kupata manufaa ya kitaaluma
yanayotokana na utafiti huo.
•     Mitaala ya somo la uraia mashuleni itafanyiwa marekebisho ili pamoja na mambo mengine
somo hilo lilenge katika kufifisha mitizamo ya vijana wa kiume dhidi ya wenzao wa kike kuwa
ni viumbe duni, dhalili, na wasio na mchango wowote wa maana kifikra katika jamii.
•     Serikali itaanzisha na kuhimiza mjadala wa kina na wa wazi kitaifa katika ngazi mbalimbali
za jamii kuhusu mgawanyo wa wajibu, majukumu, na haki katika mahusiano ya kijinsia, kwa
nia ya kuboresha mahusiano hayo.
•     Mkakati maalumu wa kitaifa wa kuwainua wanawake kiuchumi ili waondokane na madhara mbal-
imbali wayapatayo kutokana na umasikini utaasisiwa kwa kuwashirikisha wanawake wenyewe.
Vijana
Vijana ndiyo kundi lenye mchango mkubwa katika uzalishaji kuliko kundi jingine lolote, na kwa
maana hiyo umuhimu wa kundi hili kwa jamii ni mkubwa mno.
Hali ilivyo sasa;
•     Kauli mbiu ya vijana ni taifa la kesho imepelekea kundi la vijana kuendelea kusubiri bila
mafanikio. Sehemu kubwa ya vijana hawana fursa za ajira za kueleweka kitu ambacho
kinawasababisha walio wengi kujikuta wakilazimika kuingia katika vitendo viovu kupambana
na umasikini unaowakabili. Vijana wengi wamekata tamaa mno kiasi kwamba wanadhani
kwamba njia pekee iliyobaki ya kujiletea maendeleo ni wao kuondoka nchini au kutafuta
biashara za kufaida kubwa za haraka hata ikiwa ni haramu, kama kuuza madawa ya kulevya,
kujihusisha na biashara za magendo, nakadharika. Kwa kweli hali hii haiashirii mazingira
mazuri kwa maendeleo ya nchi na juhudi za kuondoa umasikini. Vijana wamekuwa wakitumika
katika kufanikisha malengo ya wanasiasa wakati wa uchaguzi pekee na hakuna sera sahihi za
kuwainua vijana kushiriki katika kustawisha maendeleo ya taifa.
•     Vijana wengi wapo vijiweni na wengine wamejiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya na
ulevi wa kupindukia, uvutaji wa bangi na kwa kiwango kikubwa si wenye uwezo wa kuajirika
72
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
kutokana na kwamba hawajaandaliwa vya kutosha kumudu ushindani wa soko la ajira katika
karne hii ya sayansi na teknolojia.
Dira ya Mabadiliko ya CUF kwa vijana nchini;
•     Elimu; Pamoja na azma ya CUF kuhakikisha kuwa kila kijana anapata elimu ya darasani (formal
education) kwa upeo wa uwezo wake, Serikali ya CUF itachukua pia hatua zifuatazo:
—     Itaongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi katika maeneo
yote ya nchi kwa lengo la kuwashawishi vijana walioshindwa kuendelea na mfumo wa
masomo ya darasani kujipatia ujuzi mbalimbali wa ufundi.
—     Itaanzisha huduma ya ushauri nasaha kuhusu chaguo la ajira na matatizo ya kijamii ili
kukabiliana na matarajio ya vijana.
—     Serikali ya CUF itahakikisha vijana wote wanaojifanyia biashara ndogondogo maarufu
kama ‘wamachinga’ wanapewa maeneo maalum ya uhakika na yenye mzunguruko wa
kibiashara kufanya shughuli zao bila kubughudhiwa. CUF itazuia kabisa utaratibu wa
mgambo kuwapiga na kuwanyanyasa vijana wanaofanya biashara ndogondogo.
•     Afya; Pamoja na azma ya CUF kuhakikisha kuwa kunakuwa na mkakati unaoigusa jamii nzima
katika kuhakikisha kuwa afya za wananchi zinaboreshwa, Serikali ya CUF pia itachukua hatua za
kuanzisha programu zitakazohusisha makundi ya vijana katika ngazi ya mtaa na kitongoji kwa
kushirikiana na asasi mbalimbali kuelimishana juu ya njia bora za kuepukana na maambukizo
ya ukimwi, Tatizo la matumizi ya dawa za kulevya na njia za kuepukana nazo.
•     Utamaduni na michezo; Pamoja na azma ya CUF kuhakikisha kuwa kunakuwa na mkakati unaoi-
gusa jamii nzima katika kuhakikisha kuwa viwango vya ubora wa ushiriki wa Taifa letu katika
medani za michezo na burudani vinapanda, Serikali ya CUF pia itachukua hatua zifuatazo:
—     Itaboresha huduma za burudani na michezo vijijini na mijini kwa kushirikisha wataalamu
wa fani mbalimbali katika medani hizo ili kusaidia kutambua vipaji na kuviendeleza.
—     Itashawishi ushiriki zaidi wa sekta binafsi katika kuwekeza katika huduma za burudani
na michezo.
—     Itashawishi vijana kuwa mstari wa mbele kuendeleza yale yote mazuri yanayopatikana
katika tamaduni zetu, na kupiga vita tamaduni mbaya za kigeni.
—     Itashawishi vijana kushiriki kwa hiari yao katika harakati mbalimbali za kijamii kama vile
uboreshaji wa mazingira na kuwasaidia wagonjwa, watoto, wazee, na mayatima.
•     Utumishi wa Taifa; Madhumuni makubwa ya uanzishwaji wa makambi ya JKT yalikuwa ni
kutoa mafunzo ya awali ya ulinzi na uchapakazi kwa vijana ili kuwatayarisha kwa maisha
yao ya baadaye. Lakini ni dhahiri kuwa kiutendaji madhumuni haya yalivurugwa kwani
wale ambao kweli wanahitaji mafunzo ya awali ndio ambao hawakulazimika kushiriki na
wale ambao walikuwa na uhakika wa ajira ndio waliolazimika kujiunga. Waliosamehewa ni
wale wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne bila kujiunga na chuo chochote, wakati
waliolazimika ni wale waliomaliza Kidato cha sita ama wenye elimu ya juu zaidi. Ni wazi basi
kuwa mfumo uliotumika haukuwa na tija.
Pili, uendeshaji wa programu mbalimbali katika makambi hayo ulilenga zaidi katika kukomoana
na kudhalilishana na hivyo matumizi ya akili yalizingatiwa kwa kiwango kidogo. Haishangazi basi
kuwa makambi ambayo kimsingi yalitakiwa yawe na uwezo wa kuzalisha kwa ajili ya kujiendesha
na ziada, hatimaye yalionekana kuwa ni yenye kuliingizia taifa hasara kubwa na kulazimika
kusitisha sehemu kubwa ya programu zake – hususan ile ya kuwachukua vijana kwa mujibu wa
73
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
sheria. Hata hivyo bado umuhimu wa utumishi kwa taifa upo ila kinachohitajika ni marekebisho
ya msingi. Serikali ya CUF itachukua hatua zifuatazo ili kuleta marekebisho yenye tija:
—     Utaratibu wa uendeshaji wa programu kwenye vituo hivi utabadilika ili kuondoa dhana
kwa vijana, wazazi, na watoa mafunzo kuwa hivyo ni vituo vya ‘mateso’ kwa vijana
wanaomaliza masomo yao. Katika kutekeleza azma hiyo, kwanza kabisa muundo wa
awali utabadilishwa na badala ya kujulikana kama makambi sasa yataitwa ni ‘vituo vya
maandalizi kwa vijana ili kulitumikia taifa’.
—     Itatenganisha kabisa masuala ya uajiri, fursa za masomo na suala la kujiunga na vituo hivi.
Itavifanya vituo hivi kuwa ni huduma muhimu ya miaka miwili katika kutoa mafunzo ya
awali ya kijeshi, ukakamavu, kazi za uzalishaji (Vocational Training), lugha za kiingereza,
huduma ya mwanzo (First Aid), sanaa mbalimbali, udereva, michezo, pamoja na stadi
zinazohusiana na shughuli za uokoaji (Rescue Operations).
—     Itatoa ruzuku mwanzoni wakati wa maandalizi, na mikakati itawekwa kukiwezesha kila
kituo kiwe kinajiendesha chenyewe.
—     Itaweka vituo katika kila mkoa kwa ajili ya uandikishaji wa wale wote ambao wangependa
kujiunga na vituo hivi na itawashauri vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne
na kukosa nafasi ya kuendelea na masomo katika shule za kawaida na vyuo wajiunge.
—     Itaweka utaratibu kuhakikisha kwamba fedha zote zitakazozalishwa na vijana kutokana
na miradi mbalimbali ya uzalishaji baada ya kuondoa gharama za kuendeshea kambi
inayohusika zinahifadhiwa kwa ajili ya kupewa vijana wakati wa kuhitimu ili ziwasaidie
kununulia zana mbali mbali zinazohusiana na stadi walizojifunza.
•     Ajira; Mapinduzi ya kilimo na uanzishwaji wa viwanda utaongeza ajira ya vijana katika sekta
rasmi. Pia serikali ya CUF itahakikisha kuwa vijana wanatumia kikamilifu fursa ya kuwepo kwa
mifuko ya mikopo ya masharti nafuu (Incubator Funds) ambayo serikali itaianzisha kwa kila
sekta ya uzalishaji mali, kupata mikopo kwa madhumuni ya kujiajiri.
Wazee na Wastaafu.
Wazee wa Tanzania wamejenga historia kubwa kwa kulifikisha taifa hapa lilipo lakini wao ndio wa-
naoishi maisha magumu kupita kiasi na hadi sasa Serikali haijafanya juhudi za dhati kuwasaidia.
Ajenda ya CUF kwa wazee na wastaafu;
Serikali ya CUF itafanya mambo yafuatayo ili kuimarisha maisha ya wazee na wastaafu;
•     Itaboresha pensheni ya wastaafu katika sekta zote ili kukidhi mahitaji yao.
•     Itawalipa wastaafu wote malimbikizo ya madeni wanayodai ili kuondoa mvutano uliodumu
kwa miaka mingi kutokana na dhuluma waliyofanyiwa.
•     CUF itawapatia wazee huduma muhimu za kijamii bila malipo na urasimu wowote.
•     Itaanzisha utaratibu wa kuwalipa pensheni wazee wote. Kwa kuanzia tutaanza na miradi ya
mifano (pilot projects) kabla ya kusambaza huduma hii kwa wazee wote.
Ustawi wa Watoto nchini;
Serikali ya CUF itawekeza rasilimali nyingi katika kuhakikisha watoto wanajengewa mazingira
thabiti yatakayowawezesha kukua vizuri kimwili na kiakili. Itawekeza katika maeneo muhimu
yanayolinda utu na heshima ya mtoto miongoni mwa masuala ya msingi yatakayosimamiwa na
serikali ya CUF ni;
74
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
—     Kuunda, kusimamia na kuwezesha kitengo maalum huru kitakachokuwa na kazi ya kuishauri
serikali juu ya nini kifanywe kuboresha mazingira mazuri katika ukuaji wa watoto.
Kitengo husika kitaundwa kwa kujumuisha asasi mbalimbali za kijamii zinazojihusisha na
utetezi wa haki za watoto. Serikali ya CUF itaanzisha na kusimamia mambo yote muhimu
yatakayoshauriwa na kitengo hiki.
—     Kuokoa maisha ya watoto dhidi ya majanga mbalimbali, na kuhamasisha upatikanaji wa
lishe bora kwa watoto.
—     Kutengeneza mifumo mizuri ya usafi wa maji na afya kwa ujumla katika shule wanazosoma
na kuwaandaa kwa kuwapatia elimu bora.
—     Kuhakikisha kuwa watoto wadogo na watoto wa kike wanalindwa dhidi ya maambukizi ya
VVU na kudhibiti upatikanaji wa mimba kwa watoto wakiwa na umri mdogo.
—     Kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum (wenye ulemavu).
Wataalamu
Tanzania haitaweza kupiga hatua za maendeleo iwapo wataalam hawatapewa kipaumbele katika
nyanja mbalimbali. Nchi yetu ina wataalam wengi katika sekta za uchumi, sekta za kijamii
na kiutamaduni lakini bado hatujaweza kuwatumia ipasavyo katika kuwakomboa watanzania
kutoka katika dimbwi la umasikini, ujinga, maradhi na mengine.
Dira ya Mabadiliko ya CUF kwa Wataalamu wa fani mbalimbali;
•     CUF itaanzisha tuzo maalum kwa ajili ya wataalam wote waliofanya kazi muhimu ya kitaalam
na ikaleta tija kwa nchi.
•     Itawapa uhuru wa kujianzishia vyama vya kitaaluma na klabu mbalimbali ili wakutane mara
nyingi kadri wawezavyo katika wilaya zao na kujadiliana mambo na mbinu mbalimbali ili
kuinua taaluma yao kulingana na asili ya maeneo waliyopo.
•     Itawapeleka wataalam wengi nje ya nchi kadri iwezekanavyo ili wakaongeze taaluma zao
kwa maslahi ya nchi. Hivi sasa wataalam wanaopelekwa nje ya nchi kuongeza mafunzo ya
kitaalam ni wachache na hakuna uzingatiaji wa vigezo sahihi katika kuwateua.
•     Itawaongezea vivutio zaidi na kuboresha maslahi yao kiutendaji ili wataalam wetu wasiichoke
kazi yao muhimu katika kuleta maendeleo ya kweli katika nchi.
MICHEZO NA BURUDANI
Hali ya michezo na burudani nchini imekuwa siyo nzuri kwa muda mrefu sasa. Viwanja vyetu vya
michezo vilivyoko katika mikoa yote vina hali mbaya sana, ahueni iko katika viwanja viwili tu
vya Dar es salaam, ni uwanya mpya wa Taifa na ule wa uhuru na wawakilishi wetu mbalimbali
kwenye michezo ya kimataifa wanaendelea kufanya vibaya kila mara. Pamoja na juhudi kubwa
za makampuni ya biashara kama NMB na mengine kufadhili kwa kiasi kikubwa gharama za timu
zetu za taifa na vilabu bado pamekuwa na tatizo kubwa la serikali kutokuwa na usimamizi mzuri
katika michezo. Aidha kumekuwa na udhaifu mkubwa katika kulinda haki na maslahi ya wasanii
mbalimbali na kuwasaidia ili waweze kunufaika ipasavyo na kazi zao hali ambayo imepelekea
kazi zao kuchapishwa hovyo mitaani huku wao wakibakia masikini na wajanja kunufaika na hali
hiyo, bila kupata msaada stahiki kutoka kwa mamlaka husika.
Hali ilivyo sasa katika sekta ya Michezo nchini;
•     Serikali ya CCM imekuwa na mtizamo wa kizamani kuhusu michezo, yaani kama suala la watu
75
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
binafsi badala ya suala la jamii nzima. Kutokana na mtizamo huu imeshindwa kabisa kuona
jinsi ambavyo michezo imekuwa ikibadilika taratibu kutoka kuwa ni burudani tu na kuwa ni
biashara kubwa inayohusisha mamilioni ya dola.
•     Kumekuwa na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kisingizio cha kuhudumia masuala ya
michezo, burudani na dini wakati katika hali halisi hakuna huduma kama hizo zinazotolewa.
•     Juhudi za kuendeleza vipaji vya vijana hazijawekewa mikakati inayopimika na yenye kuzaa
matunda.
•     Viwanja karibuni vyote vilivyojengwa kwa nguvu ya wananchi baada ya uhuru vimechukuliwa
na kumilikishwa Chama cha mapinduzi na hivi sasa vipo katika hali mbaya, havina ukarabati
wala uboreshaji wa kuviendeleza viwanja hivyo.
•     Vifaa vya michezo vimekuwa vya gharama za juu sana kiasi cha waliowengi kushindwa
kuvinunua na kutumia vifaa vya kisasa vya michezo kwa madhumuni ya kujenga afya njema.
•     Serikali ya CCM imeshindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo katika kulinda na kuendeleza haki
za wasanii.
Dira ya Mabadiliko ya CUF katika sekta ya michezo;
Ili kuboresha mazingira ya michezo nchini na kuhakikisha kuwa viwango vya uchezaji vya
wanamichezo wetu vinakua na kufikia ngazi ya ushindani wa kimataifa, Serikali ya CUF itachukua
hatua zifuatazo:
•     Uboreshaji wa viwanja vya michezo; Serikali itahimiza ujenzi wa viwanja vipya vya michezo na
uboreshaji wa vile ambavyo tayari vipo. Jukumu la kukamilisha azma hii litakabidhiwa kwa maba-
raza ya manispaa, miji na halmashauri za Wilaya ambapo kila mkoa utapaswa kujenga uwanja
mkubwa wa michezo yote, kila manispaa itapaswa kujenga kiwanja kimoja kikubwa kitakacho-
tumika kwa michezo yote huku Serikali kuu ikiwa na jukumu la kujenga viwanja vya kimataifa
na kisasa vinne vyenye uwezo wa kutumika kwa michezo yote mikuu.Viwanja hivyo vitajengwa
katika kanda ya kusini, kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini na kanda ya kati. Pamoja na vyanzo
vingine vya fedha, mamlaka hizi zitatafuta wabia wa kushirikiana nao kukamilisha jukumu hilo.
•     Kuzuia maeneo ya wazi; Serikali ya CUF itahakikisha kuwa maeneo yote ya wazi yanatunzwa
ipasavyo huku yale mengi
yaliyouzwa katika mazingira
tata yanashughulikiwa.
•     Kuongeza ushindani katika
michezo;
Ili
kuongeza
ushindani
zaidi
katika
michezo
Serikali
kwa
kushirikiana na vyama vya
michezo mbalimbali itabuni
mashindano ya ziada nje
ya ligi za kawaida ikiwa
ni pamoja na kutafuta
wadhamini wa uhakika wa
kudhamini mashindano hayo
katika ngazi za wilaya, mkoa
na Taifa.
76
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
•     Ajira ya michezo; Ili wanamichezo waweze kushindana kikamilifu taifa halina budi kukubali
kuwa Mabadiliko ya msingi ni lazima yafanyike katika sekta ya michezo ili wanamichezo
wetu waweze kuitegemea michezo wanayocheza kama ajira. Serikali itawatumia wataalamu
mbalimbali wa masuala ya michezo ili kupata mkakati bora wa kuasisi Mabadiliko hayo.
•     Kuimarisha mafunzo ya michezo; Hivi sasa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam kinatoa mafunzo ya
elimu ya michezo katika kitivo chake cha elimu. Wahitimu wa mafunzo haya wanatarajiwa kuwa
waalimu wa michezo mashuleni. Hata hivyo wahitimu hawa ni wachache sana ikilinganishwa na
mahitaji. Serikali ya CUF itapanua zaidi idara inayohusika na mafunzo haya na kuongeza idadi
ya wanafunzi wa fani ya michezo. Aidha itayaimarisha mafunzo yanayotolewa ili yalenge katika
kutoa wahitimu bora zaidi. Katika kuendeleza vipaji vya wachezaji wadogo wa michezo mbalimbali
Serikali itajenga shule za sekondari kadhaa za mchepuo wa michezo. Shule hizi zitakuwa vituo
muhimu vya kuwaandaa wawakilishi wetu mbalimbali katika michezo ya kimataifa.
•     Huduma kwa timu za Taifa; Serikali ya CUF itahakikisha kuwa timu za taifa zinazojiandaa kwa
mashindano mbalimbali ya kimataifa zitakuwa chini ya udhamini wa Serikali. Aidha Serikali
ya CUF itachukua hatua za makusudi na kuweka mkakati mahsusi kwa kushirikiana na TFF
kuhakikisha kuwa timu ya Taifa ya mpira wa miguu inashiriki mashindano ya kombe la Afrika
na kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.
•     CUF itawapeleka nchi za nje vijana wengi wenye vipaji vya michezo mbalimbali ili wakajifunze
michezo katika vituo vya michezo (Sports Academy) huku wakiendelea na masomo. Vijana hao
watarudishwa baadaye ndani ya nchi ili waweze kuwa walimu wazuri wa michezo nchini.
•     Kuwasaidia Wasanii; Serikali ya CUF itaziunga mkono kikamilifu juhudi za wadhamini
mbalimbali ambao wanajitokeza kukuza vipaji vya wasanii na kuwaendeleza. Aidha Serikali
itafanya marekebisho mbalimbali ya kisheria ili kulinda kikamilifu haki za wasanii wetu baada
ya kukutana nao na kukubaliana juu ya njia sahihi za kudhibiti wizi wa kazi za wasanii na
kutunza kazi zao ili ziwanufaishe.
Imetolewa na Baraza kuu la Uongozi la Taifa,
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-Chama Cha Wananchi)
Imezindiuliwa Peacock Hotel, Dar es Salaam. August 26, 2010
77
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
Makadirio ya Bajeti (Mapato na Matumizi) ya Serikali itakayoundwa na CUF 2010-2016
katika sekta za muhimu Kilimo, Miundo Mbinu, Elimu, Nishati, Afya, Maji, Na Mawasiliano kwa
mwaka wa fedha 2011-2016.
Makadirio ya Pato la Taifa na Bajeti 2008/09 – 2015/16 bilioni shilingi
2008/09 2009/10 2011/12
Halisi
Halisi
Pato la Taifa kwa Bei za Soko 26497.2 29764.3 37012.4
Mapato ya ndani
4293.1
4568.4
7217.4
Jumla ya Matumizi
6811.8
8639.1
9189.9
Matumizi ya Kawaida
4681.5
5813.7
5513.9
Matumizi ya Maendeleo
2130.4
2825.4
3676.0
Nakisi
-2518.8 -4070.7 -1972.5
Ukuaji halisi wa uchumi (%)
6.7
6.0
7.3
Mfumko wa bei wa PLT (%)
9.2
6.3
4.5
Mgao wa matumizi ya serikali Kisekta bilioni shilingi
Elimu
1341.9
1624.1
2021.8
Afya
790.2
898.5
1102.8
Kilimo
327.0
622.0
919.0
Miundombinu
1410.0
1606.9
2757.0
Jumla ndogo
3869.1
4751.5
6800.5
Mengine
2942.7
3887.6
2389.4
Mgao wa matumizi ya serikali Kisekta Asilimia (%)
Elimu
19.7
18.8
22
Afya
11.6
10.4
12
Kilimo
4.8
7.2
10
Miundombinu
20.7
18.6
30
Jumla ndogo
56.8
55
74
Mengine
43.2
45
26
2012/13 2013/14 2014/15 2015/16
Makadirio ya CUF
41551.7 46965.6 53430.8
8310.3
9862.8 11754.8
10295.2 11636.6 13238.4
6177.1
6981.9
7943.1
4118.1
4654.6
5295.4
-1984.8 -1773.8 -1483.7
7.8
8.5
9.3
4.5
4.5
4.5
61053.5
14042.3
15127.1
9076.2
6050.8
-1084.8
9.8
4.5
2470.8 2909.1 3309.6 3781.8
1441.3 1745.5 1985.8 2269.1
1235.4 1629.1 1985.8 2269.1
2573.8 2909.1 3309.6 3781.8
7721.4 9192.9 10590.8 12101.7
2573.8 2443.7 2647.7 3025.4
24 25 25 25
14 15 15 15
12 14 15 15
25 25 25 25
75 79 80 80
25 21 20 20
Pato la Taifa na Bajeti 2008/09 - 2010/11 trilioni shilingi
Pato la Taifa kwa Bei za Soko
Mapato ya ndani
Jumla ya Matumizi
Matumizi ya Kawaida
Matumizi ya Maendeleo
Nakisi
Ukuaji halisi wa uchumi (%)
Mfumko wa bei wa PLT (%)
Mapato ya ndani % PLT
Jumla ya Matumizi % PLT
Nakisi % PLT
78
2008/09
26.5
4.3
6.8
4.7
2.1
-2.5
6.7
9.2
16.2
25.7
-9.5
2009/10
29.8
4.6
8.6
5.8
2.8
-4.1
6.0
6.3
15.3
29.0
-13.7
2010/2011
33.1
6.2
11.6
7.8
3.8
-5.4
6.5
4.8
18.6
35.1
-16.4
79
MANIFESTO YA CUF YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010
Dira ya Mabadiliko – CUF – Vision for Change
The Civic United Front
(CUF – Chama Cha Wananchi)
P.O. Box 10979
Dar es Salaam
Tanzania
www.hakinaumma.wordpress.com
80

No comments:

Post a Comment