Tuesday, September 29, 2009

MALINYI- HOJA SI BUNGE JAMANI, AGENDA IWE NI MAENDELEO.........

jumapili, 22 juni 2008
Pekua Tovuti
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari


Ulanga wadai wilaya kwa Pinda


na Hellen Ngoromera


WANANCHI wa Jimbo la Ulanga Magharibi, wamemwandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakimwomba kuharakisha kuwapatia majibu ya ombi lao la kuanzishiwa wilaya mpya waliyopendekeza iitwe Malinyi.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba mdc/06-08/wilaya/1 ya Juni 18, mwaka huu iliwasilishwa na kamati ya kusimamia suala hilo iliyo chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti Norbert Nongwa.

Katika barua yao, walimwomba Waziri Mkuu Pinda kuwahoji Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Saidi Kalembo na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Dk. Ramadhani Lutengwe na watendaji wengine waliodai wanazembea kutekeleza baadhi ya maamuzi ya msingi yakiwemo ya kupandisha hadhi ya eneo hilo kuwa wilaya.

“Maamuzi hayo ni pamoja na kuanzishwa kwa tarafa za Malinyi, Ruaha na Mwaya na kupandisha hadhi vitongoji vya Lupunga na Madabadaba kuwa vijiji vipya,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Nongwa.

Kwa mujibu wa Nongwa, kabla ya kuwasilisha barua hiyo kwa Waziri Mkuu, Juni 8 mwaka huu, umoja wa wananchi wa Ulanga Magharibi, ulifanya kikao cha miwsho katika Ukumbi wa TCC Chang’ombe kilichojadili suala hilo na kuafikiana kuwa na wilaya mpya ya Malinyi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Nongwa alisema wanataka Malinyi iwe wilaya mpya kwa sababu inakidhi vigezo vya kuwa wilaya na imepiga hatua kubwa kimaendeleo.

Nongwa alisema vigezo vinavyohitajika ili eneo kuwa wilaya ni pamoja na eneo lenye ukubwa wa kilometa 17,000, wakazi zaidi ya 250,000, rasilimali nyingi ukiwemo uwanja wa ndege, hospitali kubwa ya Lugala ambayo kutokana na ukubwa wa miundombinu yake inaaminika kushika nafasi ya tatu kwa ubora wa ukubwa Mkoa wa Morogoro ikitanguliwa na Hospitali ya St. Francis iliyopo Ifakara na Hospitali kubwa ya Mkoa wa Morogoro, hivyo wana haki ya kudai kuwa wilaya.

“Kuna kila sababu ya Ulanga Magharibi kuwa na wilaya kwa sababu vigezo tunavyo, Ulanga Magharibi kuna shule za sekondari zaidi ya 15, Uwanja wa Ndege, kwa upande wa maliasili na utalii tangu mwaka 2005-08 jimbo hili limeweza kuanzisha hifadhi ya vitalu vya uwindaji. Ni eneo lenye chokaa na Mto Kilombero pia,” alisema Nongwa.

Alisema kwa sasa wananchi wa jimbo hilo hupata tabu kupata huduma mbalimbali zikiwemo za kibenki na nyingine kutokana na kusafiri umbali mrefu. Alisema huwalazimu kwenda Mahenge au Ifakara ili kupata huduma hizo.