Monday, August 31, 2009

NDUGU MIRADJI MWILENGA NDIYE M/KITI WA MALINYI DAR ES SALAAM -SACCOSS

MALINYI DAR ES SALAAM SACCOSS JANA J'PILI TAREHE 30.08.2009 KATIKA UKUMBI WA HOTEL YA MAMALAND HOTEL WAMEMCHAGUA KWA KAULI MMOJA NDUGU MIRADJI MYANJAMU MWILENGA KUWA M/KITI WA KWANZA WA TAASISI HIYO YA KUWEKA NA KUKOPA.
WALIOCHAGULIWA NI PAMOJA NA NDUGU SIMON NGANYWILA KWA NAFASI YA MAKAMU M/KITI NA NA MWAKILISHI WA NDANI AMECHAGULIWA NDUGU SAID MPOMBO.

UCHAGUZI ULIANZA KWA KUCHAGUA WAJUMBE WA BODI NAFASI SITA (WALIOCHAGULIWA NI MIRADJI MWILENGA, WENCE MYANJAMO,SIMON NGANYWILA,LOTLINDA MLENGE,SAID MPOMBO NA MADAM KAFIGA), KAMATI YA USIMAMIZI (WALICHAGULIWA NI TOMMY NJIGE, HERMAN NYANGI NA YUSTUS MAKELO) NA MWAKILISHI WA WANACHAMA NI NDUGU ALOYCE MWILENGA.

UCHAGUZI HUO ULISIMAMIWA NA AFISA USHIRIKA MKUU WILAYA YA KINONDONI NDUGU. RAMADHAN BUKUKU.

AKIKABIDHI HATI YA RASMI YA USAJIRI WA MALINYI -DAR ES SALAAM SACCOS , NDUGU BUKUKU ALIWAHIMIZA WANA MALINYI WOTE WAISHIO JIJINI DAR ES SALAAM KUJIUNGA KWA WINGI NA TAASISI HIYO NA KUJENGA UTAMADUNI WA KUJIWEKEA AKIBA NA KUJENGA WIGO MPANA WA KUJIKWAMUA NA UMASKINI.

AMEWATAKA WANA SACCOSS HAO KUJIAMINI NA PIA KUIGA MFANO MZURI ULIOONYESHWA NA MALINYI SACCOSS YA MKOANI MOROGORO KWA JINSI INAVYOJIENDESHA KWA FAIDA YA WANACHAMA WAKE PASIPO MIGOGORO.

NAYE MWENYEKITI WA SACCOSS NDG.MWILENGA AKITOA NENO LA SHURAN KWA WANA MALINYI-DAR ES SALAAM SACCOSS KWA KUMCHAGUA, ALIOMBA USHIRIKIANO WA DHATI TOKA WANA SACCOSS NA CHAMA MAMA MALINYI DEVELOPMENT CONCERN KTK KUFANIKISHA MALENGO YA SACCOSS.

MKUTANO WA UCHAGUZI ULIHITIMISHWA NA MWENYEKITI MAJIRA YA SAA KUMI NA MBILI KAMILI JIONI.

OFISI ZA MALINYI DAR ES SALAAM SACCOS ZIPO BARABARA YA MANDELA KATIKATI YA RIVERSIDE NA MABIBO HOSTEL KTK KITUO CHA DALADALA CHA BAKWATA, UPANDE WA KUSHOTO KUELEKEA UBUNGO.

Habari na Mh. Balozi wa Amani.